Haya mataulo bafuni ni ya nini?

Haya mataulo bafuni ni ya nini?

Shule iliyopo hapa ni ya nguvu na kwa kweli nimefurahi sana kuona wanaJF wakijitahidi kushare uelewa wa mambo mbali mbali na muhimu kwenye maisha ya kila siku. Hili la suala la kutumia vitu unavyokuta katika chumba cha hoteli na vifaa vya meza ya chakula pia jinsi ya kufanya mambo uwapo mezani (table manners) ni nyeti sana. Binafsi nimekuwa nikijifunza kila mahali ninapoenda ila wakati mwingine nakumbana na aibu pale ambapo Mtanzania mwenzangu anapofanya vitu vya aibu ambayo hakutegemewa kufanya kutegemeana na hadhi aliyopewa hadi kufika mahali hapo. Mfano, kujaza chakula kingi sana kwenye sahani, kutumia kijiko cha supu kula msosi, kuchanganya side plates n.k. Nashauri hii thread ibadilishwe au ianzishwe nyingine kwa ajili ya kutoa hii elimu na kama kuna wataalamu watusaidie. Naomba tujadili mambo kwa topic, mfano, vyumba vya hotel na matumizi yake, meza ya chakula, uvaaji katika sherehe tofauti (official, traditional Vs casual dresses) n.k. Ni mambo mengi ambayo tunahitaji kusaidiana. Jamani tunapata aibu na wakati mwingine kuwatia aibu wenzetu tunapokaribishwa misosi au kusafiri.
 
Tusimlaumu Pasco jamani ....
Madabwada, si nilisema hivi "Tena familia ya hotel za Sheraton na Marriot wao ndio wamezidi unakuta taulo 6 kila moja ni pair on top of that wanakuwekea bath robe ya taulo na tag 'you can take this with you'. Mbongo si unajua tena, nikabeba. Siku ya kuondoka nikakuta bill US$ 100. For the bath robe!"

Bado kuna tatizo?. Hata ukilala Hilton tuu hapo Nairobi, unakuta tag kwenye bathrobe, wao unalipia Shilingi za Kenya 150 enzi nilipolala mimi.

Kwa hoteli kubwa unakuta ki jokofu kidogo ndani kimeshehenezwa kila bia na vinywaji baridi, huku kabatini unakuta mini bar, hakuna popote palipoandikwa unaweza kujisevia, vyote ni mali yako, utumie usitumie ni juu yako. Nilikunywa niliweza, mgeni wangu akajitwalia alivyoweza kubeba. Siku ya kucheck out, vyote nililipishwa kwenye bili ikiwemo bili ya ajabu, ya kulipia kuangalia TV!.

Kumbe mgeni wangu hana hili wala lile, kabonyeza chaneli ya pay per view kuangalia zile movie, wanakuuliza mara mbili mbili kwa Kiingereza kwa kuonyesha kiwango cha kulipia, ukikubali, unabonyeza 'yes', ukifikiri unaulizwa kama unapenda kuangalia. Ukishabonyeza yes, unaikuta bili uwe uliangalia, au la!.
 
Mhh kutoka hapa kwetu kwa mfuga mbwa mpaka habari za Chikago parking nasikia raha utafikiri nimesafiri tayari kusoma kuzuri
 
