Haya mataulo bafuni ni ya nini?

Kuna , bath towel hii ukitoka kuoga mkuu , hand towel kwa mikono , washcloth unaweza kutumia kama dodoki mkuu .
Foot towel inatumika kama rung yah na mara nyingi halibadilishwi mara kwa mara. Ntanukuu statement hii toka answers.com pamoja na wikipedia wote naona wana article hii.
"A change of towels, as supplied by maid service in an American-style hotel, is one bath towel, one hand towel, and one washcloth. A foot towel is a small, rectangular towel which, in the absence of a rug, carpet or bathroom mat, is placed on the bathroom floor to stand on after finishing a shower or bath."

Kwa maelezo zaidi ingi hapa towel: Definition from Answers.com
 
...wajemenii eeeh, nimeulizia matumizi ya hizi bilauri, uma, visu na vijiko, naamini kuna aliye na ufahamu na hizi table etiquette. eti, mnaohudhuria ma banquet Ikulu, ikoje hii?
a= ?
b= ?
c= ?
etc...
 
Mkuu hivi kila moja vina shughuli yake na yao mambo ya loyal family na sisi wengine tunakutana navyo kwenye hotel na huwa tuviruka vingine ahaaaa.Sasa ajitokeze muungwana atu hadithi kidogo ama sivyo itabidi nifanye home work .
 
...Sita sita naona maelezo yako yanakaribiana na ukweli, taulo 'chini' ni badili ya bathmat.

kasheshe ipo hapa, utaanza na nini uishie na nini, balaaa;

...unaweza ishia kuomba bakuli la maji ya kunawa...!

Mkuu Mchongoma
Mimi si mtaalamu wa mambo ya hoteli wala sihudhurii state banq, ila kuchumbia ilikuwa shule tosha. Kwa haya madude, there is a standardized rule which is not necessarly standard
Sheria rahisi. Siku zote anza kutumia vifaa (vilivyopangwa mezani kuzunguka sahani kubwa ya kati) kutoka nje kwenda ndani. Hapo pangua A kwanza. Kama kijiko cha supu kipo mwanzo kulia (J), jua supu imo then saladi (B). Na L& K kwa ajili ya mkate na siagi. M & N ni mwisho mambo ya dizati. O ni maji P, Q na bilauri nyingine ni za mvinyo. Itakayofuata bilauri ya maji inaweza kuwa ya mvinyo wa kuruka (kama bilauri ni nyembamba ndefu) Mpango unaweza kubadilika kidogo kulingana na hadhi ya hafla au US vs Europe, ila bilauri yenye tumbo kubwa fupi, ni ya mvinyo mwekundu, na ya nyeupe itakuwa na tumbo dogo ndefu kiasi. E Saladi, F supu, G mlo mkuu. Kama meza imepangwa vingine jua sahani itakayokuwa na tumbo/bakuli ni la supu, flati ndogo ni ya saladi na sahani flati kubwa ni mlo. Ila kama mlo una samakiau wanyama wa baharini, uma wake una kikichwa cha tofauti kidogo kama kikisu, kwa picha hii unaweza kutumia D. Uzuri ni kuwa mlo ukipita, lazima wahudumu waje kukupunguzia vyombo
Haya mambo huwa yanakera sana, uswazi kijiko/uma mkono, kisu meno, kikombe maji, uji humo humo, shida ya nini?
 
It sound good brother ,thanks
 
ile taulo ya sakafuni ni kwa wale ambao wanatumia showergel au sabuni ambazo unaweza teleza kwenye tiles wakati umemaliza kuoga koz huwezi kuweka carpet chooni/bafuni...Glass bafuni unaweza tumia kadri upendavyo,waweza nywea mfano dawa,waweza wekea miswaki,waweza sukutulia etc etc...
 
