Hatimaye Mbowe apewa dhamana

Nenda kaandamane tukufanye kitu kibaya ambacho utajutia hata wazazi wako kukuzaa ! si umeona wakina Mbowe, Lissu nk tulivyowafanya, bado wewe sasa . Na sio kwamba tunakutisha

Kwani si tunajua mabosi weko wamelala ndani nyinyi mnazunguka lindo. Kama kweli na nyinyi mnataka kufanya kazi kwa raha kwa nini msishikiza hiyo serikali yenu ikatekeleza hayo matatizo ya wananchi. Mfupa umemshinda aliyeuomba sasa anawatupia na nyinyi ndio mnahangaika nao wakati kesha chukua nyama yote.

TUKIAMUA HUWEZI KUZUIA UMMA. ACHA KUTISHIA WATU.
 

waswahili tunasema utabaki na labda. CDM kuiona ikulu bado ni ndogo ya zuzu.
 
TLS ni NGO moja ya mawakili wanaoshindana kutajirika. Wapo tangu enzi hizo za Tanganyika lakini nchi imeshuhudia sheria za ajabu ikiwemo hii iloomuweka ndani Mh Mbowe, mikataba ya ajabu na mahakama za ajabu zilizooza kwa rushwa na baadhi yao wakiwa mawakala wazuri wa rushwa. Ni wakwepaji wazuri wa kodi za nchi hii. Wakae kimya tu. Hawana jipya.
 

Heshima kwako WildCard.

Mkuu tuko pamoja haswa, CHADEMA na viongozi wake hasa mwenyekiti Mheshimiwa A F Mbowe lazima wajue Tanzania [Wananchi] wanawahitaji sana hasa kwenye masuala muhimu eg katiba mpya,vita vya ufisadi,matumizi sahihi ya kodi zetu na nk.CHADEMA lazima wawe makini sana wasije kuwaangusha kama ilivyotokea kwa NCCR Mageuzi wengi wanadhani mageuzi ni lelemama.Mageuzi yanahitaji mikakati makini matatizo madogo madogo kama hili la Mheshimiwa Mbowe yalitakiwa kuepukwa mapema hapakuwepo na sababu za msingi Mwenyekiti wa chama cha upinzani kuswekwa ndani, ni jambo linaloweza kuepukwa.

CHADEMA kama cha kikuu cha upinzani lazima kikae chini kitafakari kwa kina nini kilijiri hadi mwenyekiti wake afikie hatua ya kukamatwa.Je CHADEMA hakuna wanasheria wakutosha ?,Je wasaidizi wa mwenyekiti walifanyakazi yao vyema ?,Je viongozi wa CHADEMA wafuate mkondo wa Mchg Mtikila.

Najua hapakuwa na sababu za msingi kwa kiongozi kama Mbowe kufanyiwa aliyofanyiwa.hakika mahakama na polisi wanajua dhahiri Mbowe hawezi kutoroka lakini Mbowe alitakiwa kujua kabla kwamba wakuu wa hivi vyombo wanategemea fadhila za CCM kupanda vyeo [IGP Mahita na A L Mrema] hivyo alitakiwa kuchukua tahadhari mapema.
 
Nilianza kumsikia kwa mbali alipochaguliwa kuwa mbunge Hai mwaka 2000

Alipata umaarufu zaidi alipochaguliwa kuwa mwenyekiti wa CHADEMA (2004?)

Alipata umaarufu sana alipogombea uraisi mwaka 2005, zaidi kwa kuanzisha styles za helkopta na magwanda, ambazo ni maarufu hadi leo

Alikuja kuvuma tena sana wakati wa operesheni sangara.

Katika uchaguzi uliopita, hakuvuma sana (kwa sababu ya kuwepo Slaa katika uraisi?)

Alikuja kuvuma zaidi wakati wa kuundwa kwa kambi ya upinzani

Aliendelea kuwa midomoni mwa watanzania katika matukio tofauti kwa kiwango tofauti hadi Ijumaa tarehe 3 June 2011

Kwa siku tatu mfululizo Kuanzia Ijumaa jioni, hadi leo asubuhi, Freeman Aikaeli Mbowe amengeza mstari mwingine katika historia yake ya kupigania wanyonge Tanzania. Mstari ambao kwa wanaofuatilia vyombo vya habari na kusikiliza maoni ya watu ya kisiasa, bila shaka unastahili kuandikwa bolded zaidi, na kwa font kubwa zaidi, angalau kuliko mistari yote iliyowahi kuandikwa siku ya nyuma...
 
TLS mbona mnachelewa kutoa maoni? inapendeza kama mnatoa maoni yenu mapema angalau ionekane fulani walisema

Mkuu umesema kweli, wanasubiri watu wafe ndo watowe ushauri, Je tunajenga au tunabomoa?
 
Kama kawa mpaka kieleweke, huku alipo mkweree lazima ajinyee! Nchi yetu hii!
 
