Hatimaye Mubarak aachia ngazi!

Hatimaye Mubarak aachia ngazi!

Aisee! kumbe aliwaekea mkanda wa video huku yeye akijiandaa kutokomea , hata hivyo yeye mwenyewe alisema anawakubali vijana wa kileo kwa jinsi wanavyodai mabadiliko, sasa kazi bado kwetu sisi wabongo, je tutaweza? Mtu anayefuatia nadhani atakuwa Muamar Gadafi!
 
Jamani yaani I the solidarity across the middle east is unbelivable, amazing.

Labda sisi tuanze angalau kuandamana kuunga mkono wananchi wa misri, halafu
 
tehe raha tupu jamani am so hapyyyyyy hasa kwa yanayoendelea bungeni sasa hivi
 
ni watu wengi zijawahi kuona,yaani kutoka kila sehemu ya jamii watu wamefurika sio mchezo, wanakumbatiana kwa furaha, wana chant kwa amani, yaani hata kuelezea unashindwa. U can feel their emotion is very deeply enstored in their heart
Mkuu hawa jamaa leo ndio wamepata UHURU KAMILI! ule wa Mubarak ulikuwa fake tu (kiini macho) Wa egypty hawatakuja kuisahau hii
siku kwenye kumbukumbu za maisha yao. Yaani nchi imezaliwa upya na wananchi wamezaliwa upya.
 
Ila jamaa alikuwa king'ang'anizi muda wote huo! Hawa wa kwetu nadhani huko waliko matumbo joto.
 
Young people who are unemployed are the waves of changes in many parts of the dictatorial regimes. If CCM leaders watch this they should be very very fearful and rescue things before they got out of their control. CCM govt should work more than harder now to convice young people that they can be better in the current regime(CCM Regime), otherwise freedom is is coming soon!. Kwa kuanzia tu waanze na spika wao ambaye wiki hii ameonesha kuwa ni catalyst ya kuchochea hasira za wananchi kwa kuendesha chombo cha kidemokrasia kidikteta.
Utawala wa kiimla, mabavu, wizi, rushwa, kutojali maslahi ya umma ndio mkate wetu wa kila siku katika nchi nyingi duniani na hasa za Kiafrika.
Tushukuru kuwa Tunis walianza, Misri wamefuata, na nchi nyengine takriban zote za Kiarabu moto unavukuta. Viongozi watakaoamka mapema watajirekebisha haraka, lakini moto huu hautozimika mpaka nchi zote kujinasua na janga hili la utawala. Ni imani yangu kuwa si kwa nchi za Kiarabu tu, lakini popote ulimwenguni (Afrika, Asia, Amerika na Europe vijana watayaongoza mapinduzi haya kwa mafanikio
.
 
hivi huyu pimbi muda wote huo alikuwa hajajua cha kufanya, sasa kumbe washauri wa rais huwa wanamshauri nini?
na rais wenu huwa ana shauriwa na akina nani vile?
au huwa hana washauri?:sick:
 
umeona? alikuwa bado anapima joto ajue jinsi ya kutoka kama ni kuchukua koti,mwamvuli au atoke na tshirt na jeans.
hiyo ni sitairi nzuri sana maana bila kuiandaa unaweza toka vibaya bila hata vazi la heshima:laugh::laugh::coffee:
Ila jamaa alikuwa king'ang'anizi muda wote huo! Hawa wa kwetu nadhani huko waliko matumbo joto.
 
Utawala wa kiimla, mabavu, wizi, rushwa, kutojali maslahi ya umma ndio mkate wetu wa kila siku katika nchi nyingi duniani na hasa za Kiafrika.
Tushukuru kuwa Tunis walianza, Misri wamefuata, na nchi nyengine takriban zote za Kiarabu moto unavukuta. Viongozi watakaoamka mapema watajirekebisha haraka, lakini moto huu hautozimika mpaka nchi zote kujinasua na janga hili la utawala. Ni imani yangu kuwa si kwa nchi za Kiarabu tu, lakini popote ulimwenguni (Afrika, Asia, Amerika na Europe vijana watayaongoza mapinduzi haya kwa mafanikio
.
Umenena vizuri sana mkuu! Vijana ni taifa la leo na si la kesho kama ccm walivyotulisha sumu yao ya kuwa vijana ni taifa la kesho.
Mwenye macho aambiwi ona. kiongozi yeyote aliyemadarakani kama ameuona mziki wa tunis na nchi ya farao'basi hana budi
kuamka na kuiboresha demokrasia. Vinginevyo na yeye yatamkuta
 
Na ninakuhakikishia kama kweli dhoruba hii itatua khartoom'basi amini tusiamini itatua Uganda,Tanzania,
zimbabwe,Ivory coast, yemen nk.

