Haya ndio maisha halisi ya Dar es Salaam

Haya ndio maisha halisi ya Dar es Salaam

Wahindi hawamiliki nyumba lkn wanamiliki hela ndefu. Lkn kuna wabongo hamiliki nyumba wala hana hiyo hela ndefu km mhindi, ndiyo maana mbongo anaona ni bora angalau amiliki kwake kuliko kukosa vyote. Wahindi wengi huenda kuishi Canada mambo yao yakikaa vizuri au ikatokea huku bongo kimenuka au kuna dalili ya kunuka wahindi si wa kujilinganisha nao bila kutumia akili.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwaka 2018 Canada walinikubalia kunipa uraia ingawa sikukamilisha taratibu za kwenda kuishi huko kwasababu nilikuepo kimasomo nchini Thailand kwahiyo niliwaomba wanipe mda nikimaliza naweza kwenda. Kwa wanaopafahamu Canada vizuri wanipe ramani kule maisha yapoje na kazi za kufanya zipoje . Je Wasomi ni ajira zao zinapatikana
 
Nilikuja huko miaka flani kumcheki dingi mkubwa duhh maana tangu kastafu hataki kurudi mkoa

huku vilage ana ekari 3 safi tu zimekaa mpaka tukaanza kutumia kwa kulima maharage, mahindi na mihogo tukivuna tunauza tunaweka chetu mfukoni ye kazi yake akipigika huko anatuambia megeni la eneo muuze afu hela nitumieni huku mpaka kwa sasa zimebaki hizo ekari 3 na mwendo utakuwa huo huo mpaka ekari zitaisha .... watoto wa dingi mkubwa bangi tu sio madem wala mamen wanazalia home tu... Nikamshauli mmoja Oya tusepe mkoa ukaendeleze mashamba ya dingi ako maana ukimcheki hana dalili za kurudi home jamaa akanichomolea balaa..

Nimekaa pale kama wiki 2 hivi msosi wa kulenga kwa manati yaani inafika saa 4 usiku yaani yoyote aliyefanikiwa siku hiyo anatoa chochote dagaa zinafuatwa gengeni yaan msosi wa usiku ni saa tano, au wanasubiri mgeni ndio uokoe jahazi, dingi na watoto wake ulabu wa hatari yaan wakipata hata buku jero wanaelekea kwa ulabu nikaongea weee lakini hakuna aliye nielewa.

Nilikuwa nimeenda kupokea ka mzigo kangu toka sbt japan sikuwa nimewaambia nimekuja fuata nini dar siku hiyo wakaona naingizana na mashine tu wakabaki midomo wazi nawaambia hii imetokana na kilimo na mifugo twendeni home huku sioni maisha mnasindikiza wengine tu hawaelewi wao wanafikiri vijijini kuna chawa, nyoka, na hutupigi pamba na hakuna umeme maji matibabu kama town village za siku hizi ziko poa balaa, baada ya siku mbili mashine iko poa nikatembea.

Mentality ya watu wa Dar ni kwamba hawaamini kama mtu anaweza kupata maendeleo akiwa nje ya Dar. Ndio maana utawasikia wakisema Dar ndio kila kitu, Dar ndio Tanzania, Dar mzunguko wa hela mkubwa, nk. Hii inawafanya watu wengi wa Dar kung'ang'ania hapo mjini hata kama wanaishi maisha magumu na kuendelea kujipa moyo kwamba one day yes.

Pia, kulingana na kwamba watu wengi wa Dar wanapenda sifa za kijinga, hii huwafanya kuwa waongo waongo sana hasa kwa ndugu na jamaa wa mikoani kwa kujidai kwamba huku Dar mambo yao ni supa. Hii inawafanya waogope kurudi mikoani kwa kuogopa aibu ya kuonekana maisha yamewashinda. Hivyo wanaendelea kukomaa japo moyoni wanaujua ukweli. Ndio maana siku zote mtu wa mkoani ukija Dar watu hawakubali kuonana na wewe au kukupeleka wanakoishi maana wanajua utagundua uongo wao.
 
Ukishindwa kuishi dar sijui utaishi wapi hapo ni kuwa uso wa mbuzi ukifanya chochote watu wananunua wapo wengi sehemu zingine kila unachotaka kuuza wamevuna wanacho ndani wakulima wenzio hapo hata maji ya kandoro kkoo unauza achilia mbali matunda na bidhaa zingine ni mipango ya muda mrefu itakufanya uondoke hapo ulipo...
 
Maisha ya swahili ni shida tupu hapo ndio tunazalisha vitoto malaya madawa ya kulevya uchangudoa ushoga
Mikoani kutamu saana kama mby city hali ya hewa maji umeme nyumba bora chakula ndio sio ya kuumiza kichwa maadili
 
Jamani me naona saazingine tunaipa cheo tu Dar... me naona ukiwa Dar unakula/unapata unachotaka tena kwa bei ya kawaida kabisa shida iko wapi!!!

sisemi kwa ubaya lakini kuna vijiji vingine gharama zake kuishi walahi labda kwa watu wengine lakini mtumishi utasema bora anayeishi Dar

Mimi ni mwalimu fulani kwenye shule fulani kijijini huku aisee mshahara wangu unaishia kwenye chakula yaani huku nilipo ni kijijini lakini kila kitu ni cha kununua tena bora basi iwe kununua tu (maana kwa siku hizi haikwepeki kweli kila kitu ni cha kununua) bali ni kununua kwa bei ya juu sana ...natoa mifano hapa halafu aliye dar alinganishe

