Hatimaye JK akabidhiwa ripoti ya madini

jmushi1

Platinum Member
Nov 2, 2007
26,331
25,236
ban_zitto.jpg


Hoja Binafsi ya kuunda kamati teule ya Bunge kuchunguza mkataba mpya wa madini ambao Waziri wa Nishati na Madini Karamagi ameusaini bila kuzingatia maagizo ya Rais​

Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe (MB)​

MHESHIMIWA Spika, kwanza napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa kunipatia fursa ya kuleta hoja hii hapa kwenye Bunge lako tukufu kwa mujibu wa kanuni zetu za Bunge. Kuletwa kwa hoja hii, bila kujali maamuzi ya kuhusu hoja yenyewe, ni ishara tosha ya ukomavu wa demokrasia yetu ambayo inakuzwa na mijadala ya Bunge lako tukufu. Nakupongeza kwa dhati kabisa kwa juhudi zako za kuliimarisha Bunge letu na kujenga muhimili imara wa ulinzi wa demokrasia ya vyama vingi nchini kwetu.
Mheshimiwa Spika, mnamo tarehe 16/7/2007 mara baada ya hoja ya Waziri wa Nishati na Madini kuamuliwa na Bunge lako tukufu, nilisimama mahala pangu na kutoa taarifa ya kukusudia kuleta hoja ya kuunda kamati teule ya Bunge. Nilisema kama ifuatavyo (kwa mujibu wa kumbukumbu sahihi za mijadala ya Bunge), ninanukuu ‘…naomba kutoa taarifa rasmi… kwamba nakusudia kuleta hoja ya kuunda kamati teule kuchunguza mkataba mpya wa madini ambao Waziri wa Nishati na Madini ameusaini bila kuzingatia maagizo ya rais (wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) ya kupitia mikataba ya madini aliyoyatoa mbele ya Bunge lako tukufu tarehe 30 Disemba, 2005.’ Mwisho wa kunukuu.
Mheshimiwa Spika, nimeshawasilisha hoja yangu hii kwa maandishi kwa Katibu wa Bunge na sasa nawasilisha rasmi katika kikao hiki cha Bunge kwa uamuzi. Nimezingatia kanuni 104 (2) katika kuwasilisha hoja yangu.
Mheshimiwa Spika, katika maelezo yangu niliyowasilisha bungeni wakati wa mjadala wa hotuba ya Waziri wa Nishati na Madini siku ya tarehe 16/7/2007, nilihitaji maelezo kutoka serikalini katika masuala makuu mawili yafuatayo:
  1. Kuondolewa kwa kipengele katika sheria ya kodi ya mapato ya mwaka 1973 kuhusiana na asilimia 15% ya ‘capital allowance on unredeemed qualifying capital expenditure’ bila ya kibali cha Bunge lako tukufu.
  2. Kusainiwa kwa mkataba mpya wa madini wa mgodi (mradi) wa Buzwagi kati ya serikali na Kampuni ya Barrick na sababu za mkataba huo kusainiwa nje ya nchi, London, Uingereza, na vilevile kwa nini mkataba huo umesainiwa wakati bado serikali inafanya durusu (review) ya mikataba kufuatana na maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndugu Jakaya Mrisho Kikwete.
Mheshimiwa Spika, wakati akijibu hoja zangu Waziri wa Nishati na Madini alijenga hoja zake kama ifuatavyo:
a. Kuhusiana na asilimia 15% ya ‘capital allowance on unredeemed qualifying capital expenditure’ Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini amenukuliwa na kumbukumbu za majadiliano ya Bunge akisema, ninanukuu: “…kwa hiyo pamoja na kwamba ninamheshimu sana Mheshimiwa Kabwe Zitto na sote tunamheshimu ni msomaji mzuri, lakini wakati mwingine lazima kuangalia vitu gani unasoma. Ni kwamba kipengele hiki cha sheria kililetwa hapa bungeni mwaka 2001 kwenye bajeti kikabadilishwa…” Mwisho wa kunukuu.

Mheshimiwa Spika, katika kuandaa hoja yangu hii, ilinibidi kupitia upya kumbukumbu za majadiliano ya Bunge ili kujiridhisha na maelezo ya Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini, maelezo ambayo mimi nililitaarifu Bunge lako tukufu tarehe 16/7/2007 kuwa sio sahihi.

