Haya ndiyo Maendeleo (Picha)

FM
huko inakoelekea hiyo mark2 ukiangaza macho unaiona bahari kwa mbele. Sasa hapo sijui hawakuweka mitaro wakapiga hesabu kuwa maji yatatiririka kufuata slope na kuingia baharini au sijui ni vipi.
Hivi kweli ndiyo kusema hatuna city planners??au ndiyo wako usingizini mpaka waamshwe na majanga.
 
Jamani serikali yetu ipo na viongozi wetu wapo na wanalipwa mishahara minono na wanafanya kazi kwa ari mpya,nguvu mpya na kasi mpya kwa hiyo msishangae sana subirini maendeleo yanakuja mwaka 2025!
 
Shimo la kinyesi!?

Mkuu Darwin, swali lako ni zuri sana na mshangao pia.... Hebu jiulize yale majumba yote mjini waste water (brakish and grey water) wanapelekea wapi?? Mara ngapi umeona honey sucker in town?? Ukweli ni kwamba our sewer lines in the CBD are underground designed (then during the old days) kubeba both storm water na domestic sewage.... So ukiona madimbwi Jijini Mkuu usidhani ni mvua tu, kuna mengi ndani yake... System hii pia ilikuwepo O'bay....... Hivyo usishangae Mkuu kinyesi nacho kilikuwemo!!!!

Haya waungwana nambieni swala kama hili lipo chini ya wizara gani?.. Miundombinu ama serikali za mitaa!

Mkuu Mkandara, kuna mgawanyo wa majukumu katika miundombinu hapa nyumbani wakati mwingine unachanganyikiwa.... Lakini kwa uelewa wangu developmental projects zipo kwa MoW, Maintenance ya mabarabara ya mijini na vijijini TAMISEMI, Maintenance na ujenzi wa barabara kuu TANROADS.... I welcome criticism.... Swala letu ni kuhusu drainage ambayo ipo directly under Maji safi na Maji taka in conjunction with TAMISEMI.... Tukumbuke kuwa pale CBD maji taka yanachukuliwa na underground system and in this case ni swala la collapse of structures na pia overloaded of the system.... So hapo TAMISEMI na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA, zamani walikuwa wanaitwa DSSD sasa haya ya DAWASA, ni mageni kidogo na am still confused)!!

......ndio hali halisi jamani! serikali haina fwedha. mwee, hilo shimo utafikiri upo Baghdad.

Yourna.........., Mkuu umeongea point lakini unajua budget ya TAMISEMI kwa mwaka?? Je pia unajua ni kiasi gani cha fedha hizo hurudishwa kwa mwaka (on average??)..... Kwa kweli pesa sio kigezo kabisa, nadhani nipo njiani kumfuata na kukubaliana na Nyani Ngabu, waAfrika nd.......!! Am still trying to avoid acceptance.....
 
34ispr9.jpg

Picha: hisani ya www.thisday.co.tz
 
2008-05-20 16:26:29
Na Francisca Jeremiah, Jijini

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Abas Kandoro, amestushwa na `usanii` wa mikataba ya ujenzi wa barabara kadhaa za manispaa za Jiji lake na kueleza kuwa kuanzia sasa ataripoti kwenye Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini, TAKUKURU ili ichunguze mikataba hiyo baina ya Manispaa na makandarasi wanaopata tenda hizo.

Aidha, Kandoro amesema ana hofu juu ya usahihi wa mikataba hiyo kutokana na viwango duni vya ujenzi wa barabara, tofauti na viwango vinavyostahili ambapo akasema hali hiyo husababisha upotevu wa fedha nyingi huku ujenzi ukiwa mbovu.
Bw. Kandoro ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na Wajumbe wa Kikao cha Bodi ya barabara Mkoa wa Dar , kilichoandaliwa na TANROADS na ambacho kilikuwa kikijadili uboreshaji wa miundombinu ya Jiji.

Mkuu huyo wa Mkoa alifikia hatua hiyo kutokana na kustushwa na kitendo kilichofanywa na Halmashauri ya Ilala kwa kumpa tenda ya ujenzi wa barabara ya Mtaa wa Lindi na Gerezani Mkandarasi mmoja pasipo kuandikishiana mkataba wowote ule kwa kazi hiyo.

Bw. Kandoro akasema mkandarasi huyo amepewa tenda ya kufanya kazi, lakini hakuna sehemu ya mkataba uliosainiwa kati yake na Manispaa.

``Je, malipo ya mkandarasi huyu yakoje? Nadhani kuna ubabaishaji umepita hapo,`` akasema Bw. Kandoro.

Akaongeza kuwa licha ya mkandarasi huyo kufanya kazi bila mkataba, pia barabara hizo hazina viwango vya kuridhisha ambapo mpaka sasa, zimeshakuwa na mashimo wakati hata mwaka hazijamaliza tangu zikamilike.

