Hatimaye wakili Peter Kibatala kumtetea Gwajima

Unaposema amekurupuka una uhakika na hilo na umesoma maandiko yake vizuri yaliyowekwa hapo juu...We pia ni mjuvi wa sheria au ni layman tu wa sheria? Kitu ninachoona hawa jamaa kuna mapungufu flani wameyaona kwa kumuhitaji Gwajima aje na hizo Docs na ndo maana nafikiri kwa kuliona hilo wenyewe hawakutoa maandishi yoyote kwake kwamba wamehitaji hili na hili kimaandishi,je unafikiri kwa nini police hawakutoa hiyo order katika maandishi??????

Sinema ya kusahaulisha watu mambo ya escrow
 
Ukimpiga nondo mtu ukamuumiza mtu ukawekwa ndani akakusamehe yule mtu uliyemjeruhi kesi na jamhuri iko pale pale.Kuvurumisha mitusi hadharani hata kama humtaji mtu unayemtukana ni kosa. kesi iko pale pale.

Ile mitusi imeharibu watoto.Sasa hivi mitaani mtu akitukana watu wanasema wewe ni ndugu yake na Gwajima nini?
Gwajima imekuwa brand name.Mtu akitaka kutukana nilikuwa Arusha mjini mmoja akasema nianze kukugwajima sasa hivi? wengine wakasema mgwajime? Yule kijana akaanza kuporomosha matusi mshenzi wewe,mnafiki na matusi mengine ya nguoni.Mitusi yake imeharibu jamii.

Movie ndiyo kwanza imeanza zipo movie nyingi za kuhakikisha watu wanasahau Escrow kabsa.
 
kibatali anawafurahisha akina gwajima kesi hiyo ipo kwenye upelelezi.
ni lazima apeleke vielelezo vyake kama alivyo agizwa na polisi akishapeleka wataenda mahakamani.
Polisi wanauwezo kumshitaki kibatali kwa kuzuia polisi kufanya uchunguzi
Sinema ndiyo kwanza inaanza... Tutashuhudia vioja vya kila Aina ni wakati wa Kujifunza kitu kupitia hili sakata.
 
Hivi si kisheria mtu unaruhusiwa kutotoa statement yoyote Polisi akiona inafaa kufanya hivyo? Na ikitokea hivyo unayo ruhusa ya kupelekwa mahakamani na kujitetea huko kisheria?
Nadhani Gwajima anaweza kukataa kupeleka zile document na polisi wanachoweza kufanya ni kupeleka kesi mahakamani basi! Sheria ni pana sana na tafsiri zake ziko mahakamani tu, ndio sababu mawakili wanahitaji maelezo ya polisi ili wakapate maelezo ya kisheria mahakamani:heh:
Sorry mi si mwanasheria lakini najua vitu kidogo vya kisheria maana kutojua sheria pia kunatunyima haki zetu.

Kwa kifupi, Askofu Gwajima anaweza kukataa kuwapa vielelezo vyote au baadhi (kama anavyojisikia mwenyewe) kwa jeshi la polisi pale anapoona na ama kuhisi kuwa haki zake za kimsingi na ama za kikatiba zinaingiliwa ama kutetereshwa bila ya sababu ya msingi.

Mfano halisi: ni kuwa wito wa mahojiano ulikuwa juu ya kesi ya kumtukana au kumtolea maneno ya kashfa Askofu Pengo. Sasa tazama hii list ya vitu 10 inahusiana na nini? kama si uonevu wa wazi na ufinyangaji wa haki za raia. (which is absolutely irrelevant)

Binafsi nilianza kuwa na wasiwasi mkubwa kuona jinsi Wakili John Mallya alivyokuwa ana handle hii kesi, kwani katika uwanja wa sheria unapokuwa unamwakilisha mteja wako katika mahojiano ambayo ni sensintive kama ya Gwajima (ambayo yanaweza kuzaa kesi ya jinai mbaya kabisa), Wakili unapooona ama kuhisi mtiririko wa mahojiano yanaelekea nje ya tuhuma anayokabiliwa mteja wako (yaani to exploit your client constitutional rights) una haki ya kumwambia/shauri mteja wako asilijibu swali hilo tatanishi. Na ndio sababu kuu ya kuwa pale kwenye mahojiano. Na polisi kama wanaona wana haki wanachoweza kufanya ni kukupeleka mahakamani ambako sheria itapima kila mtu kwa usawa.

