FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 92,883
- 109,212
Kabla ya kuanza ushauri wangu nachukuwa nafasi jujitambulisha.
Kwa wasionielewa, binafsi nilifanya kazi kwa miaka mingi sana nje ya Tanzania. Kazi zangu zote zilihusu sayansi ya mawasiliano na biashara. Nilipostaafu nje huko, nilirudi nyumbani nikafunguwa kazi za Ushauri wa Kibiashara (Business Consultancy) nayo ikazaa kazi zingine kadhaa ndogo ndogo. Sasa ni nusu Mstaafu (semi retired) na kazi zote nazifanya kutokea nyumbani kwangu.
Ushauri Wangu :
Kwa kuwa Tanzania tumedhamiria na tumeshaamuwa kuukuza uchumi kwa kukaribisha wawekezaji ili wawekeze Tanzania. Hilo ni jambo jema sana.
Ili tupate mafanikio ya haraka kama nchi na wananchi. Naamini mafanikio yoyote ya nchi kwanza ni muhimu sana yaonekane kwa maisha ya wananchi siyo kwenye takwimu tu. Kila mwanachi ni lazima yeye mwenyewe binagsi ayahisi mabadiliko, siyo mpaka zipigwe propaganda za kumuaminisha mwananchi kuwa Tanzania kuna mafanikio. Kama wsle. Ndugu zangu (Waarabu wa kuchovya) ambao ukimuuliza wewe kabila gani? Kukujibu mpaka aanze kwa kuapa "Wallahi mimi Mwarabu" 😂😂😂. Kwa nchi yenye mageuzi ya kweli ya kimaendeleo haitakiwi iwe hivyo hivyo, maendeleo na mafanikio ayahisi mwenyewe mwananchi.
Ni muhimu sana mambo mengibya namna tunavyoyaendesha kwenye uchumi wetu ni lazima tuyabadilishe haraka sana. Kwa kuanzia nashauri tuanze na mawili makubwa lakini ni myepesi sana serikali kuyatekeleza. Yataanza juonesha athari chanya mara moja (positive results).
1) "Peg" Kigingi.
Kwa haraka sana tuiwekee vigingi (peg) Shillingi yetu ili tuifungamanishe na pesa za nje zinazitumika kwa wingi kwenye biashara za kimataifa. Tunaweza juweka vigingi (pegs) kwenye sarafu nyingi tu duniani. Ingawa duniani huko ilizoweleka sana kuweka kigingi kwenye US Dollar peke yake, lakini dunia ya leo na mambo yanavyobadilika kwa haraka, si kazima kuweka kigingi kwenye sarafu (currency) moja tu.
Kwa kufanya hivyo kwenye biashara yetu kwa miaka mingi usoni hakutakuwa na mifumuko (inflation) zabghafla kwa bidhaa zetu kama ilivyo sasa.
Wafanya biashara na serikali wstsweza kupanga bajeti zao za mapato na matumizi kwa ufanisi zaidi.
Tutawavuta wawekezaji wengi wakubwa sana ambao kwa sasa uwekezaji wao wote unadhaminiwa kwa sarafu za nchi wanazowekeza kuwa na vigingi.
Ni vigumu kuwsvuta Tanzania. Wawekezaji wenye mitaji mikubwa kama hatuna dhamana ya uwekezaji wao kubaki na thamani ile ile ndani ya muda wa kurudisha mitaji yao (ROI), ambao mara nyingi huwa kati ya miaka 2 mpaka 5. Na dhamananrahusi ninkuwa nansarafu isyopanda na kushuka, yqani iwe pegged. Mfano, kuna nchi duniani huko leo miaka 40 mpaka 50 sarafu zao na.zingine zimebaki kiwango kile kile (stable).
Wakulima wetu watakuwa na uhakika wa bei za mazao yao wakati wote.
Walaji, wananchi walio wengi, watakuwa na uhakika wa kufanya bajeti nzuri za matumizi yetu kwa kipato chetu.
Sarafu yetu itakuwepo kwenye soko la kimataifa na tunaweza kusafiri nayo na kuibadilisha kwa thamani inayojukina bila tatizo lolote (convertible), siyo kama ilivyo sasa. Mpaka inaitwa *pesa ya madafu".
2) "Same rate taxation on everything".
Kodi zetu za mapato kwa serikali tuzibadili ziwe na kiwango kimoja tu cha kupigia mahesabu ya kodi. Siyo kama ilivyo sasa, kila kitu na namna yake ya mahesabu na vitu vinaongezeka kila siku. Hii ya kodi kuwa na viwango vingi vya namna nyingi tofauti kunafanya mianya ya rushwa iwe mingi sana na wizi wa ujwepaji kodi unaongezeka.
Hayo mawili kwa sasa yanatosha kabisa kuanzia, ni mambo yaliyopo duniani huko.
Mama na Mwigulu huu ni ushauri muhimu sana.
Nawasilisha na nakaribisha maswali.