Madabwada, si nilisema hivi "Tena familia ya hotel za Sheraton na Marriot wao ndio wamezidi unakuta taulo 6 kila moja ni pair on top of that wanakuwekea bath robe ya taulo na tag 'you can take this with you'. Mbongo si unajua tena, nikabeba. Siku ya kuondoka nikakuta bill US$ 100. For the bath robe!"Bado kuna tatizo?. Hata ukilala Hilton tuu hapo Nairobi, unakuta tag kwenye bathrobe, wao unalipia Shilingi za Kenya 150 enzi nilipolala mimi.Kwa hoteli kubwa unakuta ki jokofu kidogo ndani kimeshehenezwa kila bia na vinywaji baridi, huku kabatini unakuta mini bar, hakuna popote palipoandikwa unaweza kujisevia, vyote ni mali yako, utumie usitumie ni juu yako. Nilikunywa niliweza, mgeni wangu akajitwalia alivyoweza kubeba. Siku ya kucheck out, vyote nililipishwa kwenye bili ikiwemo bili ya ajabu, ya kulipia kuangalia TV!.Kumbe mgeni wangu hana hili wala lile, kabonyeza chaneli ya pay per view kuangalia zile movie, wanakuuliza mara mbili mbili kwa Kiingereza kwa kuonyesha kiwango cha kulipia, ukikubali, unabonyeza 'yes', ukifikiri unaulizwa kama unapenda kuangalia. Ukishabonyeza yes, unaikuta bili uwe uliangalia, au la!.
Mmmh pasco nawe kiboko, yaani umeitafuta hii thread ili uunganishe dots ujue ukweli wa tuhuma za wizi uliofanyika hotelini Arusha.
 
Pole sana Pasco. Mie nilishapambana na hiyo kitu ila sema kuwa nilishaonywa mapema juu ya kuvamia hicho ki-Friji.

Kuhusu pombe kwa bahati hata sikuwa na hamu nazo maana nilikuwa kwenye sherehe za kampuni ya Diageo (John Walker, Smirnoff vodka ......) na kwa miaka ya 90 nilikuwa na kauwezo kangu ka kunywa, siku hiyo nilinyenyua mikono maana zilikuwepo pombe zao kibao.

Nilitaka kuvamia chupa ya maji ila nikasita maana walikuwa wameandika Lats 3. Yes, hiyo ndiyo likuwa bei ya maji, chupa ya lita 1.50 ya maji ndani ya hotel iitwayo The Radisson Blu Hotel, Iala(street) Elizabete, Riga ndani ya Latvia.

Ukisikia Lats 3 unaona ni hela ndogo, mhhhh..... ukienda kubadili hela, unaambiwa ni US $ 6. Chupa ya maji $ 6/-? wanacheza na hela hawa. Kifriji kidogo nilikipishia mbali. Hata maji nikawa navuta kutoka kwenye buffet ingawa bado walikuwa wakiweka ya bure kwenye vichupa vidogo.

Ninafikiria kama mtu ukivuta taulo, hawa Radisson watakuvuta pesa kiasi gani? Mkiwa mahotelini, msione aibu kuuliza maana unaweza kuaibika kama mfuko wako ni mdogo. Kama umeshafanya kazi vya kutosha na Kadi yako ya Bank ni nzuri, unaweza kulala hata hotel za kichina maana huko vyakula ni rahisi sana ila ukitaka huduma za wale Mabinti zao hata kama ni Massage tu ya kawaida, mhhhh!!!!!!!! Ila utafaidi.
 
Shule iliyopo hapa ni ya nguvu na kwa kweli nimefurahi sana kuona wanaJF wakijitahidi kushare uelewa wa mambo mbali mbali na muhimu kwenye maisha ya kila siku. Hili la suala la kutumia vitu unavyokuta katika chumba cha hoteli na vifaa vya meza ya chakula pia jinsi ya kufanya mambo uwapo mezani (table manners) ni nyeti sana. Binafsi nimekuwa nikijifunza kila mahali ninapoenda ila wakati mwingine nakumbana na aibu pale ambapo Mtanzania mwenzangu anapofanya vitu vya aibu ambayo hakutegemewa kufanya kutegemeana na hadhi aliyopewa hadi kufika mahali hapo. Mfano, kujaza chakula kingi sana kwenye sahani, kutumia kijiko cha supu kula msosi, kuchanganya side plates n.k. Nashauri hii thread ibadilishwe au ianzishwe nyingine kwa ajili ya kutoa hii elimu na kama kuna wataalamu watusaidie. Naomba tujadili mambo kwa topic, mfano, vyumba vya hotel na matumizi yake, meza ya chakula, uvaaji katika sherehe tofauti (official, traditional Vs casual dresses) n.k. Ni mambo mengi ambayo tunahitaji kusaidiana. Jamani tunapata aibu na wakati mwingine kuwatia aibu wenzetu tunapokaribishwa misosi au kusafiri.
.Mawazo mazuri mkuu ila tu cha kusikitisha elimu hii inafaa kwa yapata asilimia moja ama mbili tu ya watanzania. Watu wengi wamepigiga kinoma hata mhogo kwa kachumbari ya maji ya nyanya ni issue. Sasa watu kama hawa ndio unataka kuwapa utaratibu na namna ya kubalance menu dinning table? Hili somo lina manufaa tu kwa watu wa per diem, posho na ma dealers, haliwasaidii matonya wa kibongo.
 
