Haya mataulo bafuni ni ya nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haya mataulo bafuni ni ya nini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwanjelwa, Dec 21, 2008.

 1. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #1
  Dec 21, 2008
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Katika Hotels nyingi kubwa kubwa sehemu mbali mbali Duniani, utakuta kwenye bafu, kuna mataulo matatu. Moja kwenye sink(spelling!) la kuogea, pili kwenye sink la kunawia/kupigia mswaki na tatu liko chini sakafuni. Acha yale mengine ya kwenye kabati ukutani.

  Naomba shule. Hivi yale matatu yanatumikaje? Kuna Hotel moja kule Manila na pia pale Mumbai, waliniomba kuwa kama taulo siyo chafu tafadhali nisiweke chini. Hapo ndiyo nikavurwa, kwani tayari lingine nimelikuta chini na kila siku nikiingia nakuta liko chini.

  Mawazo kwa anayejua?
   
 2. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #2
  Dec 21, 2008
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Jamani kama yupo humu mtu wa Hotel Management atusaidie kujibu swali hili. Si wewe tu mkuu Mwanjelwa, hata mimi nilipata shida ya hayo mataulo pale Colombo, hasa hilo la chini. Mimi nililitumia kukaushia nyayo/vikanyagio vyangu baada ya kutoka kwenye sehemu ya kuogea ili nisisambaze maji 'sebuleni', hata hivyo sina uhakika kama ndo lilikuwa lengo la kuwekwa pale.
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Dec 21, 2008
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,238
  Trophy Points: 280
  Japo sio mtu wa hotel management lakini malengo ya hayo mataulo ni kama yalivyoweka na utaona size hayalingani. Hili la chini ni taulo carpet na ukilikanyaga utasikia na kama reli au vibox vidogo vidogo.

  Utanote lile la -kwenye sink la kuogea ni kubwa zaidi na la sink la kunawia ni dogo kidogo.

  Tena familia ya hotel za Sheraton na Marriot wao ndio wamezidi unakuta taulo 6 kila moja ni pair on top of that wanakuwekea bath robe ya taulo na tag 'you can take this with you'. M'bongo si unajua tena, nikabeba. Siku ya kuondoka nikakuta bill US$ 100 for the bath robe!.
   
 4. Sita Sita

  Sita Sita JF-Expert Member

  #4
  Dec 21, 2008
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 1,197
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  I know only three towels. face towel, hands towel and bath towel. sasa hilo la chini hata cjui. Mi napitaga tu kwenye hotels, kwa raha au safari za kazi.
   
 5. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #5
  Dec 21, 2008
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35

  :D! Umenikumbusha issue ya room service. Pale Marriot Hotel, Mumbai ndani wameweka kikaratasi kimeandikwa 'room service is available free of charge.! Wame-list, mojawapo ni breakfast kuletewa ndani asubuhi kwa muda utakao! Nikaandika na kuning'niza kile paper mlangoni kwa nje. Asubuhi jamaa, kaleta, anamaliza kupanda vitu vyake, nikaambiwa nisaini. Kusaini tena?! Why? Akajibu,,,,Sir, you have to pay 15 USD for this! Mhh! Mbona mmesema free of charge! Akajibu-No Sir, you must sign! I signed and paid. Wakati kule chini kwenye lounge ni bure tu alafu unaji-mix na watu kibao!.

  Safari ni kujifunza, ila mpaka leo sijaelewa kwanini walini-charge ile hela na sijawahi rudia hiyo faulo!!
   
 6. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #6
  Dec 21, 2008
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kwi kwi kwii!! Na mimi nimekumbuka jinsi nilivyochomekewa bill ya soda kwenye hoteli moja pale Colombo, huku ukweli ukiwa ni kwamba sikuwahi kuagiza. Bill hiyo nilipewa siku ya kuondoka hotelini pale receiption. Jamaa walikuwa wanacharge according to room number, na hawakujali sana anayelala humo ni mwenye jina gani. Kumbe masikini ile charge ilikuwa iende kwa raia mmoja wa Uganda ambaye tulibadilishana room wiki mbili baada ya kufika hotelini, na tulibadilishana kutokana na maelekezo ya management ya ile hotel! Bahati nzuri yule dada wa Uganda alikuwa bado yupo, na akaitwa na kukubali kulipa. Sasa sipati picha kama Mganda huyo angeanza kuondoka kabla yangu, sijui mambo yangekuwaje !!
   