Mkuu Mchongoma
Mimi si mtaalamu wa mambo ya hoteli wala sihudhurii state banq, ila kuchumbia ilikuwa shule tosha. Kwa haya madude, there is a standardized rule which is not necessarly standard
Sheria rahisi. Siku zote anza kutumia vifaa (vilivyopangwa mezani kuzunguka sahani kubwa ya kati) kutoka nje kwenda ndani. Hapo pangua A kwanza. Kama kijiko cha supu kipo mwanzo kulia (J), jua supu imo then saladi (B). Na L& K kwa ajili ya mkate na siagi. M & N ni mwisho mambo ya dizati. O ni maji P, Q na bilauri nyingine ni za mvinyo. Itakayofuata bilauri ya maji inaweza kuwa ya mvinyo wa kuruka (kama bilauri ni nyembamba ndefu) Mpango unaweza kubadilika kidogo kulingana na hadhi ya hafla au US vs Europe, ila bilauri yenye tumbo kubwa fupi, ni ya mvinyo mwekundu, na ya nyeupe itakuwa na tumbo dogo ndefu kiasi. E Saladi, F supu, G mlo mkuu. Kama meza imepangwa vingine jua sahani itakayokuwa na tumbo/bakuli ni la supu, flati ndogo ni ya saladi na sahani flati kubwa ni mlo. Ila kama mlo una samakiau wanyama wa baharini, uma wake una kikichwa cha tofauti kidogo kama kikisu, kwa picha hii unaweza kutumia D. Uzuri ni kuwa mlo ukipita, lazima wahudumu waje kukupunguzia vyombo
Haya mambo huwa yanakera sana, uswazi kijiko/uma mkono, kisu meno, kikombe maji, uji humo humo, shida ya nini?

Tatizo linakuja kwa sisi wengine ambao huwa hatutaki starter kwenye hii milo ya Ulaya. Maana tukila starter tunakuwa tumeshashiba hata kabla ile wanaita main course!. Sasa ndipo matumizi ya hivi vitu yanapoaanza kuwa sivyo ndivyo! Labda kwa wanaojua, pia tunaomba shule hapa. Mimi kila wakati nikila stater inakuwa enough, lakini nawashangaa wenzangu wakiendela kuuchapa msosi wanaouita main course na baadaye dessert!
 
...Sita sita naona maelezo yako yanakaribiana na ukweli, taulo 'chini' ni badili ya bathmat.

kasheshe ipo hapa, utaanza na nini uishie na nini, balaaa;

...unaweza ishia kuomba bakuli la maji ya kunawa...!

mimi hapo mezani ndipo panaponipa homa kabisa. afu sasa saa inginewe unaambiwa ukajichukulie mwenyewe, sasa utabeba sahani ipi?, yaani bora uswailini unaletewa kijiko kimoja na msosi kwenye sahami moja kila kitu.
 
..mmenikumbusha kasheshe lililonikuta Chicago,mabwege nimefika Hotel sasa nacheck out after 2 days nakuta bill imezidi for almost 300$ ,nikauliza whats up with this bill? jamaa akaanza kunipa bill breakdown,then...sir,and this is for your parking,damn ng'ombe wale ilikuwa nusu waniitie police!

ahahahhahahahahah
 
Tatizo linakuja kwa sisi wengine ambao huwa hatutaki starter kwenye hii milo ya Ulaya. Maana tukila starter tunakuwa tumeshashiba hata kabla ile wanaita main course!. Sasa ndipo matumizi ya hivi vitu yanapoaanza kuwa sivyo ndivyo! Labda kwa wanaojua, pia tunaomba shule hapa. Mimi kila wakati nikila stater inakuwa enough, lakini nawashangaa wenzangu wakiendela kuuchapa msosi wanaouita main course na baadaye dessert!