Jeshi la polisi limeisha yapiga marufuku nchi nzima, nenda kaandamane sasa uone cha mtema kuni !

Hebu zijue haki zako ndugu yangu!
una haki hata ya kuing'oa serkali iliyo madarakani.
Hivi ukitaka kujamba mwenzako akuzibe na dole gumba utasikia raha weye!
kama vipi nawe usiandamane tu tatizo nini!
 
Sio hasira THINK TWICE, watu wanataka sheria zifuatwe kwa kila mtu sio kuchagua. Kwani Mbowe hakudhaminiwa hadi akamatwe kama jambazi sugu? Mtu akidhaminiwa mdhamini wake anaambiwa amtafute mtu wake ampeleke mahakamani na sio kutoa amri kwa jeshi la polisi kumkamata mtuhumiwa, au dhamana inachukuliwa (forfeited- ( Wanasheria mtanisahihisha).

Hii inaonyesha ilipangwa tu, kesho utakamatwa wewe usije ukalalamika. Bila kuwa shabiki wa chama chochote mimi naona nguvu imetumika bure. Jeshi letu lingetumia nguvu hivi wananchi tusingekufa kwa ujambazi au kuibiwa kila siku. Mbona raia hatulindwi hivi?
 
Mwenyekiti wa chadema ameshaachiwa na sasa watu wamembeba juu juu Arusha

Serikali imetumia rasilimali nyingi katika suala la Mbowe, ndege ya JWTZ (Haitumii maji kuruka), askari wengi kuliko maelezo. Mbowe kafika Arusha na kupata dhamana, sasa kulikuwa na umuhimu gani wa kumkamata na kumsafirisha kwa gharama zote hizi huku mambo ya msingi ya kitaifa yanakuwa disturbed?
Kikwete anatakiwa kutoa maelezo kuhusu rasilimali zinavyotumika bila busara. Pamoja na kwamba haya mambo yanaipandisha chati CHADEMA, lakini serikali haikuwa na umuhimu wowote wa kufanya hayo yote.

CCM ilianza na santuri ya UKABILA.....ikadoda, UKANDA.....ikadoda, UDINI....ikadoda, UMWAGAJI DAMU.....ikadoda na sasa wamekuja na kamatakamata......guess what! nayo ITADODA.
 
sio kwata ni gwaride kabisa, wanalijua, wanajua wanalicheza bt hakuna jinsi, NGUVU YA UMMA ITASHINDA, CHADEMA NDIO IMANI YETU!
 

Duh, wewe kweli hujui ku analyse mambo, hiyo ni kinyume chake sasa ! Jamaa wamemdhalilisha sana na hata wabunge wenyewe wamesema. N aelewa kuwa suala la bajeti ni suala la bunge sio la mbowe, sasa hapo pipoz powa inahusika vp?. Jamaa wamemkamata kama ndege, wameenda kumlaza sakafuni, wamemsafirisha usiku hakupata usingizi huoni heshima imepungua?. Na isitoshe hili ni suala la kisheria wala CCM haihusiki hata chembe, wenzake wao walienda mahakamani wakamdanganya mwenzao amedhalilika sana .
 
CCM Strategists ni waganga wa kienyeji
 
Reactions: FJM
Huyu mbunge wangu bana nakumbuka mwaka 1995 anagombea halafu akashindwa na alitimiza kile alichoahidi pasipo hata kuwa mbunge at that time!mbowe anatabia za uongozi huwa anaonyesha njia nini kifanyike.tumekukabidhi Hai tunahitaji kuona maendeleo endelevu!
 
wee unapimaje umaarufu,mbona alikua rumande sasa amepiganiaje hiyo haki,na kama ni hivyo kuwekwa rumande ndio umaarufu basi mch. mtikila ndie jembe zaidi kuliko yoyote tanzani.
 
sio kwata ni gwaride kabisa, wanalijua, wanajua wanalicheza bt hakuna jinsi, NGUVU YA UMMA ITASHINDA, CHADEMA NDIO IMANI YETU!

Nguvu ya ilikuwa wapi sasa? mie nilitegemea wakati yuko pale central ndio tungeona nguvu ya umma. Ila jamaa walimwagia maji washa washa wote wakakimbia aisee
 

Kwa kweli JK sasa ndo ameishiwa kabisa: kuwatuhumu viongozi wa dini kwa kujihusisha na madawa ya kulevya? ingekuwa bora kama angewataja wahusika badala ya ku genralize. hivi, inawezekana Yule mpiga ramli wake amefufuka na kumwambia upuuzi huo. Huu ni wakati mgumu sana kwa JK.

Mapambano bado yanaendelea. Lazima hatimaye kieleweke!
 
Pia nadhani kuna tatizo la ufahamu wa taratibu ndani ya jeshi la polisi. RPC wa Mwanza labda ndiye anayefaa kuwa IGP.
 

Waweza tu kumuapisha akawa rais wa familia yenu ubaya upo wapi kwani , ila yule wa watanzania aliisha apishwa !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…