Mheshimiwa Spika, Kumbukumbu hizo zinaonesha kwamba, sheria ya fedha ya mwaka 2001 (Finance Act. No.14 ya 2001) ilifanyiwa marekebisho kadhaa ikiwemo marekebisho ya sheria ya madini kifungu cha 87 ambapo kifungu kidogo cha (3) cha kifungu cha 87 kiliongezwa. Kifungu kidogo hicho kinasema, ninanukuu:
‘(3) The provisions of subsections (1) and (2) shall not apply to any person who, immediately before the first day of July, 2001 was not the holder of a mineral right granted under this Act.’
Mheshimiwa Spika, kifungu cha 87 cha Sheria ya Madini ya mwaka 1998 (No.5/199 kinazungumzia mrahaba wa madini (Remission and deferment of royalties). Hivyo, kama sheria ya fedha ya mwaka 2001 haikubadili kipenge hiki, Mheshimiwa Waziri ametoa wapi jibu aliloliambia Bunge?

Mheshimiwa Spika, suala hili linahusu haki, kinga na madaraka ya Bunge kwa mujibu wa sheria namba 3 ya 1988.
Mheshimiwa Spika, hata hivyo katika hotuba ya Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Basil Mramba, akiwasilisha hotuba ya Bajeti mwaka 2002, tarehe 13 mwezi Juni, alizungumzia kipengele hiki. Ninaomba kunukuu sehemu ya hotuba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Basili Mramba.

“Amendment to the Income Tax structure, (44) Mr. Speaker, in this area I propose to take the following measures:
(v) I propose to reinstate the additional 15 percent capital allowance on unredeemed qualifying capital expenditure as set out in the Mining Act. No. 5 of 1998.” Mwisho wa kunukuu.

Mheshimiwa Spika, nilipopitia sheria ya fedha ya mwaka 2002, nimekuta sehemu ya 8 inazungumzia mabadiliko katika kodi ya mapato ya 1973. Na hata katika ukurasa wa kwanza wa sheria hii (Arrangement of Contents), sheria ya madini haitajwi.

Mheshimiwa Spika, maelezo haya ya Waziri wa Fedha ya mwaka 2002 yanaonesha dhahiri utata wa kipengele hiki. Ni kwa vipi kifungu cha sheria ambacho hakijafutwa kirejeshwe?

Mheshimiwa Spika, tuchukulie kuwa maneno ya waziri ni ya kweli. Je, kwa nini makampuni ya madini ambayo yameingia mkataba na serikali kuanzia Julai mosi 2001 hayajaanza kulipa kodi ya mapato?

Mheshimiwa Spika, utata huu ambao umegubika sekta hii ya madini, unaweza kufafanuliwa na Bunge lako tukufu kupitia Kamati Teule. Kamati Teule ya Bunge ichunguze upitiaji wa mikataba hii na kuona kama kuna vitendo vyovyote vya uvunjifu wa sheria za nchi na kupotea kwa mapato ya serikali na ufisadi.

b. Kusainiwa kwa Mkataba wa Mgodi (Mradi) wa Buzwagi.
Mheshimiwa Spika, wakati akijibu hoja yangu kuhusiana na suala la mkataba mpya wa mgodi wa Buzwagi, Waziri wa Nishati na Madini amenukuliwa na kumbukumbu za majadiliano ya Bunge akisema kama ifuatavyo:

Mheshimiwa Spika, katika tathmini ya migodi, mgodi wa Buzwagi ni marginal mine ambao uhai wake si wa muda mrefu. Bila ya kutumia fursa ya sasa ya bei ya dhahabu, uwekezaji wake usingeweza kuwa wa faida. Hata hivyo, mkataba wa Buzwagi hauna mapungufu yaliyokuwamo kwenye mikataba ya zamani.’ Mwisho wa kunukuu.

