Hatimaye wakili Peter Kibatala kumtetea Gwajima

Hatimaye wakili Peter Kibatala kumtetea Gwajima

kibatali anawafurahisha akina gwajima kesi hiyo ipo kwenye upelelezi.
ni lazima apeleke vielelezo vyake kama alivyo agizwa na polisi akishapeleka wataenda mahakamani.
Polisi wanauwezo kumshitaki kibatali kwa kuzuia polisi kufanya uchunguzi
vitu vingine unatakiwa kuwa na elimu husika ya eneo husika. Polisi wanajua sheria kwamba mtuhumiwa anaweza kukataa kutoa ushahidi wake polisi na akautoa mahakamani
 
Wakuu hivi ile kadi ya gwajima ile ya uanachama wa chadema ni namba ngambi vile.

Swali lako limekosewa...
Ungeuliza hivi...

Wakuu hivi ile kadi ya gwajima ile ya uanachama wa CCM ni namba ngapi vile..??

NAPE%2BNA%2BGWAJIMA.jpg
 
Kwa sasa bado hakuna kesi inayomkabili Gwajima, mpaka baada ya uchunguzi ambao unaweza kuchukua muda mrefu au mfupi kutegemea na uchunguzi wenyewe.
Lakini Polisi wana haki ya kuhoji kila Jambo ambalo linawaelekeza katika kumjua vizuri mteja wao, kosa au shtaka linaweza kua matumizi ya lugha mbaya ambayo inaweza kuhatarisha amani, lakini maswali yanavuka hapo, kwa sababu inawezekana kiburi cha kutumia lugha mbaya ni kwa sababu ya Uaskofu, au Wafuasi au Umaarufu wa kujuana na wakubwa serikalini, na au Mali alizonazo ili kujua hili maswali lazima yajibiwe hakuna namna ya kukwepa/kuzuia.
huwezi kuwachagulia Polisi uchunguzi gani wafanye, kwa mfano wakikuta dawa za kulevya mfukoni kwake lazima wahoji kama anatumia au anauza na mambo kama hayo ni bora tushabikie utawala wa sheria.

Ni vifungu vipi vinavyoainisha mamlaka hayo ya keshi la polisi?
 
kibatali anawafurahisha akina gwajima kesi hiyo ipo kwenye upelelezi.
ni lazima apeleke vielelezo vyake kama alivyo agizwa na polisi akishapeleka wataenda mahakamani.
Polisi wanauwezo kumshitaki kibatali kwa kuzuia polisi kufanya uchunguzi
Kwanini unasema ni lazima? Inaonekana mambo ya sheria yamekupa kisogo.
 
Kwa dini zenu hizi za kishirikina na gwajima kamwe mungu hawezi kuwa upande wenu hata iweje.

Dini yako ndiyo ya kishirikina ndiyo maana wewe kutokana na ushirika wako na Shetani huoni haya kusema dini ya Gwajima ambayo ni ya Kikristo ni ya kishirikina. Remember onething: Satan is a deceiver on earth and a tormentor in hell.
 
Daa!!! Mungu gani huyo unayemshirikisha kwenye huu upuuzi huyo Mungu ndiyo alimtuma Gwajima amwambie Askofu Pengo anavaa pampers?

Kwani Gwajima ameulizwa cho chote kuhusu pampers? We vipi? Umesoma uzi unavyokwenda au umeamua kukurupuka kwa sababu ya udini wako?
 
Nachoona mwisho wa yote ni Polisi kuaibika; huwa wanafanya mambo yao locally sana (hasa Kamanda Kova), wanajiingiza sana kwenye siasa badala ya kuzingatoa taaluma na weledi.

Ikiwa Polisi watashindwa kwenye hili sakata dhidi ya Gwajima, itakuwa aibu kubwa kwa Polisi; imani ya watu kwa utendaji kazi wa Polisi itazidi kuporomoka.
 
ushabiki wa gwajima unapindua hata kazi za polisi.
hivi nauliza kwani akipeleka kuna kosa gani msimpoze mtu ili aharibikiwe kwani gwajima anawasiwasi gani ili ashindwe kupeleka vielelezo.
taasisi ya gwajima imesajiliwa na polisi asipopeleka wanauwezo wa kufuta taasisi yake.
sasa nyinyi mashabiki mnaempotosha gwajima mtabakia aaahaa haiwezekani lakini kishafutiwa hivyo
 
Biblia ninayosoma katika kitabu cha WARUMI 14:4 kinanikataza kumhukumu mtumishi yeyote anayemtumikia YESU kwani huo uwezo hatuna bali Mungu pekee anayeona mioyoni mwao. May be useme unaungumzia Mungu wa kabila fulani na siyo Jehova au YESU ninaye mjua

Hakuna aliye juu ya sheria. Akivunja sheria ni lazima ahukumiwe sawasawa na sheria za nchi. Mungu hana upendeleo. Ila kama akionewa Mungu atasimama upande wake.
 
kuna watu wanajidanganya eti picha ndo inaanza sidhan kama mko timamu vichwan kaz inaisha muda si mrefu wala msisumbue vichwa vyenu kufikiria hilo,gwajima ni mtu mdogo sana

Kesi zozote baada ya upelelezi huwa zinaishia mahakamani! NA hilo ulitie kichwani mwako!
 
