Haunted houses zipo, chukua hatua

Haunted houses zipo, chukua hatua

Yalinikuta haya wakati nahamia kwangu, kila siku ya Mungu naota misiba huko nyumbani. Maisha yakawa magumu kupitiliza, pesa haikai mwisho wa siku wakaninyoa nywele pande mbili za kichwa. Nikaenda kunyoa zote. Zimeota tena kidogo wakaninyoa tena, ilibidi niende kwa wazazi kupumzisha akili yangu pamoja na kupata ushauri wa nini nifanye,.
Hukuiombea hiyo nyumba yako Wakati unahamia?

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Hukuiombea hiyo nyumba yako Wakati unahamia?

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app

Mmh Mwenzangu unakuta mtu ushapata pesa ya kikoba tena presha juu juu hayo mambo Hata ufikirii unachojali ni kulipa kodi tu mambo yaende, baadae ndo unakuja kujua kumbe umeyavaa
 
Daah kweli dunia ina mambo asee kama hujawah ona haimaanishi ndo hamna sie uku kwetu ilishawah tokea ishu moja miaka ya 2012 nyumba ilikuwa inatema ela za noti tuu mda wote na apo mwanzo haikuwa ilikaliwa na mtu kwa muda yaan kama watu walikimbia vile
 
Daah kweli dunia ina mambo asee kama hujawah ona haimaanishi ndo hamna sie uku kwetu ilishawah tokea ishu moja miaka ya 2012 nyumba ilikuwa inatema ela za noti tuu mda wote na apo mwanzo haikuwa ilikaliwa na mtu kwa muda yaan kama watu walikimbia vile
Haaaaa Haaaaa 😂 sasa si mngekuwa mnachukua hizo pesa aisee
 
Same applied kwangu, aliyeniuzia eneo alitaka nigeuzia kibao, baadae maneno yakatoka kwamba anasema haiwezekani watu wa kuja waje wafanye maendeleo kwenye mji wao, kwangu amelegeza sasa kilio kwa majirani na kila mmoja ananyoosha kidole kwake
Haaaaa Haaaaa 😂 Yan jamani Yan ndo hivo hivo kama wangu huyu, mbaya zaidi Nipo nae jirani kabisa Yan nyumba zinakaribiana. Nacheka nae kwa akili kwa sababu nshagundua ubaya yake
 
Maneno yako yamenigusa sana.

Kuna mikakati mingi huwa inafanywa usiku na mchana kwa watu lakini wenyewe hawajitambui

Kwenye hii dunia kama mtu kaamua kuwa upande wa nuru...akomae kweli kweli

Kama giza..basi na iwe hivyo
'.....akomae kweli kweli'

'....basi na iwe hivyo'

umeandika kiufundi kweli hapo!!
 
Funguka mkuu, binadamu wakoje??

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Mpwa....

Niliwahi kupanga Chumba maeneo fulani ya magomeni....ile nyumba ilikuwa na vyumba saba lakini wapangaji tuliokuwa tunajuana ni mimi na jamaa mmoja.....nilikaa pale miezi miwili pasi nakuonana na wapangaji wengine zaidi ya jamaa ninayekutana naye akiwa anatoka na kurudi kazini.....lakini kipindi chote shughuli zote za kuashiria kuwa vile vyumba wanaishi watu zilikuwa zinaendelea kama vile kupika na mazungumzo yaliyojaa vicheko vya hapa na pale.......lakini ukikaa koridoni huoni mtu......kilichonifanya nikimbie ile nyumba ilikuwa siku ya jumapili...nilichelewa kuamka....muda nilio amka nikachukua ndoo yangu kwenda bafuni kujimwagia....nikakuta bafuni kuna mtu anaoga kutokana na viashiria vya kumwagika kwa maji humo bafuni.....nikasema ngoja nisubirie tu hapa hapa kuliko kujisumbua kurudi chumbani kwangu......nilikaa karibu na mlango kabisa.....baada ya muda kadhaa kimya kikatawala mule bafuni kuashiria kwamba mtu ameshatoka sasa lakini atakuwa amepitia wapi......wakati naangaza macho kwenye korido nikaona kuna kandambili zimeloa kwenye moja ya ile milango ambayo sijawahi kuwaona watu wakiingia humo.....akili yangu ikaniambiaa kuwa kuna kitu hakipo sawa.....nikaingia bafuni nikaoga.....nikarudi chumbani kwangu nikavaa nikatoka......nilipokuwa mitaani nikamtafuta mtu mzima kidogo ambaye ni mwenyeji na kumdadisi kuhusu nyumba ile.....akaniambia ile nyumba ni nzito.....na inakaliwa na watu wazito......huo ndio ukawa mwisho wa mimi kukaa mule ndani na hata vyombo niliagiza watu wanileteee......
 
Kwa kuwa kuna binadamu na majini kwa baadhi tunavyoamini
Kweli majini wapo kila sehemu na tunaishi nao
Pia wengine wanaamini kuna mizimu na kama wazungu wanaamini kuna Nafsi zilizouliwa kwenye baadhi ya nyumba

Mimi binafsi kuna hotel nililala lakini cha ajabu nilikuwa naona kila wakati kama kuna kitu kinakatisha pembeni yangu ( kimvuli)
Sikushtuka sana kwani napenda sana kukutana na mambo kama hayo na nafsi hizo
Nilijaribu kuongea nae bila kupata jibu, nikalala zangu
Ila haya mambo yapo sana na nikipata fursa ya kupata haunted house ntaenda nikaone
Hayo mambo yaskie tu,
Niliishi nyumba moja maeneo ya airport dodoma,sitosahau tuliyokua tunashuhudia,
Kubwa zaid tukahamia nyumba iliyokua haiishi mtu kwa kitambo kirefu maili mbili ikawa changamoto mno, mauza uza kila kukicha
 
Back
Top Bottom