Hatimaye Mbowe apewa dhamana

Uwezo wa hawa waheshimiwa wa kufikiri ni finyu saana, kwa nchi masikini yetu kama hii Tanzania utumie gharama zote hizo kubebana na mtu ambaye si jambazi sugu labda anaweza kutoroka. Kweli inaingia hakirini kweli hiyo??????????? Magari kwenda Air Port Ukonga, ndege Dar to KIA or Ars Aport, magari mahakamani yote hiyo ni gharama kwa mwananchi wa Tanzania!!!!!!!!! Hivi Watanzania wamekosa nini kwa Mungu wapewe adhabu za aina hii. Si busara zitumike ingawa kiasi jamani????????

Hilo ndio tatizo la nchi kuongozwa na watu wenye upeo mdogo wa kufikiri kama Jakaya Mrisho Kikwete! Hiyo ni sawa na laana!!
 
TLS ni NGO moja ya mawakili wanaoshindana kutajirika. Wapo tangu enzi hizo za Tanganyika lakini nchi imeshuhudia sheria za ajabu ikiwemo hii iloomuweka ndani Mh Mbowe, mikataba ya ajabu na mahakama za ajabu zilizooza kwa rushwa na baadhi yao wakiwa mawakala wazuri wa rushwa. Ni wakwepaji wazuri wa kodi za nchi hii. Wakae kimya tu. Hawana jipya.

Mh! Bar association hii ni NGO? Just thinking..
 
Heko TLS, angalau kuna sauti neutral imesikika.
Chama cha wanasheria Tanzania (Tanganyika Law Socitiety - TLS) kimesema mahakama haikutumia busara kwenye suala la Mh. Freeman Aikael Mbowe. Rais wa Chama hicho Francis Stolla akizungumza na Radio Sauti ya Ujerumani (Deutsche Welle) alisema katika kipindi hiki ambocho bunge la bajeti linakaribia mahakama ingeweza kusubiri mpaka shughuli ya bunge iishe kwani Mbowe ni mtu anayeweza kupatikana.

Aidha amesema hata polisi hawakutumia busara kutomwachia mapema na kumtaka aende mahakamani yeye mwenyewe, kwani ni mtu anayejulikana na si mhalifu sugu.
 
Kitu kimoja cha ajabu hapa, wanaodai Mbowe alidharau mahakama, watwambie kama ni kweli kwa nini amepelekwa Arusha hajasomewa shitaka lolote wala hajapewa adhabu yoyote! Mbona ccm wanajikanyaga sana?!
 
ilikuwa ni LAZIMA MH. Mbowe atoke, NGUVU YA UMMA ILIKUWA STAND BY KWA LOLOTE!
 
Kitu kimoja cha ajabu hapa, wanaodai Mbowe alidharau mahakama, watwambie kama ni kweli kwa nini amepelekwa Arusha hajasomewa shitaka lolote wala hajapewa adhabu yoyote! Mbona ccm wanajikanyaga sana?!
 
Kitu kimoja cha ajabu hapa, wanaodai Mbowe alidharau mahakama, watwambie kama ni kweli kwa nini amepelekwa Arusha hajasomewa shitaka lolote wala hajapewa adhabu yoyote! Mbona ccm wanajikanyaga sana?!

Inabidi IGP Mwema atoe statement na hata amwombe radhi Mbowe. Alichokisema hakimu Magessa leo ni kumkataa mdhamini wa awali wa Mbowe ambaye hakufika siku ile aliyotakiwa kufika. Hakimu alikiri kwamba washitakiwa ambao ni Wabunge waliomba udhuru wa kutohudhiria kutokana na vikao vya bajeti. Hakimu Magessa aliwakubalia lakini akasema sharti wadhamini wao wafike.

Leo hii Mbowe kapata mdhamini mwingine na Magessa kawapa washitakiwa ruhusa ya kutohudhuria mahkama siku kesi inatajwa hadi kikao cha bajeti kiishe, ila tu wadhamini ndiyo wafike.

Sijui akina Kova fuss yote hii na kupoteza hela za serikali bure ilikuwa ya nini.
 
Inabidi IGP Mwema atoe statement na hata amwombe radhi Mbowe. Alichokisema hakimu Magessa leo ni kumkataa mdhamini wa awali wa Mbowe ambaye hakufika siku ile aliyotakiwa kufika. Hakimu alikiri kwamba washitakiwa ambao ni Wabunge waliomba udhuru wa kutohudhiria kutokana na vikao vya bajeti. Hakimu Magessa aliwakubalia lakini akasema sharti wadhamini wao wafike.

Leo hii Mbowe kapata mdhamini mwingine na Magessa kawapa washitakiwa ruhusa ya kutohudhuria mahkama siku kesi inatajwa hadi kikao cha bajeti kiishe, ila tu wadhamini ndiyo wafike.

Sijui akina Kova fuss yote hii na kupoteza hela za serikali bure ilikuwa ya nini.


Kwenye highlight: Kwa kuwa Mbowe alikwenda mwenyewe central kujisalimisha siku ile ya Jumamosi, Kova na genge lake wangeweza tu kumwambia asikose kufika Arusha mahakamani Jumatatu. Lakini badala yake walipata amri kutoka juu kwamba lazima Mbowe adhalilishwe, apelekwe kwa ulinzi mkali kwa tarajio kwamba kutampunguzia umaarufu wake. Kinyume chake ndiyo kimetokea!

Halafu Kova anadai kwamba wanafuata sheria na siyo siasa! Hili suala la Mbowe limewaaibisha sana uongozi wa polisi wa Dar ukiongozwa na Kova, na inapasa Kova alitambue hilo.
 
Kwanini nguvu na juhudi kama hizi hazikutumika kumkamata Vithlani? Yule muasia aliyehusika na radar???? Hivi ni wapi ambapo taifa lingepata faida? Kama tungekuwa tumesharudishiwa zile $mln 12 leo si tungeweza kuziwekeza hata Tanesco? Hii juhudi kubwa namna hii kwa huyo Mbowe itazalisha nini kitakachosaidia kutatua matatizo yetu??
Huyu Hakimu naye yuko zaidi kutafuta masifa au ni maagizo??
Eee Mungu ibariki Tanzania, tujalie tupate angalau viongozi wachache wenye busara.
 
kwa kumwangalia tu kova ni dhahili ni mnyongaji, miaka ya nyuma watu makatili ndio walioingia kwenye jeshi la posili haya ni masalio.
ila mimi siwezi kumshanga sana kova anafafana na jk
jk anachangua watu anaofanana nao
kaweka mwema na mwema kawa mwema katulitea kova
stup....
 
