Haya ndio maisha halisi ya Dar es Salaam

Pain killer

JF-Expert Member
Aug 15, 2017
14,169
21,305
Habari wakuu

Dar ni moja kati ya mji mkubwa sana Tanzania umeojaa watu wengi sana na shughuli zao za kibiashara, ni mji ambao gharama za kuishi ni kubwa mno, kodi, maji, umeme, usafiri n.k

Hapa nazungumza na watu wa kipato cha kawaida sana, kwa mwezi 400k ndio mishahara yao, machinga, mama ntilie, bodaboda n. K, kusema kweli nimekuja kugundua Dar ni jiji ambalo usipokuwa makini unazeekea nyumba ya kupanga, hadi watoto wako wataanzia maisha ya kupanga hapo hapo unapoishi.

Watu wengi hapa Dar wanajituma, usiku na mchana, pambana sana tatizo pesa inaishia kodi, umeme, chakula, usafiri, kama una watoto ndio balaaa, kwani unapambana mchana usiku shuleni watoto, nauli, ya kula, mpaka mwezi unaisha upo hoi huna kitu, unaishi chumba kimoja cha kupanga pesa yote inaishia kwa mwenye nyumba .

Wazawa wenyewe kujenga ni mtiti, wanakomaa na nyumba ya urithi mpaka kieleweke, hili jiji sio la kuishi kabisa, kama usiposituka haki unazeeka upo chumba kimoja, huna hili wala lile, huku ukiwa umeacha historia ya kupiga kazi usiku na mchana pesa yote ikiishia njiani.

Noma sana, chumba kimoja baba, mama na watoto, ndio maana mabaharia wengi wa Dar kuoa ni kitendawili, hili jiji ni la kushitukia mapema, kusanya mpunga nenda zako pembeni mkoani jenga tulia utaenjoy maisha. Kusubiri kujenga hapa bongo ni ndoto za mchana hasa kwa basic ya 400k na kazi za kuunga unga, zaidi utamiliki ghetto chumba kimoja, tv fridge, kitanda godoro, kuoa utakwepa sana kwani inabidi uongeze chumba uishi vyumba viwili ukiwa na watoto ndio itakubidi uongeze zaidi gharama zake sasa ni kwa mwaka ni zaidi ya kuejenga nyumba mkoani.

Huku watu hawalali wanapiga kazi usiku mchana, ila sasa ndio hivo tena mpaka mtu anazeeka hana kitu,

This is Dar es salaam
 
Aliyekwambia katika maisha ni lazima umiliki nyumba ni nani ?

Wale wahindi waliowaajiri wabongo wenzako wanaishi kwenye nyumba za kupanga lakin wana pesa ndefu
Mkuu acha kuiga

kwa hapa Tanzania kuzeeka huna hata nyumba ni aibu kubwa sana, watoto utawambia nini, dharau huwa zinaanzia hapa kwa watoto.

watoto unawaacha wanaanzisha maisha ya kupanga? Wewe pia ulikuwa umepanga, sasa maana yake nini hapo?
 
Hiyo yote inategemea na watu wanaokuzunguka. Hao wanaojenga kila siku ni watu wa wapi?
 
Kwa mtazamo wangu mimi naona maisha ya Dar ni marahisi ukilinganisha na mikoa kama Arusha, nasema Arusha sababu nimekaa

Nasema maisha ya Dar ni marahisi kwa sababu zifuatazo

1. Mzunguko wa pesa ni mkubwa na hii inatokana na idadi ya watu kuwa kubwa hivyo inapelekea kila biashara utakayo fanya inapata mteja (tukumbuke Dar hakuna mashamba)

Bei za nyumba za kupanga. kwanza bei zinategemeana na location, sasa Dar bei za nyumba wiko chini sana ukilinganisha na bei za Arusha

Dar unaweza kupata nyumba hata ya 10000 kwa mwezi. njoo Arusha uone hata zile nyumba za tope za matejoo hauwezi pata kwa hiyo bei

3. Bei za viwanja. Dar kigogo xiko chini. hata hii inatokana na location ya kiwanja, mfano ukiangalia sehemu kama Chanika tuifananishe na kwa morombo hapo utaona viwanja vya kwa morombo au inter viku juu

4. Bei za huduma za kijamii, kwa Dar huduma nyingi za kijamii ziko chini na hii ni kupatikana na kuwa na watoa utuma wengi hii inapelekea kuingia kwenye ushindani ambao mwisho wa siku watoa huduma wanashusha bei ili kuwapata wateja ila kwa Arusha ni kinyume

5. Shuguli za ujenzi, kwa Dar ni rahisi sana kujenga kuliko Arusha na hii inatokana na kuwa materials ni rahisi kwa Dar, na hii inatokana na uwepo wa bandari na viwanda vingi mfano bei ya tiles ya dar ni tofauti na ya Arusha

NB nimetumia mfano wa Arusha sababu naijua, mimi mtazamo wangu naona maisha ya Dar ni marahisi kuliko ya Dar
 
Thread imeisha hiyo
 
Dathramu ‘wengi’ wanaishi kwa kuteseka sana, wengi wanateseka sana.... lakini cha ajabu wanaamini ipo siku tu.
Kuna mtu anadaiwa kodi ya miezi mitatu... hana hata mia... kodi ni 250k@ month sasa namwambia hebu hama huko hakuelewi hata kidogo.. kuishi Dar ni kama kaugonjwa fulani kanakuingia kichwani... amebaki kuomba omba tu..khaa had inaboa!poleni
 
Back
Top Bottom