Hatimaye Mbowe apewa dhamana

Hatimaye Mbowe apewa dhamana

Mwenyekiti wa chadema ameshaachiwa na sasa watu wamembeba juu juu Arusha

Haya mambo yanayofanywa na serikali pamoja na kutumia vyombo vyake vya usalama ni mambo ya aibu sanaa kwa nchi inayojigamba kuwa imekuwa katika mambo ya demokrasia!!! hizi ndiyo kero ambazo hata wakimpotezea Lowasa, Rostam na Chenge bado ni suala la kutwanga maji kwenye kinu maana watanzania waliowengi huichukia serikali kwa kero kama hizi.
 
Nilianza kumsikia kwa mbali alipochaguliwa kuwa mbunge Hai mwaka 2000

Alipata umaarufu zaidi alipochaguliwa kuwa mwenyekiti wa CHADEMA (2004?)

Alipata umaarufu sana alipogombea uraisi mwaka 2005, zaidi kwa kuanzisha styles za helkopta na magwanda, ambazo ni maarufu hadi leo

Alikuja kuvuma tena sana wakati wa operesheni sangara.

Katika uchaguzi uliopita, hakuvuma sana (kwa sababu ya kuwepo Slaa katika uraisi?)

Alikuja kuvuma zaidi wakati wa kuundwa kwa kambi ya upinzani

Aliendelea kuwa midomoni mwa watanzania katika matukio tofauti kwa kiwango tofauti hadi Ijumaa tarehe 3 June 2011

Kwa siku tatu mfululizo Kuanzia Ijumaa jioni, hadi leo asubuhi, Freeman Aikaeli Mbowe amengeza mstari mwingine katika historia yake ya kupigania wanyonge Tanzania. Mstari ambao kwa wanaofuatilia vyombo vya habari na kusikiliza maoni ya watu ya kisiasa, bila shaka unastahili kuandikwa bolded zaidi, na kwa font kubwa zaidi, angalau kuliko mistari yote iliyowahi kuandikwa siku ya nyuma...
Nakubaliana na wewe Mkuu, CCM hawasomi alama za nyakati, wanatumia vyombo vya dola wakidhani wanammaliza kisiasa CDM kumbe wanapandisha chati........Peoples'........!!!
 
Your analysis is short-sighted focusing on two days personal discomfort and lack long term strategic vision chances are your FISADI. THINK TWICE B4 YOU PRESENT your BS!!!!
 
waswahili tunasema utabaki na labda. CDM kuiona ikulu bado ni ndogo ya zuzu.

Asiyejua kwamba Watanzania walio wengi wameichoka CCM ndio yuko kwenye usingizi wa pono. Suala ni je CCM wataweza kuiba hela za umma kuwawezesha kuchakachua tena 2015 na je CDM wataweza kujipanga kulinda kura zao? Na jinsi mambo yanavyoenda CDM wako na advantage.
 
wanaongoza nchi kwa mazoea ya siasa za chama kimoja, sasa ndiyo matokeo yake haya - kujichanganya changanya kwa mihimili hii mitatu.

sasa hivi chadema ina support kubwa ya wananchi - na hii kamata kamata ndiyo inawamaliza CCM kabisa - "killing themselves softly"


Mkuu hapa ni home of great thinkers , mie nilitegemea uje na takwimu useme hivi sasa CCM wana wanachama kadhaa, na cdm kadhaa, CUF kadhaa, sasa kusema wengi , wanaweza kuwa hata 1000 ni wengi pia. Ila fanya uchunguzi utakuta usemacho kwenye hali halisi sicho. Maneno yakujifariji hayo !
 
wakimaliza miaka mitano watakuwa hawana tena hamu ya kuongoza tz, sasa hivi wanaona aibu kuachia ila moyoni wanatamani sana kuachia ngazi
 
Ccm wamempiga teke chura wakifikiri wanamkomoa!.Wananchi wanazidi kupata mwanga zaidi kuwa nani yupo upande wao.
 
Asiyejua kwamba Watanzania walio wengi wameichoka CCM ndio yuko kwenye usingizi wa pono. Suala ni je CCM wataweza kuiba hela za umma kuwawezesha kuchakachua tena 2015 na je CDM wataweza kujipanga kulinda kura zao? Na jinsi mambo yanavyoenda CDM wako na advantage.

Napenda unijibu haya yafuatayo kwa ufasaha :
1. Kura zinaibwaje ?
2. Kura zinachakachuliwaje ?
3. Kura zinalindwaje ?
 
HIVI NGOJA NIULIZE, mbona Slaa alipoitwa mahakamani alienda bila tatizo? Kwa nini Mbowe hakwenda as required? Na kama alikuwa na jambo muhimu la kufanya,kwa nini mwanasheria wake hakutoa taarifa mapema?
 