Monday, 06 June 2011 19:41 newsroom



* Abainika ana kesi ya udhalilishaji kijinsia
SHAABAN MDOE NA LILIAN Joel, ARUSHA

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Arusha imemfuta mdhamini wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, kutokana na kukabiliwa na shitaka la udhalilishaji kijinsia. Mbowe anayekabiliwa na shitaka la uchochezi, alipandishwa kizimbani jana mahakamani hapo, baada ya kutiwa mbaroni na polisi mjini Dar es Salaam Jumamosi iliyopita. Alikamatwa ikiwa ni utekelezaji wa amri iliyotolewa na Hakimu Charles Magesa kutokana na kuidharau mahakama. Hati hiyo ilifutwa jana. Katika kesi ya uchochezi inayomkabili Mbowe, viongozi waandamizi wa
freeman%20mbowe.jpg

CHADEMA na wafuasi wa chama hicho, mwenyekiti huyo alidhaminiwa na Julius Margwe. Margwe hakuhudhuria mahakamani Mei 27, mwaka huu, kumwakilisha Mbowe kesi ilipotajwa, ambapo jana ilielezwa kuwa anakabiliwa na kesi katika Mahakama ya Mwanzo Maromboso, mjini hapa. Kutokana na hilo, mahakama imemfuta kuwa mdhamini wa Mbowe na kumtaka kiongozi huyo kutafuta mwingine wa kumwakilisha, ambapo hivi sasa anadhaminiwa na diwani wa kata ya Elerai, John Bayo. Awali, Margwe alipotakiwa kujieleza ni kwa nini hakufika mahakamani kutoa taarifa kuhusu mshitakiwa, alidai Mei 27, alikuwa akihudhuria kesi inayomkabili katika Mahakama ya Mwanzo Maromboso. Hakimu Magesa alimhoji Margwe ni kwa nini hakufika mahakamani Mei 30, mwaka huu, ambapo alidai alikuwepo lakini hadi muda wa mahakama ulipokwisha hakuitwa ili kutoa udhuru kwa niaba ya Mbowe.

Magesa alimtaka kueleza chumba cha mahakama kilichotumika kuendesha kesi siku hiyo, ambapo Margwe alidai ni ukumbi namba mbili wa mahakama. Jibu hilo lilimfanya Hakimu Magesa kupigwa butwaa na kumweleza Margwe kwamba si kweli, kwa kuwa chumba kilichotumika si hicho. “Mshitakiwa (Mbowe) unapaswa kutafuta mdhamini mwingine kwa kuwa huyu anakabiliwa na kesi inayomfanya ashindwe kutimiza masharti ya udhamini,” alisema Magesa. Alisema Margwe pia ameidanganya mahakama kwamba alikuwepo Mei 30, wakati si kweli. Wakili wa Serikali Juma Ramadhan akiwasilisha hoja kabla ya uamuzi wa Hakimu Magesa, aliiomba mahakama kumfuta mdhamini huyo na pia Mbowe apewe onyo kali ili asirudie kosa la kuidharau mahakama. Kwa upande wake, wakili wa utetezi Method Kimomogolo, alidai Mbowe alikuwa na ruhusa ya kuhudhuria vikao vya kamati za Bunge. Aliiomba mahakama iwapatie ruhusa ya kutohudhuria mahakamani Juni 24, mwaka huu, washitakiwa ambao ni wabunge ili wahudhurie mkutano wa Bunge unaoanza leo mjini Dodoma. Wabunge hao ni Mbowe (Hai), Philemon Ndesamburo (Moshi Mjini), Godbless Lema (Arusha Mjini) na Joseph Selasini (Rombo).

Hakimu Magesa alikubali ombi hilo na kuwataka washitakiwa wengine, kufika mahakama. Mbowe alifikishwa mahakamani hapo saa 2.18 asubuhi akiwa ndani ya gari la Mkuu wa Upepelezi mkoa wa Arusha, Leonard Paul, aina ya Toyota Land Cruiser, lenye namba za usajili T 322 BGT. Gari hilo liliingia mahakamani likiwa chini ya ulinzi mkali wa askari kutoka Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, alikokamatwa. Akizungumza baada ya kufutiwa hati ya kukamatwa, Mbowe alilisifu Jeshi la Polisi kwa kujali misingi ya haki na kufanya kazi bila uonevu. Mbowe alisema tangu alipokamatwa, kusafirishwa na kufikishwa mahakamani, hakuteswa au kunyanyaswa na askari waliokuwa wakimlinda.

Last Updated ( Monday, 06 June 2011 19:53 )
 
Awe makini sana na aina ya usafiri huu, maana wabaya wake ni rahisi sana kummaliza kwa style yankumtumbukiza kwenye mtaro. Au yaka mtokea yaliyompata mpambanaji wetu Pasco.

Pasco alikutwa na jambo gani Mkuu? hebu tupe habari maana tusidhani yatamtokea mmoja tu!
 
Wanasheria tuambieni sheria inasema nini sio huu utani baada ya kusoma upepo una elekea wapi............
 
MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe jana aliachiwa kwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, baada ya kusomewa mashtaka ya kutotii amri halali ya kuhudhuria mahakamani katika kesi inayomkabili ya kufanya mkusanyiko wa watu bila ya kibali na vitendo vya uchochezi.Aidha, mahakama hiyo imemkataa mdhamini wake wa awali, Julius Margwe baada ya kuwa na shaka na mwenendo wake. Diwani wa Kata ya Elerai (Chadema), John Bayo alijitokeza na kuwa mdhamini mpya wa Mbowe.

Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Charles Magesa alisema mdhamini huyo amekataliwa kutokana na kukiuka masharti ya kuhudhuria mahakamani hapo pamoja na kukabiliwa na kesi katika Mahakama ya Mwanzo Maromboso hivyo, kuamua kutoa nafasi kwa mdhamini mwingine.

Juzi, Mbowe alisafirishwa chini ya ulinzi hadi Arusha akitokea Dar es Salaam baada ya kukamatwa na polisi. Akizungumzia safari hiyo, Mbowe alidai kuwa alipelekwa kwa ndege ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) usiku wa manane huku akisindikizwa kwa magari manne ya askari wa kutuliza ghasia, kuanzia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) hadi mahakamani hapo huku akilalamikia hali hiyo na kusema ni matumizi makubwa ya fedha na rasilimali za umma.

"Wamenisafirisha kuja Arusha kwa ndege ya JWTZ kama mtuhumiwa wa ujambazi. Haya ni matumizi makubwa ya fedha na rasilimali za umma. Ile ndege ina uwezo wa kubeba zaidi ya watu 100, wametuleta watu watatu, mimi kama mtuhumiwa, Kamishna mmoja wa polisi Wilaya ya Ilala na Kamishna wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU)," alidai Mbowe.

Hata hivyo, JWTZ limekanusha likisema halikuwajibika na tukio hilo la kumsafirisha huku polisi nayo ikimtaka Mbowe asijitafutie umaarufu wa kisiasa kwa mgongo wa suala hilo.