Mkuu Mwanjelwa
Kuna kitu wanasema, eti haya ma dinner au ma lunch si kula kwa afya, bali ni namna ya kukutana na kusoshalaizi ukishiba hewala. Pia ni kuonesha ukarimu na/au ujazo wa mfuko wa mwaandaji. Usishangae kula ubongo au mayai ya samaki ukaambiwa ndo dishi expe kuliko zote wakati unatamani upate mahali pa kutapikia.
Hapa itategemea na mfumo wa hafla, kama ni ya kusubiri wahudumu wahudumie na pia hutaki chochote, unatulia na bilauri ya maji au mvinyo mweupe au juisi. Akipita mhudumu unainua mkono achukue sahani. Wanajua atachukua na uma, vijiko au visu husika. Kumbuka mvinyo mweupe unanyewa kabla ya mlo, na wakati wa mlo unanywewa na nyama nyeupe (kuku, samaki) na mwekundu nyama nyekundu (kiti moto, kondoo nk). Rose huwa si mvinyo wa mlo, ila ukitaka unaweza kuitisha. Mara nyingi kama si mpenzi wa mikate, iache huwa ina tabia ya kuharibu apetaiti. Kuna watu kama Wajerumani wamezoea mikate mikavu, hata mtoto wa miezi mitatu alishwa kate gumu kavukavu na anameza bila wasiwasi.

Kasheshe kwangu ilikuwa kwenye mkao wa meza. Kuna kiti cha mwandaaji wa hafla vs mgeni mkuu (kushoto vs kulia) na kiti cha mwalikwa/waalikwa wa kawaida. Mkuu Mchongoma, una picha ya meza? Chukulia uko na binti, na wakwe wawili nani anakaa wapi na nani wapi
 
...

...la hasha hiyo sina.

...ila, 'nimeambiwa' katika restaurant (zile za kula kwa kutumia uma na kisu,) mwanaume ndio awe ana face mlango, mamsap awe ameupa mgongo.

...baba mkwe atakaa kulia na ma-mkwe akae kushoto... na hakikisha waiter analeta kwako bili zote!
 
Bahati mbaya waiter anavyoleta bill wewe unakuwa umeenda rest room kutoa nyama iliyoganda kwa meno ukirudi utafanyaje .
 
...la hasha hiyo sina.

...ila, 'nimeambiwa' katika restaurant (zile za kula kwa kutumia uma na kisu,) mwanaume ndio awe ana face mlango, mamsap awe ameupa mgongo.

...baba mkwe atakaa kulia na ma-mkwe akae kushoto... na hakikisha waiter analeta kwako bili zote!

Mkuu hii kali Mkuu. Hiyo ya bili kuna jamaa alijaribu kulipa akaambiwa arudishe waleti eti mkwe ndio kaalika. Haya mambo ya kuchanganya tamaduni ni magumu sana
 
Mkuu Mwanjelwa
Kuna kitu wanasema, eti haya ma dinner au ma lunch si kula kwa afya, bali ni namna ya kukutana na kusoshalaizi ukishiba hewala. Pia ni kuonesha ukarimu na/au ujazo wa mfuko wa mwaandaji. Usishangae kula ubongo au mayai ya samaki ukaambiwa ndo dishi expe kuliko zote wakati unatamani upate mahali pa kutapikia.
Hapa itategemea na mfumo wa hafla, kama ni ya kusubiri wahudumu wahudumie na pia hutaki chochote, unatulia na bilauri ya maji au mvinyo mweupe au juisi. Akipita mhudumu unainua mkono achukue sahani. Wanajua atachukua na uma, vijiko au visu husika. Kumbuka mvinyo mweupe unanyewa kabla ya mlo, na wakati wa mlo unanywewa na nyama nyeupe (kuku, samaki) na mwekundu nyama nyekundu (kiti moto, kondoo nk). Rose huwa si mvinyo wa mlo, ila ukitaka unaweza kuitisha. Mara nyingi kama si mpenzi wa mikate, iache huwa ina tabia ya kuharibu apetaiti. Kuna watu kama Wajerumani wamezoea mikate mikavu, hata mtoto wa miezi mitatu alishwa kate gumu kavukavu na anameza bila wasiwasi.

