Haunted houses zipo, chukua hatua

Haunted houses zipo, chukua hatua

Kwa kuwa kuna binadamu na majini kwa baadhi tunavyoamini
Kweli majini wapo kila sehemu na tunaishi nao
Pia wengine wanaamini kuna mizimu na kama wazungu wanaamini kuna Nafsi zilizouliwa kwenye baadhi ya nyumba

Mimi binafsi kuna hotel nililala lakini cha ajabu nilikuwa naona kila wakati kama kuna kitu kinakatisha pembeni yangu ( kimvuli)
Sikushtuka sana kwani napenda sana kukutana na mambo kama hayo na nafsi hizo
Nilijaribu kuongea nae bila kupata jibu, nikalala zangu
Ila haya mambo yapo sana na nikipata fursa ya kupata haunted house ntaenda nikaone
Uliongea nayo vipi sasa
 
Acha ufala Mkuu .. eti “Nilijaribu kuongea naye bila kupata jibu”.

Binafsi hapa ninapokaa sipaelewi elewi yaani.! Juzi juzi nilichelewa kulala, ilikuwa mida ya saa nane hivi ndio nikaenda kulala basi na pembeni kwangu nikaweka PC juu ya kistuli cha pembeni mwa kitanda.! Nilizima taa, na ule mwanga wa PC nikauelekeza kwangu nanikaupunguza kidogo. Lengo nikuwa naangalia kuna kitu nilikuwa nakipakuwa.
Nikajilaza ubavu ubavu nikaelekeza kichwa upande wa Ukutani. Sasa wakati nangojea kasingizi .. macho makavu mara nikaona kivuli kama mtu amevalia nguo kajifunika kichwa amekatiza mbele ya Pc na kivuli chake nikakiona huku ukutani. Sikugeuka haraka haraka, nikawa nimevunga kama sijaona chochote nikarudisha kichwa pole pole kuangalia sikuona chochote. Niligeuza pc ika face away. Nikaomba kimoyo moyo siku hiyo ikapita.
Na pia hii Nyumba nakaa sijui ina nini, ila Mungu naamini ananitumiaga walinzi, kuna wakati nahisi kabisa kuna vitu mle ndani. Kwa mfano, Kila ninapokuwa nataka kuingia ndani hata kabla sijagusa kitasa utasikia Mlango umejitikisa as if mtu ameusukuma alfu ukiwa umefungwa. Kuna muda huwa ikafanya hivyo natamkaga *Fucccccck * basi tu kujikaza na nimezoea tu sio siku moja mara kwa mara yaani.

Hizi Nyumba hizi mmh acha tu, ila kikubwa uzima. Kama unaamka salama hakuna shida nikumshukuru Mungu
Mkuu kutikisika kwa mlango isije ikawa ni upepotu
 
Km kule kwetu Songea, kuna sehemu ipo nyumba ya mfanya biashara maarufu wa usafiri na nyinginezo, aitwae OTTAWA, Yaan hiyo imeshashindikana misukule yanavizia wapita njia jion jion hivi kuelekea giza,

Siku hiyo yakawavizia wanafunzi wa secondary, wacha yawakimbize had barabara kuu ya lami, ndo wakatoa taarifa kwa uongozi, OTTAWA akajibu "watu waache kupita maeneo Yale, litakalowakuta sihusiki" sehemu inatisha hiyo hatari, afu sasa bonge la jumba tena la kifahari.

Kama bado ipo itabidi nije nimuone OTTAWA nifunge camera nione horror movie
Yaani natamani sana kuona mambo haya zaidi
Kuna wazungu kazi zao hizo kuzitafuta nyumba za hivyo na wanalala humo na wengine wanalipwa
 
Wapo wanaojibu kwa makofi
Wengine wanavunja vyombo inategemea na mood zao
Hujawahi kuangalia hata vipindi vya Haunted house
Mkuu ninachouliza mimi uliongea nae vipi kwa ishara au ulitoa sauti au uliongea kimoyomoyo yani sio kuhusu majibu yao
 
Labda kwasababu sijaelezea mazingira na muonekano wa hiyo nyumba ndio maana naonekana kama mzushi tu

Nyumba yenyewe kwa nje ya geti imezungukwa na vichaka hadi njia ya kuingilia haionekani, ndani ya geti ni vichaka vitupu, vioo vya madidirisha vilishapasuka yani kiufupi ni kama gofu.
Hakuna myu anayelipia umeme?
 
Kwa kuwa kuna binadamu na majini kwa baadhi tunavyoamini
Kweli majini wapo kila sehemu na tunaishi nao
Pia wengine wanaamini kuna mizimu na kama wazungu wanaamini kuna Nafsi zilizouliwa kwenye baadhi ya nyumba

Mimi binafsi kuna hotel nililala lakini cha ajabu nilikuwa naona kila wakati kama kuna kitu kinakatisha pembeni yangu ( kimvuli)
Sikushtuka sana kwani napenda sana kukutana na mambo kama hayo na nafsi hizo
Nilijaribu kuongea nae bila kupata jibu, nikalala zangu
Ila haya mambo yapo sana na nikipata fursa ya kupata haunted house ntaenda nikaone
Nenda ukakutane na yenye popo bawa ulete mrejesho mkuu.
 
Hizo nyumba kule lushoto Tanga niliwahi ziona nyumba hazikaliwi na watu ziko ziko tu

Nikadadasi kwa watu vipi hizi nyumba mbona hazikaliwi na watu wakadai zina Mambo ya kimizimu humo ndani

Wanadai mwenye nyumba wakati anakufa hakuletwa ndani ya nyumba yake ndio yakatikea hayo
 
Hahaha

Ahsante Mkuu..Mungu atusaidie sana kwenye hii dunia tuishiyo,Iliyojaa wivu,chuki + malaana ya ajabu.

Hahaha

Ahsante Mkuu..Mungu atusaidie sana kwenye hii dunia tuishiyo,Iliyojaa wivu,chuki + malaana ya ajabu.
Siyo siri kiongozi, msaada Wa Mungu wahitajika haswaa! Dunia hii yastaajabisha mno.
 
Siyo siri kiongozi, msaada Wa Mungu wahitajika haswaa! Dunia hii yastaajabisha mno.
Hakika Mkuu.

Vita ya maombi ni silaha sana,angalau 1hr inasaidia...

Mtu akishazoea maombi Mungu anamuonyesha mambo kwa njia ya ndotoni tuu,kazi inakuwa ni jinsi ya kutafsiri.
 
Back
Top Bottom