Mheshimiwa Spika, mapitio ya mikataba ya madini ni mchakato ambao mwisho wake ni kuletwa kwa sheria ya madini hapa bungeni na kuifanyia marekebisho ili kuiboresha na kuondoa mapungufu. Hivyo, mpaka hapo sheria itakaporekebishwa, ndipo tutasema tumemaliza zoezi la kupitia mikataba ya madini na hivyo kusaini mikataba mipya na makampuni yote ya madini yaliyopo nchini na yatakayokuja kuwekeza.

Mheshimiwa Spika, suala ambalo linanipelekea kuomba kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza mkataba huu mpya, ni kuhusu uharaka uliopelekea Waziri wa Nishati na Madini kusaini mkataba huu. Sheria ya Madini bado haijarekebishwa, je, waziri anatumia vigezo gani kusema mkataba mpya wa Buzwagi aliousaini London hauna mapungufu?

Mheshimiwa Spika, Waziri wa Nishati na Madini aliliambia Bunge lako tukufu kuwa Buzwagi ni marginal mine. Vile vile waziri anasema kuwa Kampuni ya Barrick inamiliki migodi mitatu tu kupitia kampuni zake tanzu ambazo ni Bulyanhulu Gold Mine, North Mara Gold Mine na Pangea Minerals Limited Tulawaka. Kwa maelezo haya ya Waziri Karamagi, Buzwagi sio mgodi.

Mheshimiwa Spika, hoja hii ya kuwa Buzwagi sio mgodi inashabihiana kabisa na hoja ya Kampuni ya Barrick kwamba Buzwagi ni Project. Taarifa ya kampuni hii ya Barrick Gold Corporation-Global operations-Africa- Buzwagi, inaonesha kuwa Buzwagi ni mradi. Taarifa hii ninaiambatanisha katika hoja hii.

Mheshimiwa Spika, taarifa ya Barrick, Annual Review 2006 inasema ifuatavyo katika ukurasa wa 23, ninanukuu. ‘A major milestone was reached in February 2007 when we signed a mineral Development Agreement (MDA) with the Tanzanian government. In 2007, we expect to complete a detailed construction design and receive EIA approval.’
Mheshimiwa Spika, suala ambalo vile vile linanisukuma kuomba Bunge lako tukufu kuunda Kamati Teule ni kwamba, iwapo Buzwagi sio mgodi bali ni mradi, ni kwa nini tumesaini Mineral Development Agreement (MDA) mpya? Kwa kuwa Pangea Minerals Tulawaka ndio inaonekana kumiliki mradi huu, je, serikali imefanya marekebisho tu ya MDA na Kampuni ya Barrick? Naomba Kamati Teule ichunguze ni nini kilichosainiwa, marekebisho ya mkataba wa Tulawaka au MDA mpya ya Buzwagi?

Mheshimiwa Spika, Buzwagi inashika nafasi ya pili kwa uwekezaji wa Barrick katika migodi hapa nchini. Wakati kampuni hii inawekeza dola za Kimarekani 400 milioni katika Buzwagi, imewekeza dola za Kimarekani 600 katika Bulyanhulu. Je, ni kwa vipi Buzwagi iwe marginal mine wakati uwekezaji wake unashinda uwekezaji wa Tulawaka na North Mara?

Mheshimiwa Spika, chini ya kifungu cha 47 cha Sheria ya Madini ya Mwaka 1998 (Na.5/9, pamoja na mambo mengine kinataka leseni yoyote isitolewe mpaka taarifa ya mazingira iwe imetolewa na kuruhusu mgodi kuendelea na kazi.

Mheshimiwa Spika, wakati Waziri wa Nishati na Madini ameweka saini mkataba wa Buzwagi juma la mwisho la mwezi Februari 2007, Baraza la Mazingira nchini limetoa kibali (Environmental Impact Assessment- EIA approval) tarehe 11 mwezi Mei 2007. Ni kwa nini Waziri wa Nishati na Madini, Mheshimiwa Nazir Karamagi alisaini MDA ya Buzwagi na Kampuni ya Barrick kabla Baraza la Mazingira la Taifa (NEMC) halijatoa ruhusa?

