Jamaa zangu sikuingine nishachangia hivi vuguvugu la mabadiliko afrika na namna yanvyofanyika. Kwangu mimi Tunisia sasani unruled state kwa jinsi ilivyoachwa. Kwa upande wa Misri kwa mtazamo wangu Mubark ni heroingawa kuna mtu anamwita pimbi lakini ujue huyu bwa amekua preda for 30 years. Kwanini nasema ni hero? ameweza kujipanga pamoja na Jeshi la Misri ambalo linasifika kuwa ndilo jeshi litiifu na lenye nguvu afrika na kwa baadhi ya nchi za kiarabu. Mubarack ni senior officer wa jeshi makamu wake ni senior officer wa jeshi na pia alikua Mkurugenzi wa intelligence Service (Usalama wa Taifa) na kumbuka toka mwanzo aliagiza mwenyewe kuwa askari na jeshi lisimpige mtu wala kutumia nguvu kubwa kuzuia maandamano maana ni haki yao ila tu atakaye vunja sheria akamatwe na tuliona wakati waliojidai wafuasi wa Mubarak walipokua wakirusha mabom ya petrol walikamatwa, waliokua wanaiba walikua wanakatwa. Kuna mengi ya kumsifia lakini amejipanga na kuhakikisha haiachi nchi katika hali isiyotawalika ameiacha kwa Military Council naye yupo palepale misri kama alivyosema atafia misri naye ni Baba wa Misri. Ikitokea hapa kwetu itakuwa kama tunisia ambapo vyama vya sias vinapigania kutawala nchi. El Baradei siku nilipokutana naye alizuru na kutoa mhadhara UDSM alisema Mubarak ni kichocheo cha umasikini nchini mwake na amejisahau kwa kupumbazwa na Marekani, saudi arabia na izrael maana wanadhani Muslim brotherhood wakichukua nchi wataungana na al Qaeda, Hizbullah na hamas na kuwageuzia waizrael wadhalimu kibao.
Mwisho tusiombee hapa yatokee ya Tunisia bali ya Misri ila yatupasa kuwa makini sana maana mwisho wake ambaye hatumtaki anaweza akawa anaendesha nchi kichinichini yaani akawa na ushawishi mkubwa kama itakavyo kuwa kwa Mubarack.