Ncha Kali
JF-Expert Member
- Sep 19, 2019
- 15,404
- 29,370
Point Dar unatakiwa usiwe mpenda starehe
Kama hupendi starehe sasa Dar unafaidi nini.?
Point Dar unatakiwa usiwe mpenda starehe
kwanza siku zote ukitakiwa kufanikiwa ishi maisha yako kulingana na uwezo wako. sasa kama wewe unalipwa 400k ni vizuri kutafuta maisha ambayo yanaendana na kipato chakoHuo mzunguko wa pesa unaousema wewe unawanufaisha wengine, wewe na take home yako ya 400k kwa hapa dar utaishi maisha ya kibinadamu?
usafiri watoto, kodi, maji, umeme, wewe una mshahara fixed 400k hivi unadhani utafanya lolote la maana!
Mkuu acha kisema in general, watu wanaishi maisha ya chumba kimoja dar, kuoa ni waoga, hata walioa chumba kimoja watoto wanalala hadi kwa majilani, mkuu kwani unaishi dar ipi wewe?
Unasema dar kunasehemu ya 10k kwa mwez?
Wapi huko
Hicho sio chumba ni store am sure
Kopo 1 unapikia siku ngapi manake km kwa siku moja basi huyo mhusika anaweza kumiliki mtungi wa gesi hadi wa kilo 15 na akaumudu akachana na mkaa
Sent using Jamii Forums mobile
Siku nojaapp
Dar kweli mzunguko uko juu..lakini maisha yko juu jombaa! Mkaa kakopo kamoja 1500!
Dar kuna wanaoishi na wasindikizaji!
Lakini kwa ugali wa Dar anaweza kutumia wiki huo mkaa, wewe huko mkoani ni siku moja tu. [emoji23][emoji23][emoji23]
Mkuu watu wanahaso sanaKila nikitaka kuhama dathramu nasogeza mwaka mmoja mbele, kwa sasa natumia sababu ya ‘watoto wangu’ wamalize la saba kwanza.... kiwanja mkoani kwetu ukiwa na milioni tu kiwanja hilooo.
Na pia heshima ya kuishi, kwa kipato changu ni ‘mtu’ maalumu nikiishi mkoani bila stress... mjini napata pesa nyingi ila nobody’s givin’ a fvck about me nasota kama fala tu.
Ni mchache mkuu..hata kuivishia maharage sidhani ..
mkuu sasa kama maisha ni magumu kwa nini tunaishi dar inatakiwa tuondoke zetu tuiache dar kwende kwenye mikoa yenye unafuu wa maisha ,Mkuu watu wanahaso sana
Wanalala saa kumi usiku, saa kumi na mbili wapo barabarani lakin hakuna kitu cha maana wanachoambulia zaidi ya pesa ya nauli kwa watoto, umeme,maji ,kodi, chakula. Kila akiwaza nyumba anaona mlima mkubwa sana hawezi kabisa!
Hili jiji usipojitoa akili utabaki kuzeekea mjini tu huna hili wala lile
Baba anapanga, watoto wanapanga hapo hapo, mwenye Nyumba anakula tu jasho lako
Cha ajabu hadi wazawa, jiji linawagalagaza wamejichimbiaa kwenye nyumba za urithi
Ukisikia mtu anaishi dar, usifikili labda yupo maisha mazuri kivile, nenda ujione mwenyewe
Hhhahaaa...nimejaribu kuattach kideo uone wa mkoani tunavyoishi imekataa..mie maisha y kupanga room moja aisee...!Maharage wanapikia kwenye Chupa za Chai (thermos), maji ya moto kisha hufungia humo maharage usiku kucha.... msiwaone wajinga sana.
Maisha ni kupanga na kupambana,kwn hata ukiwa mkoani na hauna kujenga ni shidahabar wakuu
Dar ni moja kati ya mji mkubwa sana Tanzania umeojaa watu wengi sana na shughuli zao za kibiashara,ni mji ambao gharama za kuishi ni kubwa mno, kodi, maji, umeme, usafiri n.k
Hapa nazungumza na watu wa kipato cha kawaida sana, kwa mwezi 400k ndio mishahara yao, machinga, mamantilie, bodaboda n. K, kusema kweli nimekuja kugundua dar jiji ambalo usipokuwa makini unazeekea nyumba ya kupanga, hadi watoto wako wataanzia maisha ya kupanga hapo hapo unapoishi.
Watu wengi hapa dsm wanajituma, usiku na mchana, pambana sana tatizo pesa inaishia kodi, umeme, chakula, usafiri, kama unawatoto ndio balaaa, kwani unapambana mchana usiku shulen watoto, nauli, ya kula, mpaka mwezi unaisha upo hoi huna kitu, unaishi chumba kimoja cha kupanga pesa yote inaishia kwa mwenye nyumba .
