Hatimaye ZIKA Tanzania ndani ya CCTV

Hatimaye ZIKA Tanzania ndani ya CCTV

Kukurupuka ni kufanya maamuzi kienyeji na yasiyo na tija kwa taifa kwa mfano kuna mtaalamu aliyesomea maswala ya uchunguzi wa binadamu anaondolewa kwenye taasisi nyeti ya uchunguzi wa magonjwa ya binadaamu analetwa mtaalamu wa mambo ya samaki wa kwenye viboksi vya vioo na mtu huyo tayari mchaguwa na mtenguwa alishambalasa na kumpa kila neon baya huko alikotokea na kuuthibitishia umma kwamba hafai kuongoza taasisi yeyote , je maamuzi kama hayo yana tija kwa nchi ndipo watanzania tunasema mtoa maamuzi ni mkurupukaji aliyelewa madaraka asiyejielewa na mwenye maono mafupi
Bado huyu mnayemuita mkurupukaji ambaye hufanya maamuzi ya kizalendo tena mara nyingi tu kuliko wale wanamtandao ambao kundi moja la marafiki lilipokuwa njiani kuondoka likataka liache mjengo mweupe kwa kundi jingine la watoto wa mjini wapigaji wa kimataifa.

Bora huyu aliyewatumbua watu wa mishahara hewa na dili nyingine chafu kuliko nchi kuuziwa mbuzi kwenye gunia.
 
kwa kweli hao siwajuwi namjuwa mkurupukaji aliyeko ikulu kwa sasa ambaye anaharibu siha Amani uwezo wa watu wakufikiri na ujasiri wa mawasiliano anayebaguwa watu kwa kanda ambaye ameshindwa kupandisha pato la taifa ambaye ameharibu utendaji wa kawaida wa mfumo wa umma ,sekta za kibiashara na mfumo wa watu binafsi, ambaye anadhani yuu juu ya sheria na katiba ya nchi na kwamba Mungu sio yule wa kuabudiwa bali yeye ndio mwenye uwezo.Namzungumzia kwa sababu fedha yangu ninayoipata kwa jesho jingi sana ndio inamfanya avae ale alale ikulu hao wengine utajijuwa wewe na wao
 
Rais anapofanya maamuzi watu mnakurupuka na kumsimanga kwa kila aina ya kejeli na matusi. Watanzania hatuna tabia kufikiria mbeleni inakuwaje. Ipo siku mtamuelewa Mh. Rais anachokifanya kwamba si kwa maslahi yake binafsi bali ni kwa maslahi ya taifa nawatanzania wote.
Nashindwa kuelewa mnachopinga ni mini?wakati wataalam wanasema ugonjwa upo.hata hyo report angepewa magufuli kwanza.ndo ingezuia huo ugonjwa usiwepo?
 
Ugonjwa upo mnaambiwa ukweli mnafukuza aliyefanya utafili huu ujinga
 
Kama ugonjwa wa ZIKA haupo tanzania
tushukuru Mungu,maana kama kweli
ungekuwepo sijui kungetokea nini
Kipindupindu bado kinaua watu sembuse ZIKA?
Huyo DR.kama alisema ukweli Mungu atampa kazi nyingine.

Kutumbuliwa si mwisho wa maisha,
Naomba tu,tuambiwe namna ya kujikinga
na huo ugonjwa endapo utafika
badala ya kuishia kubishana,mabishano hayatatusaidia.
 
Kwa SIZONJE ni kosa Lkn Dr. Yupo sahihi kabisaa. Shida inabaki kwenu nyie mazombi[emoji83] mnaoona SIZONJE yuko sawa
Hivi utafiti ulikuwa na kipengele cha malengo mahsusi kuwa NIMR itangaze matokeo ya utafiti hadharani? Maana kutangaza ugonjwa hadharani kunaweza kufanyika ikiwa ni mkakati wa ufumbuzi wa kupatikana kwa tiba/chanjo ya kutokomeza ugonjwa husika. Mara nyingi tafiti nyingi za magonjwa/afya ya umma hufanyika na matokeo yake hayatangazwi ila mbinu na mikakati ya kupata ufumbuzi hufanyika na magonjwa kushughulikiwa.
 
