Haunted houses zipo, chukua hatua

warumi

R I P
May 6, 2013
16,298
2,000
Sijui why leo nipo kwenye mood ya kuongelea hii Topic , I hope itagusa watu na kuwasaidia kuchukua hatua. Mara nyingi tumekua tukiangalia Film’s za kutisha huko Hollywood kuhusu hizi haunted houses na mikasa ya kutisha kuhusu hizo nyumba zilizotawaliwa na ma roho /majini/ mapepo machafu. Na wengi wetu tumekua tukifikiria tu kuwa hizo ni hadithi na kamwe matukio kama hayo hayapo kwenye ulimwengu wetu.

Watu wengi wamejikuta wakipata mikosi kwenye maisha yao, nuksi kwa kuhamia , kupanga or kununua nyumba zilizofanyiwa mazindiko ya kishetani pasipo wao wenyewe kujua.

Unakuta mtu unapanga nyumba, ghafla mambo yako yanaanza kwenda hovyo, matatizo kazini, ndoa hakuna mawasiliano mazuri, mara ukiamka asubuhi unakuta umenyolewa nywele, mara unakua mvivu mvivu tu , biashara haiendi Sawa yani kila kitu kwako kinakua hovyo mwanzo mwisho , pesa zinakukimbia, marafiki hamna

Tuwe Makini sana na nyumba tunazohamia, Ni vizuri mtu kufanya spiritual cleansing before kuhamia kwenye nyumba za kupanga kila mtu kulingana na imani yake kama muislam, mkristo au mshirikina, kwa sababu hatujui hizo nyumba zimefanyiwa manuizi au matambiko na sisi bila kujua tunahamia tu , kwa vile nyumba iko masaki , mbezi beach tunaamini huko hakuna mambo ya kishirikina wakati wamiliki wengi wa hayo maeneo wanafuga majini kwa ajili ya kulinda mali zao , unajikuta mtu huna hili wala lile unahamia kwenye apartments hapo ndo unakua mwanzo wa mabalaa na nuksi katika maisha yako .
 
DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
14,302
2,000
Mtaani hapa kuna nyumba ilishashindikana kukalika, sasahivi naona majini ndio yanajitawala maana ikifika jioni yanawasha taa asubuhi yanazima.
Wabongo bhana

Usikute mwenye nyumba kafunga zake photocell, Nyumba Haina mtu

Kasafiri kaenda zake uko taa zinajiwasha usiku, asbh zinajizima.

Majirani mnazusha kua Kuna majini mle yanazima na kuwasha taa yenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Coolant

JF-Expert Member
Apr 19, 2015
980
1,000
Wabongo bhana

Usikute mwenye nyumba kafunga zake photocell, Nyumba Haina mtu

Kasafiri kaenda zake uko taa zinajiwasha usiku, asbh zinajizima.

Majirani mnazusha kua Kuna majini mle yanazima na kuwasha taa yenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app

Labda kwasababu sijaelezea mazingira na muonekano wa hiyo nyumba ndio maana naonekana kama mzushi tu😃

Nyumba yenyewe kwa nje ya geti imezungukwa na vichaka hadi njia ya kuingilia haionekani, ndani ya geti ni vichaka vitupu, vioo vya madidirisha vilishapasuka yani kiufupi ni kama gofu.
 
DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
14,302
2,000
Labda kwasababu sijaelezea mazingira na muonekano wa hiyo nyumba ndio maana naonekana kama mzushi tu

Nyumba yenyewe kwa nje ya geti imezungukwa na vichaka hadi njia ya kuingilia haionekani, ndani ya geti ni vichaka vitupu, vioo vya madidirisha vilishapasuka yani kiufupi ni kama gofu.
Haijalishi vichaka, Kama umeme upo Lazima taa zitawaka TU.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NIMEONA

JF-Expert Member
Aug 4, 2019
1,486
2,000
kuna rafiki yangu mmoja alihamia kwenye nyumba flani. usiku wa kwanza ulipita kwa kuzisikia sauti za nyingi mbweha.....walilia kwa muda mrefu hadi akazoea sauti na mwishowe kupata usingizi katika hali hiyo. ila mji huo hauna mbweha kabisaa, sijui walitoka wapi?!!

kama hiyo haitoshi, siku ya pili akaota anajisaidia haja kubwa (anakunya) pale kitandani lakini alipoamka akiangalia na kujikagua hakuna kitu. siku ya pili tena, ya tatu tena...

mh! akaona ngoja ajaribu kuwahadithia watu flani anaowaamini. alipowahadithia, wote alipowahadithia walimuangalia kwa mshangao na hofu flani bila kumueleza la maana. jamaa akaamza kuhisi hapo kutakuwa na issue za kuingiliana hapo; akatimua mbio.
 
Mgeni wa Jiji

JF-Expert Member
Jul 27, 2017
4,704

Hahah mwamba kanyanyaswa kijinsia
 
Mgeni wa Jiji

JF-Expert Member
Jul 27, 2017
4,704
2,000
Mikosi ni nini na nuksi ni nini na ipi tofauti baina ya maneno haya ?

Nuksi ni hali, mkosi ni tukio. Mfano mtu kakwambia hautarndesha tena gari huyo kakutia nuksi, sasa ukaendesha gari yako ukapata ajali ukakatika mikono yote. Huo ni mkosi.

Inshort Mkosi ni nuksi iliyo advance. Ina vi element vya laana na roho mbaya.

Laana zote ambazo hazijatimia ni Nuksi ila zinapotimia zinageuka mikosi
 
sala na kazi

JF-Expert Member
Aug 19, 2017
4,884
2,000
HUWEZI KUJUA KUWA DUNIA INA MAMBO MPAKA LIKUKUTE JAMBO........

Walimwengu ni zaidi ya unavyowaona au unavyowatazama.......

NB;
DUNIA MSONGAMANO.......
Maneno yako yamenigusa sana.

Kuna mikakati mingi huwa inafanywa usiku na mchana kwa watu lakini wenyewe hawajitambui

Kwenye hii dunia kama mtu kaamua kuwa upande wa nuru...akomae kweli kweli

Kama giza..basi na iwe hivyo
 
black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
17,745
2,000
Kwa kuwa kuna binadamu na majini kwa baadhi tunavyoamini
Kweli majini wapo kila sehemu na tunaishi nao
Pia wengine wanaamini kuna mizimu na kama wazungu wanaamini kuna Nafsi zilizouliwa kwenye baadhi ya nyumba

Mimi binafsi kuna hotel nililala lakini cha ajabu nilikuwa naona kila wakati kama kuna kitu kinakatisha pembeni yangu ( kimvuli)
Sikushtuka sana kwani napenda sana kukutana na mambo kama hayo na nafsi hizo
Nilijaribu kuongea nae bila kupata jibu, nikalala zangu
Ila haya mambo yapo sana na nikipata fursa ya kupata haunted house ntaenda nikaone
 
Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
24,543

Unaishi wapi tubadilishane vyumba kwa muda uliobaki hapa ninapoishi?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom