Kwa mtazamo wangu mimi naona maisha ya Dar ni marahisi ukilinganisha na mikoa kama Arusha, nasema Arusha sababu nimekaa
Nasema maisha ya Dar ni marahisi kwa sababu zifuatazo
1. Mzunguko wa pesa ni mkubwa na hii inatokana na idadi ya watu kuwa kubwa hivyo inapelekea kila biashara utakayo fanya inapata mteja (tukumbuke Dar hakuna mashamba)
Bei za nyumba za kupanga. kwanza bei zinategemeana na location, sasa Dar bei za nyumba wiko chini sana ukilinganisha na bei za Arusha
Dar unaweza kupata nyumba hata ya 10000 kwa mwezi. njoo Arusha uone hata zile nyumba za tope za matejoo hauwezi pata kwa hiyo bei
3. Bei za viwanja. Dar kigogo xiko chini. hata hii inatokana na location ya kiwanja, mfano ukiangalia sehemu kama Chanika tuifananishe na kwa morombo hapo utaona viwanja vya kwa morombo au inter viku juu
4. Bei za huduma za kijamii, kwa Dar huduma nyingi za kijamii ziko chini na hii ni kupatikana na kuwa na watoa utuma wengi hii inapelekea kuingia kwenye ushindani ambao mwisho wa siku watoa huduma wanashusha bei ili kuwapata wateja ila kwa Arusha ni kinyume
5. Shuguli za ujenzi, kwa Dar ni rahisi sana kujenga kuliko Arusha na hii inatokana na kuwa materials ni rahisi kwa Dar, na hii inatokana na uwepo wa bandari na viwanda vingi mfano bei ya tiles ya dar ni tofauti na ya Arusha
NB nimetumia mfano wa Arusha sababu naijua, mimi mtazamo wangu naona maisha ya Dar ni marahisi kuliko ya Dar