Haya sasa hawa ndo ACACIA!

Haya sasa hawa ndo ACACIA!

WA TZ bhn nchi ya kwenu, Mali za kwenu, Acacia wako kwenu, Wameiba mali yenu, Nashangaa sana mnavyosambaza woga kwa wananchi., Ili iweje..?? Kama mtu kaamua na kasema anaweza mpeni walau support bhas....

Sipati picha km TZ leo hii ikiingia vitani sidhani kama kutakua na wazalendo wa kufia nchi hii....!?? Yaan hatuna umoja hata kidogo..!! Muda mwingine hua naona bora chama kimoja tu kingebaki, Upinzani walifanya vizuri lkn kwa hii sumu walowapa wananchi nawalaumu sana..!!
You are really great thinker...unaona mbali sana
 
Jamani hapa mimi sioni majadiliano yoyote. Kuna madai ambayo yana ushahidi. Issue hapa si nani ataongea lugha gani. Issue ni kulipa hela zetu na kuweka mikataba sawa kwa siku za usoni au wasepe. Mara zote mtu akienda kwenye kesi kama hizi unakuwa umejicholea msitari wako kwamba hapa ni mwisho na ni kitu ambacho mi sina wasiwasi nacho. Kina Prof. Kabudi hawashindwi hilo.
 
Wakati esta anaingia malangoni pa mfalme kuomba ili awakomboe wayahudi mikonon mwa Haman wayahud walikua wakifunga na kuomba juu ya malikia nashangaa sana kuona viongozi wa dini hadi sasa wako kimya badala ya kuwasihi waumini kufunga na kuomba juu ya Serikali na raisi wetu ili tutakapo kutana na acacia mezan tz tushinde kwa msaada wa mungu
 
Kisicho na mafisadi na wapiga kelele bila mpango...!! Unaweza ukakipa jina mwenyewe unalolijua, lolote lile.!
Ahaaa unaongelea kile kinachopiga meza tena kwa mikono 2 mwisho wanamalizia na NDIOOOOOOOOOOOOOOOO
Waliosema Ndio wameshinda
 
WA TZ bhn nchi ya kwenu, Mali za kwenu, Acacia wako kwenu, Wameiba mali yenu, Nashangaa sana mnavyosambaza woga kwa wananchi., Ili iweje..?? Kama mtu kaamua na kasema anaweza mpeni walau support bhas....

Sipati picha km TZ leo hii ikiingia vitani sidhani kama kutakua na wazalendo wa kufia nchi hii....!?? Yaan hatuna umoja hata kidogo..!! Muda mwingine hua naona bora chama kimoja tu kingebaki, Upinzani walifanya vizuri lkn kwa hii sumu walowapa wananchi nawalaumu sana..!!
Watu wamepumbazwa na uzalendo, wakati wengine wanatumia mgongo wa uzalendo kwa kuila nchi.
 
Soma na haya maneno ya mwenzenu hapo kwenye blue hivi wakala ni yule anayesema kutetea uhalisia wa tukio au yule aliyeweka saini kwenye sheria na mikataba ili hao wezi waibe? Duhh!! nalaani sana kuzaliwa Tanzania

WAZIRI NCHEMBA ATOA SIRI SABABU YA MKAPA NA KIKWETE KUHUSISHWA SAKATA LA MAKINIKIA

KITAIFA

BY RABI HUME

JUNE 18, 2017

Ikiwa zimepita siku chache tangu Rais Magufuli kuzuia watu kuwahusisha Marais wawili wastaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete na Benjamin Mkapa katika sakata la mchanga wa dhahabu (makinikia) kwani katika ripoti zote mbili hakuna sehemu ambayo imewataja wastaafu kuhusika.

Waziri wa Mambo ya ndani na Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba amesema wezi hao walitafuta kichaka cha kutaja viongozi waliostaafu ili kuzia serikali iache kufatilia sakata hilo.

“Viongozi wetu hawajawai kuwa mawakala wa wale wanao tuibia, mawakala tumewabaini ni wale wanao watetea wezi,” alisema Waziri Nchemba.

Waziri Mwigulu ameongeza kusema sifa ambayo inafanya viongozi walioko madarakani wasing’ang’anie madaraka ni viongozi wastaafu kuheshimiwa baada ya muda wa uongozi.

Waziri Mwigulu ameyaongea hayo akiwa katika kijiji cha Zinzirigi katika Tarafa ya Ndago katika mwendelezo wa ziara jimbo kwake Iramba Magharibi kuongea na wananchi kuwaeleza alipofikia kuhusu ahadi ambazo walikubaliana kutekeleza hasa suala la umeme kutokufika katika vijiji vingi akieleza kuwa sababu ni mkandarasi aliyekuwepo mkoa wa Singida aliyetolewa baada ya kushindwa kazi lakini sasa ameambiwa na watu wa wizara ya nishati kuwa wakandarasi wawili wameshapatikana hivyo kuanzia sasa zoezi la kuunganisha umeme vijijini utaendelea kwa kasi hasa wa REA awamu ya Tatu.

