CHAMA kipya cha Alliance for Change and
Transparency (ACT-Tanzania) sasa kimetinga
mahakamani.
Lucas Kadavi Limbu, mmoja wa waasisi na
mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, amefungua
shauri Na. 17 la mwaka 2015 dhidi ya Samson
Mwigamba ambaye ni katibu mkuu wa muda na
Peter Mwambuja na Masange M. Masange.
Katika shauri hilo la madai, lililofunguliwa
Mahakama Kuu, kanda ya Dar es Salaam, Limbu
anataka mahakama itoe amri ya kumzuia
Mwigamba na âmawakala wake,â kujihusisha na
chama hicho; kukiongelea katika vyombo vya
habari na kutoa maelekezo yoyote yale kwa
wanachama na viongozi wake.
Wadai wengine katika shauri hilo, ni naibu katibu
mkuu (Bara); Grason Nyakarungu, katibu mwenezi
na mwenyekiti wa vijana taifa; na Ramadhani
Suleiman, makamu mwenyekiti (Zanzibar).
Kesi hii imetajwa kwa mara ya kwanza leo na
imepangwa kusikilizwa tarehe 25 Machi mwaka
huu, ambako mahakama itasikiliza maombi ya
kuzuia mkutano mkuu wa chama.
Kabla ya kujiunga na ACT-Tanzania, Mwigamba
alikuwa mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (Chadema), mkoa wa Arusha.
Alifukuzwa uanachama mwaka mmoja uliopita.