Hatimaye 'mid-life crisis' imenifikia

Hatimaye 'mid-life crisis' imenifikia

Mimi quarter-life crisis imenifikia na imeniamsha kutoka usingizini, sijui nini kimetokea hapo kati... kutoka 20 mpaka 26 kama ndoto vile. Kama wanavyosema kuna baadhi ya watu huchelewa kuamka au wengine hawaamki kabisa, maisha yanawapitia na usingizi wa milele unawakuta wakiwa wamelala.

"Hakuna wa kukuamsha kukuambia kuwa umekua, miyeyusho ya majukumu tu, utakuja tukuombee dua."

Hakuna kukata tamaa: unafeli, unajifunza, unajaribu tena, mara hii ukiwa na maarifa zaidi na umejifunza kupitia makosa yako.

Maisha ni zaidi ya umri, jamii imetuweka kwenye box, na kutupangia tunapaswa kuwa wapi kwenye maisha kwa umri husika. Jamii inategemea ukifika 30s maisha yako yawe figured out, ila inasahaulika kuwa binadamu wote hatuanzii mbio za maisha kwenye mstari sawa.

Jitahidi uwe nje ya box. Mwisho wa siku hapa Duniani upo peke yako: ulikuja mwenyewe, na utaondoka mwenyewe. Ukiwa unajitafuta fanya kile ukipendacho na kinachoujaza moyo wako mpaka pumzi ya mwisho. Ukifanikiwa/kufeli utakuwa siyo wa kwanza wala mwisho... Dunia ilikuwepo kabla hujazaliwa, na itaendelea hata siku utakayoondoka

Just, keep going!
 
Knowledge sahihi ni ile inayosababisha utumie siku zako za kuishi ukiwa na amani na furaha siyo mifumo ya kufungwa akili iliyowekwa na wenye akili ili wafurahie maisha kupitia rasilimali unazozikosa kwa kufungwa akili.
So true, until you realize that education is different from knowledge and wisdom utakuwa a cog in a mashine
 
  • Kicheko
Reactions: Tsh
Midlife crisis inatukumbusha kuwa maisha hayasubiri mtu. Tatizo ukiwa kwenye 20's unaona una muda wa kutosha. Mara paaap 30s hiyo

Miaka inakimbia, wazazi wanazeeka, marafiki wa karibu wanapotea kila mtu na hustle zake kuna wakati ni kama uko peke yako unapambana

Na ndoto zinaendelea kusogezwa mbele
Hakikaa
 
Midlife crisis inatukumbusha kuwa maisha hayasubiri mtu. Tatizo ukiwa kwenye 20's unaona una muda wa kutosha. Mara paaap 30s hiyo

Miaka inakimbia, wazazi wanazeeka, marafiki wa karibu wanapotea kila mtu na hustle zake kuna wakati ni kama uko peke yako unapambana

Na ndoto zinaendelea kusogezwa mbele
Mtafutaji kama wewe tu
Duuh aisee, kweli hakuna usawa
 
Walituambia by 30s tayari tutakuwa na nyumba, gari, mke na watoto.

Kumbe 30s za wazee wako sio kama 30s za leo,

Mtu ana miaka 50s bado anaishi nyumba ya kupanga? 😂

Wazee, we are cooked.

Kila mtu ashinde mechi zake.

Kweli kabisa love is for, women children and dogs... A man is only respected for what he brings to the table.
Usipanic mkuu. Pia fikiria, kila mtu akimiliki gari maisha yangekuwaje? Kila mtu akijenga nyumba maisha yangekuwaje? uhalisia kuna vitu unaambiwa kama matarajio ila sio wote watakaofikia, ridhika na kile Mungu alichokujalia alafu panga mambo yako pasipo na stress.
 
Na hii mitandao imeharibu zaidi. Unakuta vitoto kama kina Niffer vinasukuma ndinga za mamilioni... sema kila mtu na maisha yake hatuwezi kuwa sawa. Shikilia ulicho nacho kwa wivu mkubwa.
 
Mistari wa Tupac 'since I've got only one life to live...' nilikua siuelewi zamani,siku hizi nauelewa vizuri
Kwenye ngoma yake ya dear mama kuna line inaenda..

"I wish I could take your pain away,
If you can make it through the night there's a brighter day"

Actually alikuwa anaomba kuhusu struggle za mama ake mzazi.

It's only this life, Atleast do what it takes
 
Back
Top Bottom