Mheshimiwa Spika, sheria ya madini, niliyoitaja hapo awali, imeunda Kamati ya Ushauri ya Madini (Mining advisory Committee). Kabla ya waziri kusaini mkataba wowote ni lazima apate ushauri kutoka kamati hii. Kwa taratibu za kiserikali, kama kamati ikimshauri waziri na waziri akakataa ushauri huo, inampasa waziri atoe sababu ni kwa nini anakataa ushauri. Je, waziri alifuata ushauri wa Kamati ya Ushauri ya Madini kuhusiana na wakati mwafaka wa kusaini mkataba huu?

Mheshimiwa Spika, inawezekana kabisa MDA ya Buzwagi kusainiwa Uingereza sio tatizo. Kwa mfano, mwaka 2006 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilisaini mikataba kadhaa. Ni mingapi kati ya mikataba hii imesainiwa nje ya nchi? Nini madhara ya kisheria kwa mkataba kusaniwa Uingereza? Je, mkataba umeandikwa “signed in London...” au “signed in Dar es Salaam...? Kamati Teule ya Bunge ndio chombo pekee kitakachoweza kutoa majibu ya maswali haya.

Mheshimiwa Spika, suala hili ni suala la kitaifa. Halina hata chembe ya itikadi za kivyama. Ninaamini wabunge wataamua kwa maslahi ya taifa letu. Uundwaji wa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza mapitio ya mikataba ya madini na mazingira ya kusainiwa kwa mkataba mpya wa Buzwagi yatatoa msaada mkubwa kwa azma ya Rais wetu ndugu Jakaya Mrisho Kikwete ya kuona rasilimali za madini zinafaidisha nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, ninaomba kutoa hoja.

…………………………….
KABWE ZUBERI ZITTO (MB)
JIMBO LA KIGOMA KASKAZINI
 
Kwa nini nimewalk out? Ni kwa sababu ya Principle - Misimamo isiyoyumba

Ni makusudi yangu kuhakikisha kwamba tunaendelea na mjadala wa kamati ya Rais
Hivyo basi,Mh Zitto akiwa kama mmoja wa wanakamati hao ambaye pia ni wazi kwa kiasi kikubwa;hoja yake ya kamati teule kule bungeni ilichangia maamuzi ya Mh Rais kuiunda kamati hiyo.

Ni wazi kwamba kamati hii imeundwa mara baada ya mzozo kuwa mkubwa,mzozo ambao wakina Zitto waliuanzisha kule bungeni kutokana sakata la "UFISADI"? na mikataba mibovu ya madini.
Nimeamua kum"quote"Mh Zitto pale alipokuwa akisisitiza ni kwanini ali"walk out"kule bungeni pale alipoibua issue hii kule bungeni, na sababu aliyoitoa ni ya kwamba yeye ni mtu mwenye "PRINCIPLE"ambapo yeye mwenyewe aliwarahisishia wasomaji kwa kuwapa definition sahihi kwamba ni"MISIMAMO ISIYOYUMBA"

Kwa maana nyingine ni kwamba;alikuwa radhi kuyatema maslahi yake binafsi kama vile posho na mishahara,kwa ajili ya kutetea maslahi ya wananchi wote!thats a principle,hakubadili msimamo..na ndio maana nafikiri CHADEMA wanamuaminia baba lao Mh Zitto kwamba atarepresent maslahi ya taifa,hata humo kamatini.
Natumia fursa hii kuwaalika wana forum wote kuchangia wakati huu ambapo CHADEMA wameshatoa msimamo wao kuwa wanamsapoti Mh ZittoHivyo ni wazi kwamba kazi inaanza mara moja.

Tunatumia pia fursa hii kumshawishi Mh Zitto aendelee kuwa mtu mwenye principle kama ambavyo tume mquote,na kwamba tunafuatlia kwa makini kwani bado hatujajua kazi halisi watakayoifanya.

Hivyo basi tunaomba aendelee kuwa na principle ileile aliyokuwa nayo huko bungeni pale atakapoanza kazi humo "KAMATINI"Tumejaribu mara nyingi kuona kama Mh Zitto angewasili hapa jamvini ili kulonga na wana jf kwamba ni nini haswa anachokwenda kufanya humo kamatini,kwakuwa hakufanya hivyo..then basi mjadala unaanza na tunategemea kuwa tutaendelea kuchangia kuanzia sasa hadi hapo kamati hiyo itakapo wasilisha ripoti yake kwa Mh Rais.

Thread hii sijaifunga,kwani bado sijajua tarehe kamili kamati hiyo itakapo"wrap up"na kuwasilisha kwa mkuu matokeo ya hiyo "assignment yao"Haya tena wana forum..mchango wenu,na pia changamoto kwa mbunge wetu huyu kijana,machachari,mwenye uchungu na maslahi ya wananchi na taifa lake kwa ujumla..!unakaribishwaMh Zitto uje utueleze kama bado wew ni mtu mwenye "PRINCIPLE".
 
November 13th, 2007. Rais Kikwete alitangaza kuundwa kwa kamati ya madini. Kamati ambayo ilipewa miezi mitatu kutoa mapendekezo ya nini kifanyike katika sekta ya madini.

Hii thread ninaanzisha itakuwa ina-count down weeks kutokea ya kumi na mbili hadi ya mwisho ili kujua maendeleo ya kamati hiyo na kupata mambo ya ndani kuhusu kinachoendelea. Kama report za ile kamati ya bunge ya Richmonduli zinavyoonyesha, hizi kamati mbili zimeundwa kula pesa tu na kupoteza muda.

Hata hivyo kwa vile Wabunge Zitto Kabwe na Mwakyembe wameomba wapewe muda na imani ya wananchi "kwa maslahi ya taifa", basi mimi binafsi nawapa muda ili ijulikane kama kweli hii kamati iliyoundwa italeta chochote tofauti na yale yaliyopatikana toka katika kamati kama sita hivi zilizoundwa na kutumia mabilioni kisha kutoa report na mapendekezo ambayo yamewekwa kapuni.

  • 1. Hadi leo tarehe 4 dec, wiki tatu zimepita tangu kuundwa kwa kamati ya madini ya raisi.......

    week ya 12 - checked
    week ya 11 - checked
    week ya 10 - checked
    week ya 09 - ................
 
Haya bwana, ngoja tuwasubiri. Yale maneno ya Richmond hayatoi mwanga mzuri sana kwa hii ya akina Bomani! Still optimistic though
 
Haya bwana, ngoja tuwasubiri. Yale maneno ya Richmond hayatoi mwanga mzuri sana kwa hii ya akina Bomani! Still optimistic though

I like your courage Kitila,

So far as I said in the last debate I had with you on this issue, I am reluctantly giving you guys all the time and peace to prove your argument.

I dont know why but I dont expect anything new from this kamati. I hope and pray that I am wrong!
 
I would like to differ, mimi sioni kama kuna lolote la maana litafanyika i am very persmistic. I do not have trust with the Government. Hizi kamati zitasema zimegundua mianya mingi na kushauri namna ya kuiziba, lakini hakuna hatua ufisadi utaowekwa hadharani na wala hatua zozote hazitachukuliwa kwa wahusika....kitakachotikea ni kuwafunga midomo watu, watasema hakuna haja ya kuzungumzia hili, kwani tume iliundwa ilifanya uchunguzi ikaotoa mapendekezo na sasa yanafanyiwa kazi.
Ni kama tumeanza kurudi kwenye ujinga wa awamu ya pili, kila kitu kinaundiwa tume na hizo tume zinakuwa ni loop holes za kula zaidi pesa za umma. Najua wanajambo mtazungumza hapa baada ya ripiti kutolewa, i believe wakati huo mtakaosoma mtasema mimi nilikuwa right!
Hata hiyo ya BOT ambayo inapitapita kwenye mikono ya watu serikalini hivi sasa, haitakuwa na jipya unaweza kusganaa same story, tunaziba mianya ili makosa yasirudiwe, hakuna mtu atakayechukuliwa hatua, wait and see!!!!! WE POOR TANZANIANS.
 
hakuna kitu hapo ni usanii tuu,na wala siamini kama JK au Karamagi walikula rushwa,tatizo ni sheria za madini zilizopo ndio zimetufanya vibaya na wala tusianze kutafuta nani mchawi ni kubadilisha sheria tuu
 
hakuna kitu hapo ni usanii tuu,na wala siamini kama JK au Karamagi walikula rushwa,tatizo ni sheria za madini zilizopo ndio zimetufanya vibaya na wala tusianze kutafuta nani mchawi ni kubadilisha sheria tuu

Hata details za mikataba ya madini kufanywa siri kwa wamiliki wa rasilimali hizo (Watanzania) huoni kama kuna kitu hapo! Duh!
 