Mkuu,niko ndani ya jiji la dsm kwa sasa,na niko busy kuyachunguza mahotel ya hapa twn...na hilo ni moja kati ya mambo niliyoyagundua,zaid stay on...
 
Nenda ketembee bukoba utajua hilo la chini ni la nini
 
Pole sana Pasco. Mie nilishapambana na hiyo kitu ila sema kuwa nilishaonywa mapema juu ya kuvamia hicho ki-Friji.

Kuhusu pombe kwa bahati hata sikuwa na hamu nazo maana nilikuwa kwenye sherehe za kampuni ya Diageo (John Walker, Smirnoff vodka ......) na kwa miaka ya 90 nilikuwa na kauwezo kangu ka kunywa, siku hiyo nilinyenyua mikono maana zilikuwepo pombe zao kibao.

Nilitaka kuvamia chupa ya maji ila nikasita maana walikuwa wameandika Lats 3. Yes, hiyo ndiyo likuwa bei ya maji, chupa ya lita 1.50 ya maji ndani ya hotel iitwayo The Radisson Blu Hotel, Iala(street) Elizabete, Riga ndani ya Latvia.

Ukisikia Lats 3 unaona ni hela ndogo, mhhhh..... ukienda kubadili hela, unaambiwa ni US $ 6. Chupa ya maji $ 6/-? wanacheza na hela hawa. Kifriji kidogo nilikipishia mbali. Hata maji nikawa navuta kutoka kwenye buffet ingawa bado walikuwa wakiweka ya bure kwenye vichupa vidogo.

Ninafikiria kama mtu ukivuta taulo, hawa Radisson watakuvuta pesa kiasi gani? Mkiwa mahotelini, msione aibu kuuliza maana unaweza kuaibika kama mfuko wako ni mdogo. Kama umeshafanya kazi vya kutosha na Kadi yako ya Bank ni nzuri, unaweza kulala hata hotel za kichina maana huko vyakula ni rahisi sana ila ukitaka huduma za wale Mabinti zao hata kama ni Massage tu ya kawaida, mhhhh!!!!!!!! Ila utafaidi.

Nimekumbuka nimecheka mwenyewe tu!
Hii ya kifriji nilikutana nayo hotel moja huko Thailand(Former Thai hotel). Jamaa walikuwa wamejaza vinywaji vya kila aina. Mi nilichofanya ni kujisevia tu. Kilichonistua ni ule utaratibu wao kila asbh unasain vikaratasi vyao pale reception. Nilikuta bill ya US $ 5 kwa bia mbili nilizokunywa jana yake. Ila aliyenihudumia ni mtu mmoja raia wa italy anayefanya kazi hapo basi kwwa muda huo tukawa tumezoeana naye kwa kiasi fulani, nikamuuliza hivi vile vinywaji kwenye friji si vimo kwenye bill ya chumba? Akasema hapana, ila akasema jioni nitakupeleka sehemu ambapo kuna bia za bei rahisi. Kweli jioni nilipotoka kwenye workshop naye alikuwa anatoka zamu yake akanipeleka kwenye supermaket ambapo US $1 unapata bia 6,kwa kweli maisha yalikuwa safi sana,baada ya hapo akanipeleka kwny restaraunt moja msosi bei rahis ni kama US $1(kwa hela yao ni 10Baht). Kwa kweli tulifanya saving bab kubwa yaani kwa siku mtu unatumia US $19 (Hotel three star,chakula na vinywaji).
 