Hitimisho ni kuwa Gwajima ana haki ya kutopeleka hati yeyote ile ambayo anahisi hazihusiana na wito wa majhojiano juu ya tuhuma zilizojengwa mbele yake. Mwisho namshauri Gwajima kuwa imefika mahali sasa ajenge wigo mzito wa timu nzito ya Wanasheria, John Mallya naona kama hii kesi ni kama inamzidi kimo. Nafarijika kuona Mwanasheria mahiri na makini Peter Kibatala ameongezea nguvu na ameanzia na 'strategy' makini tu ya kuhoji uhalali. Na polisi wakileta ubabe unafungua shauri la kikatiba kuhoji mamlaka ya polisi juu ya kuitisha documents zote hizo katika tuhuma ya kumtukana mtu na tuone mahakama itatamka vipi.
 
Kwa kifupi, Askofu Gwajima anaweza kukataa kutoa vielelezo vyote polisi walivyovitaka pale anapoona na kuhisi haki zake za kimsingi na zile za kikatiba zinaingiliwa ama kutetereshwa bila ya sababu ya msingi.

Mfano halisi ni kuwa wito wa mahojiano yalikuwa juu ya kesi ya kumtukana au kumtolea maneno ya kashfa Askofu Pengo Vs.(dhidi) Rejea list ya vitu 10 (which is absolutely irrelevant) ambao ni uonevu wa wazi na ufinyangaji wa haki za raia.

Binafsi nilianza kuwa na wasiwasi mkubwa kuona jinsi Wakili John Mallya alivyokuwa ana handle hii kesi, kwani katika uwanja wa sheria unapokuwa unamwakilisha mteja wako katika mahojiano ambayo ni sensintive kama ya Gwajima (ambayo yanaweza kuzaa kesi ya jinai), Wakili unapooona ama kuhisi mtiririko wa maswali yanaelekea nje ya tuhuma anayokabiliwa mteja wako (yaani to exploit your client constitutional rights) una haki ya kumwambia mteja wako asilijibu swali hilo. Na polisi kama wanaona wana haki wanachoweza kufanya ni kukupeleka mahakamani ambako sheria itapima kila mtu kwa usawa.

Hitimisho ni kuwa Gwajima ana haki ya kutopeleka hati yeyote ile ambayo anahisi hazihusiana na wito wa majhojiano juu ya tuhuma zilizojengwa mbele yake. Mwisho namshauri Gwajima kuwa imefika mahali sasa ajenge wigo mzito wa timu nzito ya Wanasheria, John Mallya naona kama hii kesi ni kama inamzidi kimo. Nafarijika kuona Mwanasheria mahiri na makini Peter Kibatala ameongezea nguvu na ameanzia na 'strategy' makini tu ya kuhoji uhalali. Na polisi wakileta ubabe unafungua shauri la kikatiba kuhoji mamlaka ya polisi juu ya kuitisha documents zote hizo katika tuhuma ya kumtukana mtu na tuone mahakama itatamka vipi.

Mpaka hapa watanzania wameshasahau Escrow wapo busy na Sakata kati ya gwajima na police. Hii movie inaenda vizuri
 
Kibatala hamna kitu hii kesi atapinduka kichwa chini miguu juu.Hivi Polisi Traffic akikuomba umwonyeshe leseni yako huwa katumia kifungu gani cha sheria? Au afisa biashara akikuomba umwonyeshe kleseni anatumia kifungu gani cha sheria?

Wakili mzima anaandika kabarua kaliko chini ya upeo kama hako na watu wanashangilia? Gwajima ataliwa hela hadi auze helikopta kulipa huyu wakili.Huyu wakili anachofanya ni kuongeza masaa mengi achaji tu invoice kwa Gwajima

Yule kijana wakili Malya yuko vizuri kwa approach yake hata kama Gwajima kamtoa.Ikumbukwe kuwa yule kijana kipindi chote cha uwakili kwa Gwajima hakuna kesi iliyofunguliwa dhidi ya Gwajima ya kumpeleka kizimbani wala rumande.Lakini Approach ya Kibatala ni ya kutaka kesi iende mahakama kuu chap chap mteja wake awe kizimbani!!!!

