Haya ndiyo Maendeleo (Picha)

Hivi hilo shimo lilivyokaa ni kama yale mahandaki yanayotokea baada ya vizibo kuchukuliwa kwa ajili ya metal market. Sasa inawezekana mtu aliyechukua mfuniko huo hana garii hivyo shimo la katikati ya barabara halimhusu?
 
Mwanakijiji Unafikiri Suluhisho La Tatizo Hilo Kama Ulivyoeleza Kwa Njia Ya Picha Ni Nini ? Naamini Utakuwa Na Wazo Moja Au Mengi Katika Kukabiliana Na Tatizo Hilo Hapo Juu =
 
Barabara mara nyingi uharibika kipindi cha masika, na wengi wetu tumeona jinsi gani masika ya Bongo mwaka huu ilivyokuwa... zaidi kuna wizi wa vyuma vya mifuniko ya misingi ya maji taka...
 
3565.jpg

Shimo kubwa ambalo lililopo katika barabara ya Morogoro karibu na NSSF jijini Dar es Salaam. (Picha na Hamisi Athumani)

My Take:

Kwa aliye kwenye Benz ameendelea sana; kwa anayetembea kwa miguu anaona maendeleo ya mwenye Benz na kuyatamani. Kwa mhandisi wa barabara, na yeye anatamani kuwa na Benz na viongozi wa Halmashauri wanajiuliza ni jinsi gani wataweza kuagiza Benz kwa watendaji wake.

Hivi barabara hiyo JK amewahi pita maeneo hayo toka awe rais??
Tatizo la viongozi wetu mpaka waone mkubwa anapita ndo wanaanza kukarabati lazima hapo mawaziri kibao wanapita hapo na wamenyamaza tuliiii..
 
Barabara mara nyingi uharibika kipindi cha masika, na wengi wetu tumeona jinsi gani masika ya Bongo mwaka huu ilivyokuwa... zaidi kuna wizi wa vyuma vya mifuniko ya misingi ya maji taka...

Mkuu! Ukiangalia kwa haraka haraka kune mengine kama matatu ambayo yako mbioni kugeuka mahandaki! Nayo yanasubiri masika ijayo................
 
Kipi bora? Kutengeneza barabara hiyo au kununua magari mazuri ya kutufanya tujisikie vizuri?

Magari wanayotumia viongozi wetu ni ya bei mbayaa kuna magari pale ya 100m alafu yapo kibao sasa haya mashimo kweli wanashindwa kuyadhibiti kweli??ukienda pale wilayani utasikia kila mwaka wametenga fedha za miundo mbinu nyingi tu sasa miundo mbinu yenyewe ndo kama hivi mnaona hata huko wilayani kuna MIFASI kibaooo tutawataja tu..
 
Mkuu! Ukiangalia kwa haraka haraka kune mengine kama matatu ambayo yako mbioni kugeuka mahandaki! Nayo yanasubiri masika ijayo................

Ukiacha wizi wa mifuniko, mahandaki aka mashimo kwenye barabara za mijini huchangiwa sana na mvua hii inatokea hata kwenye nchi zilizoendelea, Tumewahi kujadili kwa kina hapa JF juu ya matatizo ya misingi ya maji taka na nina hakika yale tuliojadili yanaweza kutoa suluhisho katika picha hii...

Aidha MKJJ amefanya unazi mkubwa kwa kuweka picha hiyo na kuzungumzia maendeleo, ilhali mvua haina msalie hata kama una maendeleo ya aina gani...

Pengine kilichokosekana hapo ni alama za tahadhali kwa wenye magari na watembeao kwa miguu.
 
Last edited:

Kibunango wa Tampere! Huko kwenu si kuna snow kibao? Umewahi kuwasikia wenyewe wakisingizia snow kwa ajili ya matatizo yao? Mvua inajulikana, na wanao'design' hizi barabara wanatakiwa watilie hilo maanani (kuna kitu kinaitwa storm water drainage). Hapa ni uzembe, period. Uzembe wa kutosafisha hizo drains. uzembe wa kutochukua hatua mara tatizo linapojitokeza. Hilo shimo si saizi ya mfuniko. Mfuniko umeibwa, wakaangalia. Mvua ya kwanza ikaja na ikapanua shimo, wanaangalia! Mvuo ya pili imekuja na kupanua shimo zaidi, wanaangalia! Mpaka siku ambapo gari la mkubwa litakapodumbukia ndipo watakimbia kwa hao walio kwenye hilo benzi kuomba ufadhili wa kutengeneza barabara UPYA maana imeharibika beyond repair! Wizi najua upo lakini kwa nini wasitafute solution ( vifuniko vya zege, kuweka lock kwenye vifuniko ambazo si rahisi kuvunja n.k) ya hilo badala ya kungoja mtu aje apoteze maisha kwenye haya makorongo? Hapa, Mkuu hamna cha kujitetea. Ni dalili ya matatizo tuliyonayo na jawabu ni kutafuta namna ya kutoka hapa tulipo.

Amandla!
 
Kibunango wa Tampere! Huko kwenu si kuna snow kibao? Umewahi kuwasikia wenyewe wakisingizia snow kwa ajili ya matatizo yao? Mvua inajulikana, na wanao'design' hizi barabara wanatakiwa watilie hilo maanani (kuna kitu kinaitwa storm water drainage). Hapa ni uzembe, period. Uzembe wa kutosafisha hizo drains. uzembe wa kutochukua hatua mara tatizo linapojitokeza. Hilo shimo si saizi ya mfuniko.....
Amandla!
Nimekupata vizuri sana, Sikua na lengo la kutetea uzembe ila nilikuwa najaribu kuangalia ni nini chanzo cha tatizo hilo, kwani mada yenyewe imekuja kwa namna ya kejeli na ikaendelea kuchangiwa katika mitiririko wa kejeli.

Hilo la mifuniko ya vyuma ni bora asasi husika zikawazinafuatilia wale wauzaji na wayeyushaji wa vyuma chakavu kwani ndipo upelekwa huko na hao wezi.
 
Mwanakjj,

Tunasubiri tupewe chochote toka ughaibuni, si unajua badget yetu haijitosherezi, subiri tukishapata mambo yatakuwa murua.
 
Unajua kila mtu ana tafsiri yake juu ya maendeleo, Mwanakijiji nimefurahishwa sana ulichoandika chini ya picha. Hii ni ndogo tena bora kwa walio dar ambao wanafaidi lami ukiondoa mashimo madogo kazi ipo kwa sisi wa mikoani hivi kuna mtu ameshajaribu kutembelea maeneo ya Mtwara kama unatoka Ndanda kwenda ruangwa!

Hatuhitaji mabenzi, tunataka barabara tuwahi huduma
 
Wakuu, heshima mbele... M.M.M, hayo ndiyo mambo ya Jijini wakuu.... Kuna thread tuliongelea kuhusu mafuriko Jijini Dar inaitwa "Dar Mambo Tambarare" or something. Haya mahandaki wakuu sababu sio kama wengi ambavyo tungetegemea kuwa ni wizi wa mifuniko, la hasha, mahandaki yanatokana na colapse of underground storm water drains ambazo la kushangaza zaidi zimejengwa less than 3 years ago by our good ol' friends, Chinese Contractors!!

So haya tunayoyaona ni mwanzo tu many more will come manake walichimba kwelikweli.... maswali ya kujiuliza ni:
1. Hizi so-called underground storm water systems mbona hazifanyi kazi? Angalia mafuriko mara mvua zinyeshapo hapa Jijini!

2. Design ya hizi vitu na construction yake ilikuwaje manake ni more of a premature failure if you ask me!!

3. Hawa wajenzi na designers wameachukuliwa hatua gani kwa hili?? Baadhi ya failures zilianza hata wakati kazi inaendelea maeneo ya Samora na Zanaki streets na nakumbuka Michuzi kule kwenye blogu yake aliongelea hili na mapicha mengi kuonyesha kuzibwa kwa mahandaki yale kwa kutumia matope! Je wahusika hawakuliona hili??

4. Sasa imeshaonekana kuna tatizo, je, wahusika ambao ni so called "City Fathers" wanachukua/wamechukua hatua gani?? Au wapo busy "kukamata Machinga, Mama Ntilie" na "so-called illegal bomoabomoa" jamani??