Mbowe alifikishwa mahakamani mjini Arusha jana saa moja asubuhi akiwa chini ya ulinzi mkali. Alikuwa katika gari la polisi aina ya Toyota Land Cruiser VX, lililokuwa likisindikizwa na magari mengine manne ya FFU.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuachiwa kwa dhamana, Mbowe alisema hajutii kuwekwa mahabusu na kusafirishwa hadi Arusha.Pia alisema kukamatwa kwake na kuwekwa mahabusu kamwe hakutasitisha harakati za Chadema kudai haki na demokrasia ya kweli ndani na nje ya Bunge.Alisema alipokuwa katika mahabusu katika Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam, hakuteswa na polisi wala kupigwa lakini alikuwa chini ya ulinzi hadi alipofikishwa Arusha jana alfajiri.

Kukamatwa kwake mwishoni mwa wiki kulichafua hali ya hewa ya kisiasa baada ya juzi, mamia ya mashabiki wa Chadema kupiga kambi Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam, wakishinikiza mwenyekiti wao aachiwe huru kabla ya kupelekwa mahakamani Arusha.
Baadaye, juzi saa 7:00 usiku vyanzo huru vilidokeza kwamba Mbowe alisafirishwa kwa ndege hiyo ya JWTZ akiwa na maofisa waandamizi wa polisi kutoka Dar es Salaam na wanajeshi watatu.

Kauli ya JWTZ
Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe alisema hadi jana mchana hakuwa na taarifa zozote kuhusu jeshi kuwajibika katika suala hilo.
Alisema hilo lilikuwa suala la polisi na mahakama huku akisisitiza kuwa hajaona nafasi ya JWTZ katika mchakato huo.

"Ndiyo kwanza unaniambia wewe (mwandishi) kuhusu JWTZ kutumia ndege yake kumsafifirisha huyo mtu. Ninachoweza kukwambia hakuna kitu kama hicho na jeshi halikuwajibika kwa lolote," alisisitiza Mgawe na kuongeza:
"Tukio hilo linawahusu polisi na mahakama wao ndiyo wanaojua na ndiyo waliopaswa kuwajibika siyo jeshi. Kwa hiyo kama una vyanzo vyako vingine sijui sisi tunasema hakuna kitu kama hicho.''

Mahakamani Arusha
Baada ya kufikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka na kisha kuchiwa kwa dhamana, wafuasi wake waliokuwa wamefurika mahakamani hapo, walishangilia na kumbeba juu kwa furaha.

Kabla ya kuachiwa kwa dhamana Hakimu Magesa alisema mdhamini wa awali wa Mbunge huyo wa Hai, Margwe amekataliwa kwa sababu mbali na kuieleza uongo mahakama kuwa alikuwa akifika mahakamani hapo, haina sababu ya kuendelea naye kwani tayari ana kesi ya jinai ambayo hatima yake haifahamiki.Kuhusu Mbowe hakimu huyo alikiri kwamba mahakama iliruhusu washtakiwa wabunge kuhudhuria kikao cha Bunge la Bajeti , lakini kutokana na kukosekana kwa mdhamini wake, ndiyo sababu walitoa amri kwamba akamatwe.

“Ila sasa mkaendelee na vikao vyenu vya Bunge kama tulivyosema awali, lakini wadhamini wenu lazima waje mahakamani kila kesi itakapotajwa na tunaondoa amri ya kukamatwa na sasa utaendelea na dhamana yako ya awali,” alisema Magesa.

Kabla ya hakimu huyo kutoa uamuzi huo, alimpa nafasi Margwe ya kueleza sababu za kutofika mahakamani.
Margwe alisema Mei 27, mwaka huu hakufika kwa sababu alikuwa na kesi Mahakama ya Mwanzo Maromboso na Mei 30 alifika mahakamani lakini kwa sababu hakupewa nafasi ya kusema lolote, hakujitokeza.

Wakili upande wa utetezi, Method Kimomogoro aliiomba mahakama hiyo, kuondoa amri ya kukamatwa kwa mteja wake na kutaka apewe dhamana yake ya awali ili aweze kuhudhuria vikao vya Bunge la Bajeti ambalo yeye ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani.

Alimtetea mdhamini huyo kwa kutofika mahakamani na kusema kuwa hiyo ipo kwa kila mtu hata kwa mawakili akisema huwa wanasahau tarehe za mahakama na ndiyo sababu huziandika, hivyo kwa mwananchi wa kawaida ni lazima atasahahu tarehe hizo.

Wakili wa Serikali, Juma Ramadhani aliiomba mahakama hiyo itoe onyo kali kwa mshtakiwa kwa kutofika mahakamani hapo mara anapohitajika na pia kumtaka yeye na wenzake wawe na mawasiliano ya karibu na wadhamini wao ili wasikose kufika mahakamani hapo.

“Mnajua hii ni kesi ya jinai, lazima muwepo mahakamani na mkikosa lazima wadhamini wawepo ili kuondoa utata, ila hofu tuliyo nayo ni pale tutakaposubiri kikao cha Bunge kiishe ndipo washtakiwa waje mahakamani ni muda mrefu sana, hivyo naomba wakili wa utetezi awasiliane na washtakiwa kupata siku ya nafasi ili kuanza kutoa maelezo ya awali,” alisema Juma.Alisema hana shaka juu ya dhamana ya Mbowe isipokuwa mdhamini wake akisema hajui anachokifanya na kusema hafai kuwa mdhamini. Aliiomba mahakama kutoa uamuzi juu ya mdhamini huyo.

Hata hivyo, Wakili Kimomogoro alipinga hoja ya kutaka mahakama impe onyo Mbowe kwa sababu kosa lililojitokeza halikuwa ka kwake na kwamba Mahakama ilimpa udhuru Aprili 29, mwaka huu kesi hiyo ilipotajwa na kutoa sababu kwamba watakuwa katika vikao vya Bunge la Bajeti hivyo kuiomba mahakama imrejeshee dhamana yake ya awali.

Baadaye Hakimu Magesa alitoa uamuzi wa kumwachia Mbowe kwa dhamana ili aendelee na vikao vya Bunge la Bajeti hadi hapo Juni 24 mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa tena. Hata hivyo, Mbowe na wabunge wenzake wanaohusika na kesi hiyo, hawatakuwapo mahakamani katika tarehe hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari na wafuasi waliofurika mahakamani hapo mara baada ya kuachiwa, Mbowe alisema hakuwa na kosa la kukamatwa na ndiyo sababu mahakama haikumhoji hata swali moja.

“Ila mimi naheshimu mahakama, lakini sitakosa kusema pale wanapokosea kama vile baadhi ya watumishi wa mahakama wanakubali kupewa amri na viongozi wa serikalini ili mradi tu kutimiza matakwa yao,” alisema Mbowe.
Alisema hakukuwa na sababu za msingi za kutumia rasilimali za Serikali ambayo ni mali za umma na kumsindikiza kama mhalifu ilihali hakuwa hata na silaha moja.Alisema anashukuru kwamba polisi hawakumfanyia vitendo vyovyote vibaya isipokuwa walimnyima haki yake ya msingi ya kuwa na uhuru wa kuwasiliana na watu.


