Hayati Magufuli alipambana na makundi matatu hatarishi na akafanikiwa kuyaangamiza kwa 85%. Je, Rais Samia ataweza kupambana na haya mawili yaliobaki?

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
6,860
12,293
Habari zenu wanaJF wenzangu,

Leo naomba nije na mada inayohusu "maadui mamboleo" wa taifa letu, tukiachana na wale watatu wa zamani waliokuwa wakijulikana kwa majina ya (1) maradhi, (2) uvivu, (3) umasikini.

Sasa tuna maadui wapya watano ambao ni (1) ufisadi, (2) ujinga, (3) ushoga, (4) uteja, na (5) ushamba.

Maadui hawa baadhi yao wana nguvu na hawadhibitiki kiurahisi, kwani wamekuwa wakifadhiliwa hadi na nchi kubwa au ndogo za nje kwa kisingizio cha kutetea haki zao nk.

Sasa ili serikali iweze kupambana vilivyo, na kuwaangamiza maadui hao watano..
1. Ni lazima kwanza kiongozi wa nchi (Rais) awe na nia ya dhati ya kupambana na maadui hao, bila kujali kelele, lawama, dhihaka au matusi atakayokumbana nayo kutoka kwa maadui zake.

2. Ni lazima serikali ipate support kubwa kutoka kwa wananchi ambao ndio huishi na hayo makundi mitaani. Nasema hivi kwa sababu nchi yoyote duniani, wananchi ndio huwa na nguvu kuliko serikali au makundi yoyote ya kihalifu. Ndio maana maadui wengi wa taifa hukimbilia kujificha nyuma ya migongo ya wananchi aidha kwa kutumia 'ujinga' wa wananchi husika, au kuwahonga baadhi ya wananchi ili wale waliohongwa waweze kuwashawishi wenzao waanzishe malumbano au mapigano na serikali yao ili kuwa cover maadui husika.
Hivyo hivyo kwa upande wa serikali pia hujificha nyuma ya migongo ya wananchi ili kuweza kupata information fulani kuhusu mtu au kundi fulani nk.

Ndio maana tuliona aliekuwa raisi wetu wa awamu ya tano hayati John Pombe Magufuli alipotaka, au alipoanza kupambana na "maadui mamboleo" watatu wa taifa letu, alihitaji sana support kutoka kwa wananchi ili aweze kukamilisha mission zake. Na kwa vile wananchi tulimuelewa basi wengi tulikuwa upande wake.

Tofauti na upande wa maadui japo walitumia vijipesa vyao kuwahadaa baadhi ya wananchi na wanasiasa kadhaa wa vyama vya upinzani na tawala, lakini walishindwa vita na kuangukia pua. Kila mtu anafahamu jinsi hayati Magufuli alivyofanikiwa kwa 85% kuwadhibiti maadui watatu na vibaraka wao. Kwa wale wanaotaka kuwafahamu maadui hao waliogalagazwa na hayati Magufuli ni 👇
1. Uteja.
2. Uvivu.
3. Ushoga.

Sasa Rais Samia ameingia na kukutana na maadui wawili ambao ni "ufisadi" na "ujinga".

Na tayari maadui hao washaungana na kuanza mashambulizi dhidi yake, hasa baada ya kugundua kwamba Rais Samia anataka kuikabidhi bandari kwa watu ambao hawatokuwa wanacheka na kima (mafisadi) yale mambo ya kumpigia shemeji simu pale bandarini na kumwambia kuwa 👉kuna mzigo wangu unatoka China nimeuandika kwa jina la "matembele" ukifika hapo naomba unitolee afu mimi nitakuja nyumbani usiku kuuchukua nikuachie ni soda yako mkononi.👈 yatakuwa hayapo.

Mafisadi wengi waliitumia bandari kama kichochoro cha kupitishia mazabe yao mbali mbali yakiwemo madawa ya kulevya, ukwepaji kodi nk, ndio maana serikali ilikuwa ikibadilisha viongozi wa bandari kila leo bila mafanikio.

Sasa kundi hili au adui huyu (fisadi) lazima alalamike kama walivyolalamika wale maadui wengine wa madawa ya kulevya (uteja) nk. Ila kama raisi ana nia ya dhati kama aliyokuwa hayati Magufuli basi na yeye atashinda vita hii kwa asilimia zilezile au zaidi.

