Haunted houses zipo, chukua hatua

Haunted houses zipo, chukua hatua

Kama bado ipo itabidi nije nimuone OTTAWA nifunge camera nione horror movie
Yaani natamani sana kuona mambo haya zaidi
Kuna wazungu kazi zao hizo kuzitafuta nyumba za hivyo na wanalala humo na wengine wanalipwa
sasa hiyo imeshashindikana, maana kuna wazungu walipanga humo, japo waliambiwa wao wakawa wabishi,
Unaambiwa walicharazwa bakora, na kulazimishwa waongee kiswahili

Siku ya pili mbna walihama wenyewe, chezea ndondocha weyeeeh.

Yaan hapa mbavu sina wallah, huyo OTTAWA kakimbila makambako sahivi ndo anakofanya shughuri zake, mweeeeh
 
Kwa hiyo wazungu wenyewe wamecharazwa na ukiherehere wao
Ndondocha balaaa
 
Mpwa....

Niliwahi kupanga Chumba maeneo fulani ya magomeni....ile nyumba ilikuwa na vyumba saba lakini wapangaji tuliokuwa tunajuana ni mimi na jamaa mmoja.....nilikaa pale miezi miwili pasi nakuonana na wapangaji wengine zaidi ya jamaa ninayekutana naye akiwa anatoka na kurudi kazini.....lakini kipindi chote shughuli zote za kuashiria kuwa vile vyumba wanaishi watu zilikuwa zinaendelea kama vile kupika na mazungumzo yaliyojaa vicheko vya hapa na pale.......lakini ukikaa koridoni huoni mtu......kilichonifanya nikimbie ile nyumba ilikuwa siku ya jumapili...nilichelewa kuamka....muda nilio amka nikachukua ndoo yangu kwenda bafuni kujimwagia....nikakuta bafuni kuna mtu anaoga kutokana na viashiria vya kumwagika kwa maji humo bafuni.....nikasema ngoja nisubirie tu hapa hapa kuliko kujisumbua kurudi chumbani kwangu......nilikaa karibu na mlango kabisa.....baada ya muda kadhaa kimya kikatawala mule bafuni kuashiria kwamba mtu ameshatoka sasa lakini atakuwa amepitia wapi......wakati naangaza macho kwenye korido nikaona kuna kandambili zimeloa kwenye moja ya ile milango ambayo sijawahi kuwaona watu wakiingia humo.....akili yangu ikaniambiaa kuwa kuna kitu hakipo sawa.....nikaingia bafuni nikaoga.....nikarudi chumbani kwangu nikavaa nikatoka......nilipokuwa mitaani nikamtafuta mtu mzima kidogo ambaye ni mwenyeji na kumdadisi kuhusu nyumba ile.....akaniambia ile nyumba ni nzito.....na inakaliwa na watu wazito......huo ndio ukawa mwisho wa mimi kukaa mule ndani na hata vyombo niliagiza watu wanileteee......
Basi mkuu na wewe ni mzito uliwezaje kuishi bila tabu 🤔
 
Aya mambo yapo..
Kuna jamaa nilimtembelea kwake na kulala..Usiku mara tukasikia watoto wanalia sebuleni..Jamaa akaniambia usiwe na wasiwasi hiyo nyumba ni kawaida.Siku ya pili mara nasikia nyumba kama vile inaelea juu ya maji.
Kuangalia nje kwenye kioo nikaona maji kama bahari aisee..
Jamaa nikamuuliza vipi..akasema ndiyo hivyo tupo safarini.
Kulipo kucha nikamwambia naondoka aisee nakumshauri atoke apo ...Jibu lake daah Eti akijaribu kuondoka apo basi atakua kichaa maana ndiyo alivyo ambiwa baada ya kusimuria kuhusu hiyo nyumba
 
Muongo huyo mchawi ni yeye mwenyewe, au uchawi wake ndo masharti yake hayo.
 
View attachment 1792138View attachment 1792139
Lambertville High School
Hii ni shule ipo USA ilifungwa kutokana na mauzauza.

View attachment 1792143View attachment 1792144
Yorktown Memorial Hospital ipo texas ulikuwa kama una tattoo ama umetoboa sehemu yeyote ya mwili wako ukiingioa humo hospital unakufa ukafungwa.