Askari wa Usalama barabarani amepewa mamlaka na The Road Traffic Act ya mwaka 1973. Tatizo lipo kwa polisi kudai nyaraka 10 kwa mdomo. Huyu Wakili amefanya sahihi kabisa, ila kwakuwa ni wakili mzoefu na maarufu, ma-bushlawyer wameamua kumshambulia ili wapate '1 minute of fame'. Hata Ridhiwani ni mwanasheria, lakini hajawahi kushinda hata kesi ya wizi wa Kuku.
 
Polisi hawazuiwi kufanya upelelezi na mahojiano kuhusu chochote si lazima wakikuita wakuhoji kitu kimoja.Ukibisha waweza kuambia haya nenda.Halafu ukitoka nje wanakuita tena njoo kwa mahojiano ya kitu kingine.Yule wakili mwerevu kijana Malya alichofanya ni kuwaacha polisi wahoji vitu vyote wanavyotaka kwa Gwajima ili akitoka awe ametoka akapumzike aendelee na shughuli zake badala ya kila siku kuwa kiguu na njia kwenda hojiwa na polisi leo kuhojiwa hiki kesho kuhojiwa kile.

Wakili huyu mpya Kibatala ambaye wengine mnamwita mzoefu wakati hamna kitu anachotaka kufanya ni kuwa polisi wahoji kitu kimoja kimoja.Waanze na hilo la kutukana pengo halafu waendelee na hayo mengine.What is the difference sababu at the end of the day atahojiwa maeneo yote polisi wanataka kuhoji anataka Gwajima kutwa awe kiguu na njia polisi.

Wakili Kibatala anataka Gwajima awe na kesi nyingi tofauti tofauti sababu ndipo aweza pata hela nyingi kwa kesi tofauti tofauti.Wakati yule kijana wakili Malya lengo lake alijua polisi waweza fungua kesi moja tu wakimaliza vyote wanavyotaka kuhoji Gwajima hivyo ingekuwa vizuri kwa mteja wake upande wa gharama na upande wa kupata muda wa mambo mengine badala ya kila siku kushinda mahakamani leo kwa kesi hii kesho kwa kesi ile.

Gwajima kaingia mtego kwa wakili Kibatala.Atakuwa kazi yake kushinda mahakamani kwa mikesi kibao yenye tarehe tofauti tofauti.Na atakefaidi ni wakili kwa gharama za uwakili atakazomchaji.

Wakili Malya kwangu naona kakijana kako vizuri kuliko hawa wanaojifanya wazoefu.
 
Siku penda matusi ya Gwajima wala sikuwahi kumshabikia ila kwa mashataka haya yasiyo na grounds za kisheria nafikiri alionewa. Hebu tuone sheria inasemaje kwa watu formal kufanya mambo informal.
ni kweli wengi hatukupenda yale maneno aliyotumia siku ile kwa Pengo, kama jeshi la Polisi lingesimamia kwenye zile zile tuhuma basi watanzania wengi tusingetilia shaka!! lakini sasa badala ya yale mashitaka ya msingi wao wamerukia mambo mengine ambayo kimsingi hayaendani na hili shauri la kutoa lugha chafu!! kwa nini awakilishe nyaraka zote hizo? zinahusikaje na kutoa kwake lugha chafu?? kama alikuwa na tuhuma nyingine basi fungueni shauri jingine kwa wakati tofauti ili watu wasiwe na shaka!!

Haya masuala ya kuunganisha tuhuma ni ya kizamani.
 
Polisi hawazuiwi kufanya upelelezi na mahojiano kuhusu chochote si lazima wakikuita wakuhoji kitu kimoja.Ukibisha waweza kuambia haya nenda.Halafu ukitoka nje wanakuita tena njoo kwa mahojiano ya kitu kingine.Yule wakili mwerevu kijana Malya alichofanya ni kuwaacha polisi wahoji vitu vyote wanavyotaka kwa Gwajima ili akitoka awe ametoka akapumzike aendelee na shughuli zake badala ya kila siku kuwa kiguu na njia kwenda hojiwa na polisi leo kuhojiwa hiki kesho kuhojiwa kile.

