Haunted houses zipo, chukua hatua

Haunted houses zipo, chukua hatua

Acha tu ndugu yangu. Yamenikuta. Sijui kama ni stage tu ya maisha nakumbana nayo au kuna mtu anajaribu kunikwamisha. Ila kama ni mtu ananikwamisha siku nitakuja kumgundua ataisoma namba!! Na naomba kama kuna mtaalamu yeyote anaeweza kunisaidia nipo tayari kutoa ushirikiano ila asiwe tapeli

Miaka kama mitatu hivi nilibahatika kupata kazi sehemu flani, kazi ilikuwa na maslahi kweli kweli na ukizingatia mimi nilikuwa bahili kweli kweli. Hela yangu ilikuwa hailiwi kizembe.

Nikawa pia nafanya kilimo, kilimo nacho kikawa kinanilipa kweli kweli. Hela ikanitembelea kweli kweli. Kila nikichungulia kwenye akaunti ikawa inanona vilivyo. Kabla nikiwa naenda likizo akaunti yangu ilikuwa inasoma 57M.

Kufika home kijiji cha kwanza nikamwambia mzee anionyeshe sehemu ya kujenga. Nikaanza chapu maana nilikuwa na likizo ya mwezi m1 tu.

Of course mimi napenda vitu quality. Nikaanza ujenzi wa nyumba ya ndoto zangu ambayo itakuwa ni ya familia yangu pia. Ni nyumba kubwa tu.

Likizo ilivyoisha tu nikarudi zangu mzigoni nyuma nikaacha ujenzi ukiendelea. Nikapaua, nikaweka dirisha na milango ya chuma, nikapiga plasta, wiring na plumbing. Ikawa gumzo pale kijiji. Bwana bwana bwana weee, ghafla mambo yakawa yamebadilika kwa speed ya 5G

Mara vuuup, nikafukuzwa kazi. Lakini akaunti yangu ikawa iko vizuri tu. Nikasema isiwe tabu. Nikasema suburi nifanye biashara pamoja na kuendelea na kilimo kama kawa. Cha kushangaza kila nikitia hela huko inafia huko hairudishi hata mtaji. Nikatia mzigo kwa mara nyingine safari hii nilipigwa hasara mpaka nikikumbuka natetemeka.

Ikawa najikingoja tu hivyo hivyo. Miezi 7 haikuisha 22M sijui zikivyokauka kauka na sasa nipo sina hata mia.

Bado sijakata tamaa, nipo napambana kutafuta chaka lingine maana kama elimu na mavyeti ninayo ya kutosha ila hili nuksi lililonijia sitakaa nilisahau kamwe.

Kimsingi roho hata hainiumi kwa vile kila nikiangalia mjengo wangu natabasamu najisemea kimoyomoyo "Asante Mungu" japokuwa haijaisha ila kwa umri wangu wa 30's nina imani nitapambana nikamilishe nyumba ya ndoto zangu kijijini kwanza ila sijui ni kwa namna gani maana kila nachofanya hakiendi.

Napitia wakati mgumu sana ndugu zangu. Niombeeni. Au nasema uongo ndugu zangu???

KAMA KUNA MTU YUKO NYUMA YA HILI NASEMA AJIANDAE, TENA NASEMA AJIANDAE KWELI KWELI. ONCE NITAKAPOMJUA, hiiiiiiiiiiiiiiii!!!!!!
Pole sana ndugu yangu......

umeongea kama hayati magu 😄😄
 
Labda kwasababu sijaelezea mazingira na muonekano wa hiyo nyumba ndio maana naonekana kama mzushi tu😃

Nyumba yenyewe kwa nje ya geti imezungukwa na vichaka hadi njia ya kuingilia haionekani, ndani ya geti ni vichaka vitupu, vioo vya madidirisha vilishapasuka yani kiufupi ni kama gofu.
Nipe mmiliki wa nyumba aone kama sintakaa na kula bata mwanzo mwisho
 
Mtaani hapa kuna nyumba ilishashindikana kukalika, sasahivi naona majini ndio yanajitawala maana ikifika jioni yanawasha taa asubuhi yanazima.
Hayo yatakuwa na undugu na haya ya mtaani kwetu. Unashangaa tu unaona bodaboda inapita, anayeendesha humwoni. Geti linafunguliwa bodaboda inaingia ndani. Aliyefungua geti hata haonekani...
 