Wafuasi Chadema wasitisha shughuli za mahakama
Mamia ya wafuasi wa Chadema waliokuwa wamefurika katika Viwanja vya Mahakama hiyo walisababisha kusitishwa kwa muda kesi nyingine kutokana na eneo hilo kutawaliwa na kelele. Kesi nyingine ziliendelea kusikilizwa saa 5:00.

Wafuasi hao wa Chadema bila kujali eneo hilo la mahakama, walikuwa wakipiga kelele za 'peoples power' na baada ya Mbowe kuachiwa walianza kuimba: “Wamebana wameachia, wamebana wameachia,” huku wakimbeba kiongozi huyo juu juu.

Mamia ya watu walizuiwa kuingia ndani ya Mahakama hiyo huku polisi wakiwa wametanda kudhibiti uvunjifu wa amani.Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema mara kadhaa alikuwa akitoka nje ya Ukumbi wa Mahakama kuwaeleza wafuasi wa chama hicho kilichokuwa kikiendelea ndani huku akiwahimiza kutokatishwa tamaa katika kudai haki yao.

Lema alisema kukamatwa kwa Mbowe ni ishara ya ushindi wa chama hicho kuchukua dola miaka ijayo.
"Msihofu hata kina Mandela waliteseka hivi hivi, lakini baadaye walikamata dola na chama. Tutaongoza nchi hii miaka michache ijayo, hawa polisi watakuwa wakitulinda sisi badala ya kutukamata kamata," alisema Lema.

Maoni ya wananchi
Baadhi ya wakazi wa Arusha wameelezea kushangazwa kwao na matumizi makubwa ya fedha za umma katika kumkamata Mbowe na kumfikisha Arusha kisha kuachiwa kwa dhamana.
Mmoja wa wakazi hao, George Kavishe alisema kitendo cha kujisalimisha Dar es Salaam na kisha kusafirishwa kwa ndege ya jeshi na kusindikizwa kwa magari ya Serikali ni matumizi mabaya ya fedha za umma.

"Sasa kama walijua akifika hapa atapewa dhamana tu kwa nini wasingemalizia Dar es Salaam suala hili? Ni jambo la ajabu," alisema Kavishe ambaye ni mfanyabiashara. Mkazi mwingine Lucas Kaaya, alisema hatua ya polisi kumfikisha Mbowe mahakamani akiwa chini ya ulinzi imedhihirisha kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria.

"Ingekuwa sisi watu wa chini, leo hapa dhamana isingetoka tena tungepewa siku 14 za kukaa magereza sasa hili ni funzo tuheshimu vyombo vya sheria kwani hakuna amani bila haki," alisema Kaaya.

Polisi wadhibiti maandamano kwa amani
Polisi jana, walifanikiwa kuzima maandamano ya wafuasi wa Chadema ambao walikuwa wamejiandaa kufanya hivyo wakiwa wamebeba majani wakiashiria amani. Viongozi wa jeshi hilo walifanya mazungumzo na Mbowe na viongozi wa Chadema mkoani Arusha na kuwasihi waondoke mahakamani kwa magari yao, ili kuzuia maandamano yasiyo na kibali.

Baada ya kukubaliana, Lema aliamua kuondoka mahakamani hapo kwa pikipiki aina ya Toyo na wafuasi wachache, hasa vijana walianza kumfuata nyuma lakini walipofika makutano ya Barabara ya Nyerere walitawanywa na polisi.

Polisi:Mbowe hakuonewa
Akizungumzia kitendo cha Jeshi hilo kumkamata Mbowe, Kamishna wa Operesheni wa Polisi, Paul Chagonja alisema kuwa kiongozi huyo alikamatwa kama ilivyo kwa watu wengine na hakuonewa inavyodhaniwa na baadhi ya watu.
Aliwataka Watanzania kutokubali kutumiwa na wanasiasa wanaotaka umaarufu kwa nguvu kwa kulazimisha kufanya maandamano kinyume na sheria.

Chagonja aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa, kiongozi anayetaka kuingia madarakani kwa mtindo wa kushawishi wananchi kufanya maandamano si mzuri.

“Wapo viongozi wa kisiasa wanaotumia wananchi kujipatia umaarufu. Nawaonya wananchi wakumbuke kwamba yatakayowapata ni hasara kwa familia zao, kwa nini ukubali kushinikizwa na mtu mwenye lengo la umaarufu na wewe unakubali?”

“Alikamatwa baada ya kushindwa kutii amri ya mahakama ni utovu wake wa nidhamu na sheria iko wazi kwamba kama mtu hajafika mahakamani bila sababu za msingi hati ya kukamatwa inatolewa. Kama kuna ugomvi, Chadema ingeilalamikia mahakama si Jeshi la Polisi.”

“Nchi hii ni ya amani, mtu yeyote atakayeleta uchokozi hatutamuonea aibu, hatuwezi kukubali kumnyamazia mtu wa namna hii, kama anachimba shimo basi atumbukie mwenyewe,” alisema Changonja na kuongeza:“Mbunge akitoka nje ya Ukumbi wa Bunge atapigwa pingu tu, maneno yanayosemwa kuwa mbunge ana kinga ni ya kutapatapa tu.”

Kaimu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Peter Kivuyo alisema katika mafunzo ya jeshi hilo kuna aina moja tu ya kumkamata raia: “Ili kumkamata Rais wa nchi kuna taratibu zake, lakini watu wengine wanakamatwa kwa mujibu wa sheria zilizopo.”

Katika hatua nyingine, Jeshi hilo Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linawashikilia watu watatu wakiwamo wanafunzi wawili wa vyuo kwa tuhuma za kufanya fujo na maandamao, huku wakiwa na mabango yenye ujumbe unaochochea nchi kuingia katika machafuko ya umwagaji wa damu.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema waliokamatwa ni pamoja na mwanafunzi mmoja wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ambaye ni mkazi wa Kijitonyama na mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) anayeishi katika Hosteli za Mabibo pamoja na mkazi mwingine wa Tegeta.

Kova alisema kukamatwa kwa watu hao kunatokana na vurugu zilizojitokeza baada ya Mbowe kukamatwa na jeshi hilo kwa kukaidi agizo la mahakama.
Kova alisema kumejitokeza tabia ya baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa kuwachochea vijana kuingia mitaani kufanya fujo kwa madai ya kuwa wanadai haki yao kikatiba.

