Mbunge Idd Kassim aomba Maboresho ya sera na sheria ili kuwanufaisha wachimbaji wadogo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942
Mbunge wa Jimbo la Msalala Mkoani Shinyanga ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mheshimiwa Iddi Kassim Iddi ameomba kufanyika kwa mabadiliko ya Kisera na Kisheria ili kuendelea kuwanufaisha wachimbaji wadogo wa madini hapa nchini.

Mhe. Iddi ametoa maombi hayo jana Septemba 30, 2023 wakati akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwenye kilele cha maonesho ya sita ya Teknolojia ya Madini yaliyofanyika katika viwanja vya Bombambili mkoani Geita.

Katika hotuba yake Mhe. Iddi amemuomba Waziri wa Madini kufanya mbadiliko ya kisera yatakayoruhusu wachimbaji wadogo kusamehewa kodi za vifaa vya uchimbaji watakavyoingiza hapa nchini.

Aidha Mhe. Iddi ameiomba serikali kupeleka muswada wa mabadiliko ya sheria Bungeni utakaoyataka makampuni makubwa ya uchimbaji kutoa taarifa za tafiti za madini katika maeneo ambayo hawana nia ya kuyaendeleza ili taarifa hizo ziwasaidie wachimbaji wadogo kufanya shughuli zao kwa kuzingatia tafiti hizo zilizofanyika.

Mbali na maombi hayo Mhe. Iddi alimuomba Mgeni rasmi katika shughuli hiyo Mhe. Hemed Suleiman Abdullah ambaye ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kufikisha salamu za kamati ya Nishati na Madini kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan na kwamba wao kama kamati wanaunga mkono Juhudi zinazofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuinua sekta ya madini hususani wachimbaji wadogo hapa nchini

F7XMSGnXYAAz1nr.jpg
 
Back
Top Bottom