Tofauti ya Legacy ya Magufuli na Membe hii hapa!

Desprospero

JF-Expert Member
Feb 1, 2023
887
2,201
Ijulikane kwamba Dikteta John Magufuli na Kachero Bernard Membe wote Sasa ni marehemu. Wote walikuwa ni wana-CCM. Wote wamehudumu kama Mawaziri chini ya Dk. Jakaya Kikwete. Wote waliutaka Urais 2015 lakini kwa isiyo bahati kwa Membe hakufanikiwa kuwa Mgombea wa chama chao, CCM.

Toka 2015 wawili hawa waliingia katika vita kuu ya kisiasa na mahusiano (great political battle) kiasi cha hata kutojuliana hali. Huku Dikteta Magufuli akiamini Membe anamhujumu lakini naye Membe akiamini Magufuli hakuwa na sifa za kiuongozi. Wote Vifo vyao vimejaa maswali na utata mwingi.

Katika maziko yao ilishuhudiwa umati mkubwa na makaburi ya kifahari. Kaburi la Dikteta Magufuli likiwa "sild" mpaka siku ya ufufuo (kama upo) kaburi la Membe ni la ku-slide muda wowote na kuuona mwili wake uliokaushwa. Wakati mwili wa Dikteta Magufuli ukiwa ulifikishwa kijijini kwa gari maalumu na kusimamiwa na JWTZ, Kachero Membe mwili wake ulifikishwa kijijini kwa usafiri wa elikopta maalumu ya JWTZ lakini kila kitu kikisimamiwa na TISS. Mmoja alikuwa Mkuu wa nchi mwingine akiwa ni kiongozi wa kitaifa na Kimataifa.

Swali langu, Iko wapi tofauti ya Legacy yao chanya? Kila mmoja alikuwa mabaya/mazuri yake. Nitaongea kuhusu mazuri yao tu.

Magufuli atakumbukwa kwa kuacha vitu: madaraja, barabara, viwanja vya ndege nk. Magufuli aliamini katika maendeleo ya vitu. Kachero Membe ameacha alama ya watu wanaoweza kuunda vitu maana vitu haviwezi kuunda watu. Aina ya watu waliofika Rondo kumzika kipenzi chao ni ushahidi kwamba alijenga watu na si vitu.

Ikumbukwe 2012 Membe akiwa na ndoto ya Urais 2015 chini ya macho makali ya Jakaya Kikwete alifanikiwa kuwapeleka vijana zaidi ya 129 katika mafunzo ya ujasusi katika nchi mbalimbali kama Cuba, Venezuela, Marekani, Misri, Uingereza na Israeli. Vijana hawa akiwemo "Kigogo2014" walirejea nchini 2014 na kujumlishwa ndani ya TISS. Wakati huo JPM hakuwa na ndoto ya Urais tofauti na Lowassa.

Hii maana yake ni kwamba hata JPM alipokuwa Rais lakini timu ya vijana hawa walikuwa royal kwa Membe na hii ilimsaidia kupata taarifa yoyote aliyotaka kutoka Ikulu ikiwa ni pamoja na mwenendo wa PSU kwa JPM. Licha ya kuhamia ACT-Wazalendo lakini bado alifanikiwa kuwafanya vijana wengi wa CCM kupata Ubunge na kisha Mawaziri. Orodha yao ni ndefu.

Membe alifanikiwa kuwa na watu katika taasisi nyingi nyeti: Ikulu, TRA, TPA, Makanisa, Misikitini, vyama vya siasa, Bunge, vyuo vikuu, Cabinet, Mahakama nakadhalika.

Hali inamfanya Membe aache Legacy ya kutengeneza watu nyuma yake na hivyo kuwa taasisi ilhali mwendazake akiacha Legacy ya daraja la Mfugale, Busisi na vitu vingine. Tuwekeze kwa watu sio vitu. Maendeleo ya watu sio vitu kama Nyerere alivyotuasa.

Pumzikeni kwa Amani Dikteta Magufuli na Kachero Membe.
 
Nilitaka kukuambia neno gumu ila mwanasheria wangu yuko maternity leave as we speak kajifungia jioni hii🤪
 
Hivi kweli unaweza kuthubutu kumlinganisha Rais Magufuli na Benard ?