Tafta na hizi
ancient ram inn
Wicklow Gaol
chateau de chateaubriant

Sasa hapo jiulize kama kwa wazungu mwenye utajiri kuzidi hao wa masaki na oysterbay kuna haya mambo vipi kwa waafrika itakuweje?
Kama halijakufika ni bora unyamaze tu
Tatizo la maskin huwa wanajua pesa ni solution ya kila kitu kumbe wanajidanganya
 
Vitu hivi vipo sana sio stori za bla bla tu,majengo mengi ambayo ni magofu na yalikua yanatumika zipo sababu nyingi nyuma yake...na mengi huwa zinazo nafsi zizungukazo humo ndani na yote hiyo kuna sababu ndani yake.Kuna kipindi cha "the ghost asylum" huwa kinaonesha wanavyotafta hizo nafsi na kuongea nazo.Kinatisha kwakweli
 
HUWEZI KUJUA KUWA DUNIA INA MAMBO MPAKA LIKUKUTE JAMBO........

Walimwengu ni zaidi ya unavyowaona au unavyowatazama.......

NB;
DUNIA MSONGAMANO.......
Acha tu ndugu yangu. Yamenikuta. Sijui kama ni stage tu ya maisha nakumbana nayo au kuna mtu anajaribu kunikwamisha. Ila kama ni mtu ananikwamisha siku nitakuja kumgundua ataisoma namba!! Na naomba kama kuna mtaalamu yeyote anaeweza kunisaidia nipo tayari kutoa ushirikiano ila asiwe tapeli

Miaka kama mitatu hivi nilibahatika kupata kazi sehemu flani, kazi ilikuwa na maslahi kweli kweli na ukizingatia mimi nilikuwa bahili kweli kweli. Hela yangu ilikuwa hailiwi kizembe.

Nikawa pia nafanya kilimo, kilimo nacho kikawa kinanilipa kweli kweli. Hela ikanitembelea kweli kweli. Kila nikichungulia kwenye akaunti ikawa inanona vilivyo. Kabla nikiwa naenda likizo akaunti yangu ilikuwa inasoma 57M.

Kufika home kijiji cha kwanza nikamwambia mzee anionyeshe sehemu ya kujenga. Nikaanza chapu maana nilikuwa na likizo ya mwezi m1 tu.

Of course mimi napenda vitu quality. Nikaanza ujenzi wa nyumba ya ndoto zangu ambayo itakuwa ni ya familia yangu pia. Ni nyumba kubwa tu.

Likizo ilivyoisha tu nikarudi zangu mzigoni nyuma nikaacha ujenzi ukiendelea. Nikapaua, nikaweka dirisha na milango ya chuma, nikapiga plasta, wiring na plumbing. Ikawa gumzo pale kijiji. Bwana bwana bwana weee, ghafla mambo yakawa yamebadilika kwa speed ya 5G

Mara vuuup, nikafukuzwa kazi. Lakini akaunti yangu ikawa iko vizuri tu. Nikasema isiwe tabu. Nikasema suburi nifanye biashara pamoja na kuendelea na kilimo kama kawa. Cha kushangaza kila nikitia hela huko inafia huko hairudishi hata mtaji. Nikatia mzigo kwa mara nyingine safari hii nilipigwa hasara mpaka nikikumbuka natetemeka.

Ikawa najikingoja tu hivyo hivyo. Miezi 7 haikuisha 22M sijui zikivyokauka kauka na sasa nipo sina hata mia.

Bado sijakata tamaa, nipo napambana kutafuta chaka lingine maana kama elimu na mavyeti ninayo ya kutosha ila hili nuksi lililonijia sitakaa nilisahau kamwe.

Kimsingi roho hata hainiumi kwa vile kila nikiangalia mjengo wangu natabasamu najisemea kimoyomoyo "Asante Mungu" japokuwa haijaisha ila kwa umri wangu wa 30's nina imani nitapambana nikamilishe nyumba ya ndoto zangu kijijini kwanza ila sijui ni kwa namna gani maana kila nachofanya hakiendi.

Napitia wakati mgumu sana ndugu zangu. Niombeeni. Au nasema uongo ndugu zangu???

KAMA KUNA MTU YUKO NYUMA YA HILI NASEMA AJIANDAE, TENA NASEMA AJIANDAE KWELI KWELI. ONCE NITAKAPOMJUA, hiiiiiiiiiiiiiiii!!!!!!
 
Kujenga nyumba nzuri kijijini ili bidi ujiandae na Vita mapema
 
Back
Top Bottom