Zitto Kabwe: Tunataka Mabadiliko Zaidi ya Sekta ya Madini

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
610
1,540
Ilikuwa furaha kubwa Jana kuzungumza kwa mara nyingine na Wananchi wa Kahama Jana. Maisha yangu ya kisiasa hayawezi kuandikwa bila ya Hoja ya Buzwagi, mgodi wa madini uliokuwa hapa Kahama. Baadhi ya mafanikio makubwa ya Hoja ya Buzwagi ni Pamoja na;

1. Kampuni za madini kuanza kulipa Ushuru wa Huduma kwa Halmashauri za Wilaya zenye Migodi. Kabla mikataba ya madini ilitaka Migodi kulipa Dola 200,000 kwa Kila Halmashauri. Hivi Sasa Halmashauri ya Wilaya Msalala inapata TZS Bilioni 4 kila Mwaka kutoka mgodi wa Bulyanhulu. Geita, Tarime, Kahama na Kila sehemu yenye Migodi nchini sasa inafaidika na matunda ya hoja ile.

2. Kampuni za Madini kuanza kulipa Kodi ya Mapato nchini. Kabla ya hoja ya Buzwagi Kampuni zilitumia mbinu za kihasibu kufanya kinachoitwa Base Erosion and Profit Shifting na hivyo kutolipa Kodi hapa Tanzania. Baada ya Sheria mpya ya Madini na Sheria za Kodi sasa Kampuni zinalipa Kodi hapa nchini.

Bado tunataka mabadiliko zaidi ya Sekta ya madini ili utajiri wa Nchi kunufaisha Watu wote. Tunataka Madini ya wote kwa faida ya wote.

- tunataka sera ya madini iwape Haki Wananchi kwenye Vijiji vyenye madini kutoa ruhusa ya uchimbaji ( Free prior informed consent) ambayo itazingatia faida kwao.

- tunataka sera ya madini itamke sehemu ya mrahaba, angalau 30%,

tunataka mfuko wa Fidia kupisha maeneo ya uchimbaji kuzingatia Mfumo wa LAND FOR EQUITY ili kutumia ardhi kama Hisa kwenye Migodi.
 
Back
Top Bottom