 7. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #7
  Dec 21, 2008
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Hiyo nadhani itakuwa 'transport' service, au?
   
 8. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #8
  Dec 21, 2008
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...Sita sita naona maelezo yako yanakaribiana na ukweli, taulo 'chini' ni badili ya bathmat.

  kasheshe ipo hapa, utaanza na nini uishie na nini, balaaa;  ...unaweza ishia kuomba bakuli la maji ya kunawa...!
   
 9. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #9
  Dec 21, 2008
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  :eek::confused: Ya kutoka wapi? Ya kuleta breakfast?!
   
 10. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #10
  Dec 21, 2008
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Jikoni mpaka chumbani kwako..
   
 11. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #11
  Dec 21, 2008
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mwanjelwa, si mataulo tu, umewahi kukumbana na glasi zinazowekwa mule bafuni? Jamani mnaojua kazi zake tusaidieni kutoa ushamba, manake mi nilikuwa naziona tu hata kutumia sikuthubutu. Cha ajabu ni glasi kama zile zile tunazokutana nazo kwenye misosi. Ina maana ndo ni hizo hizo wanatuchanganyia au wanazijua hizi ziende wapi?
   
 12. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #12
  Dec 21, 2008
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...tumia kusukutulia maji baada ya kupiga mswaki, :)

  ...naam, naam,...mtindiowaubongo, lugha sahihi ni "service charge", uamue ushuke ukajilambe na Buffet restaurant au ung'ang'anie chumbani 'uletewe' tosti na chai sababu ya haya zako halafu uchajiwe zaidi! :D

   
 13. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #13
  Dec 21, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Yeap hiyo ni service charge since hukutaka kushuka lobby for breakfast na ukataka kuletewa chumbani kwako...so you have to pay for the service.
   
 14. K

  Koba JF-Expert Member

  #14
  Dec 21, 2008
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  ..mmenikumbusha kasheshe lililonikuta Chicago,mabwege nimefika Hotel sasa nacheck out after 2 days nakuta bill imezidi for almost 300$ ,nikauliza whats up with this bill? jamaa akaanza kunipa bill breakdown,then...sir,and this is for your parking,damn ng'ombe wale ilikuwa nusu waniitie police!
   
 15. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #15
  Dec 21, 2008
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...aibu inaweza kukukumba na zile mini bars (fridge ndogo chumbani), wewe unajiona umependwa, kuna full stock incl Mars bar, John Mtembezi miniatures, nk...

  siku ya ku check out ukiiangalia bili unabakia :eek:...!
   
 16. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #16
  Dec 21, 2008
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Hivi, room service na sevice charge kuna tofauti gani? Wenyewe wamesema kila kitu bure ndani ya chumba chako. Na hiyo breakfast imo kwenye list. Sasa unaweka order, bado wanadai dola 15! Hii inakuwaje? Mimi nililipa, kwa ubishi sana, ingawaje kwa kweli mpaka leo inaniuma kwa kuwa nahisi nililipishwa kwa ushamba tu. Mpaka nitakapota maelezo,, nikirudi pale sitakaa hata siku kidogo.
   
 17. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #17
  Dec 21, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Service charge is kind similar to room service is $5 delivery plus 20% service charge not to include price of your meal (BREAKFAST)...basically your breakfast was free (included in your room) besides kama ungeshuka kwenda lobby you wouldnt pay a dime since you decided to call for roomservice then you have to pay for delivery and service charges which is similary to TIPS...
   
 18. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #18
  Dec 21, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Parking in chicago ni mimba usicheze na parking in chicago...for just an hour parking in a meter ni $1.00,na hiyo ni meter only bado hujapark garage..inaelekea wewe ulitumia min bar na simu ndiyo maana bill yako ikawa si kisenge.
   
 19. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #19
  Dec 22, 2008
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Kila siku unajifunza kitu kipya. Ndiyo maisha yenyewe.
   
 20. W

  Wandugu Masanja JF-Expert Member

  #20
  Dec 22, 2008
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 1,535
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  katika mtu anyepata malipo kidogo kwenye hotel ni room service person huwa anapata kama $2.5 kwa saa malipo zaidi ni tipps na order ya chakula huwa anajipatia 10% sasa akija chumbani zitakutoka za 10% na sio charge ya chakula, ikiwa chakula ni bure la kama ni kulipia chakula 10% inakuwa tayari imetiwa kwenye bili ya chakula
   
Loading...