Haya ndio maisha halisi ya Dar es Salaam

Haya ndio maisha halisi ya Dar es Salaam

humu ndani wamo sana

Muda wote wana mahasira, jua kali wanaamua kuja kuzimalizia kwenye kivuli huku jf
Huko mikoani nyie hamna hasira, hakuna stress, hakuna maisha magumu? Umeongea too general hadi hoja yako imekosa pa kushika.

Ndio Dar life lipo tight, lakini popote pale life's tight usipojibidisha.
 
Kuna watu wanapenda kuwa kwenye comfort zone.Eti kimbia Dar ukarelax mkoani kivipi labda ukainvest mkoani.Hujaona wanaijeria wanatoka kwao anaenda Newyork anaanza from scratch lakini anatoboa.

Dar kuna fursa kibao.Usafiri 24hr,population, umeme, kuna evening classes na siku hizi maji ya uhakika,foleni zimepungua.

Unataka ujana wako uwe unalala saa tatu ukiwa huko mkoani sawa.Lakini watu wanapambana huku jijini hawana uoga.Ndio maana watanzania diaspora wachache kwa sababu waoga kupambana nje.
 
Lakini wengi wao maisha yao magumu sana ,wanatupiga vizinga sana sisi tulioko mikoani
 
Kuna watu wanapenda kuwa kwenye comfort zone.Eti kimbia Dar ukarelax mkoani kivipi labda ukainvest mkoani.Hujaona wanaijeria wanatoka kwao anaenda Newyork anaanza from scratch lakini anatoboa.

Dar kuna fursa kibao.Usafiri 24hr,population, umeme, kuna evening classes na siku hizi maji ya uhakika,foleni zimepungua.

Unataka ujana wako uwe unalala saa tatu ukiwa huko mkoani sawa.Lakini watu wanapambana huku jijini hawana uoga.Ndio maana watanzania diaspora wachache kwa sababu waoga kupambana nje.
Sawa mnapambana sana, tatizo mtokeo hayaonekani, watu hadi wanazeeka bado wapo chumba kimoja, wakati kila siku yupo kazini, analala saa tisa usiku anaamuka saa kumi na mbili yupo barabaran
 
Kuna mtu anadaiwa kodi ya miezi mitatu... hana hata mia... kodi ni 250k@ month sasa namwambia hebu hama huko hakuelewi hata kidogo.. kuishi Dar ni kama kaugonjwa fulani kanakuingia kichwani... amebaki kuomba omba tu..khaa had inaboa!poleni
Maisha kokote , watu wako Somalia wanasaka life sembuse Dar.

Hata mikoani watu wanadaiwa Kodi na maisha sio rahisi kwa wote Kama ilivyo kwa dar maisha sio magumu kwa wote. Kuna watu hapa dar kwa siku wanatengeneza hata milion 100 ...

Kila mtu abaki na anachotaka kufanya.
 
Yaan hiyo ni maisha yangu in a nutshell, pitapita yote hii jf nasocial media, kusoma viji ktabu siku nafasi ikipatikana yote nikujarbu kutafuta formula yaku survive hapa mjin. Miaka inaenda tu hakuna kinachoongezeka
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]huu ni mji wa waliovurugwa

Dar kila mtu kachanganyikiwa muda wote tupo na leso anafuta jasho, muda wote wanahasira, jaribu tu kumuongelesha uone.

Watu wa dar sio binadamu wa kawaida kabisa
Mazombi
 
Nilikuja huko miaka flani kumcheki dingi mkubwa duhh maana tangu kastafu hataki kurudi mkoa

huku vilage ana ekari 3 safi tu zimekaa mpaka tukaanza kutumia kwa kulima maharage, mahindi na mihogo tukivuna tunauza tunaweka chetu mfukoni ye kazi yake akipigika huko anatuambia megeni la eneo muuze afu hela nitumieni huku mpaka kwa sasa zimebaki hizo ekari 3 na mwendo utakuwa huo huo mpaka ekari zitaisha .... watoto wa dingi mkubwa bangi tu sio madem wala mamen wanazalia home tu... Nikamshauli mmoja Oya tusepe mkoa ukaendeleze mashamba ya dingi ako maana ukimcheki hana dalili za kurudi home jamaa akanichomolea balaa..