Kasheshe kwangu ilikuwa kwenye mkao wa meza. Kuna kiti cha mwandaaji wa hafla vs mgeni mkuu (kushoto vs kulia) na kiti cha mwalikwa/waalikwa wa kawaida. Mkuu Mchongoma, una picha ya meza? Chukulia uko na binti, na wakwe wawili nani anakaa wapi na nani wapi

Yes. Kuna mayai ya samaki wanaita wenyewe Carvier. Siku nikaambiwa ni sehemu ya menu muhimu wakati wa x-mas na ni very expensive. Sikuelewa maana yake. Nilichofanya, kwa hicho expensive ni kuchota zaidi ya vingine. yaani ile Kibongo-bongo!. Baadaye jamaa ndiyo wakaniuma sikio na kunipa habari yangu!. Haya mambo makubwa kweli Duniani.
 
Bora walikushtua, maana hayafai sana kwa afya kama huyahitaji. Ndio maana acha samaki wakae huko huko kwenye maji sie tuhangaike na mayai ya ndege tu
 
Tatizo linakuja kwa sisi wengine ambao huwa hatutaki starter kwenye hii milo ya Ulaya. Maana tukila starter tunakuwa tumeshashiba hata kabla ile wanaita main course!. Sasa ndipo matumizi ya hivi vitu yanapoaanza kuwa sivyo ndivyo! Labda kwa wanaojua, pia tunaomba shule hapa. Mimi kila wakati nikila stater inakuwa enough, lakini nawashangaa wenzangu wakiendela kuuchapa msosi wanaouita main course na baadaye dessert!

ukiwa kwenye shughuli rasmi ambayo wenyeji wameandaa "courses" zaidi ya 4, inabidi mtu ule kidogo kidogo na ikibidi uruke nyingine.

umeingia restaurant na jamaa/marafiki n.k. basi ni rahisi kuruka mtiririko na kuagiza main dish moja kwa moja.
 
Mkuu Mwanjelwa
Kuna kitu wanasema, eti haya ma dinner au ma lunch si kula kwa afya, bali ni namna ya kukutana na kusoshalaizi ukishiba hewala. Pia ni kuonesha ukarimu na/au ujazo wa mfuko wa mwaandaji. Usishangae kula ubongo au mayai ya samaki ukaambiwa ndo dishi expe kuliko zote wakati unatamani upate mahali pa kutapikia.
Hapa itategemea na mfumo wa hafla, kama ni ya kusubiri wahudumu wahudumie na pia hutaki chochote, unatulia na bilauri ya maji au mvinyo mweupe au juisi. Akipita mhudumu unainua mkono achukue sahani. Wanajua atachukua na uma, vijiko au visu husika. Kumbuka mvinyo mweupe unanyewa kabla ya mlo, na wakati wa mlo unanywewa na nyama nyeupe (kuku, samaki) na mwekundu nyama nyekundu (kiti moto, kondoo nk). Rose huwa si mvinyo wa mlo, ila ukitaka unaweza kuitisha. Mara nyingi kama si mpenzi wa mikate, iache huwa ina tabia ya kuharibu apetaiti. Kuna watu kama Wajerumani wamezoea mikate mikavu, hata mtoto wa miezi mitatu alishwa kate gumu kavukavu na anameza bila wasiwasi.

Kasheshe kwangu ilikuwa kwenye mkao wa meza. Kuna kiti cha mwandaaji wa hafla vs mgeni mkuu (kushoto vs kulia) na kiti cha mwalikwa/waalikwa wa kawaida. Mkuu Mchongoma, una picha ya meza? Chukulia uko na binti, na wakwe wawili nani anakaa wapi na nani wapi

kama wewe si mnywaji wa mvinyo ukishakaa tu unazipindua/unazifunika hizo bilauri za mvinyo na wahudumu wakiona hivyo wanakuja kuziondoa hizo bilauri.

aidha kama mtatumia mikate hakikisha unatumia kisahani kidogo kilichopo mkono wako wa kushoto. mara nyingi hii huwa inazengua watu hususan kama meza ya maakuli ni ya duara :)
 
Back
Top Bottom