Hata kama kuna dalili za Virus wa ZIKA ndo utangaze wewe?

huyu Dr. Mwele sijui la wapi hili?

halafu, linakomaa kwenye media eti, "Tukubali tusikubali, ZIKA ipo Tanzania"... hivi hiyo ni language ya kutoa taarifa kweli?

Yaan sijui likoje, Sasa kapata faida gani kutuchafulia nchi yetu?

Hivi kama mkeo ana tatizo au mumeo ana tatizo, utaanza kulitangaza tu hovyo hovyo bila mashauriano ya ndani?
Humu hadi mapunga yamo
 
kwa kweli hao siwajuwi namjuwa mkurupukaji aliyeko ikulu kwa sasa ambaye anaharibu siha Amani uwezo wa watu wakufikiri na ujasiri wa mawasiliano anayebaguwa watu kwa kanda ambaye ameshindwa kupandisha pato la taifa ambaye ameharibu utendaji wa kawaida wa mfumo wa umma ,sekta za kibiashara na mfumo wa watu binafsi, ambaye anadhani yuu juu ya sheria na katiba ya nchi na kwamba Mungu sio yule wa kuabudiwa bali yeye ndio mwenye uwezo.Namzungumzia kwa sababu fedha yangu ninayoipata kwa jesho jingi sana ndio inamfanya avae ale alale ikulu hao wengine utajijuwa wewe na wao
Mkuu pole sana, hayo ndio mnayoyaongea mnapokuwa mmekaa kijiweni kwenu!!.

Ni lazima reforms ziwe na maumivu. Huo unaouita kukurupuka ndio dawa ya mentality za kivivu za kitanzania.

Ni suala la muda tu na anachokifanya sasa hivi kitakuwa kimeeleweka. Dawa inapoendelea kuingia kweye damu ndivyo ugonjwa unavyozidi kutoka mwilini.
 
Hivi utafiti ulikuwa na kipengele cha malengo mahsusi kuwa NIMR itangaze matokeo ya utafiti hadharani? Maana kutangaza ugonjwa hadharani kunaweza kufanyika ikiwa ni mkakati wa ufumbuzi wa kupatikana kwa tiba/chanjo ya kutokomeza ugonjwa husika. Mara nyingi tafiti nyingi za magonjwa/afya ya umma hufanyika na matokeo yake hayatangazwi ila mbinu na mikakati ya kupata ufumbuzi hufanyika na magonjwa kushughulikiwa.
Hayo mambo ya kimya kimya ndo sisi hatuyataki.
 
IPO siku itakuja kutokea Ebola.alafu watapiga kimya.kuja kutangaza hali ishakuwa mbaya.huu ujinga wanaofanya ndo maana kipindu pindu uwa kinauwa sana.uwa najiuliza inakuwaje kipindu pindu.kinaenea kwa kwa nguvu sehemu kubwa?kumbe inawezekana dalili waliziona ila wamepiga kimya.wanataka wauzuie kimya kimya.wakiona wameshindwa ndo wanatangaza.wakati huo ni majanga.
 
Hayo mambo ya kimya kimya ndo sisi hatuyataki.
wewe na hao wenzako hamjui chochote katika practice ya public health ethics. Mnadhani kula kitu kinaendeshwa kwa empty politics! Hapana sivyo!
 
Bado huyu mnayemuita mkurupukaji ambaye hufanya maamuzi ya kizalendo tena mara nyingi tu kuliko wale wanamtandao ambao kundi moja la marafiki lilipokuwa njiani kuondoka likataka liache mjengo mweupe kwa kundi jingine la watoto wa mjini wapigaji wa kimataifa.

Bora huyu aliyewatumbua watu wa mishahara hewa na dili nyingine chafu kuliko nchi kuuziwa mbuzi kwenye gunia.

..mkulu amekosea kumtimua kazi Dr.Mwele.

..matokeo ya uamuzi huo yamesababisha habari hii kuwa kubwa zaidi.

