Hayati Magufuli alikosea kwenye mambo mengi mno. Kubwa mojawapo ni kumchagua huyu mtu

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,242
113,627
Mtu huyo ni Rais Samia!

Nashawishika kabisa kuamini kuwa huyu Samia alichaguliwa kutokana na jinsia yake tu [kama ilivyojuwa kwa Kamala Harris…the word salad queen…kule Marekani]. Ref: Uchaguzi 2020 - Mkutano Mkuu wa CCM 2020 wamchagua John Magufuli kuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Amteua Samia Suluhu kuwa Mgombea Mwenza ambapo Marehemu Magufuli alisema "Nawaambia hii siri, Hussein Mwinyi nilimteua kuwa mgombea mwenza pamoja na Mama Samia (2015), lakini kwakuwa Mama Samia ni mwanamke akashinda kuwa makamu wa rais, maana huwezi kushindana na Wanawake ukashinda, wanawake wanatuzidi kwa mambo mengi, wanawake oyee."

Kamala yeye alichaguliwa na Biden kuwa mgombea mwenza kwa sababu ni mwanamke mweusi [ingawa kiuhalisia ni chotara wa Kihindi na Kijamaica].

Kamala ni mweupe kabisa. Yaani hovyo to the nth degree. Anaongeaga mashudu tu [word salads].

Hana kabisa uwezo wa kuongoza. Yeye ni kucheka cheka tu na kuongea mambo yasiyoeleweka.

Ukimwangalia Biden, unaona kabisa jamaa anapaswa awe nyumbani. Kazi ya urais wa Marekani kwa sasa haiwezi.

He is a creepy old guy. Hebu angalia hapa



Hivi alikuwa anafanya nini hapo kwa hako katoto? Na hiyo ni wiki iliyopita alipokuwa Finland baada ya kutoka Lithuania kwenye mkutano wa NATO.

Biden muda wowote anaondoka. Iwe kwa kujiuzulu, kuamua kutogombea tena muhula wa pili, au hata kufa [ingawa kifo hakina mwenyewe].

Wazo la Kamala kuja kuwa Rais wa Marekani endapo Biden ataondoka, linatisha watu wengi sana.

Haya, tuje kwa huyu wa kwetu hapa.

Huyu naye alichaguliwa kwa sababu ya identity politics tu. Ni mwanamke na ni Mzanzibari.

Kwa ninayoyaona, ni mtu asiye na uwezo wa kiuongozi ngazi ya Rais wa nchi.

Hakuchaguliwa kutokana na sifa zake za kiuongozi.

Inavyoonekana Magufuli alikuwa anataka sifa ya kuwa na mgombea wa kwanza wa CCM kumchagua mwanamke kuwa mgombea mwenza wake.

Haiwezekani kabisa kuwa Samia alichaguliwa kutokana na sifa zake kiutendaji [kwa sababu hana].

Jahazi limeshamshinda hivi sasa. Kabaki kutoa vitisho na kutumia dola kukabiliana na wanaompinga.

Na ukiongeza na inferiority complex aliyonayo kutokana na jinsia yake, ndo kabisa anakuwa paranoid kwamba kila anayempinga, anafanya hivyo kwa kusukumwa na chuki dhidi yake kwa sababu yeye ni mwanamke!

Rais Magufuli hakuwa kiongozi mzuri. Nilishasema mara nyingi tu kuwa yeye alikuwa msimamizi/ mnyapara mzuri.

Yeye mpe kazi au mradi ausimamie, halafu umpe mamlaka ya kutosha kuweza kufanya maamuzi ndani ya ukomo fulani, utampenda maana hakuwa wa mchezo mchezo.

Sidhani kabisa kuwa Magufuli aliwaza kuhusu yeye kuishia njiani na kumwacha Samia ndo awe Rais.

Nadhani alidhani kuwa atamaliza vipindi vyote viwili na kustaafu kama walivyofanya waliomtangulia.

Lakini haikuwa hivyo. Tumeachiwa huyu Samia.

Makamu wa Rais, Dkt. Mpango, kwa mtazamo wangu, ni bora mara 100 kuliko Samia [I got bars too 😀].
 
Mtu huyo ni Samia!

Nashawishika kabisa kuamini kuwa huyu Samia alichaguliwa kutokana na jinsia yake tu [kama ilivyojuwa kwa Kamala Harris…the word salad queen…kule Marekani].

Kamala yeye alichaguliwa na Biden kuwa mgombea mwenza kwa sababu ni mwanamke mweusi [ingawa kiuhalisia ni gu, ni bora mara 100 kuliko Samia [I got bars too 😀].
Kwenye mkutano mkuu wa ccm 2020 Magufuli alisema wazi kabisa kwamba yeye chaguo lake namba moja la mgombea mwenza alikuwa Hussein Mwinyi ila wazee wakamchagua Samia yeye hakumpenda kabisa ila chama kiliamua
 
Ndio bahati mbaya iyo clip sina ila alisema wakati akimsifu Hussein Mwinyi kuwa anafaa kuwa rais wa Zanzibar na hapo hapo akimteua Samia kuwa mgombea Mwenza kwa awamu ya pili. Mwisho alisema ukishindana na mwanamke lazima ushindwe ndio maana Samia alimshinda Hussein Mwinyi
🤣🤣🤣

Yaani Samia alimshinda Hussein Mwinyi?

Sifa za uongo hizo.
 
Mtu huyo ni Samia!

Nashawishika kabisa kuamini kuwa huyu Samia alichaguliwa kutokana na jinsia yake tu [kama ilivyojuwa kwa Kamala Harris…the word salad queen…kule Marekani].



Makamu wa Rais, Dkt. Mpango, kwa mtazamo wangu, ni bora mara 100 kuliko Samia [I got bars too ].
Hata huyu JPM kupata huo uraisi ilikua bahati nasibu tu using kua ugomvi kati ya Lowassa na marehemu Membe JPM angekufa kama Msukuma wa kawaida.
 
Uliona wapi mtu anachagua msaidizi smart kuzidi yeye
Siyo mashindano ya akili.

Ni suala la uwezo.

Ronald Reagan alikuwa na George H. Bush.

Bill Clinton alikuwa na Al Gore.

George W. Bush alikuwa na Dick Cheney.

Hata Donald Trump alikuwa na Mike Pence.

Hao makamu wa Rais wote walikuwa na uwezo wa kuwa marais wa Marekani.
 
Tujilaumu wenyewe Kwa kumpinga na kumtukana Magu aliyedhamiria kuibadili Nchi Kwa muda mfupi,

Hivi sasa, watu wameficha petrol na diesel na hawafanywi kitu,

Magu aliwatisha kufutia lesseni walipogomea EFD na waliufyata.

Aje Dikteta mwingine tafadhali🙏🙏
 
Kila kitu kimepangwa kuhusu Kamala, wakubwa wa Dunia wanataka kudestroy western Christian civilization na ndiyo maana wamemuweka Biden ambaye atamuachia Kamala ambaye anakwenda kuizika USA na Western christian world kimoja tuombee sana Ukristo (western) usishindwe, kuhusu kwetu Magufuli hakujua wala hakuwahi kudhani nafikiri kama Uraisi wake ungekatishwa nadhani aliamini kabisa kama Maraisi wengine kwamba angeongoza Miaka 5 na mitano mingine na kumwachia mwingine lkn sidhani kama alifikiria hata kidogo kama mambo yangebadilika/shwa wengi TZ maraisi hawakukifikira sana cheo cha Umakamu wa raisi kwa kifupi ni president in waiting.

Women Destroy Nations …
 
Back
Top Bottom