Kuhusu ujenzi wa zahanati amesema mpaka sasa zahanati katika vijiji vingi alipopita zimefika hatua nzuri ya kupaua na kuwahidi kuwa pelekea mabati na mbao na mifuko ya saruji 100 ili zahanati hizo zikamilike na kuanza kutoa huduma mapema sana.
Hatujadili historia. Kama rais anafanya juhudi kunusuru nchi halafu mwingine anapinga kila hatua inayochukuliwa huoni kama ni usaliti? Hovyo kabisa
 
Wakati esta anaingia malangoni pa mfalme kuomba ili awakomboe wayahudi mikonon mwa Haman wayahud walikua wakifunga na kuomba juu ya malikia nashangaa sana kuona viongozi wa dini hadi sasa wako kimya badala ya kuwasihi waumini kufunga na kuomba juu ya Serikali na raisi wetu ili tutakapo kutana na acacia mezan tz tushinde kwa msaada wa mungu
Nani awaombee
Hao c ndio wabunge ficem na wakati huo Pombe alikuwemo akipiga makofi na wanazomea mjengoni kupinga wapinzani wasitetee Mali ya nchi isiibiwe
Leo mnataka maombi baada ya miaka 19 ya ufisadi wenu
JIOMBEENI WENYEWE
 
Watu tushaanza kwenda driving skull ya Noah,hatupendagi ujinga sisi! Trillion 108 izoooo
 
Wanabodi kuna hiyo kitu hapo. Je, tutachomoka wakituletea hao wataalamu kwenye mazungumzo?
95b74b177c2be5a1b1edae75c7117160.jpg

Hiyo "plomatic" ndiyo mdudu gani?
 
Nitawaona mna point kidogo mngejikita kutoa point za tunashindaje kwa tuliokwisha yaanza..!! Na sio kusambaza woga huo.. Alafu ulipokosea umem refer Millardayo ambaye kaishia la nne...!!
Cha kushangaza zaidi ni kuwa wewe ambaye PhD holder ulishiriki kuipitisha mikataba hiyo ndioooooooooo. Labda siku hiyo wewe ulikuwa umeshikiwa akili zako na Bashite.
 
Hatujadili historia. Kama rais anafanya juhudi kunusuru nchi halafu mwingine anapinga kila hatua inayochukuliwa huoni kama ni usaliti? Hovyo kabisa
Hivi kipindi hicho wapinzani wanatoa hoja za kusaidia kuinusuru nchi na huo wizi mpaka mkawafukuza bungeni ndo ulikuwa uzalendo!? Au huyo Magufuli mnayemuona kama mkombozi wenu yeye hakushiriki kuitikia ndioooooooooo tena kwa mbwembwe zote!?
 
Wapumbavu pekee ndiyo wanaoliombea taifa hili lisifanikiwe.

Usije ukategemea kuwa katika nchi ya watu milioni 55, kika mtu atakuwa na mawazo kama yako. Pia elewa kuwa siyo wananchi wote hawana uwezo wa kun'gamua ukweli na uongo ni upi.
 
Watanzania tuko wajabu sana....wale wale wanaotuletea taifa hili hasara ndo haohao wanaotushawishi tuwapongeze wanapoanza move nyingine.....hizi move zenu mnazozianza kwa mbwembwe na baadaye wenyewe mnawatangazia wananchi kwanba zimeleta hasara katika nchi tutakuwa mazuzu kuwapongeza.... zingekuwa na matokeo mazuri mgekuwa na haki ya kutulaumu tunapowapinga.
Move kama za Bulyankhuru,
Richmond, IPTL, Gesi, ESCROW, EPA....Sheria na mikataba
yake...hivyo hivyo mlitushawishi sana tuwapongeza..leo mnataka
tuwapongeze kwa kutuonyesha hasara mliosababishia taifa...badala ya kutuomba samahani kama kweli ni wazalendo.
 
Nitawaona mna point kidogo mngejikita kutoa point za tunashindaje kwa tuliokwisha yaanza..!! Na sio kusambaza woga huo.. Alafu ulipokosea umem refer Millardayo ambaye kaishia la nne...!!
mshakosea wanzo sasa sisi tufanyeje ujuaji wingi mwisho mnaomba tuwaunge mkono unaleta sifa kwenye mikataba za kimataifa unazani barric ni manji moto mnao
 
Back
Top Bottom