JPM aikuwa zaid ya Kiongozi yule japo alikuwa na rabsha za hapa ba pale na nyingi katika hizo ni kuzaliwa …watu wengi wa maeneo aliyotoka JPM wako vile

Kama angekuwa hai hadi leo sijui angekuwa kushafumua miradi mipya mingapi ?

Najua Stiglers gauge na Standard gage zingekuwa tayari na mingine mikubwa ingekuwa ishaanza japo ku a watu wangekuwa wamenyooshwa ama kwa kuonewa au kwa makosa yao
 
Magufuli atakumbukwa hata baada ya miaka Mia mbili ijayo kama aliwahi kuwa Rais wa Tanzania.

Kipindi hicho hakuna atakayekuwa anakumbuka kitu kinaitwa Membe.
 
Legacy ya kweli ni ile inayojitangaza. Huhitaji kuambiwa huyu kaacha legacy fulani. Wewe mwenyewe tu ukikiona kitu alichoacha unasema kweli huyu kaacha legacy. Hakuna haja ya kuanza kubishana kwamba fulani kaacha legacy.
 
Magufuli atakumbukwa hata baada ya miaka Mia mbili ijayo kama aliwahi kuwa Rais wa Tanzania.

Kipindi hicho hakuna atakayekuwa anakumbuka kitu kinaitwa Membe.
Juzi tu ilikuwa Magufuli day dodoma. Ukipanda fly over ni Magu, ukipanda ndege Magu, ukipanda treni ya SGR ni Magu. Haya tuambie ukifanya nini unapata Membe au ndio kama unavyosema mpaka tukasukume kaburi ndio tunapata Membe?
 
Juzi tu ilikuwa Magufuli day dodoma. Ukipanda fly over ni Magu, ukipanda ndege Magu, ukipanda treni ya SGR ni Magu. Haya tuambie ukifanya nini unapata Membe au ndio kama unavyosema mpaka tukasukume kaburi ndio tunapata Membe?
Soma posti vizuri uelewe Hadi mwisho. Legacy sio vitu ni watu. Watu hujenga vitu vitu havijengi watu. Read between the lines
 
Huu uzi unatofauti gani na simulizi ya tour za mfalme Zumaridi mbinguni?
 
Sema hivi.. Magufuli alikuwa anatumia maguvu bila akili, wakati Membe alikuwa smart mtu wa intelijensia
 
Nisahihishe kidogo "dictator JPM, " u - dictator wake ulikuwa mtakatifu kwa maana ya kuwalazimisha watu kuwajibika. Tz iliyokuwa imepindishwa na mafisadi ilibidi anyooshe mambo kwa nguvu. Hakika, amini nawaambia, hatutapata tena mkombozi wa namna hiyo.
 
Hivi kweli unaweza kuthubutu kumlinganisha Rais Magufuli na Benard ?

JPM aikuwa zaid ya Kiongozi yule japo alikuwa na rabsha za hapa ba pale na nyingi katika hizo ni kuzaliwa …watu wengi wa maeneo aliyotoka JPM wako vile

Kama angekuwa hai hadi leo sijui angekuwa kushafumua miradi mipya mingapi ?

Najua Stiglers gauge na Standard gage zingekuwa tayari na mingine mikubwa ingekuwa ishaanza japo ku a watu wangekuwa wamenyooshwa ama kwa kuonewa au kwa makosa yao
Kwa pesa ipi? Magufuli alishaanza kukopa kwenye mabenki ya biashara nchini. Halafu Rais SSH kakopa sana mikopo nafuu ya multilateral financial institutions (IDA/WB, ADF/ADB, etc.) ili kuendeleza utekelezaji wa hiyo miradi ambayo hadi sasa bado kabisa kukamilika. SGR yenyewe hata kufika Morogoro tu tabu.

Angekuwa hai wakati huu, hakika watu "wangelimia meno" kama alivyoahidi - very crudely. Mishahara serikalini ingekuwa kama Zaire ya Mobutu, pensheni ndio kabisa, zingefutwa. Pesa za bajeti zingekuwa zinatolewa kishikaji kwa Ujenzi, Majeshi na wateule wachache. It would have been a time of reckoning. Bahati yake na Watanzania kaepushwa na dhahama hiyo.
 
Back
Top Bottom