Hapa hamna lolote litakalotokea na CCM watashinda tena kwa kishindo mwaka 2010. Na tena kabla ya uchaguzi mkuu kutaibuka na skendo ingine kubwa zaidi ya hii ya madini. Kwa hiyo mtalia weee hadi machozi yatawakauka
 
Hapa hamna lolote litakalotokea na CCM watashinda tena kwa kishindo mwaka 2010. Na tena kabla ya uchaguzi mkuu kutaibuka na skendo ingine kubwa zaidi ya hii ya madini. Kwa hiyo mtalia weee hadi machozi yatawakauka

Pevusha fikra zako,
We kila kitu unawaza uchaguzi tu, watu wanazungumzia maslahi ya umma we fikra zako zinakutuma kwingine.

Pitia post zote hapo juu, umeona yeyote aliyezungumzia uchaguzi zaidi ya kutaka kuona maisha yanakuwa bora kwa watanzania kama yalivyoahidiwa?
 
Hata kama zitaundwa kamati zenye wajuzi wa-kimila hakutakuwa na jipya la kuikomboa Tanzania yetu! Mtazamo mpana sana unahitajika hasa namna ya ku-deal na hawa ma-bwana wa dunia hii particularly US, EU. Angalau nafarijika hapa ndani ya JF kuna-wabongo wenye nia ya dhati ya kuikomboa nchi yetu.

mh mwanakijiji na walio wakongwe ndani ya JF pls someni alama za nyakati na muwe tayari kutoa tafsiri sahihi kwa manufaa ya umma wa watanzania ambao moyo wa matumaini ni second nature!

siku zote historia huwa inatuhukumu na mimi ninaamini hivyo ! wapi ambapo democrasia ya marekani imepata kuleta nuru ya kweli? wako wapi wahindi wekundu wenye asili ya ardhi ya marekani? aborigin wa oz kwanini wanapungua kila kwa kasi kubwa? kwanini Tanzania yetu inarudi nyuma ki-maendeleo pamoja na kuwa na rasili mali ngingi? kwanini hatuna brand inayotamba ktk soko la dunia pamoja na kuwa na tanzanite? kwanini vita haviishi popote pale palipo na interest za hawa mabwana wa dunia hii?? ni nini malengo ya utandawazi kwa nchi changa kama tanzania? IMF na WB wapi wameikomboa nchi kutoka ktk lindi la umaskini? kwanini hatuna uchungu na nchi yetu sisi watanzania??... nina maswali mengi sana waheshimiwa wa JF... UZALENDO UZALENDO lini tutakuwa wazalendo wakweli?... Ndani ya uongozi huu tulionao mmmmmh!!! hakuna jipya !!, vijana tujipange , wazee wenye kuweza kusoma alama tuwenao tupande mbegu imara kwa vizazi vilivyopita , vilivyopo na vitakavyokuja.... God bless Tanzania!
 
November 13th, 2007. Rais Kikwete alitangaza kuundwa kwa kamati ya madini. Kamati ambayo ilipewa miezi mitatu kutoa mapendekezo ya nini kifanyike katika sekta ya madini.

Hii thread ninaanzisha itakuwa ina-count down weeks kutokea ya kumi na mbili hadi ya mwisho ili kujua maendeleo ya kamati hiyo na kupata mambo ya ndani kuhusu kinachoendelea. Kama report za ile kamati ya bunge ya Richmonduli zinavyoonyesha, hizi kamati mbili zimeundwa kula pesa tu na kupoteza muda.

Hata hivyo kwa vile Wabunge Zitto Kabwe na Mwakyembe wameomba wapewe muda na imani ya wananchi "kwa maslahi ya taifa", basi mimi binafsi nawapa muda ili ijulikane kama kweli hii kamati iliyoundwa italeta chochote tofauti na yale yaliyopatikana toka katika kamati kama sita hivi zilizoundwa na kutumia mabilioni kisha kutoa report na mapendekezo ambayo yamewekwa kapuni.