Yapo kila Wilaya , na maji yake yanawasha balaa, ukimwagiwa yale maji hakuna la zaidi ya kukimbia tu. Na sio maji tu, jamaa wana silaha za kijeshi pia full masinonda kwa lolote. Hiyo ndio dola sasa
Dola inayotamka Bungeni (through PM) kuwa mafisadi wakiguswa nchi itasambaratika? hiyo sio dola hata kidogo ila kundi la matapeli.
 
wakimaliza miaka mitano watakuwa hawana tena hamu ya kuongoza tz, sasa hivi wanaona aibu kuachia ila moyoni wanatamani sana kuachia ngazi

Kumbe mna hamu na Ikulu, hilo sasa watanzania bado hawajawaruhusu, subirini labda 2050
 
wee unapimaje umaarufu,mbona alikua rumande sasa amepiganiaje hiyo haki,na kama ni hivyo kuwekwa rumande ndio umaarufu basi mch. mtikila ndie jembe zaidi kuliko yoyote tanzani.

Elewa topic kwanza mkuu...
Sijamfananisha na Mtikila, wala sijasema yeye ni maarufu kuliko mtu yeyote Tanzania
Unaelewa maana ya umaarufu?
Kuna watanzania wangapi leo wako rumande? au wanasafirishwa kwenda mahakamani? au wamesomewa mashitaka?
Naomba utumia kamusi yako kuangalia maana ya neno 'umaarufu'...
 
ili kodi inayokusanywa na ccm iende wapi? kama mmeshindwa kuongoza nchi si mkae pembeni we ndunya
 
huyu hakimu naomba nipate detail zake maana nina mtu nilisoma naye Kahunda sekondari (senegerema) mwaka 1996 the same name Charles Magessa kama ni huyo najua ana misimamo ya ajabu sana sijui kama ni yeye au la. pleaseeeeeeeeee kama kunamtu anamfahamu naomba anijulishe hapa.
 
Duh, wewe kweli hujui ku analyse mambo, hiyo ni kinyume chake sasa ! Jamaa wamemdhalilisha sana na hata wabunge wenyewe wamesema. N aelewa kuwa suala la bajeti ni suala la bunge sio la mbowe, sasa hapo pipoz powa inahusika vp?. Jamaa wamemkamata kama ndege, wameenda kumlaza sakafuni, wamemsafirisha usiku hakupata usingizi huoni heshima imepungua?. Na isitoshe hili ni suala la kisheria wala CCM haihusiki hata chembe, wenzake wao walienda mahakamani wakamdanganya mwenzao amedhalilika sana .

Wengine tuko kwenye vita ya kuikomboa nchi yetu. Kulala sakafuni ni jambo la kawaida sana, tunalitegemea na tumeshalizoea. Ukishavaa kombat huwezi ogopa kulala sakafuni. Heshima unaipata kwa watu wanaokuheshimu. Kuna tofauti kubwa sana kati ya kukojolewa na kichaa na kukojolewa na mtu mwenye akili timamu analujua analolifanya. Na kwa taarifa yako CCM inahusika sana na hili jambo kwa kuingilia kazi za mahakama. Order ya kukamatwa Mbowe imetoka Lumumba.
 
wee unapimaje umaarufu,mbona alikua rumande sasa amepiganiaje hiyo haki,na kama ni hivyo kuwekwa rumande ndio umaarufu basi mch. mtikila ndie jembe zaidi kuliko yoyote tanzani.

:help::help:
 
waswahili tunasema utabaki na labda. CDM kuiona ikulu bado ni ndogo ya zuzu.

Nafikiri ni ndoto ya zuzu kwa CCM kushinda uchaguzi, na ni ndoto ya zuzu kwa CDM kutangazwa washindi. Ila mwisho wa CCM kung'ang'ania madaraka kwa mtutu wa bunduki haupo mbali. Ni nani aliamini Mubarak na chama chake leo hii wangekuwa powerless baada ya kujitangazia ushindi wa bunge kwa 90%?. Sooner or later mabadiliko makubwa ya uongozi yatafanyika Tanzania kwani mamlaka hutoka kwa wananchi na si kwenye umiliki wa maghala ya silaha.

Ni mwendawazimu pekee kuwa na mawazo kuwa upinzani Tanzania hauwezi kuongoza nchi. CCM inaweza kuzifanya ndoto hizi za upinzani kushindwa kuwa za kweli kwa kuhakikisha kuwa 90% ya vijana wana ajira zinazowaingizia kipato cha kukidhi mahitaji ya siku 30 kwa mwezi na ziada ya siku 15. Kuhakikisha rushwa imeisha Tanzania, kuhakikisha uchumi umekua, kujenga miundombinu, kuhakikisha usalama wa raia ni priority, kuondoa uonevu wa vyombo vya dola dhidi ya raia, kupatikana katiba mpya iliyotokana na wananchi. Haya yote yakifanyika siyo tu CCM inabaki madarakani bali itakuwa pia ni oneway ticket out of power. Watanzania wanahitaji kitu kipya na hilo halikwepeki. Ni nature tu, tena kitu kizuri ni kwamba hizi nguvu za ziada za dola zinazotumika sasa dhidi ya raia ni kama training ya uvumilivu na kuongeza ujasiri, the more they do the more people's fear will disappear.
 
Back
Top Bottom