Nimekaa pale kama wiki 2 hivi msosi wa kulenga kwa manati yaani inafika saa 4 usiku yaani yoyote aliyefanikiwa siku hiyo anatoa chochote dagaa zinafuatwa gengeni yaan msosi wa usiku ni saa tano, au wanasubiri mgeni ndio uokoe jahazi, dingi na watoto wake ulabu wa hatari yaan wakipata hata buku jero wanaelekea kwa ulabu nikaongea weee lakini hakuna aliye nielewa.

Nilikuwa nimeenda kupokea ka mzigo kangu toka sbt japan sikuwa nimewaambia nimekuja fuata nini dar siku hiyo wakaona naingizana na mashine tu wakabaki midomo wazi nawaambia hii imetokana na kilimo na mifugo twendeni home huku sioni maisha mnasindikiza wengine tu hawaelewi wao wanafikiri vijijini kuna chawa, nyoka, na hutupigi pamba na hakuna umeme maji matibabu kama town village za siku hizi ziko poa balaa, baada ya siku mbili mashine iko poa nikatembea.
 
Kila sehemu kuna maisha rahisi na magumu inategemea utafutaji wako na circle ya watu uliokuwa nao.Mf.Arusha kule sinon daraja mbili kuna watu wana maisha magumu balaa.

Ukiishi wilayani ni full kuwa bored.Yaani mnajuana wewe daktari,mwalimu,askari mnaonana bank bar. Akili inalala.
 
Habari wakuu

Dar ni moja kati ya mji mkubwa sana Tanzania umeojaa watu wengi sana na shughuli zao za kibiashara, ni mji ambao gharama za kuishi ni kubwa mno, kodi, maji, umeme, usafiri n.k

Hapa nazungumza na watu wa kipato cha kawaida sana, kwa mwezi 400k ndio mishahara yao, machinga, mama ntilie, bodaboda n. K, kusema kweli nimekuja kugundua Dar ni jiji ambalo usipokuwa makini unazeekea nyumba ya kupanga, hadi watoto wako wataanzia maisha ya kupanga hapo hapo unapoishi.

Watu wengi hapa Dar wanajituma, usiku na mchana, pambana sana tatizo pesa inaishia kodi, umeme, chakula, usafiri, kama una watoto ndio balaaa, kwani unapambana mchana usiku shuleni watoto, nauli, ya kula, mpaka mwezi unaisha upo hoi huna kitu, unaishi chumba kimoja cha kupanga pesa yote inaishia kwa mwenye nyumba .

Wazawa wenyewe kujenga ni mtiti, wanakomaa na nyumba ya urithi mpaka kieleweke, hili jiji sio la kuishi kabisa, kama usiposituka haki unazeeka upo chumba kimoja, huna hili wala lile, huku ukiwa umeacha historia ya kupiga kazi usiku na mchana pesa yote ikiishia njiani.

Noma sana, chumba kimoja baba, mama na watoto, ndio maana mabaharia wengi wa Dar kuoa ni kitendawili, hili jiji ni la kushitukia mapema, kusanya mpunga nenda zako pembeni mkoani jenga tulia utaenjoy maisha. Kusubiri kujenga hapa bongo ni ndoto za mchana hasa kwa basic ya 400k na kazi za kuunga unga, zaidi utamiliki ghetto chumba kimoja, tv fridge, kitanda godoro, kuoa utakwepa sana kwani inabidi uongeze chumba uishi vyumba viwili ukiwa na watoto ndio itakubidi uongeze zaidi gharama zake sasa ni kwa mwaka ni zaidi ya kuejenga nyumba mkoani.

Huku watu hawalali wanapiga kazi usiku mchana, ila sasa ndio hivo tena mpaka mtu anazeeka hana kitu,

This is Dar es salaam

Mbona akili yako imeishia kwenye laki 4?
Wewe kama huna akili ya kupata milion hilo ni tatizo lako, usijumuishe mambo kizembe zembe
 
Back
Top Bottom