“Jeshi la polisi haliko tayari kuvumilia tabia hii na tutatoa adhabu kali kwa yeyote atakayehusika kuwahamasisha au kuwachochea vijana kuleta machafuko. Kama fujo za jana (juzi) zilizochochewa na viongozi wa ngazi za juu wa vyama vya siasa kuhamasisha vijana kuingia mitani wakiwa wamevaa fulana pamoja na kubeba mabango yenye ujumbe unaochochea nchini kuingia katika machafuko ya umwagaji damu,” alisema.

Habari hii imeandaliwa na Mussa Juma na Moses Mashalla, (Arusha); Ramadhan Semtawa, Fidelis Butahe, Hadija Jumanne na Aziza Masoud (Dar).



View attachment 31609

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiwa amebebwa na wafuasi wa chama hicho, baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, kukubali dhamana ya kesi yake, muda mfupi baada ya kufikishwa Arusha akiwa chini ya ulinzi mkali wa Polisi. Picha na Mussa Juma
 
Mbowe aachiwa, mdhamini alimponza

KUKAMATWA kwa Mwenyekiti wa Chadema ambaye pia ni Kiongozi wa Upinzani bungeni, Freeman Mbowe, kulisababishwa na mdhamini wake.

Julius Margwe ambaye jana alikataliwa na Mahakama ya Hakimu Mkuu Mkazi wa Mkoa wa Arusha kuendelea kumdhamini Mbowe, alikiuka masharti ya Mahakama kwa kutofika mahakamani kumwakilisha mdhaminiwa ambaye naye hakuwapo Mei 27.

Hakimu Charles Magesa badala yake jana alimkubali John Bayo ambaye ni Diwani wa Elerai mkoani Arusha kuwa mdhamini mpya wa Mbowe.

Mbowe aliachiwa jana kwa dhamana baada ya kusafirishwa kwa ndege maalumu kutoka Dar es Salaam alikokuwa akishikiliwa tangu Jumamosi, baada ya Hakimu Magesa kuamuru akamatwe mara moja kwa yeye na mdhamini wake kutofika mahakamani siku hiyo.

Magesa, alisema, hawezi kumkubali tena mdhamini Maligwe kumdhamini Mbowe, kwani alishindwa kutii amri ya kufika mahakamani, mshitakiwa aliposhindwa kufika.

Baada ya kukubaliwa dhamana na kuachiwa, mamia ya watu waliofurika mahakamani hapo wakiwamo wafuasi wa Chadema, walilipuka kwa shangwe, vifijo na vigelegele na kumbeba hadi nje ya chumba cha mahakama.

Walisikika wakiimba nyimbo zikiwamo zenye ujumbe wa kumkataa Meya wa Manispaa ya Arusha, Gaudence Lyimo.

Akizungumza mahakamani, Hakimu Magesa, alisema kutokana na mdhamini huyo kukiuka masharti ya kuhudhuria mahakamani, kwa sababu kwamba naye anakabiliwa na kesi katika Mahakama ya Mwanzo ya Maromboso, ameamua kutoa nafasi kwa mdhamini mwingine.

"Mahakama hii imeona kuwa mdhamini huyu ana makosa na hawezi kueleza mahakamani hapa ukweli kuhusu tarehe alizokuwa anahudhuria, tunaona hana sifa za kuwa mdhamini na hivyo tunamkubali John Bayo awe mdhamini wa Mbowe," alisema Magesa.

Alisema mbali na kusema uongo mahakamani hapo kuwa alikuwa akifika mahakamani, bado Mahakama haina sababu na kuendelea naye kwa sababu tayari ana kesi ya jinai ambayo hatma yake haifahamiki.

Kuhusu Mbowe, Hakimu alisema, ni kweli Mahakama iliruhusu washitakiwa wabunge wahudhurie vikao vya Bunge la Bajeti na hivyo hawana sababu na Mbowe, ila kutokana na kukosekana kwa mdhamini wake, ndiyo sababu walitoa amri ya kukamatwa kwake.

"Ila sasa mtaendelea na vikao vyenu vya Bunge, ila wadhamini wenu lazima waje mahakamani kila kesi itakapotajwa na tunaondoa amri ya kukamatwa na sasa utaendelea na dhamana yako ya awali," Magesa alimwambia Mbowe.

Kabla ya Hakimu kutoa uamuzi huo, alimpa nafasi Maligwe aeleze sababu za kutofika mahakamani.

Akijieleza, Margwe alidai kuwa Mei 27, hakufika kwa sababu alikuwa na kesi katika Mahakama ya Mwanzo ya Maromboso na Mei 30 alifika mahakamani ila kwa kuwa Mahakama haikumpa nafasi ya kusema lolote, hakujitokeza.

Awali kabla ya uamuzi kutolewa na Hakimu, Wakili wa Utetezi, Method Kimomogoro, aliiomba Mahakama, iondoe amri ya kukamatwa kwa Mbowe na kutaka apewe dhamana yake ya awali, ili aweze kuhudhuria vikao vya Bunge la Bajeti ambalo yeye ni kiongozi wa Upinzani.

Aidha Wakili huyo alimtetea mdhamini wa Mbowe kwa kutofika mahakamani na kudai kuwa hiyo ipo kwa kila mtu na hata wao mawakili husahahu tarehe za mahakama na ndiyo sababu huandika, hivyo kwa mwananchi wa kawaida ni lazima asahau tarehe.

Pia alipinga kauli ya Wakili wa Serikali ya kutaka Mahakama impe onyo Mbowe kwa sababu kosa si lake na Mahakama ilimpa udhuru Aprili 29, kesi hiyo ilipotajwa na kutoa sababu ya kuwa watakuwa katika vikao vya Bunge la Bajeti na kuomba Mahakama imrejeshee dhamana yake ya awali.

Wakili wa Serikali, Juma Ramadhani, aliiomba mahakama hiyo itoe onyo kali kwa mshitakiwa, kwa kutofika mahakamani na pia kumtaka mshitakiwa na wenzake wawe na mawasiliano ya karibu na wadhamini wao, ili wasikose mahakamani hapo.

"Mnajua hii ni kesi ya jinai na kama ni ya jinai lazima muwepo mahakamani na mkikosa lazima wadhamini wawepo, ili kuondoa utata, ila hofu tuliyonayo sisi ni pale tutakaposubiri Mkutano wa Bunge uishe ndipo washitakiwa waje mahakamani … ni muda mrefu sana, hivyo naomba wakili wa utetezi awasiliane na washitakiwa kupata siku ya nafasi ili kutoa maelezo ya awali," aliomba Ramadhani.

Alisema kwamba kuhusu dhamana ya Mbowe hana shaka nayo, isipokuwa mdhamini wake hana uhakika na hajui nini anachokifanya, hivyo hafai kuwa mdhamini na kuomba Mahakama itoe uamuzi wa mdhamini huyo.

Baada ya pande hizo zote kuzungumza, Hakimu alimwachia huru kwa dhamana Mbowe na kutoa idhini ya kuendelea na Mkutano wa Bunge la Bajeti hadi Juni 24 mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa tena.

Akizungumza na wafuasi wa Chadema pamoja na waandishi wa habari, kwenye viwanja vya Mahakama hiyo, mara baada ya kuachiwa huru kwa dhamana, alisema inasikitisha kuona Serikali inatumia nguvu kubwa ya kumdhibiti kama mhalifu.

Kwa mujibu wa Mbowe, Serikali ilitumia ndege ya Jeshi yenye uwezo wa kubeba watu 100, ambayo ilichukua watu watatu; yeye, Kamishna wa Polisi Kanda ya Ilala na Kamishna wa Polisi wa Kikosi cha Kuzuia Ghasia wa Tanzania (FFU) hadi uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) saa 9 alfajiri kuamkia jana.

Pia alisema mbali na kusafirishwa kwa ndege hiyo kubwa, pia kulikuwa na magari manane ya FFU ambayo yalikuwa na mabomu na silaha kama wanasindikiza mhalifu.

Mbowe alisema hakuwa na kosa la kukamatwa na ndiyo sababu mahakama haikumhoji hata swali moja, kwa sababu waliona mwenye shida ni mdhamini wake.

"Ila mimi naheshimu Mahakama, lakini sitakosa kusema pale wanapokosea, kama vile baadhi ya watumishi wa Mahakama kukubali amri za viongozi wa Serikali, ilimradi tu kutimiza matakwa yao," alisema Mbowe.

Alisema hakukuwa na sababu za msingi za kutumia rasilimali za Serikali ambazo ni mali za umma kumsindikiza kama mhalifu, mtu ambaye hakuwa na silaha.

"Mimi nasema nawashukuru wananchi na viongozi wote walioshiriki kunitia moyo wakati huu wa siku mbili nilizokaa ndani," alisema na kuongeza kuwa anaahidi kufanya kazi nzuri katika mkutano wa Bunge la Bajeti unaoanza leo.

Hata hivyo, alisema anawashukuru polisi kutomfanyia unyama, kwani walikaa naye vizuri, isipokuwa alinyimwa haki yake ya msingi ya kuwa na uhuru wa kuwasiliana na watu.
Katika kesi hiyo inayomkabili Mbowe na wabunge 13 wa Chadema, wanadaiwa kuandaa mkutano na kuandamana kinyume cha sheria Januari 2011.

Wengine katika kesi hiyo ni Kabwe Zitto, Halima Mdee, Godbless Lema, Suzan Kiwanga, Ezekia Wenje, Christina Lissu, Paulina Gekulu, Israel Natse, Suzane Lyimo, Joseph Mbilinyi, Rahya Ibrahimu, Joyce Mukya na Joseph Selasini.

Baadhi ya wananchi waliozungumza na waandishi wa habari jijini hapa, walieleza kusikitishwa na magari na polisi wenye mabomu na silaha, kutanda kona zote za Jiji, kana kwamba kulikuwa na wahalifu wakubwa wanaoletwa jijini. Walidai hali hiyo ilisababisha wasiwasi kiasi cha baadhi ya maduka kufungwa.

Flora Mwakasala anaripoti kutoka Dar es Salaam, kwamba wanachama watatu wa Chadema walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kwa tuhuma za kuandamana bila kibali na kusababisha uvunjifu wa amani.

Washitakiwa hao ambao walisomewa mashitaka mawili mbele ya Hakimu Sundi Fimbo, ni Jenerali Kaduma, Juliana Daniel na Joseph Msetti.

Kulingana na taarifa iliyotolewa jana na Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi Dar es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi, Suleiman Kova, Kaduma ni mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na mkazi wa Kijitonyama, Daniel ni wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mkazi wa hosteli za Mabibo na Msetti ni mkazi wa Tegeta, Dar es Salaam.

Wakili wa Serikali, Elizabeth Kaganda, alidai mahakamani hapo kuwa Juni 5 eneo la Ufipa, Kinondoni, Dar es Salaam, washitakiwa hao na wenzao ambao bado hawajafahamika, walikula njama za kutenda kosa hilo.

Ilidaiwa kuwa juzi saa 11 jioni Magomeni, washitakiwa walifanya mkusanyiko na kuandamana bila kibali, kitendo kilichosababisha uvunjifu wa amani kwa wakazi wa eneo hilo.
Washitakiwa ambao wanatetewa na Wakili Mabere Marando, walikana mashitaka na upande wa mashitaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Hakimu Fimbo alisema dhamana iko wazi endapo washitakiwa watatimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili wanaofanya kazi katika kampuni zinazotambulika, ambao watasaini hati ya Sh milioni nne.

Upande wa mashitaka uliiomba Mahakama iwape muda wa siku moja wapitie na kukagua barua za wadhamini kwa kuwa kipindi hiki kimekuwa na wadhamini waongo.

Hakimu Fimbo aliahirisha kesi hiyo hadi leo, kwa ajili ya kutoa dhamana kwa kuwa wadhamini waliofika walikuwa si waajiriwa na wengine hawakuwa na barua wala vitambulisho vya kazi.
 
Mbowe atikisa nchi

• DK. SLAA ASEMA HUU NI MWISHO WA UVUMILIVU WAO

HATUA ya polisi kumshikilia Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, imeibua simanzi na hasira miongoni mwa viongozi, wanachama, mashabiki wa CHADEMA na watetezi wa demokrasia ya vyama vingi.

Hali hiyo ilianza kujionyesha mapema jana asubuhi jijini Dar es Salaam na katika mikoa mingine nchini baada ya taarifa za kukamatwa kwa kiongozi huyo kusambaa.

Tofauti na ilivyo ada, eneo zima linalozunguka Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam anakoshikiliwa kiongozi huyo lilikuwa limezingirwa na Askari wa Kutuliza Ghasia (FFU) waliokuwa na zana za kijeshi.

Ili kuhakikisha kuwa hali inakuwa ni ya usalama, askari hao walikuwa wakirandaranda na kuwauliza watu waliokuwa wameanza kukusanyika katika eneo hilo shughuli walizokuwa wakifanya katika maeneo hayo.

Hata hivyo askari hao hawakuweza kuwazuia vijana walioanza kukusanyika eneo hilo na kuimba nyimbo za kulaani kukamatwa kwa kiongozi huyo kabla ya askari hao kutoa tangazo la kuwatawanya.

Katika eneo la Magomeni, polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanachama na wapenzi wa CHADEMA waliokuwa wakiandamana kuelekea Kituo Kikuu cha Polisi kulaani na kupinga kukamatwa kwa Mbowe.

Katika ofisi za makao makuu ya CHADEMA zilizoko Kinondoni, Katibu Mkuu wa chama hicho, Willibrod Slaa, aliitisha mkutano wa waandishi wa habari na kulaani tukio la kukamatwa kwa Mbowe na lile la kushikiliwa kwa muda na polisi mjini Singida kwa Naibu Katibu Mkuu wao, Zitto Kabwe.