Hakuna aliye juu ya sheria. Akivunja sheria ni lazima ahukumiwe sawasawa na sheria za nchi. Mungu hana upendeleo. Ila kama akionewa Mungu atasimama upande wake.

Sheria sio za kova na jeshi la kutetea wanaEscrow(double standard) bali kesi zooote ni mahakamani na hapo ndo hizo nyaraka hutolewa!
 
Leo wanatakA nyaraka za Gwajima mbona wasomAli na waarabu na wahindi wamejaa hapa Tanzania wanapora mali kupeleka mAkwao,Gwajima anayetumia kuna tatizo gani na ana waumini,Kova umeshazeeka usitafute sifa ili upandishwe cheo, umekaribia kustaafu!
 
kibatali anawafurahisha akina gwajima kesi hiyo ipo kwenye upelelezi.
ni lazima apeleke vielelezo vyake kama alivyo agizwa na polisi akishapeleka wataenda mahakamani.
Polisi wanauwezo kumshitaki kibatali kwa kuzuia polisi kufanya uchunguzi

Kimsingi polisi hawana mamlaka ya kuomba vielelezo hivyo labda kama mahakama na labda wangekwenda na search warrant tena kutoka mahakamani!

Lakini bado najiuliza kwanini Kibatala hakujitokeza kumtetea Sheikh Ponda?
 
We Pumbavu, Pengo Alishamsamehe Na Hakufungua Kesi Yeye, Sasa Atakwendaje Mahakamani?

Ukimpiga nondo mtu ukamuumiza mtu ukawekwa ndani akakusamehe yule mtu uliyemjeruhi kesi na jamhuri iko pale pale.Kuvurumisha mitusi hadharani hata kama humtaji mtu unayemtukana ni kosa. kesi iko pale pale.

Ile mitusi imeharibu watoto.Sasa hivi mitaani mtu akitukana watu wanasema wewe ni ndugu yake na Gwajima nini?
Gwajima imekuwa brand name.Mtu akitaka kutukana nilikuwa Arusha mjini mmoja akasema nianze kukugwajima sasa hivi? wengine wakasema mgwajime? Yule kijana akaanza kuporomosha matusi mshenzi wewe,mnafiki na matusi mengine ya nguoni.Mitusi yake imeharibu jamii.
 
Hawa watu wakiamua hata usimamishe Wakili mzuri kiasi gani watakufunga tu nasema Watakufirisi tu...!!

Kikubwa hapa huyo Gwajima awaombe radhi ikibidi awadanganye hata kuwapigia kampeni kanisani kwake, vinginevyo ataokomea nakwambia mkuu jamaa wamedhamiria kumtokomeza na hakika atatokomea ni suala la muda tu, Huu ndio ukweli mchungu..!!

Unakumbuka Amri Kombe alipigwa risasi huku kanyoosha mikono juu kama ishara ya Kusarenda pamoja na kwamba hakushika hata fimbo??

Naam aliitwa Jambazi na akauliwa kama Jambazi..!!! Kisha.waliomuua wamasema ooooh tulukosea tukadhani ni Jambazi...!!!

BACK TANGANYIKA

Kwa kiasi fulani uko sahihi; lakini watafute mbinu nyingine za kummaliza na si hizi za kudai nyaraka ambazo hazihusiani na kesi ya msingi!
 
Kimsingi polisi hawana mamlaka ya kuomba vielelezo hivyo labda kama mahakama na labda wangekwenda na search warrant tena kutoka mahakamani!

Lakini bado najiuliza kwanini Kibatala hakujitokeza kumtetea Sheikh Ponda?
sheikh ponda hakuwa na pesa ya kulipia gharama za uwakili. yule alikuwa mropokaji tu na sadaka hakushanyi. bora gwajima amekusanya sadaka, itamsaidia kulipa gharama za uwakili.
 
Mkuu Ritz heshima yako, sasa hata kama Gwajima anamakosa ya kutumia hayo maneno makali ya kuudhi, si wamshitaki kwa hilo kosa, haya ya kutakiwa kuleta mapaka hati ya kanisa, bodi ya wadhamini, mchanganuo wa mapato yake na malizake yanatoka wapi etc, yanaingilianaje mkuu>> huoni kuna jambo limejificha hapo, Gwajima kaanza leo kuwa na kanisa??.. Wamuhumuku kwa kosa alilotenda, kama kuna mengine wafungue shauli lingine.. tuwe wakweli mkuu....

Polisi wanataka hati ya kanisa wakati makanisa na taasisi za dini husajiriwa na wizara ya mambo ya ndani. Imekaaje hii?!
 
Back
Top Bottom