Kuhusu lile la mchanga kurudi barabarani kama alivyosema nadhani Steve D (kama nimekosea kunradhi Mkuu), swala ni kwamba kuna vitu tunafanya bila kuangalia umuhimu wake. Mfano ni kama ifuatavyo:

1. Areas where the road is below the existing ground (road as a drain): Hapa kwa kweli jamaa inabidi wajitahidi kupanda majani na kuweka walkways mfano ni ule wa UN Road. Najua kuna mapungufu pia lakini idea was good but implementation/design had its flaws!

2. Areas ambapo kuna median (dual carriageways): Hapa kwa kweli kuna swala la post construction-compaction/consolidation pamoja na swala la kulima/kupalilia median zenyewe. Hapa inabidi City Fathers waangalie uwezekano wa kufanya excavation to allow for some nominal head during rain season/watering ili kusiwe na excessive overflow ambayo itapelekea kupeleka mchanga/udongo kwenye njia. Pili ni mfano pale Selander Bridge ambapo kwenye ile barabara utaona zile median zina udongo mwingi kuliko kerb height!! Hapa ni post-construction compaction/consolidation ikichangiwa na mambo ya kulima eneo husika katika kupanda majani.

3. Eneo jingine ni kwenye barabara zilizo level with existing/surrounding grounds: Hapa kuna maswala mengi ya kuangaliwa kutokana na cost, safety, aesthetics etc. Njia za kudhibiti ni pamoja na kerb stones (both inverted and vertical), provissional of shoulers (paved/selected compacted materials), controlled exit points/juntions and crossing points (paved, pitched etc), na nyingine nyingi. Hapa ukiangalia mfano wa Bagamoo Roads (new and old) hatuna control ya hizi na hivyo barabara inaishia kupokea mchanga kutoka kwenye mitaro na njia za miguu pembezoni.

Hivyo wakuu, kama nilimuelewa vizuri JK, kupinga kuchagua kandarasi kutokana na bei pia ni lazima wahandisi waangalie swala la design based on importance/requirement and not solely based on cost!!!

Naomba kuwalkilisha!!!
 
tatizo si mvua bwana, kama kungekuwa na miundombinu dhabiti tusingeyapata haya, hebu piteni barabara ya Nyerere pindi mvua inaponyesha, ni aibu drainage system mbovu, inapeleka maji taratibu sana hivyo haiwezi kuhimili mvua hata kidogo tu, ni mto unageuka pale kama siyo ziwa kabisa, ngoja siku wapate aibu ya kuogelea na washaipata naona wameanza kuchimba chimba mitaro, manake ile barabara si ndiyo ya kuelekea majuu, just imagine siku hao wageni wao wa sullivan wakianza kuwasili waogelee kwenye maji ya kinyesi.
 
Kibunango wa Tampere! Huko kwenu si kuna snow kibao? Umewahi kuwasikia wenyewe wakisingizia snow kwa ajili ya matatizo yao? Mvua inajulikana, na wanao'design' hizi barabara wanatakiwa watilie hilo maanani (kuna kitu kinaitwa storm water drainage). Hapa ni uzembe, period. Uzembe wa kutosafisha hizo drains. uzembe wa kutochukua hatua mara tatizo linapojitokeza. Hilo shimo si saizi ya mfuniko. Mfuniko umeibwa, wakaangalia. Mvua ya kwanza ikaja na ikapanua shimo, wanaangalia! Mvuo ya pili imekuja na kupanua shimo zaidi, wanaangalia! Mpaka siku ambapo gari la mkubwa litakapodumbukia ndipo watakimbia kwa hao walio kwenye hilo benzi kuomba ufadhili wa kutengeneza barabara UPYA maana imeharibika beyond repair! Wizi najua upo lakini kwa nini wasitafute solution ( vifuniko vya zege, kuweka lock kwenye vifuniko ambazo si rahisi kuvunja n.k) ya hilo badala ya kungoja mtu aje apoteze maisha kwenye haya makorongo? Hapa, Mkuu hamna cha kujitetea. Ni dalili ya matatizo tuliyonayo na jawabu ni kutafuta namna ya kutoka hapa tulipo.

Amandla!

Nimekupata vizuri sana, Sikua na lengo la kutetea uzembe ila nilikuwa najaribu kuangalia ni nini chanzo cha tatizo hilo, kwani mada yenyewe imekuja kwa namna ya kejeli na ikaendelea kuchangiwa katika mitiririko wa kejeli.