Huku tulipo mafuta ya kupikia ni sh5000 kwa lita, ndizi mbivu vile vidogo kabisa visivyofaa kupikwa mbichi sh 100 moja na hakunaga ndizi aina nyingine, machungwa ya msimu ya kufanya kuletewa kutoka mbali sh 100 respectively, unga wa ugali mpaka kwa siku hii ya leo naandika ni sh 2000, mahindi kwa kipindi hiki cha kiangazi ni sh 800@kg lakini mvua zikichanganya ni 1500, mchele ndo naona bei ya 2000 iliyozoeleka sehemu nyingi, sukari hivi leo naandika ni 5000@kg hapa kijijini,

Hiyo ni mifano michache tu kwenye misosi bado mengi mengineyo ambayo yanagharimu sana mfano kodi za nyumba wahuni hawana hata nyumba za maana lakini kodi zao ni balaa... maji mtiti, ishu ndogo tu ukimuita mtu akufixie hela atakayotaka utashangaa mwenyewe,
 
Huo mzunguko wa pesa unaousema wewe unawanufaisha wengine, wewe na take home yako ya 400k kwa hapa Dar utaishi maisha ya kibinadamu?

Usafiri watoto, kodi, maji, umeme, wewe una mshahara fixed 400k hivi unadhani utafanya lolote la maana!

Mkuu acha kisema in general, watu wanaishi maisha ya chumba kimoja Dar, kuoa ni waoga, hata walioa chumba kimoja watoto wanalala hadi kwa majilani, mkuu kwani unaishi Dar ipi wewe?

Unasema Dar kuna sehemu ya 10k kwa mwezi?
Wapi huko

Hicho sio chumba ni store I'm sure
Vingunguti

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
kujenga ni dalili za uogam wahindi mbona wanaishi bila kujenga mambo yanaenda. unakiwa kuwa na usafiri basiii
 
Kuna mtu anadaiwa kodi ya miezi mitatu... hana hata mia... kodi ni 250k@ month sasa namwambia hebu hama huko hakuelewi hata kidogo.. kuishi Dar ni kama kaugonjwa fulani kanakuingia kichwani... amebaki kuomba omba tu..khaa had inaboa!poleni
Watu walio Mikoani huwa wanaposikia fulani anakaa Dar wanaona tayari maisha ameyapatia kumbe hamna kitu.
 
Dar es salaam Moto chini Daslama Moto juu...
kuna Dar es Salaam na Daslama inategemea unakaa wapi.....
 
Huo mzunguko wa pesa unaousema wewe unawanufaisha wengine, wewe na take home yako ya 400k kwa hapa Dar utaishi maisha ya kibinadamu?

Usafiri watoto, kodi, maji, umeme, wewe una mshahara fixed 400k hivi unadhani utafanya lolote la maana!

Mkuu acha kisema in general, watu wanaishi maisha ya chumba kimoja Dar, kuoa ni waoga, hata walioa chumba kimoja watoto wanalala hadi kwa majilani, mkuu kwani unaishi Dar ipi wewe?

Unasema Dar kuna sehemu ya 10k kwa mwezi?
Wapi huko

Hicho sio chumba ni store I'm sure
Habari wakuu

Dar ni moja kati ya mji mkubwa sana Tanzania umeojaa watu wengi sana na shughuli zao za kibiashara, ni mji ambao gharama za kuishi ni kubwa mno, kodi, maji, umeme, usafiri n.k

Hapa nazungumza na watu wa kipato cha kawaida sana, kwa mwezi 400k ndio mishahara yao, machinga, mama ntilie, bodaboda n. K, kusema kweli nimekuja kugundua Dar ni jiji ambalo usipokuwa makini unazeekea nyumba ya kupanga, hadi watoto wako wataanzia maisha ya kupanga hapo hapo unapoishi.

Watu wengi hapa Dar wanajituma, usiku na mchana, pambana sana tatizo pesa inaishia kodi, umeme, chakula, usafiri, kama una watoto ndio balaaa, kwani unapambana mchana usiku shuleni watoto, nauli, ya kula, mpaka mwezi unaisha upo hoi huna kitu, unaishi chumba kimoja cha kupanga pesa yote inaishia kwa mwenye nyumba .

Wazawa wenyewe kujenga ni mtiti, wanakomaa na nyumba ya urithi mpaka kieleweke, hili jiji sio la kuishi kabisa, kama usiposituka haki unazeeka upo chumba kimoja, huna hili wala lile, huku ukiwa umeacha historia ya kupiga kazi usiku na mchana pesa yote ikiishia njiani.

Noma sana, chumba kimoja baba, mama na watoto, ndio maana mabaharia wengi wa Dar kuoa ni kitendawili, hili jiji ni la kushitukia mapema, kusanya mpunga nenda zako pembeni mkoani jenga tulia utaenjoy maisha. Kusubiri kujenga hapa bongo ni ndoto za mchana hasa kwa basic ya 400k na kazi za kuunga unga, zaidi utamiliki ghetto chumba kimoja, tv fridge, kitanda godoro, kuoa utakwepa sana kwani inabidi uongeze chumba uishi vyumba viwili ukiwa na watoto ndio itakubidi uongeze zaidi gharama zake sasa ni kwa mwaka ni zaidi ya kuejenga nyumba mkoani.

Huku watu hawalali wanapiga kazi usiku mchana, ila sasa ndio hivo tena mpaka mtu anazeeka hana kitu,

This is Dar es salaam
yaan ww unaongea afu unajibishia mwenyewe[emoji5]
 
Back
Top Bottom