Akizungumza kwa hasira, Dk. Slaa aliwataka wanachama na wapenzi wa chama hicho nchi nzima kujitokeza hadharani na kuchukua hatua za kupinga unyanyasaji na ukiukwaji wa demokrasia unaofanywa na jeshi la polisi na serikali ya CCM.

Katika tamko hilo, Dk. Slaa alisema viongozi wake hao waliokamatwa juzi, hawakukamatwa kwa mujibu wa sheria bali walikamatwa kwa mujibu wa maagizo ya kisiasa ya CCM, ambayo imeamua kutumia udikteta ili kujaribu kudhoofisha harakati za chama hicho za kuikomboa nchi.

Dk. Slaa ambaye kwa kawaida huzungumza taratibu na kwa upole, aliwataka wana CHADEMA kuacha kile alichokiita ukondoo na uvumilivu ambao wamekuwa wakiuonyesha siku zote.

Alisema tayari chama chake kimeshawasilisha malalamiko yote rasmi kwa Bunge la Uingereza (House of Commons) na vyama vya mabunge vya kimataifa kama "International Parliamentary Union" ili vichukue hatua za kidiplomasia za kukomesha unyanyasaji wanaofanyiwa wabunge wa upinzani Tanzania.

Pia alisema wameshawasilisha taarifa rasmi na yenye ushahidi wa kutosha kwa serikali ya Uingereza ya kuitaka ichukue hatua dhidi ya serikali ya Tanzania, kwani mabilioni ya pesa yaliyotolewa na nchi hiyo kwa ajili ya mafunzo na programu nzima ya uboreshaji wa Jeshi la Polisi, yamefujwa huku polisi wakiwa bado hawajaelimika jinsi ya kuwatendea haki raia kwa mujibu wa sheria.

"Kamanda wa Upelelezi wa Mkoa (RCO) alinipigia simu akiniomba niwasihi wale vijana waondoke pale kituoni, na mimi nilimwambia sitawaambia waondoke. Sasa natangaza kuwa wafuasi wetu wote, nchi nzima sasa ni ruksa kuingia barabarani kupinga unyanyasaji huu. Viongozi waliokamatwa ni viongozi wa Watanzania.

"Asitokee mtu akatuambia tunakosa uzalendo, asitokee mtu akatuambia tunaharibu amani ya nchi. Wanaoharibu amani ya nchi ni Kikwete, CCM, na Jeshi la Polisi. Uvumilivu wetu umefika mwisho, ukondoo wetu umefika mwisho," alisema Dk. Slaa na kushangiliwa na wafuasi kadhaa waliokuwa wakisikiliza tamko hilo.

Dk. Slaa alitumia muda mwingi kueleza jinsi Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi ya mkoani Arusha, alivyokiuka vipengele kadhaa vya sheria kwa sababu za kisiasa, ili kujaribu kumdhalilisha na kumnyamazisha Mbowe na wabunge wa chama hicho, hasa katika kipindi hiki wanapokwenda kuipa changamoto kubwa serikali katika mkutano wa Bunge la Bajeti.

Alisisitiza kuwa, haikuwa halali kwa hakimu huyo kuamuru Mbowe akamatwe, kwani tayari alishatoa ruksa rasmi ya kimahakama ambayo iliwapa uhuru wa kuhudhuria shughuli za Bunge, wabunge wote wa chama hicho wanaokabiliwa na kesi hiyo iliyotokana na maandamano yaliyofanyika Arusha Januari 5 mwaka huu.

Katika tamko lake hilo, Dk. Slaa alieleza mambo makuu manne kuthibitisha jinsi hakimu huyo anavyoiendesha kesi hiyo kisiasa badala ya kufuata sheria.

Kwanza alisema hakimu huyo alishatoa ruksa rasmi ya kuwaruhusu Mbowe na wabunge wenzake kuendelea na shughuli za bunge, lakini kwa makusudi uamuzi wa ruksa hiyo haukurekodiwa kimaandishi katika kumbukumbu za mwenendo wa kesi hiyo kama ilivyo kawaida.

Hawakufanya hivyo ili kujijengea uhalali wa kuja kumkamata Mbowe kama walivyofanya.

Pili, alisema hakimu huyo hadi Ijumaa iliyopita wakati anatoa amri hiyo, alikuwa bado hajatoa hati ya kuitwa kwa mdhamini wa Mbowe ili ajieleze kwanini yeye na mshtakiwa wake hawajaonekana mahakamani kama taratibu za uendeshaji wa kesi zinavyotaka.

Badala yake, alisema kuwa hakimu huyo alikimbilia kutoa amri ya kutaka Mbowe akamatwe ili kutimiza kile alichoagizwa na serikali ya CCM.

"Na mdhamini wa Mbowe hakuweza kufika mahakamani kwa sababu ni mgonjwa, sasa anakimbilia kutoa amri ya kutaka watu wakamatwe bila kutoa haki ya mdhamini kujieleza….hii si sheria, ni siasa," alisema Dk.Slaa.

Tatu, alisema wakati hakimu huyo anaamuru Mbowe akamatwe wakili wake hakuwepo mahakamani kwa sababu alikuwa akihudhuria kesi nyingine mbele ya Jaji kutokana ratiba za kesi kugongana.

Alisema kwa sababu wakili wa mshitakiwa Mbowe alikuwa akihudhuria kesi nyingine, kesi hiyo ilipaswa kuahirishwa siku hiyo kama taratibu za kisheria zinavyotaka, lakini kwa sababu ya kutaka kuifurahisha serikali ya CCM iliyomtuma, hakimu huyo hakufanya hivyo.

Badala yake aliiendesha kesi hiyo bila wakili kuwepo na akatoa hati ya Mbowe kukamatwa.

"Kwanza kesi yetu huanza saa 3:00 asubuhi, lakini katika hali isiyo ya kawaida siku hiyo alianza kesi hiyo mapema, saa 2:30 huku akijua fika kuwa wakili wa Mbowe hayupo. Sasa mdhamini wa mshtakiwa hakuwepo na hakuwa amepewa hati ya kuitwa kujieleza, na wakili wake pia hakuwepo alikuwa mbele ya Jaji akihudhuria kesi nyingine.

"Kwa taratibu za kimahakama, alipaswa kuiahirisha kesi hiyo, lakini yeye ili aifurahishe serikali iliyomtuma, aliiendeleza na kuamuru Mbowe akamatwe," alisema Dk. Slaa.

Nne, Dk. Slaa alisema hata yeye na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, walipokwenda wenyewe mahakamani hapo wiki iliyopita, bado hakimu huyo alionekana kuwasikiliza wanasheria wa serikali waliotaka kesi hiyo isiendelee mpaka wakamatwe na polisi, wakati kwa taratibu za kisheria hati ya kumkamata mshitakiwa huisha mara tu mshitakiwa huyo anapokuwa ndani ya mahakama.