Hilo la mifuniko ya vyuma ni bora asasi husika zikawazinafuatilia wale wauzaji na wayeyushaji wa vyuma chakavu kwani ndipo upelekwa huko na hao wezi.

tatizo si mvua bwana, kama kungekuwa na miundombinu dhabiti tusingeyapata haya, hebu piteni barabara ya Nyerere pindi mvua inaponyesha, ni aibu drainage system mbovu, inapeleka maji taratibu sana hivyo haiwezi kuhimili mvua hata kidogo tu, ni mto unageuka pale kama siyo ziwa kabisa, ngoja siku wapate aibu ya kuogelea na washaipata naona wameanza kuchimba chimba mitaro, manake ile barabara si ndiyo ya kuelekea majuu, just imagine siku hao wageni wao wa sullivan wakianza kuwasili waogelee kwenye maji ya kinyesi.

Wakuu, wote hapo juu mmesema mambo muhimu sana.... Lakini kikubwa na muhimu ni kama alivyosema Fundi, UZEMBE!!!

Wakuu mnajua barabara inavyokuwa designed kuna vifuatavyo ambavyo kila Mhandisi lazima aangalie:
1. Traffic number and mass: Current, construction, generated and future - estimated to a minimum of the whole design period

2. Drainage: Estimation based on a minimum of 25 years floods (in bridges inaenda mpaka 50 - 100 years depending on size/importantce etc). Hili ni muhimu halina discussion ya design period

3. Weather: Lazima uwe na joto, baridi etc ili kujua ile mix ya materials kuweza kuhimili mabadiliko ya hali ya hewa kwa design period

4. Population/development: Kuna tofauti ya urban and rural areas meaning kuna vitu kama developed areas, possible/future developments including maji safi, umeme, sewage disposals etc.

So wakuu unless mnaniambia kuwa mvua zetu ni kubwa sana kila mwaka and magari na maendeleo yana resiprocate so fast kwamba yamechukua 25 year design period in 2/3years sidhani kama nitaweza kubali kuwa kuna cha zaidi ya UZEMBE!!

Swali ni kwamba hao wahandisi waliofanya hizi errors (alghout I would call them mistakes but sina ushahidi so lets open that avenue), nadhani wanatakiwa wawajibishwe na vyombo mbadala kama ERB, ACET, NCC etc!!!

Naomba kuwakilisha!!!
 
Dar es Salaam panakatisha tamaa sana, watu wanajenga majumba ya kifahari, wananunua na magari ya kifahari, ila miundombinu ni zero kabisa! Hakuna drainage system, barabara siku hizi zinajengwa kwa kulipuliwa tu, haiishi hata miaka miwili tayari zinakuwa na mashimo, mfano ni barabara ya kwenda Tabata na Segerea. Pia kuna barabara moja inapita mtaa wa Ursino, kwenye nyumba binafsi ya Kikwete, imewekwa lami mara baada ya Mheshimiwa kuingia madarakani, lakini tayari ina shimo!!!! Hiyo ni mifano michache tu.

Katikati ya jiji ni balaa, hakuana parking za kutosha, wala barabara lakini ndio kwanza yanajengwa maghorofa marefu sana tu! Sijui itakuwaje huko mbeleeni. Karikoo ndio kabisa, maghorofa yamelaliana!
 
Ningefurahi zaidi kama ningeona plate number nijue kama ni TZ au Vipi?
Lakini shimo linaonyesha siyo bongo maana walau wakati wa mafuriko maji yangekuwa hayajaii.
Na kama ni ki "assume" ni bongo, naona tatizo sio tofauti ya gari na barabara ila tofauti ya fikra sahihi na utekelezaji wake.
 
Dar es Salaam panakatisha tamaa sana, watu wanajenga majumba ya kifahari, wananunua na magari ya kifahari, ila miundombinu ni zero kabisa! Hakuna drainage system, barabara siku hizi zinajengwa kwa kulipuliwa tu, haiishi hata miaka miwili tayari zinakuwa na mashimo, mfano ni barabara ya kwenda Tabata na Segerea. Pia kuna barabara moja inapita mtaa wa Ursino, kwenye nyumba binafsi ya Kikwete, imewekwa lami mara baada ya Mheshimiwa kuingia madarakani, lakini tayari ina shimo!!!! Hiyo ni mifano michache tu.
Katikati ya jiji ni balaa, hakuan......................!

Masaki, Pole sana Mkuu tunaona frustration zako kaka.... Yaani unajua kuna wakati wengine tulisema tukimbilie mikoani labda kuna afadhali lakini napo mambo ni yaleyale...... Tatizo kama alivyosema FM huko nyuma na in my second coment vile vile, UZEMBE!!! Kama wahusika wanakataa kuwa ni uzembe basi wakubali kuwa "Wameshindwa kutumia common sense in translating proper engineering principles" kutupa a quality of work that we deserve..... Kuna wanaodhani kuwa eti pesa inagomba, mimi nipo tayari kusema kwamba kwa bei iliyolipwa na WB kwenye barabara za mradi wa "Maendeleo ya Makazi" na pia kwenye USRP zingeweza kufanya kazi maradufu kulinganisha na hizi barabara longolongo ambazo tunazo!!! Kinachotumaliza pamoja na 10% pia ni UZEMBE au kutokujali kwa watendaji wetu!!! Jiji la Dar sasa hivi kwa kweli wale mliokuwa nje mjue kuwa halifai kabisaaaaaaa, mvua zimetuvua nguo hadharani manake kuendesha gari kero, daladala kero, kutembea kwa miguu kero........ Kisa cha yote haya ni UZEMBE (kama hawataki basi wakiri kuwa wameshindwa kazi)!!
 
Ningefurahi zaidi kama ningeona plate number nijue kama ni TZ au Vipi?
Lakini shimo linaonyesha siyo bongo maana walau wakati wa mafuriko maji yangekuwa hayajaii.
Na kama ni ki "assume" ni bongo, naona tatizo sio tofauti ya gari na barabara ila tofauti ya fikra sahihi na utekelezaji wake.

MpakaKie...., karibu Jijini kaka wakati kunanyesha utagundua mafuriko na sasa hivi pita mitaa ya Kisutu, Zanaki karibu na Masjid moja pale, pia nenda maeneo ya mjini katikati pale nyuma ya India Street utagundua ukweli ni upi.... Pia hebu tembelea www.issamichuzi.blogspot.com kwa kweli Michuzi anajitahidi sana kuweka what he calls "The Handakiz" kwa waTanzania wenzetu walio mbali ya Jiji waone hali halisi ndani ya Jiji!!

Hapo swala la fikra nipo pamoja nawe, wanaweza kusema wametumia technical/engineering principles but kuna uwezekano kwenye swala la utekelezaji (common sense, experience, logic) kukawa na mushkeli..... Lakini pia kuna vijimambo vya UZEMBE!!
 
Mkuu uliyesema kuwa hii ni photoshop nakushauli urudi kwenu tanzania kwani alichoweka MKJ ni kidogo sana kulinganisha na matatizo yaliyomo kwenye barabara za dar es salaam.

Wachina wakati wanajenga underground storm water drainage system walifumua barabara karibu zote na kupitisha mabomba chini yake, wakati walipomaliza hawakushindilia vizuri tena yale matabaka ya barabara waliyoyachimba, kwahiyo kama mvua inaweza kuongezeka kwa muda wa mwezi mmoja mashimo mengi sana yatafumuka na kusababisha barabara kutopitika.

barabara nyingine kama ya uhuru eneo la amana mpaka malapa ni hatari kupita especially kama una haraka kwani mashimo ni mengi kiasi cha kutumia saa nzima wakati ile sehemu nia dakika tano tu.

Hivi ninavyoandika hapa nimepita barabara ya nelson mandela eneo la Buguruni al hamza ni hatari kwani kuna mzinga wa shimo katiakati ya barabara wakati ile ni highway usipoangalia unaacha ream ya gari hapo na lipo kwa mwezi mzima sasa.

Pamoja na wezi wa mifuniko lakini uzembe ni mkubwa sana mtu anakarabati barabara kama ya nelson mandela kwa zege anamwagia shimo wakati yanapita magari makuwa sana na mvua zinanyesha baada ya siku mbili lile shimo linaibuka upya, wakazi wa tabata wanaweza kudhitisha hili kwani ndo wanavyo karabati makutano ya tabata na nelson madela.
 
Back
Top Bottom