Sasa jamni ebu twende mbele turudi nyuma na kuchambua maswala badala ya kushabikia. Huyu mwenyekiti wa ACT Limbu yeye kuwa mwenyekiti ndio inampa madaraka ya kuwafukuza wanachama? Yaani unamfukuza madakani Katibu mkuu kwa sababu zako ati chama hakimtambui ilihali maamuzi hayo umeyafanya wewe na baadhi ya watu kwa kuhofia nafasi hiyo pengine itachukuliwa na Zitto na hivyo wewe umewekwa kama Kioo tu. Chama kinazinduliwa rasmi tarehe 25 ni wanachama gani hao walokaa na kufikia maamuzi haya!
Kisha basi mikutano yote tujuavyo huandaliwa na katibu mkuu, iweje leo mwenyekiti uanze kuweka madai hadi makahamani ikiwa hayajapitia vikao vya chama maana chama ni wanachama na ndio watakao amua. Kwa kwenda mahakamani Je, ina maana madai yako yamekataliwa ndani ya Chama. Na iweje chama hiki kinazinduliwa rasmi tarehe 25 na ndio siku ambayo mahakama pia inataka kuskiliza kesi yako! Ama kweli cheo sio dhamana watu wakipewa cheo hukitumia kama wamekirithi.
Kwa sisi wenye kuona mbali tunajua fika kwamba kuna mkono wa Mtu na haiwezekani ghafla baada ya kusikia Zitto kajiunga na ACT tayari umekimbilia mahakamani wakati kuna kikao cha kwanza cha chama tarehe 25, siku ambayo ungewakilisha hoja yako na wanachama wote wakaisikiliza. Mbona hii inaonekana kama ni marudio ya sinema ya Chadema.. Ama kweli siasa za Bongo kiboko!..