You are very right kwa hili, uganda, sudan, algeria, zimbabwe...mh!!
 
umeona? alikuwa bado anapima joto ajue jinsi ya kutoka kama ni kuchukua koti,mwamvuli au atoke na tshirt na jeans.
hiyo ni sitairi nzuri sana maana bila kuiandaa unaweza toka vibaya bila hata vazi la heshima:laugh::laugh::coffee:
Nasikia alitoka na chupi tu' watu wakamwambia -mfalme u uchi nenda ndani tena
ili uvae nguo. Ndipo alipoendandani na apotoka tena akawa yupo ndani ya msuli
na familia yake pembeni teyari kwa safari
 
Ila jamaa alikuwa king'ang'anizi muda wote huo! Hawa wa kwetu nadhani huko waliko matumbo joto.
Kaka sahizi ma...yanagonga chupi yanarudi' yanagonga tena chupi yanarudi. Yaani wakhaaka tupu. Lol!
 
Maji yamemzidi kaamua kutimkia mafichoni, hata hotuba aliyoitoa jana haikutoka kwenye kasri yake. Hilo ni fundisho kwa JK na CCM yake

Kama nilivyochangia katika thread mojawapo leo asubuhi ni kwamba Nasser, Sadat,Mubarak na makamu wake wote ni wanajeshi waliovaa nguo za kiraia na walifanya kazi kubwa ya mapinduzi ya kuuondoa utawala wa kifalme. Nikasema Mubarak hawezi ondoka kirahisi rahisi au la ataliachia jeshi madaraka. Na ndivyo imetokea usiku huu. Mubarak kaiachia madaraka SUPREME COUNCIL OF ARMED FORCES. Wana JF tatizo linaweza kuwa sio Mubarak bali ni mfumo mzima wa utawala. Kwa mfano hapa Tanzania tatizo linaweza kuwa sio Kikwete bali mfumo wa CCM. Kikwete kama Muthalika wa Malawi anaweza kujiunga na CHADEMA akawa mtu tofauti sana. Kwa Masri kama jeshi linachukua madaraka bado hawatakua wamehitimisha ukombozi na huenda jeshi likachomekea watu wake. Wamasri wakazanie kuufumua mfumo wa utawala wa tokea enzi za Abdu Gamal Nasser.
 
kweli pipo power sio yakuchezea siku 18 akuna kukata tamaa kweli wanaitaji pongezi kidhati nawatamani na hii njia nzuri kwelikweli yakuwakomesha ccm wanaotegemea tume ya uchaguzi iwatangaze washindi wasome alama ya nyakati
 
Ila ifahamike kuwa kwa wakati huu jamaa wa USALAMA hapa bongo watakuwa wanafanya kazi kubwa sana kutazama nini hisia zetu watanzania kwa yanayojiri kaskazini mwa Afrika.
Kwa wiki nzima hii tutakuwa nao busy saana wanausalama humu kwenye forum tena mtaona jinsi hoja zitakavyopotoshwa na kuondoka kwenye mada,
 
Kikwete hajatoa tamko hadi sasa?? Dr Slaa yeye keshatoa tamko lake via social networks.

Peoples power forever
 
Ila ifahamike kuwa kwa wakati huu jamaa wa USALAMA hapa bongo watakuwa wanafanya kazi kubwa sana kutazama nini hisia zetu watanzania kwa yanayojiri kaskazini mwa Afrika.
Kwa wiki nzima hii tutakuwa nao busy saana wanausalama humu kwenye forum tena mtaona jinsi hoja zitakavyopotoshwa na kuondoka kwenye mada,

mpevu..upo makini sana... hasa ukizingatia kwamba tools zilizotumika ku aggravate pressure katika mapinduzi ya nguvu za ummma huko
tunisia na misri ni web portals kama facebook na twitter ... hawa jamaa watakua wanatumia binocular au theodolite humu JF
 
sijafuatilia historia ya Muba kwa undani lakini lazima tukubali huyu jamaa ametumia hekima kubwa sana ktk ku handle situation ya Masr. Kama unabisha umweke JMK hapo uone moshi utakaofuka hapo....all the best Muba, let the Egyptians go ahead!
 
This marks the continuation of the long sought out rebelation of African. Hope the spirit spreds southwards & starts with sisiemuu
 
Back
Top Bottom