Haunted houses zipo, chukua hatua

Haunted houses zipo, chukua hatua

'.....akomae kweli kweli'

'....basi na iwe hivyo'

umeandika kiufundi kweli hapo!!
Hahaha

Ahsante Mkuu..Mungu atusaidie sana kwenye hii dunia tuishiyo,Iliyojaa wivu,chuki + malaana ya ajabu.
 
Mtaani hapa kuna nyumba ilishashindikana kukalika, sasahivi naona majini ndio yanajitawala maana ikifika jioni yanawasha taa asubuhi yanazima.

Hiyo wameweka zile taa za kujizima zenyewe na kujiwasha zenyewe
 
Labda kwasababu sijaelezea mazingira na muonekano wa hiyo nyumba ndio maana naonekana kama mzushi tu

Nyumba yenyewe kwa nje ya geti imezungukwa na vichaka hadi njia ya kuingilia haionekani, ndani ya geti ni vichaka vitupu, vioo vya madidirisha vilishapasuka yani kiufupi ni kama gofu.
Hiyo nyumba ipo nansio?
 
Wabongo bhana

Usikute mwenye nyumba kafunga zake photocell, Nyumba Haina mtu

Kasafiri kaenda zake uko taa zinajiwasha usiku, asbh zinajizima.

Majirani mnazusha kua Kuna majini mle yanazima na kuwasha taa yenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
Jirani kwetu kulikuwa na nyumba. Mke akafariki kwa kuwa nyumba ilikua ya mwanamke na mwanaume alikua na mke mwingine akaicha akaenda kuishi kwenye nyumba yake nyingine. Pale wakatafuta mtu wa kupanga ikashindikana wakawa wanakaa kaa tu watu (ndugu zao) basi wakawa hawamalizi muda wanahama.

Baadae wana mtaa wakaja na story kuwa yule mama kachukuliwa msukule na mume wake kawekwa kwenye chumba kimoja mule ndani kwahiyo usiku anawachapa watu viboko wanaolala kwenye nyumba yake.

binadamu na mambo yetu.
 
Hayo mambo yaskie tu,
Niliishi nyumba moja maeneo ya airport dodoma,sitosahau tuliyokua tunashuhudia,
Kubwa zaid tukahamia nyumba iliyokua haiishi mtu kwa kitambo kirefu maili mbili ikawa changamoto mno, mauza uza kila kukicha

Tuhadithie kidogo mkuu walikuwa wanafanya nini?
Kama kupigwa ndio mbaya zaidi lakini kubamiza milango ni kawaida sana
Ila sasa watu nao wabaya sana na tamaa zao
Yaani nyumba ina matatizo bado unasukumiwa tu
 
Yalinikuta haya wakati nahamia kwangu, kila siku ya Mungu naota misiba huko nyumbani. Maisha yakawa magumu kupitiliza, pesa haikai mwisho wa siku wakaninyoa nywele pande mbili za kichwa. Nikaenda kunyoa zote. Zimeota tena kidogo wakaninyoa tena, ilibidi niende kwa wazazi kupumzisha akili yangu pamoja na kupata ushauri wa nini nifanye,.
walikupa ushauri ufanye nn?
 
Labda kwasababu sijaelezea mazingira na muonekano wa hiyo nyumba ndio maana naonekana kama mzushi tu😃

Nyumba yenyewe kwa nje ya geti imezungukwa na vichaka hadi njia ya kuingilia haionekani, ndani ya geti ni vichaka vitupu, vioo vya madidirisha vilishapasuka yani kiufupi ni kama gofu.
Tuma picha
 
Tuhadithie kidogo mkuu walikuwa wanafanya nini?
Kama kupigwa ndio mbaya zaidi lakini kubamiza milango ni kawaida sana
Ila sasa watu nao wabaya sana na tamaa zao
Yaani nyumba ina matatizo bado unasukumiwa tu
Kifupi ilikua kila usiku kuna ndege analia katika gutter za kushusha maji ya mvua,na ukitoka nje kuangalia mlio unapotea ukirudi ndani mlio unaendelea na katika wiki lazima upatikane mzoga wa kuku ama ndege na wote walikua weusi,kingine ni kusikika kishindo cha mtu kutembea katika korido pasipo kuonekana na ukijaribu kutoka utasikia kishindo kikikimbia na ukimya utatawala.
Dada pekee ndiye alikua muathirika mkubwa wa haya mambo,alikua mweupe mno peke yake katika nyumba na alikua akiamka na majeraha ya kukatwa na kitu mfano wa kisu butu ama kinachokata kwa shida mara kwa mara,aliamua kuondoka baada ya kuandamwa sana na sisi wengine hatukuendelea kuishi hapo baada ya dada kuondoka .
 
Duu poleni sana now this is real
 
Sijui why leo nipo kwenye mood ya kuongelea hii Topic , I hope itagusa watu na kuwasaidia kuchukua hatua. Mara nyingi tumekua tukiangalia Film’s za kutisha huko Hollywood kuhusu hizi haunted houses na mikasa ya kutisha kuhusu hizo nyumba zilizotawaliwa na ma roho /majini/ mapepo machafu. Na wengi wetu tumekua tukifikiria tu kuwa hizo ni hadithi na kamwe matukio kama hayo hayapo kwenye ulimwengu wetu.

Watu wengi wamejikuta wakipata mikosi kwenye maisha yao, nuksi kwa kuhamia , kupanga or kununua nyumba zilizofanyiwa mazindiko ya kishetani pasipo wao wenyewe kujua.

Unakuta mtu unapanga nyumba, ghafla mambo yako yanaanza kwenda hovyo, matatizo kazini, ndoa hakuna mawasiliano mazuri, mara ukiamka asubuhi unakuta umenyolewa nywele, mara unakua mvivu mvivu tu , biashara haiendi Sawa yani kila kitu kwako kinakua hovyo mwanzo mwisho , pesa zinakukimbia, marafiki hamna

Tuwe Makini sana na nyumba tunazohamia, Ni vizuri mtu kufanya spiritual cleansing before kuhamia kwenye nyumba za kupanga kila mtu kulingana na imani yake kama muislam, mkristo au mshirikina, kwa sababu hatujui hizo nyumba zimefanyiwa manuizi au matambiko na sisi bila kujua tunahamia tu , kwa vile nyumba iko masaki , mbezi beach tunaamini huko hakuna mambo ya kishirikina wakati wamiliki wengi wa hayo maeneo wanafuga majini kwa ajili ya kulinda mali zao , unajikuta mtu huna hili wala lile unahamia kwenye apartments hapo ndo unakua mwanzo wa mabalaa na nuksi katika maisha yako .
Asante sana brother. I can relate
 
Km kule kwetu Songea, kuna sehemu ipo nyumba ya mfanya biashara maarufu wa usafiri na nyinginezo, aitwae OTTAWA, Yaan hiyo imeshashindikana misukule yanavizia wapita njia jion jion hivi kuelekea giza,

Siku hiyo yakawavizia wanafunzi wa secondary, wacha yawakimbize had barabara kuu ya lami, ndo wakatoa taarifa kwa uongozi, OTTAWA akajibu "watu waache kupita maeneo Yale, litakalowakuta sihusiki" sehemu inatisha hiyo hatari, afu sasa bonge la jumba tena la kifahari.
 
Mpwa....

Niliwahi kupanga Chumba maeneo fulani ya magomeni....ile nyumba ilikuwa na vyumba saba lakini wapangaji tuliokuwa tunajuana ni mimi na jamaa mmoja.....nilikaa pale miezi miwili pasi nakuonana na wapangaji wengine zaidi ya jamaa ninayekutana naye akiwa anatoka na kurudi kazini.....lakini kipindi chote shughuli zote za kuashiria kuwa vile vyumba wanaishi watu zilikuwa zinaendelea kama vile kupika na mazungumzo yaliyojaa vicheko vya hapa na pale.......lakini ukikaa koridoni huoni mtu......kilichonifanya nikimbie ile nyumba ilikuwa siku ya jumapili...nilichelewa kuamka....muda nilio amka nikachukua ndoo yangu kwenda bafuni kujimwagia....nikakuta bafuni kuna mtu anaoga kutokana na viashiria vya kumwagika kwa maji humo bafuni.....nikasema ngoja nisubirie tu hapa hapa kuliko kujisumbua kurudi chumbani kwangu......nilikaa karibu na mlango kabisa.....baada ya muda kadhaa kimya kikatawala mule bafuni kuashiria kwamba mtu ameshatoka sasa lakini atakuwa amepitia wapi......wakati naangaza macho kwenye korido nikaona kuna kandambili zimeloa kwenye moja ya ile milango ambayo sijawahi kuwaona watu wakiingia humo.....akili yangu ikaniambiaa kuwa kuna kitu hakipo sawa.....nikaingia bafuni nikaoga.....nikarudi chumbani kwangu nikavaa nikatoka......nilipokuwa mitaani nikamtafuta mtu mzima kidogo ambaye ni mwenyeji na kumdadisi kuhusu nyumba ile.....akaniambia ile nyumba ni nzito.....na inakaliwa na watu wazito......huo ndio ukawa mwisho wa mimi kukaa mule ndani na hata vyombo niliagiza watu wanileteee......
 
Jirani kwetu kulikuwa na nyumba. Mke akafariki kwa kuwa nyumba ilikua ya mwanamke na mwanaume alikua na mke mwingine akaicha akaenda kuishi kwenye nyumba yake nyingine. Pale wakatafuta mtu wa kupanga ikashindikana wakawa wanakaa kaa tu watu (ndugu zao) basi wakawa hawamalizi muda wanahama.

Baadae wana mtaa wakaja na story kuwa yule mama kachukuliwa msukule na mume wake kawekwa kwenye chumba kimoja mule ndani kwahiyo usiku anawachapa watu viboko wanaolala kwenye nyumba yake.

binadamu na mambo yetu.
ipo hiyo sana tyuuh
 
Back
Top Bottom