Tindo
Platinum Member
- Sep 28, 2011
- 71,871
- 128,949
Hivi nini tofauti ya hao unaosema aliagiza wafungwe na kufungwa Freeman muda wote aliokaa gerezani..kwa hiyo aliyewafunga hao unaosema alikosea ila aliyemfunga Mbowe alikuwa sawa..halafu usiongee km kuku amekatwa kichwa, makada gani unaowajua wewe walipaswa wawe kifungoni lakin haikuwa hivyo, usiongee jumla jumla..taja mifano, hakuna anayetetea uovu tunalazimika kuwasaidia juu ya lawama mnazotoa zisizo na msingi au kuleta majibu.
Rugemalila na Kalasinga Seth waliwekwa ndani kwa tuhuma ya fedha za Escrow, nitajie watu wa CCM/serekali walioshirikiana nao kwenye hiyo kashfa waliowekwa nao ndani.
Baada ya kutoka ripoti ya kina profesa Ossoro kuhusu mikataba ya madini, Andrew Chenge, Nadhiri Karamagi, Daniel Yona walitajwa kwa majina, na ripoti ikataka wakamatwe. Na Magufuli akaagiza wakamatwe, mbona hakuna hata mmoja alikamatwa au kusumbuliwa?
Magufuli aliamua kuwekeza kwenye miradi wa maji baada ya kusema kubwa gas sio yetu maana imeuzwa. Mbona hakuwachukulia hatua waliouza hiyo gas yetu. Njoo na majibu haraka ili usiendelee kunipotezea muda kwa kutetea kiongozi muovu.