  • 1. Hadi leo tarehe 4 dec, wiki tatu zimepita tangu kuundwa kwa kamati ya madini ya raisi.......

    week ya 12 - checked
    week ya 11 - checked
    week ya 10 - checked
    week ya 09 - ................

Hayawi hayawi hayawi hayawi hayawi hayawi sasa yamekuwaaaaaaaa


Time is up!


  • Week ya 08 - checked
    Week ya 07 - checked
    Week ya 06 - checked
    Week ya 05 - checked
    Week ya 04 - checked
    Week ya 03 - checked
    Week ya 02 - checked
    Week ya 01 - checked


Time is Up! miezi mitatu imekwisha na sasa inabidi report ya tume hii iletwe hapa hapa wakati huu huu kwa watu hawa hawa na viongozi wale wale walikuja na sababu zile zile .... kwa hisani ya Kibaki wa kenya (our evil neighbor to the north)
 
ndugu yangu, unajua ulichofanyia hesabu? tik tak tik tak..

We acha tu,

Nilikubali kuchukua breki kipindi kile na kuwapa waheshimiwa sana muda wa kutosha. Nilimwandikia Mwakyembe kumwambia kuwa February 04 sio mbali (this was back in November) naye akanyamaza na hakujibu email yangu!

OK Mzee wangu Mwakyembe........tik tak tik tak..... time is up!
 
Huyo Zitto mwenyewe washam-tuliza ball... kaingizwa kwenye kamati, posho Tshs 100,000 kwa siku, VX la nguvu kioo juu full time kimyaaaaaaaaaaaaaaa

We achaa tu penye udhia penyeza rupia.....

Mpaka sasa wao 3 sisi 0 na tunaingia kwenye added minutes na ubao unasomeka zimeisha!
 
Huyo Zitto mwenyewe washam-tuliza ball... kaingizwa kwenye kamati, posho Tshs 100,000 kwa siku, VX la nguvu kioo juu full time kimyaaaaaaaaaaaaaaa

We achaa tu penye udhia penyeza rupia.....

Mpaka wao 3 sisi 0 na tunaingia kwenye added minutes na ubao unasomeka zimeisha!

kwi kwi kwi,

hilo VX zitto alipewa lini tena mbona intelligency report yangu inaonyesha vinginevyo? au ndio yaleyale kuwa sasa hii report ni ya zitto tena na sio sitta, kikwete, karamagi, mwakyembe, lowasa na wengineo....

zitto uko wapi? nitumie message nifikishe ujumbe wako hapa kama uko bize!

kwi kwi kwi
 
Hayawi hayawi hayawi hayawi hayawi hayawi sasa yamekuwaaaaaaaa


Time is up!


  • Week ya 08 - checked
    Week ya 07 - checked
    Week ya 06 - checked
    Week ya 05 - checked
    Week ya 04 - checked
    Week ya 03 - checked
    Week ya 02 - checked
    Week ya 01 - checked


Time is Up! miezi mitatu imekwisha na sasa inabidi report ya tume hii iletwe hapa hapa wakati huu huu kwa watu hawa hawa na viongozi wale wale walikuja na sababu zile zile .... kwa hisani ya Kibaki wa kenya (our evil neighbor to the north)

Jamani mbona mnaharaka, kuna tume nyingine inaundwa kuchunguza tume ya akina Mwakyembe hii itafanya uchunguzi miezi sita, watanzania tupo pamoja? ......ndio mzeee
 
Jamani mbona mnaharaka, kuna tume nyingine inaundwa kuchunguza tume ya akina Mwakyembe hii itafanya uchunguzi miezi sita, watanzania tupo pamoja? ......ndio mzeee

kwi kwi kwi,

yaani hii sasa ni kali ya mwaka, hii tume sasa itamshirikisha shehe Alfan na Mchungaji Mkogeke ili kuipa nguvu kidogo. Na inaonekana kuwa Kikwete ataomba baadhi ya wanafunzi wa geology wa UDSM pia wahusishwe kwenye hii kamati ambayo kazi kubwa itakuwa ni pamoja na kuwachunguza kina Mwakyembe kama kuna kitu chochote walisahau kwenye kazi zao za kila siku.....
 
Back
Top Bottom