Haya ni makosa makubwa mawili yanayofanywa na wajasiriamali wengi na kuishia kujuta.

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,223
22,301
Kuna wajasiriamali wengi huishia kujuta kwa kupoteza mitaji yao bila hata kufanya starehe yoyote wala matumizi mengine mabaya. Leo tutaangazia sababu mbili ambazo zinachangiwa sana na hawa wanaojiita Motivational speakers na life coaches.

1. Kudhani wanaijua biashara na kutojifunza zaidi

Huu ni ugonjwa mkubwa. Ili biashara idumu inabidi mfanyabiashara kila siku awe anafuatilia kila kitu kinachoendelea kwenye biashara yake. Kwa mfano mtu wa IT inabidi awe makini kufuatilia mabadiliko yanayotokea kwenye teknolojia kila siku. Kujifunza Marketing skills mpya. Yaani kimsingi kufuatilia hadi rate of exchanges na hata mabadiliko ya sheria kama yanayogusa biashara. Hii inasaidia kujua status ya biashara ili uchukue hatua stahiki. Kuna watu huwa hawataki kujifunza lolote na kuishia kukimbilia kwa waganga ili kupata mvuto wa biashara. USIIZOEE BIASHARA YAKO. KILA SIKU IONE MPYA.

2. Kuanzisha biashara nyingine wakati ya kwanza bado haijakaa sawa

Motivational speakers husema usiweke mayai yote kwenye kikapu kimoja. Wanaweza kuwa sawa ila ukifuata huo msemo bila kutafakari lazima ukwame. Mayai unaweza weka kwenye kapu moja ukayapanga vizuri na kuwa makini kwenye ubebaji. Mtu anaanzisha duka la nguo leo kisha after 3 months anachukua hela kwenye nguo anafungua banda la kuku. Hii ni kuumiza biashara ya kwanza kipuuzi. Matokeo yake biashara zote mbili zinakuwa dhaifu na mwishowe kufa.
 
Kingine wafanya biashara wengi wanadharau sana wateja.
 
3. kutokukubali kwenda na kasi ya dunia inafanya biashara nyingi zikose wateja na hatimar kufa kabisa
 
Back
Top Bottom