Mi huwa napenda sana kuona mambo kama haya kwa jicho la taswira.
Wazungu wanaovyoona tunabana sana watakuja na story nyingi sana za kutuyumbisha tena kwa kutumia watu wa ndani kama huyu mkurugenzi wa NIMR .
Labda kama mtu hatamuelewa kwa sasa Rais Dr.Magufuli, ila tutaelewa baadaye sana kwa kuona matokeo ya kazi yake.
Ukiangalia mipango ya Tanzania sasa hivi kama ikitekelezeka vizuri bila kikwazo uchumi wetu utapaa sana, mfano. chukulia pana ndege za Tanzania zikaanzisha safari kwenda nchi ambazo hazina safari za mashirika mengine na hapa Tanzania na sehemu zingine ambako hazifiki, tutakamata soko hilo jambo hilo ni kikwazo kwa wazungu katika mipango yao ya akina fastjet.
Pia, viwanda vikakua kwa kasi hapa Tanzania ni wazi kuwa nchi zingine za EAC na SADC zitategemea bidhaa kutoka kwetu, ila sasa wanataka kutuyumbisha ili tupoteze mwelekeo huo wa kiuchumi na kuanza kushughulikia ZIKA.
Pia, mtu yeyote ajue kuwa kuonekana ZIKA nchini kama taarifa ya NIMR ilivyoletwa inaonesha hali ya hatari hivyo utalii na baadhi ya mipango yetu na mataifa ya nje mingi itakwama kutekelezwa hapa nchini kwa hofu hiyo.
Tena, nchi kupitia mamlaka husika wanatakiwa kutangaza hali ya hatari jambo ambalo ni changamoto kwa mipango yetu.
Mfano wa kwanza ni, BRAZIL na ZIKA ; wazungu ni wanafiki sana, kuhusu ZIKA pale Brazil, kwa Brazil jambo halikuwa ZIKA wala Mbu wa ZIKA tatizo lilikuwa Brazil kupata michezo ya olimpiki wote wenye akili walielewa kuwa kuna mataifa makubwa ""wanaojiita nchi za dunia ya Kwanza"" hawakutaka na kupenda kuona Brazil kupata hiyo nafasi ya kuandaa olimpiki, waliitumia zika ili hata kupunguza watakao shiriki ili makadilio ya billioni za mapato zipotee ili Brazil ipate hasara na kufilisika kutokana na maandalizi yale kutumika pesa nyingi na ukumbuke kuwa Brazil iko katika BRICS na wazungu wanona inavyopiga hatua kimaendeleo sasa janga linatengenezwa ; USA, NA Ulaya wako nyuma ya hilo.
Mfano, mwingine ni ugonjwa wa Ebola pale Afrika ya Magharibi, ugonjwa umeua wengi sana na kuwatesa ila tatizo ni dogo sana ni pale walipokuwa na maandalizi ya kuwa na ushirikiano wa sarafu moja (common currency ) na kuzuia matumizi ya dollar, pound na euro katika shughuli zao zote za kiuchumi , sasa ili wawaharibie wakatibua mipango hiyo kwa kuleta ebola ili kila mtu aangalie nchi yake na hilo likafa kabisa hadi leo hakuna anayesema tena kuhusu sarafu. Hapa USA, na Ulaya wamo tena.
Mfano, Rwanda, budget yake wanahitaji wamepiga hatua hii ya kujiwezesha kwa 66% ila 34% tu ni misaada na juzi Rais wao kasema anahitaji kufuta kabisa utegemezi katika budget, sasa hapo utaona povu la wanzugu litakavyowatoka.
Utaona kila kukicha IMF na World Bank [WB] hawaishi kuwashawishi kuchukua mikopo na misaada.
Rwanda moots deadline to end aid dependency
Sasa ukitathimini vizuri ukiangalia mipango yetu kama Tanzania, pia ikitekelezwa hapo pa misaada na utegemezi tutausikia kwa majirani zetu wengine na nchi zingine na hilo ndilo wazungu hawataki kuona likiondoka katika akili zetu na nchi zetu hizi za kiafrika.
Pia unaweza tafuta kitabu hiki usome juu ya mipango ya kujikwamua na papo hapo mwandishi kaonesha mipango inayotumika na wazungu ili kukwamisha nchi za Afrika na Tanzania ikiwemo.
Mwandishi ni A. M. BABU . "AN ECONOMIC STRATEGY FOR THE SECOND LIBERATION OF AFRICA".
Ndani ya kitabu hiki utaelewa ni namna gani Rais Dr. Magufuli yuko makini na kama akiendelea hivi tutafika pazuri sana kama nchi.
Ahsanteni sana.