Jamani me naona saazingine tunaipa cheo tu Dar... me naona ukiwa Dar unakula/unapata unachotaka tena kwa bei ya kawaida kabisa shida iko wapi!!!
sisemi kwa ubaya lakini kuna vijiji vingine gharama zake kuishi walahi labda kwa watu wengine lakini mtumishi utasema bora anayeishi Dar
Mimi ni mwalimu fulani kwenye shule fulani kijijini huku aisee mshahara wangu unaishia kwenye chakula yaani huku nilipo ni kijijini lakini kila kitu ni cha kununua tena bora basi iwe kununua tu (maana kwa siku hizi haikwepeki kweli kila kitu ni cha kununua) bali ni kununua kwa bei ya juu sana ...natoa mifano hapa halafu aliye dar alinganishe
Huku tulipo mafuta ya kupikia ni sh5000 kwa lita, ndizi mbivu vile vidogo kabisa visivyofaa kupikwa mbichi sh 100 moja na hakunaga ndizi aina nyingine, machungwa ya msimu ya kufanya kuletewa kutoka mbali sh 100 respectively, unga wa ugali mpaka kwa siku hii ya leo naandika ni sh 2000, mahindi kwa kipindi hiki cha kiangazi ni sh 800@kg lakini mvua zikichanganya ni 1500, mchele ndo naona bei ya 2000 iliyozoeleka sehemu nyingi, sukari hivi leo naandika ni 5000@kg hapa kijijini,
Hiyo ni mifano michache tu kwenye misosi bado mengi mengineyo ambayo yanagharimu sana mfano kodi za nyumba wahuni hawana hata nyumba za maana lakini kodi zao ni balaa... maji mtiti, ishu ndogo tu ukimuita mtu akufixie hela atakayotaka utashangaa mwenyewe,