Wakuu funga kazi ni pale Washington Suite pale DC ZAMANI IKIITWA Double Tree Hotel karibu na Tyson Squire, Habari ya rm service kitu ingine kabisa kila kitu ndani hata shuka inajirekodi siku ukishuka reception una check out ndo utajua maisha si rahisi pahala pale.Yaani niliwaasha TV kuangalia mambo ya kiutu uzima,Nikawasha mtandao kuwasiliana na bongo,Oven kupasha BF moto nk Lololoooh nilijuta kwanini nili bk kukaa pale.Bill niloikuta ni $640 hebu niambie per diem yangu ni $420 panakalika kweli hapo??????
 
Kwahiyo yule mama akajitoa akili akadhani gharama ya chumba imecover na gharama za mataulo, hahaah .
 
Pole sana Pasco. Mie nilishapambana na hiyo kitu ila sema kuwa nilishaonywa mapema juu ya kuvamia hicho ki-Friji. Kuhusu pombe kwa bahati hata sikuwa na hamu nazo maana nilikuwa kwenye sherehe za kampuni ya Diageo (John Walker, Smirnoff vodka ......) na kwa miaka ya 90 nilikuwa na kauwezo kangu ka kunywa, siku hiyo nilinyenyua mikono maana zilikuwepo pombe zao kibao. Nilitaka kuvamia chupa ya maji ila nikasita maana walikuwa wameandika Lats 3. Yes, hiyo ndiyo likuwa bei ya maji, chupa ya lita 1.50 ya maji ndani ya hotel iitwayo The Radisson Blu Hotel, Iala(street) Elizabete, Riga ndani ya Latvia. Ukisikia Lats 3 unaona ni hela ndogo, mhhhh..... ukienda kubadili hela, unaambiwa ni US $ 6. Chupa ya maji $ 6/-? wanacheza na hela hawa. Kifriji kidogo nilikipishia mbali. Hata maji nikawa navuta kutoka kwenye buffet ingawa bado walikuwa wakiweka ya bure kwenye vichupa vidogo. Ninafikiria kama mtu ukivuta taulo, hawa Radisson watakuvuta pesa kiasi gani? Mkiwa mahotelini, msione aibu kuuliza maana unaweza kuaibika kama mfuko wako ni mdogo. Kama umeshafanya kazi vya kutosha na Kadi yako ya Bank ni nzuri, unaweza kulala hata hotel za kichina maana huko vyakula ni rahisi sana ila ukitaka huduma za wale Mabinti zao hata kama ni Massage tu ya kawaida, mhhhh!!!!!!!! Ila utafaidi.
Sikonge, nimeipenda hii ya mabinti wa kichina na mambo yao ya massage, bongo wapo njoo Giraffe Hotel ujikumbushe mambo ya Radisson.
 
Mmmh pasco nawe kiboko, yaani umeitafuta hii thread ili uunganishe dots ujue ukweli wa tuhuma za wizi uliofanyika hotelini Arusha.
No nilisema wanamsingizia, kuna tofauti kati ya kuiba na kichukua. Nikawathibitishia mambo hayo yapo baadhi ya hoteli kwa upande wa bathrobe ila inailipia. Usichanganye thread, hii ni thread kuhusu matumizi ya mataulo mahotelini.
 
Na mimi nauliza kwa hapa kwetu ukiingia Guest House mbona unakuta kuna malapa sakafuni moja rangi nyekundu na lingine rangi ya kijani halafu yote ni ya kushoto nini maana yake?
 

Madabwada, si nilisema hivi "Tena familia ya hotel za Sheraton na Marriot wao ndio wamezidi unakuta taulo 6 kila moja ni pair on top of that wanakuwekea bath robe ya taulo na tag 'you can take this with you'. Mbongo si unajua tena, nikabeba. Siku ya kuondoka nikakuta bill US$ 100. For the bath robe!"

Bado kuna tatizo?. Hata ukilala Hilton tuu hapo Nairobi, unakuta tag kwenye bathrobe, wao unalipia Shilingi za Kenya 150 enzi nilipolala mimi.