Nipe mmiliki wa nyumba aone kama sintakaa na kula bata mwanzo mwisho
Kuna mchungaji mmoja wa kilokole alijifanya hamnazo akaingia kwenye nyumba iliyoshindikana ili aiombee... Alichezea bakora za kufa mtu, hiyo siku ndo nikashangaa kwanini watanzania tunachemka kwenye mashindano ya riadha wakati kuna Filbert Bay mpya ametulia tu huku Bunju
 
Siyo hamnazo,hakuwa na nguvu za kupambana na hayo madude.Alikuwa mwepesi kiimani.Kuna wenye kuziweza hizo shughuli ambao akitia mguu tu.........
 
🤣🤣🤣
 
hahaha nimecheka hapo kwa hao ndondocha kutojua kiinglishi
Wale wazungu walicharazwa bakora vibaya, sasa sijui wakawa wana lalama kwa kimombo, lahaulaa tobaaah ndondocha wa watu hata Pre form One hawaijui,

Ndo wakazidi kuwapa vichapo wazungu wa watu, huku wana walazimisha waongee kiswahili,

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Ha Ha Ha
 
Siyo hamnazo,hakuwa na nguvu za kupambana na hayo madude.Alikuwa mwepesi kiimani.Kuna wenye kuziweza hizo shughuli ambao akitia mguu tu.........
Thubutuuuuh, labda awe mganga wa kienyeji, sio imani ya kiroho tyuuuj, atachezea kichapo hadi asahau na uchungaji wake wenyewe

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Mpwa....

Niliwahi kupanga Chumba maeneo fulani ya magomeni....ile nyumba ilikuwa na vyumba saba lakini wapangaji tuliokuwa tunajuana ni mimi na jamaa mmoja.....nilikaa pale miezi miwili pasi nakuonana na wapangaji wengine zaidi ya jamaa ninayekutana naye akiwa anatoka na kurudi kazini.....lakini kipindi chote shughuli zote za kuashiria kuwa vile vyumba wanaishi watu zilikuwa zinaendelea kama vile kupika na mazungumzo yaliyojaa vicheko vya hapa na pale.......lakini ukikaa koridoni huoni mtu......kilichonifanya nikimbie ile nyumba ilikuwa siku ya jumapili...nilichelewa kuamka....muda nilio amka nikachukua ndoo yangu kwenda bafuni kujimwagia....nikakuta bafuni kuna mtu anaoga kutokana na viashiria vya kumwagika kwa maji humo bafuni.....nikasema ngoja nisubirie tu hapa hapa kuliko kujisumbua kurudi chumbani kwangu......nilikaa karibu na mlango kabisa.....baada ya muda kadhaa kimya kikatawala mule bafuni kuashiria kwamba mtu ameshatoka sasa lakini atakuwa amepitia wapi......wakati naangaza macho kwenye korido nikaona kuna kandambili zimeloa kwenye moja ya ile milango ambayo sijawahi kuwaona watu wakiingia humo.....akili yangu ikaniambiaa kuwa kuna kitu hakipo sawa.....nikaingia bafuni nikaoga.....nikarudi chumbani kwangu nikavaa nikatoka......nilipokuwa mitaani nikamtafuta mtu mzima kidogo ambaye ni mwenyeji na kumdadisi kuhusu nyumba ile.....akaniambia ile nyumba ni nzito.....na inakaliwa na watu wazito......huo ndio ukawa mwisho wa mimi kukaa mule ndani na hata vyombo niliagiza watu wanileteee......
Jamaa uliyemkuta ulimuacha?
 
Back
Top Bottom