Wazawa wenyewe kujenga ni mtiti, wanakomaa na nyumba ya urithi mpaka kieleweke, hili jiji sio la kuishi kabisa, kama usiposituka haki unazeeka upo chumba kimoja, huna hili wala lile, huku ukiwa umeacha historia ya kupiga kazi usiku na mchana pesa yote ikiishia njiani.
Noma sana, chumba kimoja baba,mama,na watoto, ndio maana mabaharia wengi wa Dar kuoa ni kitendawili, hili jiji ni la kushitukia mapema, kusanya mpunga nenda zako pembeni mkoani jenga tulia utaenjoy maisha. Kusubiri kujenga hapa bongo ni ndoto za mchana hasa kwa basic ya 400k na kazi za kuunga unga, zaid utamiliki geto chumba kimoja, tv fridge, kitanda godoro, kuoa utakwepa sana kwani inabidi uongeze chumba uishi vyumba viwili ukiwa na watoto ndio itakubid uongeze zaidi gharama zake sasa ni kwa mwaka ni zaidi ya kuejenga nyumba mkoani.
Huku watu hawalali wanapiga kazi usiku mchana, ila sasa ndio hivo tena mpaka mtu anazeeka hana kitu,
This is dar es salaam
Faida wanayoipata ni tofauti na na kipato cha 400k per month,hii ulipe kodi,nauli,uache matumizi home!!Za kuambiwa changanya na zako.Aliyekwambia katika maisha ni lazima umiliki nyumba ni nani ?
Wale wahindi waliowaajiri wabongo wenzako wanaishi kwenye nyumba za kupanga lakin wana pesa ndefu
Usipopenda starehe uzuri wa Dar itakua Nini Sasa?Point dar unatakiwa usiwe mpenda starehe
Hao wahindi ni watanzania?Aliyekwambia katika maisha ni lazima umiliki nyumba ni nani ?
Wale wahindi waliowaajiri wabongo wenzako wanaishi kwenye nyumba za kupanga lakin wana pesa ndefu
habar wakuu
Dar ni moja kati ya mji mkubwa sana Tanzania umeojaa watu wengi sana na shughuli zao za kibiashara,ni mji ambao gharama za kuishi ni kubwa mno, kodi, maji, umeme, usafiri n.k
Hapa nazungumza na watu wa kipato cha kawaida sana, kwa mwezi 400k ndio mishahara yao, machinga, mamantilie, bodaboda n. K, kusema kweli nimekuja kugundua dar jiji ambalo usipokuwa makini unazeekea nyumba ya kupanga, hadi watoto wako wataanzia maisha ya kupanga hapo hapo unapoishi.
Watu wengi hapa dsm wanajituma, usiku na mchana, pambana sana tatizo pesa inaishia kodi, umeme, chakula, usafiri, kama unawatoto ndio balaaa, kwani unapambana mchana usiku shulen watoto, nauli, ya kula, mpaka mwezi unaisha upo hoi huna kitu, unaishi chumba kimoja cha kupanga pesa yote inaishia kwa mwenye nyumba .
Wazawa wenyewe kujenga ni mtiti, wanakomaa na nyumba ya urithi mpaka kieleweke, hili jiji sio la kuishi kabisa, kama usiposituka haki unazeeka upo chumba kimoja, huna hili wala lile, huku ukiwa umeacha historia ya kupiga kazi usiku na mchana pesa yote ikiishia njiani.
Noma sana, chumba kimoja baba,mama,na watoto, ndio maana mabaharia wengi wa Dar kuoa ni kitendawili, hili jiji ni la kushitukia mapema, kusanya mpunga nenda zako pembeni mkoani jenga tulia utaenjoy maisha. Kusubiri kujenga hapa bongo ni ndoto za mchana hasa kwa basic ya 400k na kazi za kuunga unga, zaid utamiliki geto chumba kimoja, tv fridge, kitanda godoro, kuoa utakwepa sana kwani inabidi uongeze chumba uishi vyumba viwili ukiwa na watoto ndio itakubid uongeze zaidi gharama zake sasa ni kwa mwaka ni zaidi ya kuejenga nyumba mkoani.
Huku watu hawalali wanapiga kazi usiku mchana, ila sasa ndio hivo tena mpaka mtu anazeeka hana kitu,
This is dar es salaam
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]huu ni mji wa waliovurugwaDar es salaam sio mji wa binaadamu wavivu na wasio na maarifa wala uvumilivu. Ni mji wa wachakarikaji tu ukija na uvivu wako utakumbuka ugali wa bure na maji ya bure ya huko mkoa ulipotoka hapa ni kazikazi mabishoo wa wasio na hela Dar ndio kiboko yao,, Dar kitambo hauwezi kuona mzoga wa kuku au mbuzi kama mikoani mzoga ni chakula safi hatutaki kujua kachinja nani tunakula tu.