"Lengo lao lilikuwa lazima watukamate hata ndani ya mahakama, ili mradi tu watekeleze mkakati wao wa kutaka kutukandamiza na kutudhalilisha, sisi tulikataa….tulisema polisi hamjui sheria. Baada ya kubishana nao kwa hoja za kisheria ndio wakatuacha, vinginevyo hakimu yule alikuwa tayari tukamatwe mbele yake wakati ‘arrest warrant' inakwisha mara baada ya mshtakiwa kufika mwenyewe mahakamani," alifafanua Dk. Slaa.

Alisisitiza kwa namna yoyote Mbowe kwa nafasi yake kama mbunge na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni (KUB) hakupaswa kukamatwa wakati huu ambao anatekeleza majukumu mengi ya kibunge yanayohusiana na bajeti.

Alisema mbali na ruksa iliyokuwa imetolewa na ambayo kwa makusudi haikurekodiwa, pia hakimu alipaswa kujua kuwa kiongozi huyo alikuwa akihudhuria vikao vya kamati mbalimbali za Bunge, vikiwemo vile vya kamati za chama chake (party caucus) ambavyo vinatambuliwa na kanuni ya 110 ya Bunge.

Akizidi kuonyesha jinsi kamata kamata hiyo ya wabunge na viongozi wa upinzani ilivyo ya kisiasa badala ya kuwa ya kisheria, Dk. Slaa alisema Zitto alikamatwa juzi akiwa Singida kwa hoja kuwa alifanya kosa kuhutubia mkutano hadi saa 12:20 badala ya kumaliza saa 12:00 jioni.

Alisema huo pia ulikuwa ni uonevu wa dhahiri kwani sheria inasema wazi kuwa kwa wakati huu ambao si wa uchaguzi, mikutano ya kisiasa ruksa kufika hadi saa 12:30, kwa hiyo alifafanua kuwa Zitto hakukiuka sheria yoyote kuhutubia hadi saa 12:20.

Alisema kukamatwa kwa Mbowe na Zitto kutasababisha kikao cha kamati ya uongozi ya bunge kilichopangwa kukaa leo ili kupanga ratiba ya bunge la bajeti kisifanyike kama inavyotakiwa, kwani ni lazima mmoja wao kati ya viongozi hao wahudhurie kwa mujibu wa kanuni za Bunge.

"Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni ni mjumbe wa lazima katika kikao cha kamati ya uongozi ya Bunge, asipohudhuria ni lazima ateue mwakilishi wa kuhudhuria kama kanuni zinavyotaka, sasa tutamwambia Zitto asiende, kwa sababu anayepaswa kumteua kumwakilisha yupo ndani," alisema Dk. Slaa.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA), John Heche akizungumza na wanafunzi wahitimu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu, Augustine Mwanza, pamoja na mambo mengine, alitoa onyo kwa Rais Kikwete kuwa atakuwa rais wa kwanza kuandika historia mbaya kabisa ya kusababisha machafuko katika nchi hii iwapo hataacha kulitumia Jeshi la Polisi vibaya kukandamiza wapinzani.

"Tutaendelea kuheshimu sheria za nchi na kulinda amani ya nchi hii, lakini kamwe hatutalinda uonevu, dhuluma wala unyanyasaji unaoanza kufanywa kwa kasi na Jeshi la Polisi, kwa kuwakamata wabunge na viongozi wetu wa kitaifa bila sababu za msingi. Hatuko tayari kuvumilia udikteta wa serikali ya CCM inayotaka kuigeuza nchi yetu kuwa dola ya kipolisi. Tutapigania haki bila kuogopa risasi, mabomu na virungu vya polisi.

"Tunalionya Jeshi la Polisi na CCM, Tunamuonya Rais Kikwete, tunamtaka achunge mwenendo wa serikali yake na vyombo vyake vya usalama, vinginevyo atakuwa Rais wa kwanza kuandika historia mbaya ya kusababisha machafuko katika nchi hii. BAVICHA tunaendelea kufuatilia na tuko tayari kuchukua hatua. Busara na uwezo wetu wa kulinda amani na kupigania haki, si vya kutiliwa shaka," alisema Heche.

Wakati Heche akitoa kauli hiyo, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba ambaye alifika Kituo Kikuu cha Polisi na kukutana na Mbowe alilaani kitendo hicho cha polisi.

Mbali ya hilo, Profesa Lipumba alimtaka Spika wa Bunge kutoa tamko la kupinga kamatakamata hiyo ya wabunge wa upinzani ambayo imemgusa pia mbunge mmoja wa CUF.

Mbali ya Lipumba viongozi wengine wa kisiasa waliofika kituoni hapo kuonana na Mbowe ni Mbunge wa Ubungo, John Mnyika na Profesa Abdallah Safari.

Viongozi wa CHADEMA mikoani watoa tamko

Viongozi wa CHADEMA wa mikoa mbalimbali jana pia walitoa matamko ya kulaani na kupinga kukamatwa kwa Mbowe.

Mkoani Mara, Mkurugenzi wa Sera na Utafiti wa CHADEMA, Mwita Mwikwabe Waitara akisoma maazimio tisa ya mkutano mkuu wa dharura wa chama hicho kwa waandishi wa habari mjini Musoma jana alisema, kitendo cha polisi kumkamata Mbowe wakati wakielewa ni kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni hakivumiliki.

Alisema, endapo serikali na jeshi la polisi haitamwachia Mbowe mara moja, wana-CHADEMA wa mkoani Mara wataungana na mikoa mingine nchini kutumia nguvu ya umma ili kiongozi huyo aachiwe huru.

Waitara alisema kukamatwa kwa Mbowe ni kinyume cha sheria ya mwaka 1992 inayotoa kinga kwa wabunge kudhalilishwa hadharani na kusisitiza kwamba serikali inapaswa kuomba radhi kwa kitendo hicho, tena kinachofanywa kwa wabunge wa upande mmoja tu wa upinzani.

Mkoani Dodoma, viongozi wa chama hicho nao walitoa tamko hiyo jana wakitaka Mbowe aachiwe kwani vikao vya bajeti vinaanza kesho.

Tamko hilo lililosomwa na Katibu wa CHADEMA mkoa wa Dodoma, Steven Masawe, pamoja na kuungwa mkono na umoja wa vyuo vikuu mkoani hapa.

Kwa pamoja wameazimia kufanya maadamano ili kusitisha shughuli za Bunge kwa madai kuwa kama Mbowe hataachiwa, bunge halitakuwa na uwakilishi mzuri wa kutetea maslahi ya Watanzania.

"Inasikitisha kuona serikali ikiiacha kukamata mafisadi wanaolisababishia hasara kubwa taifa, na badala yake inakamata viongozi wema kama mwenyekiti wetu bila sababu zozote za msingi," alisema Kalogi.
 
Back
Top Bottom