Hii ni sawa na vita ya mwenye duka na muuzaji wake, ambapo muuzaji anamlalamikia mwenye duka kuwa kwanini analeta mtu mungine dukani asimamie mauzo ya duka, wakati yeye yupo. Huku mwenye duka nae akisema anafanya hivyo baada ya kuona kila siku mzigo unaisha dukani bila yeye kuona hela.

Tunajua mafisadi yana nguvu ya kuwahonga baadhi ya wanasiasa uchwara wa upinzani na tawala, ili kuwahadaa wananchi ambao baadhi yao wanaendeshwa na adui mungine (ujinga) ila raisi asimame imara maana wazalendo tusioendeshwa na siasa uchwara, pamoja na hongo ya shilingi mbili tatu tupo nyuma ya Serikali yake.

Bila shaka mafisadi yanapata uungwaji mkono, na hata viela vya kuongeza mapambano dhidi ya serikali yao kutoka kwa jirani yetu ambae ni adui yetu mkubwa kiuchumi. Lakini naamini serikali yetu itashinda na wao watashindwa, kama walivyoshindwa kwenye swala la ngoro ngoro.

Swali ni, je Rais Samia ataweza kukaza ili kuwashinda maadui hao kama hayati Magufuli?
 
Magufuli hakumuogopa au kumhofia mtu yoyote katika mapambano yake.
Chenge, Karamagi, Daniel Yona walitajwa kwenye ripoti ya Profesa Ossoro kuhusu uhujumu uchumi kwenye madini, na tume ile ikapendekeza wakamatwe, mbona hakuwakamata wala kuwafungulia mashtaka ili tujue hakumuogopa yoyote?
 
Kama kuukataa mkataba wa DP na ubovu wake na usio na kikomo ni kuwa fisadi! Na Mimi nimo kwenye huo ufisadi

Hivi nyinyi mtaelewa lini kwamba, wananchi hawapingi mkataba ila masharti ya kijinga yaliyopo kwenye mkataba?

Nikuulize!

Ni lini sisi watanzania mmetupima na mkajiridhisha kuwa, tangu hivi leo mpaka mwisho wa dunia, hatutakuwa na uwezo kabisa wa kusimamia Bandari zetu, hadi kuamua kuwapa warabu uhai wote wa bahari na Bandari nchini?
 
Hakuna adui baya na lenye laana kama kumwaga damu ya binadamu.
Watawala wote ulimwenguni waliolipenda nq walioshindwa kulidhibiti adui hili waliishia pabaya.
 
Kama kuukataa mkataba wa DP na ubovu wake na usio na kikomo ni kuwa fisadi! Na Mimi nimo kwenye huo ufisadi

Hivi nyinyi mtaelewa lini kwamba, wananchi hawapingi mkataba ila masharti ya kijinga yaliyopo kwenye mkataba?

Nikuulize!

Ni lini sisi watanzania mmetupima na mkajiridhisha kuwa, tangu hivi leo mpaka mwisho wa dunia, hatutakuwa na uwezo kabisa wa kusimamia Bandari zetu, hadi kuamua kuwapa warabu uhai wote wa bahari na Bandari nchini?
Usiseme wananchi hawapingi, sema hatupingi (jisemee mwenyewe) maana wengine hatuko upande wa walioshikiwa akili na wanasiasa uchwara waliozoea kudandia kila wanachoona kitawapa credit bila kujali kama walichodandia kina faida au hasara kwa taifa.

Unaposema ni lini mlipimwa kama mnaweza kuendesha bandari, je toka uhuru hadi leo bado haujaona kama mlipimwa na mkashindwa kuendesha bandari.

Sana sana bandari ilikuwa inatumika kupitisha mizigo ya watu kwa njia za magendo, na kuwanufaisha wachache waliofanya kazi bandarini.
 
Hakuna adui baya na lenye laana kama kumwaga damu ya binadamu.
Watawala wote ulimwenguni waliolipenda nq walioshindwa kulidhibiti adui hili waliishia pabaya.
Bahati nzuri adui huyo unaemsema hapa hajawahi kujitokeza nchini kwetu mkuu. Ndio maana mimi sikumuongelea.
 
Back
Top Bottom