Kwa hoteli kubwa unakuta ki jokofu kidogo ndani kimeshehenezwa kila bia na vinywaji baridi, huku kabatini unakuta mini bar, hakuna popote palipoandikwa unaweza kujisevia, vyote ni mali yako, utumie usitumie ni juu yako. Nilikunywa niliweza, mgeni wangu akajitwalia alivyoweza kubeba. Siku ya kucheck out, vyote nililipishwa kwenye bili ikiwemo bili ya ajabu, ya kulipia kuangalia TV!.

Kumbe mgeni wangu hana hili wala lile, kabonyeza chaneli ya pay per view kuangalia zile movie, wanakuuliza mara mbili mbili kwa Kiingereza kwa kuonyesha kiwango cha kulipia, ukikubali, unabonyeza 'yes', ukifikiri unaulizwa kama unapenda kuangalia. Ukishabonyeza yes, unaikuta bili uwe uliangalia, au la!.

Pasco! ulirekebisha nanihii nini hahaha ahahah!!!!
 
Wale wa Dar nilishawaona maana tulienda pale kula usiku na wakati tumekaa ghafla tunamuona Klyn (Mwimbaji) na Wazungu wake wawili (wanaume) wameingia. Mimi na ushamba wangu nikawa nauliza, huyu kama namfahamu, half-cast gani huyu? Wakaniambia huyo ndiyo Klyn mwenyewe.

Msosi safi sana na bei ni nzuri mno. Ila jamaa alipouliza kama kuna huduma ya Massage, akaambiwa ndiyo ipo, huko juu. Ila bei yake ilimkatisha jamaa tamaa maana ilikuwa inatisha. Hiyo hotel wala sifahamu iko wapi maana kama nilivyosema nilishakuwa mshamba tayari pale Dar ila nakumbuka tu kuwa wakati tunakwenda, tulipita ubalozi wa USA na kutoka hapo, haikuwa mbali sana.

Wachina inapokuja kwenye kulala/massage, huwa wana bei kubwa sana. Nashindwa kuelewa sijui kwa nini. Spa zao bei iko juu mno.

Anyway, nafikiri hata wengine hili somo litakuwa limewasaidia sana hasa kunywa vinywaji kwenye Kifriji na kuangalia Film kwenye TV (Film za watu wazima) na baadhi ya hotel kutumia Internet. German hadi leo ni common sana. Mshikaji wangu juzi nimeongea naye akaniambia kuwa nusuru alipishiwe Euro 12 kwa kutumia Internet kwa siku. Ila sema walikuwa wamepangiwa vile vyumba vya bei mbaya na jamaa wakaona AIBU na kumwambia, ahh... waweza kutumia BURE.
Sikonge, nimeipenda hii ya mabinti wa kichina na mambo yao ya massage, bongo wapo njoo Giraffe Hotel ujikumbushe mambo ya Radisson.
 
Wachina inapokuja kwenye kulala/massage, huwa wana bei kubwa sana. Nashindwa kuelewa sijui kwa nini. Spa zao bei iko juu mno.
Its true massage za Wachina wako bei juu na sabu ni moja tuu, wanafanya massage za ukweli. Massage za ukweli kwanza zinatakiwa kufanywa na mtu anaezijua vizuri zile meridians na points za acu pressure, pili lazima awe na mkono wenye power to press.

Dada zetu wengi wana bonyeza bonyeza kwa guess work na mikono yenyewe ndio hiyo hiyo ifulie nguo, isugulie masufuria ndipo ije kufanya massage!.
 
Its true massage za Wachina wako bei juu na sabu ni moja tuu, wanafanya massage za ukweli. Massage za ukweli kwanza zinatakiwa kufanywa na mtu anaezijua vizuri zile meridians na points za acu pressure, pili lazima awe na mkono wenye power to press.Dada zetu wengi wana bonyeza bonyeza kwa guess work na mikono yenyewe ndio hiyo hiyo ifulie nguo, isugulie masufuria ndipo ije kufanya massage!.
Hahahahahaa! Vey true kaka! Wanaguess sana kupiga message utafikiri wanampaka mafuta mtoto na viganja vigumu kweli aisee!
 
Back
Top Bottom