Wakili huyu mpya Kibatala ambaye wengine mnamwita mzoefu wakati hamna kitu anachotaka kufanya ni kuwa polisi wahoji kitu kimoja kimoja.Waanze na hilo la kutukana pengo halafu waendelee na hayo mengine.What is the difference sababu at the end of the day atahojiwa maeneo yote polisi wanataka kuhoji anataka Gwajima kutwa awe kiguu na njia polisi.

Wakili Kibatala anataka Gwajima awe na kesi nyingi tofauti tofauti sababu ndipo aweza pata hela nyingi kwa kesi tofauti tofauti.Wakati yule kijana wakili Malya lengo lake alijua polisi waweza fungua kesi moja tu wakimaliza vyote wanavyotaka kuhoji Gwajima hivyo ingekuwa vizuri kwa mteja wake upande wa gharama na upande wa kupata muda wa mambo mengine badala ya kila siku kushinda mahakamani leo kwa kesi hii kesho kwa kesi ile.

Gwajima kaingia mtego kwa wakili Kibatala.Atakuwa kazi yake kushinda mahakamani kwa mikesi kibao yenye tarehe tofauti tofauti.Na atakefaidi ni wakili kwa gharama za uwakili atakazomchaji.

Wakili Malya kwangu naona kakijana kako vizuri kuliko hawa wanaojifanya wazoefu.

kasome tena ile barua ya Kibatala,
Kibatala hajakataa kuhojiwa, ila kw akuw ani mapya leteni Barua na Vifungu vinavyoruhusu kuletwa kw anyaraka hizo.

na pia kumbuka Wiki hii anakwenda kufungua kesi ya Kikatiaba amesema kuhusu hayohayo ya polisi na Gwajima.
 
Polisi hawazuiwi kufanya upelelezi na mahojiano kuhusu chochote si lazima wakikuita wakuhoji kitu kimoja.Ukibisha waweza kuambia haya nenda.Halafu ukitoka nje wanakuita tena njoo kwa mahojiano ya kitu kingine.Yule wakili mwerevu kijana Malya alichofanya ni kuwaacha polisi wahoji vitu vyote wanavyotaka kwa Gwajima ili akitoka awe ametoka akapumzike aendelee na shughuli zake badala ya kila siku kuwa kiguu na njia kwenda hojiwa na polisi leo kuhojiwa hiki kesho kuhojiwa kile.

Wakili huyu mpya Kibatala ambaye wengine mnamwita mzoefu wakati hamna kitu anachotaka kufanya ni kuwa polisi wahoji kitu kimoja kimoja.Waanze na hilo la kutukana pengo halafu waendelee na hayo mengine.What is the difference sababu at the end of the day atahojiwa maeneo yote polisi wanataka kuhoji anataka Gwajima kutwa awe kiguu na njia polisi.

Wakili Kibatala anataka Gwajima awe na kesi nyingi tofauti tofauti sababu ndipo aweza pata hela nyingi kwa kesi tofauti tofauti.Wakati yule kijana wakili Malya lengo lake alijua polisi waweza fungua kesi moja tu wakimaliza vyote wanavyotaka kuhoji Gwajima hivyo ingekuwa vizuri kwa mteja wake upande wa gharama na upande wa kupata muda wa mambo mengine badala ya kila siku kushinda mahakamani leo kwa kesi hii kesho kwa kesi ile.

Gwajima kaingia mtego kwa wakili Kibatala.Atakuwa kazi yake kushinda mahakamani kwa mikesi kibao yenye tarehe tofauti tofauti.Na atakefaidi ni wakili kwa gharama za uwakili atakazomchaji.

Wakili Malya kwangu naona kakijana kako vizuri kuliko hawa wanaojifanya wazoefu.

We ni polisi nn mkuu
 
Lkn mkumbuke, serikali nayo sio wajinga, hawajakurupuka, wameshaqngalia yote hayo, kuna somebody behind mwenye nguvu
 
Hawa jamaa wanapoanzaga kupambana kwa vifungu vya sheria napataga burudani tosha. Watu wanadadavua vifungu utadhani wamechanjiwa! BTW mwenyewe nilikua nashangaa haya mamlaka ya mtu unashitakiwa kwa kosa la kuiba kuku, ghafla unaanza kushitakiwa kwa kosa la ubakaji!
 
Back
Top Bottom