Hatimaye JK akabidhiwa ripoti ya madini

Ripoti ya Richmond 'kuanikwa' leo

Na John Daniel, Dodoma

HATIMAYE hamu ya wabunge kutaka kuona na kujua wahusika katika mkataba wenye utata wa kampuni ya kuzalisha umeme ya Richmond itakidhiwa leo wakatakapokabidhiwa rasmi ripoti ya Kamati Teule ya Bunge iliyoundwa Katika mkutano uliopita.

Habari za uhakika kutoka vyanzo mbalimbali zilieleza kuwa hadi jana asubuhi, kazi ya kukamilisha ripoti hiyo ilikuwa ikiendelea na ilitarajiwa kumalizika jioni na kuwasilishwa mezani kwa Spika leo na baadaye kugawiwa kwa wawakilishi hao wa wananchi.

“Ripoti ile ni kubwa sana, si kama zile ambazo tulizoea kutoka kwa mawaziri (kauli za mawaziri), kuanzia wiki nzima inafanyiwa kazi ya maandalizi na leo (jana) ilikuwa kwenye hatua za kuwekwa majalada ili kesho (leo) wagawiwe wabunge,” kilisema chanzo chetu.

Akizungumza na Majira kwa njia ya simu jana, Spika wa Bunge, Bw. Samwel Sitta, hakukataa wala kukubali kuwasilishwa kwa ripoti hiyo leo na kusisitiza kuwa atatangaza kila kitu leo asubuhi.

“Nitatangaza kila kitu kesho (leo) saa nne asubuhi, kikubwa tu mtu wako asikose kuwapo,” alisisitiza Bw. sitta na kuomba mwandishi wa habari hizi kuvuta subira mpaka leo atakapoweka mambo hadharani.

Wakizungumza na Majira baadhi ya wabunge wa CCM ambao hawakupenda majina yao yatajwe, walisema wao hawana taarifa hizo, ila wamepata matumaini mapya kama itakuwa hivyo, hasa baada ya Spika kusitisha ziara yake ya Marekani na kusisitiza kuwa ndicho walichokuwa wanasubiri kwa hamu.

“Ni wazi, kwamba hizo ni habari njema sana kwetu na kwa wananchi waliotutuma kuwasemea, lakini nakuhakikishia kuwa hatutamlinda mtu yeyote atayeonekana alishiriki kinyume na taratibu,” alisema mmoja wa wabunge wa CCM.

Kuanzia juzi, vikao kadhaa vya wabunge wa CCM vilikuwa vikiendelea huku jambo kubwa ikidokezwa kuwa ni juhudi za kutaka kuweka mambo sawa, hasa baada ya joto zaidi kupanda, hata wabunge kugoma kujadili muswada wa umeme na biashara ya mafuta, hadi watakapopokea ripoti ya Richmond na kujua kilichomo.

Katika hali iliyoonekana kuwa si ya kawaida, kikao cha Kamati ya Uongozi ya CCM, pia kilifanyika juzi na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusufu Makamba, ambapo ilidaiwa kuwa ajenda kuu ilikuwa ni kujipanga kwa ajili ya ripoti ya Richmond.

Awali akitoa matangazo baada ya kipindi cha maswali na majibu jana asubuhi, Naibu Spika wa Bunge, Bi Anna Makinda, alisema kikao cha Kamati ya Wabunge wa CCM ambacho kilipangwa kufanyika jana sasa kitafanyika leo saa 2 usiku.

“Kwa hali ilivyokuwa, kuna uwezekano mkubwa kuwa ndicho chanzo cha kuahirishwa kwa kikao chetu leo (jana), kuna mambo ambayo yalikuwa hayajakaa sawa, hivyo ilibidi kwanza kiahirishwe mpaka hayo yakamilike kwanza,” kilisema chanzo chetu kutoka miongoni mwa wabunge wa CCM.

Habari zaidi zilieleza kuwa Kamati ya Uongozi ya chama hicho kilichofanyika juzi, kilihoji uwezekano wa wabunge wa CCM kukutana kabla ya kukabidhiwa ripoti hiyo na kwamba yaliyomo ni lazima yajadiliwe kwanza na wabunge hao kabla ya kutoa mawazo yao bungeni kesho.

Wakati huo huo, Rais Jakaya Kikwete, anatarajiwa kuwasili mjini hapa kuongoza kikao cha Baraza la Mawaziri huku kukiwa na taarifa kwamba baada ya kikao hicho, kutakuwa na jambo jipya linaloweza kuleta mabadiliko makubwa katika siasa na uongozi wa nchi.
 
Tik tak tik tak.......

siku moja imepita na report bado haijatolewa!

Siku moja imepita na hakuna hata minong'ono kuhusu lini wanategemea kuitoa ripoti hiyo rasmi. Ikichelewa zaidi itabidi waulizwe, je ni sababu zipi zilizofanya mshindwe kuitoa ripoti katika kipindi cha miezi mitatu mliyopewa kukamilisha hiyo? Kama mlijua kwamba miezi mitatu isingetosha kukamilisha ripoti hiyo kwa nini hamkumuomba Muungwana ili awaongezee muda wa kutimiza jukumu alilowakabidhi? Hizi tume ni usanii mtupu. Ripoti ya ukaguzi wa BoT Muungwana kaamua kuificha na wabunge wanapigwa dana dana kuhusiana na lini watakabidhiwa rasmi ripoti hiyo. Ripoti ya richmonduli wabunge pia wanapigwa dana dana na mawaziri kuwekewa mkwara mzito kuhusu kuisupport siri kali kwenye sakata la richmonduli maana hawa mawaziri hawana uwezo wa kufikiri wakiambiwa wasupport govt bila hata kujua wanacho support wao wamo tu! Kweli tuko katika ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya ya kuiangamiza Tanzania!
 
siku zinaendelea kupita na hii report inasubiriwa kwa makini na wana JF! walizani watanzani watasahau lakini hapa ndio mwanzo watu wameamka.... tik tak tik tak.........
 
...its time sasa,mbona kimya,waandishi wa bongo mbona hawaanzi kurusha makombora ya kuwachokonoa ili waseme kitu,lakini ninavyojua mimi hawa mafisadi na utendaji wao utasikia report imeshakabidhiwa kwa raisi na sasa inafanyiwa kazi kabala ya kusomwa kwa wananchi basi hapo raisi atachukua mwka tena kuja kuongelea....upuuzi mtupu!
 
Watanzania jamani! Hii Kamati iliyoundwa ni Kamati ya Rais na si ya Bunge. Hivyo, kina Zitto na wenzake hawawezi kusema lolote hadi wampatie Rais ripoti hiyo. Na Rais halazimiki kuiweka hadharani (kama alivyofanya ya EPA) hivyo msitegemee kuiona hadharani hivi karibuni, ila mapendekezo yake yataangaliwa na kufanyiwa kazi. La maana ni wananchi kuendelea kusubiri kwani "subira yavuta kheri" kama alivyosema mtani wangu juzi.

Asanteni.
 
...sasa kuja kututangazia na mbwembwe zote ilikuwa ni nini? seems ilikuwa ni kuzuia maswali tuu ili kuficha ufisadi,leo kibao kimegeuka eti report ni ya raisi na haya mambo ya siri siri zisizo na maana ni nini?toa report hapo,yaani viongozi wa Africa wana too much power bila sababu na ndio mwanzo wa uzembe na ufisadi tuu
 
Watanzania jamani! Hii Kamati iliyoundwa ni Kamati ya Rais na si ya Bunge. Hivyo, kina Zitto na wenzake hawawezi kusema lolote hadi wampatie Rais ripoti hiyo. Na Rais halazimiki kuiweka hadharani (kama alivyofanya ya EPA) hivyo msitegemee kuiona hadharani hivi karibuni, ila mapendekezo yake yataangaliwa na kufanyiwa kazi. La maana ni wananchi kuendelea kusubiri kwani "subira yavuta kheri" kama alivyosema mtani wangu juzi.

Asanteni.

Kwani ripoti ya EPA iliwekwa hadharani? au unazungumzia ile summary aliyoitoa Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Luhanjo? kama ni ile bado/siyo ripoti ile!

Bado sijaona ripoti ya Kamati iliyoundwa na Rais ikitolewa wazi. Refer ripoti za Kamati za akina Mboma... juu ya madini (hakuna hatua zilizochukuliwa). Kamati ya vijana wanne waliouawa Dar wale wafanya biashara kutoka Mahenge(ila hatua zimechukuliwa).

Kuna mwandishi mmoja amenifurahisha, amemkumbusha Rais kwamba ameajiriwa na wananchi, hivyo wananchi ndiyo mabossi, wakisema lete hiki anatakiwa kutii. sasa the oposite is true.

Ripoti iwekwe wazi, kwa sababu wananchi tunaitaka.
 
Kamati ndio ipo inaandika ripoti hivi sasa. Ni kweli muda wao ulikwisha lakini waliomba na kuongezewa muda. kazi hiyo itakamilika hivi karibuni ingawa vyanzo vyangu havijanithibitishia ni lini hasa.
 
Watanzania jamani! Hii Kamati iliyoundwa ni Kamati ya Rais na si ya Bunge. Hivyo, kina Zitto na wenzake hawawezi kusema lolote hadi wampatie Rais ripoti hiyo. Na Rais halazimiki kuiweka hadharani (kama alivyofanya ya EPA) hivyo msitegemee kuiona hadharani hivi karibuni, ila mapendekezo yake yataangaliwa na kufanyiwa kazi. La maana ni wananchi kuendelea kusubiri kwani "subira yavuta kheri" kama alivyosema mtani wangu juzi.

Asanteni.

Pamoja na haya kwamba ni Kamati ya rais lakini kuna Zitto ambaye Taifa linamtegemea alitetee lazima awe na report yake mbadala kabisa .
 
Watanzania jamani!
Hii Kamati iliyoundwa ni Kamati ya Rais na si ya Bunge. Hivyo, kina Zitto na wenzake hawawezi kusema lolote hadi wampatie Rais ripoti hiyo.

Na Rais halazimiki kuiweka hadharani (kama alivyofanya ya EPA) hivyo msitegemee kuiona hadharani hivi karibuni, ila mapendekezo yake yataangaliwa na kufanyiwa kazi.

La maana ni wananchi kuendelea kusubiri kwani "subira yavuta kheri" kama alivyosema mtani wangu juzi.

Asanteni.

Hata kama kamati ni ya raisi, sidhani kama ni kweli kuwa riport yake haiwezi kuwekwa hadharani mpaka akubali, unless kama TOR zilisema hivyo. Kama hazina kipengele hicho cha kuwazuia sioni kwa nini isitolewe hadharani. Ripoti nyingi tu ziliwahi kuwekwa hadharani na sidhani kama walipata rukhsa toka kwa Raisi.

Umuhimu wa kuziweka hadharani ni kuwa zinaweza kutumika kama miongozo au kama reference kwenye mijadala bungeni, kwenye seminar na kwenye masuala mengine mengi kama vile research nk. Mfano mzuri ni ile ya wariona, ambayo institution nyingi za nyumbani na za kimataifa ziliipenda sana na ni moja kati ya vitu vilivyompatia Mkapa ujiko mkubwa, ingawa hakuitekeleza yote, kabla ya kubadilisha damu na kuuvaa ufisadi.

Madini ni rasilimali ya taifa kwa hiyo ni haki ya kila Mtanzania, hasa wawakilishi wao Bungeni, kufahamu nini kinachoendelea na ipi itakuwa hatima ya resources zao. Hili halipaswi kuwa suala la siri na hili la kusubiri mpaka mwisho wa dunia, wakati uchimbaji unaendelea litakuwa gumu kwetu.
 
Hope JK will be real na kuitoa kwa haraka maana anazidi kujimaliza kwa kweli .
 
Bado hii report inasubiriwa hapa ili kujua nani anajua nini na wapi katika uuzwaji wa Mgodi wa Buzwagi kwa bei ya karanga huku wakubwa wakipata 10 percent zao juu kwa juu!

Ile short memory ya watanzania imeanza kurefuka kidogo na hapa halali mtu hadi kieleweke na hayo maazimio yenu ya Butiama mnayotaka kuleta!
 
Bado hii report inasubiriwa hapa ili kujua nani anajua nini na wapi katika uuzwaji wa Mgodi wa Buzwagi kwa bei ya karanga huku wakubwa wakipata 10 percent zao juu kwa juu!

African Lady,

Umeshafanikiwa kuziona hadidu za rejea ambazo kamati ya madini ilipewa na mheshiwa rais? Hapa nataka nijue scope ya hii kamati ni ipi!

Mimi nilifikiri hii kamati iliundwa kutathimini mikataba iliyopo na kuishauri serikali jinsi ya kuiboresha ili iwe na manufaa zaidi kwa nchi na wananchi kwa ujumla, sidhani kama kuna kukamatwa mchawi yeyote hapa like wale walio husika na Buzwagi etc.
 
Hili neno hadidu za rejea sijui limeanza kutumika lini na sijui lina maana gani....lol. Inaonekana kuna uwezo mkubwa sana wa kutumia maneno kuliko kufanya the right thing huko magogoni.

Kama ni kamati ya kupendekeza cha kufanya, je zile kamati kumi na tano zilizopita zilifanya nini?
 
Ha ha ha dada,
Hadidu za rejea=Terms of reference.
Hata hivyo viongozi wetu wanajua kutumia misamiati ya kiswahili zaidi ili kupotezea attention za wananchi walio serious.Yaani mwananchi wa kawaida kule kijijini akisikia waziri au mbunge akitamka hadidu za rejea anaweza kufikiria sijui ni msaada gani tena huo tumeletewa ndugu yangu! Duh,Mola tunusuru na haya mazingaombwe.

Hii statement poa sana,"eti if you cannot comvince them,comfuse them" Nakumbuka hata high school kwenye Debate ukaona hoja zinakuelemea inabidi uipotezee kwa kutumia bombastics,So hawa viongozi wetu wanatuendesha kama high school debate club!

Uzuri mmoja kwenye hii kamati ya madini ina watu makini ambo umakini wao utaonekana pale wanapobaini usanii na kuamua kujitoa mhanga kwa ajili ya taifa lao.
 
Hili neno hadidu za rejea sijui limeanza kutumika lini na sijui lina maana gani....lol. Inaonekana kuna uwezo mkubwa sana wa kutumia maneno kuliko kufanya the right thing huko magogoni.

Kama ni kamati ya kupendekeza cha kufanya, je zile kamati kumi na tano zilizopita zilifanya nini?

Hadidu za rejea kwa mara ya kwanza nilisikia kwenye report ya kina mwakyembe, na neno hilo lilitumika kumaanisha kitu kama dondoo za kuchokonoa au ''areas of focus''

Nime kuuliza hivi cause kwa mtazamo wangu sitegemei kama report ya kamati hii itakuja na kitu cha ajabu especially ikataja kwamba huyu alifanya hivi na vile kimakosa etc For your info niko karibu sana na mwanakamati mmoja, sasa nikiangalia mpaka sasa progress ya kazi hii according to him, naona haita kuwa na jipya kabisa!!
 
Walete hata kama hayo ambayo si mapya na itajulikana namna gani wanajaribu kucheza na watanzania. Wana bahati mbaya sana kuwa memory ya watanzania imeanza kuongezeka na walifanya makosa sana kutangaza mkutano wa ccm kwenye TV (ambako Kikwete aliahidi kuwa angeshughulikia Buzwagi na mikataba mingine ya madini).

Sasa pamoja na maazimio yao hayo ya butiama sijui wapi tena huko wanataka kwenda, wajue kuwa halali mtu hapa mpaka kieleweke kuwa Kikwete alikatiwa kiasi gani na kina Sinclair kwenye issue ya Buzwagi.
 
Back
Top Bottom