..sasa itaonekana kwamba Tz kuna zika lakini serikali iko ktk denial and
cover up.

..
 
Kama ultaka kuleta taarifa, ungeleta kilichosemwa kwenye taarifa hiyo na sio kutuletea picha yenye heading bila kujua maudhui.

Kwa kifupi hujaleta habari. Ila umeleta umbea ndio nkwambia umefurahi sana.
Huwa sijadiliani na watu wanaopenda ligi,mjadala unafahamika,habari inaonekana kuwa kati ya Watz 535 waliochukuliwa sample za vipimo vya virusi vya Zika,80 wameathirika,na kati ya hao,30 ni watoto wameonekana kuathirika na ugonjwa huu.

Kwamba taarifa hii ni "Habari" kwa sbb sasa imevuka mipaka ya nchi na kulipotiwa na chombo kikubwa kama CCTV...Haikuhitaji "nyama" kwa sbb wenye uelewa wameelewa ndio maana unaona wanajadili.Siku zote hata darasani sio wote huwa wanamuelewa mwalimu kwa wakati mmoja...Wengine huenda taratibu

Hilo la "umbea" sio jadi yangu;wanaolewa na tunaojadiliana humu JF wanajua kuwa mimi si "mbea"...Sitaki kwenda huko,maana tutatoka kwenye mjadala
 
..mkulu amekosea kumtimua kazi Dr.Mwele.

..matokeo ya uamuzi huo yamesababisha habari hii kuwa kubwa zaidi.

..sasa itaonekana kwamba Tz kuna zika lakini serikali iko ktk denial and
cover up.

..
Hii habari haihusiani na watu wawili tu yaani Mkulu na Dr Mwele. Hapo kuna wizara ya afya inaingia pia. Hakuna coordination kati ya wahusika wote wa issue hii.

Kama ingekuwepo hali isingefikia ilipofika. Halafu yapo ambayo mimi na wewe hatuyajui.

Wanachokosea wajuaji wengi hapa Jamii Forum ni kusahau kwamba taarifa zote nyeti za nchi hii ni lazima zimfikie mkulu kwanza kabla ya yoyote mwingine. Utendaji wa jengo jeupe upo kimfumo zaidi sio kama ni jengo lisilokuwa na muelekeo kama watu wengi wanavyodhania.
 
Phillipo Bukililo,

..i agree with u.

..kwamba taarifa zote nyeti hufika jengo jeupe.

..sasa hii ya utafiti wa Zika ilipofika jengo jeupe hatua gani zilichukuliwa?

..kwanini hakukuwa na coordination ya suala hili mpaka jengo jeupe na wizara ya afya wanakurupuka baada ya Dr.Mwele kuzungumza na vyombo vya habari?

..halafu baada ya kuwa Dr.Mwele ametangaza anatimuliwa kazi. Hivi jengo jeupe hawajui madhara ya uamuzi huo kimataifa na ktk viunga vya watafiti wa magonjwa hatari?

..suala hili limekuwa mishandled ktk ngazi zote na hatua zote.
 
Huwa sijadiliani na watu wanaopenda ligi,mjadala unafahamika,habari inaonekana kuwa kati ya Watz 535 waliochukuliwa sample za vipimo vya virusi vya Zika,80 wameathirika,na kati ya hao,30 ni watoto wameonekana kuathirika na ugonjwa huu.

Kwamba taarifa hii ni "Habari" kwa sbb sasa imevuka mipaka ya nchi na kulipotiwa na chombo kikubwa kama CCTV...Haikuhitaji "nyama" kwa sbb wenye uelewa wameelewa ndio maana unaona wanajadili.Siku zote hata darasani sio wote huwa wanamuelewa mwalimu kwa wakati mmoja...Wengine huenda taratibu

Hilo la "umbea" sio jadi yangu;wanaolewa na tunaojadiliana humu JF wanajua kuwa mimi si "mbea"...Sitaki kwenda huko,maana tutatoka kwenye mjadala
Wapuuze wengine kujikomba kwa watawala walinyonyea!![emoji6] [emoji6] [emoji6]
 
Back
Top Bottom