``Inawezekana pia kwamba kuna uzembe unaofanywa na wahandisi wetu kwa kukubali kuburuzwa na makandarasi wao ama kukaa ofisini na si kuwajibika katika sehemu zao za kazi... au fedha hizo zinatafunwa. Yote yanawezekana,`` akasema Mkuu huyo.

Akasema anashtushwa na taarifa zinazotolewa kuhusu utendaji kazi wa wakandarasi kwa kuonesha barabara nyingi zimejengwa, lakini barabara zote ni mbovu na kamwe hazidumu.

Naye Mbunge wa Jimbo la Temeke Bw. Abbas Mtemvu, aliomba wajumbe wa kikao hicho kumsimamisha kazi mara moja mkandarasi ambaye alipewa tenda ya kujenga barabara ya Tandika Devis Corner kutokiana na kitendo chake cha kutomaliza kazi kwa haraka.

Bw. Mtemvu akasema kuwa kazi inayofanywa na mkandarasi huyo hairidhishi na amekuwa akitumia muda mwingi katika ujenzi huo na hadi sasa hakuna maendeleo ya maana.

``Cha kusikitisha zaidi tulipofika katika eneo lake la ufanyaji kazi na baadhi ya wajumbe, mkandarasi huyo alitukimbia kwa kujua hana cha kutueleza... hata alipokuwa akipigiwa simu, hakutaka kupokea kwa kuogopa maswali yetu,`` akasema Bw. Mtemvu .
 
Sitashangaa mpaka mwaka unaisha hilo shimo litabaki hivyo hivyo sijui wanasubiri mpaka atumbukie fisadi mmoja apige kelele then watatengeneza....utadhani wako usingizini
 
Mkuu mwanakijiji
Naamini pia Kandoro atastushwa sana kila siku maana siku hizi serikli haifanyi kazi mpaka media itoe malalamiko yetu wananchi kuhusu kutoridhishwa na jambo fulani. Hivi serikali ni nani na yuko wapi?? Who is who??
 
Hizi ajira mil moja kweli inabidi kuzoa taka iwe mojawapo.

Umekosea kitu kimoja thawgh.... taka ni mbolea na sio mali.....
"Taka ni mali" Ilikupasa kuuliza ni kwa nini taka ni mali? Kupitia taka unaweza kuongeza ajira kwa mamima ya vijana, Taka kwa upande mwingine ni malighafi, Hivyo wakusanyaji wa taka wananufaika na uuzaji wa taka, kumbuka kuwa taka siku hizi hazizolewi bure... Huko kwenye mbolea ni baada ya kutenganisha taka malighafi na taka zinazoweza kutengeneza mbolea, aidha mbolea nayo haiuzwi bure au kugawiwa bure... Mwisho wa siku unabaki vilevile kuwa Taka ni Mali
 
Haya mkuu nimekukubali...... bonge la pass ya Jayson Kidd nimekupatia hapo na umedanki vizuri kabisa.

Thanks!
 
Haya mkuu nimekukubali...... bonge la pass ya Jayson Kidd nimekupatia hapo na umedanki vizuri kabisa.

Thanks!
Tatizo sichezi mpira wa kikapu, na huko kwenye mabingwa wa kudanki wala sipajui...

Huku nilipo nahamasisha kila wadi kuwa na CBO ili kuweza kuondoa kero zao kwa njia ya kujitolea au kuchangia...
 
Tatizo sichezi mpira wa kikapu, na huko kwenye mabingwa wa kudanki wala sipajui...

Huku nilipo nahamasisha kila wadi kuwa na CBO ili kuweza kuondoa kero zao kwa njia ya kujitolea au kuchangia...

usianze kuringa sasa maana nitaondoa shukurani yangu na nianze kukushikia bango na fani yako ya kuzoa taka.... kwi kwi kwi
 
usianze kuringa sasa maana nitaondoa shukurani yangu na nianze kukushikia bango na fani yako ya kuzoa taka.... kwi kwi kwi
:D :D
Leo hii hapo TZ mamia ya kinamama wajane na waliokuwa kwenye ndoa kupitia CBO wanatengeneza pesa kwa ajili ya taka

Nyani yuko wapi leo?
 
"Taka ni mali" Ilikupasa kuuliza ni kwa nini taka ni mali? Kupitia taka unaweza kuongeza ajira kwa mamima ya vijana, Taka kwa upande mwingine ni malighafi, Hivyo wakusanyaji wa taka wananufaika na uuzaji wa taka, kumbuka kuwa taka siku hizi hazizolewi bure... Huko kwenye mbolea ni baada ya kutenganisha taka malighafi na taka zinazoweza kutengeneza mbolea, aidha mbolea nayo haiuzwi bure au kugawiwa bure... Mwisho wa siku unabaki vilevile kuwa Taka ni Mali

Kamanda, kweli sasa nimeamini wewe hii ni "fani".
 
Back
Top Bottom