Hatimaye Jerry Muro ashinda kesi yake

Mwita ni sheria ipi inatamka hayo mkuu
Maana naamini Jerry hakuwa guilty of the offence
Angepatikana na hatia hapo hata hivyo akifungwa akirudi bado ni raia wa kawaida na ana haki kama raia wengine ikiwemo ya ajira
naomba hiyo sheria mkuu inayosema ukipatikana na hatia huruhusiwi kuajiriwa tena
Kichwa panzi huyo.....
 
Mkuu hii ni kwa mujibu wa sheria gani? Wanatakiwa washitakiwe hao manake kwa mujibu wa ELRA mtuhumiwa hatakiwi kukatwa mshahara anatakiwa alipwe wote hadi atakapopatikana na hatia. Na kama hatapatikana na hatia basi anarudishwa kazini na kuendelea na kazi hili suala la kukatwa mshahara ama kutolipwa halipo hata kidogo!

sheria siilewi vizuri ila mimi nimeripoti kile nilichokisoma kwenye magazeti na si kwamaba natoa ufafanuzi wa namna TBC ilivyotakiwa kuact
 
Hamna aliye juu ya sheria Maria. Watu wanajua kucheza tu na sheria. Issue ya Jerry Muro ni obvious kila mtu alikuwa anaifahamu. Mahakama imeshaamua, hatuwezi tena kumuhukumu hapa JF
Sasa unapata ujasiri wapi wa kumhukumu Jery Muro kuwa alikuwa anachezea watu wasio chezewa hapa TZ? na wewe ni mmoja wao???
 
Mwita ni sheria ipi inatamka hayo mkuu
Maana naamini Jerry hakuwa guilty of the offence
Angepatikana na hatia hapo hata hivyo akifungwa akirudi bado ni raia wa kawaida na ana haki kama raia wengine ikiwemo ya ajira
naomba hiyo sheria mkuu inayosema ukipatikana na hatia huruhusiwi kuajiriwa tena

Obama alikuwa na jibu moja tu kwa wale ambao hawakuamini kuwa Osama amekufa. Obama alisema ' you will never see Osama walking on this planet again'. Mimi nasema ' you will never see Jerry Muro employed again'
 
Hawakuwa na kesi; toka mwanzo wengine tulibeza kesi nzima na kile kilichoitwa 'ushahidi' wa 'pingu'! waste of people's resources kwa kweli. grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr keep fighting!
 
Nchi hii imekuwa ni ya uonevu hasa kwa wale wenye kuitakia mema nchi yetu kama ilivyokuwa kwa huyu Jerry Muro,kipindi kile cha usiku wa habari kilikuwa kinafichua mengi ambayo watanzania wengi tulikuwa hatuyajui.
Hongera sana Jerry,sasa ni wakati wa kujipanga upya na kurudi katika kazi kwa mbinu mpya na za kisasa katika kuwafichua wale wote wanaoenda kinyume na sheria na taratibu za kazi na nchi kwa ujumla.
 
walio achiwa ni jerry muro, deogratias na edwin kapama. ni kwamba wameonekana hawana hatia katika kesi ya rushwa ya sh 10,000,000/-. Jerry kasema mapambano bado yanaendelea. kawashukuru viongozi wa dini zote. anasema kawasamehe wote walio panga kumuangamiza wakiwemo viongozi wake, polisi, serikali na wote walioshiriki katika kumuangamiza. anasema yaliyopita si ndwele tugange yajayo. Kasema sasa kilichobaki ni kuchapa kazi kwa bidii na mapambano yanaendelea.source ITV. Mia
 
Hahaha... Sio mipasho bht ni ukweli halisi, afu kuna watu wanakerwa j muro kuachiwa lol, shame on them. Ndio kaachiwa sasa wajinyweshe tu 'vyumu'
Ile rushwa aliiomba. Nchi hii vyombo vya dola vyote vimeoza. Polisi, hakimu wote kama Muro.
 
Hahaha... Sio mipasho bht ni ukweli halisi, afu kuna watu wanakerwa j muro kuachiwa lol, shame on them. Ndio kaachiwa sasa wajinyweshe tu 'vyumu'

Tutasikia mengi leo hapa mwayego....
Lakini cha muhimu Jerry yu huru, uhuru mtamu SL bana....

Ajira ajira, siku zote hizi alikuwa anaishije tangu ashtakiwe?
Hivi kila mtu lazima aajiriwe?
 
Sheria za nchi zinasema ukishashtakiwa mahakamani hutakiwi kuajiriwa tena na kampuni yoyote ile. Huyu Jerry Murro imekula kwake moja kwa moja.
Kaka hiyo sheria nenda kaisome upya, mie ninavyojua ni kwamba ukishitakiwa na mwisho wa kesi ukapatikana na hatia hapo ndipo unayoyasema yanakuwa sahihi, lakini pia angalia Mh Chenge na yule mbunge wa Mbeya wote walihukumiwa na wakatoa faini, sasa nashindwa kuelewa kwani wao sio waajiliwa?
 
walio achiwa ni jerry muro, deogratias na edwin kapama. ni kwamba wameonekana hawana hatia katika kesi ya rushwa ya sh 10,000,000/-. Jerry kasema mapambano bado yanaendelea. kawashukuru viongozi wa dini zote. anasema kawasamehe wote walio panga kumuangamiza wakiwemo viongozi wake, polisi, serikali na wote walioshiriki katika kumuangamiza. anasema yaliyopita si ndwele tugange yajayo. Kasema sasa kilichobaki ni kuchapa kazi kwa bidii na mapambano yanaendelea.source ITV. Mia
Mia....
 
Obama alikuwa na jibu moja tu kwa wale ambao hawakuamini kuwa Osama amekufa. Obama alisema ' you will never see Osama walking on this planet again'. Mimi nasema ' you will never see Jerry Muro employed again'

Siamini kama maneno haya yanatoka kwenye key board unayotumia Mwita na umetumia mikono yako na ubongo wako kuyaandika
Jerry hana hatia kwa mashtaka aliyofunguliwa
Kisheria hata TBC walifanya makosa kwa kuwa hakustahili kufukuzwa kazi (kama amefukuzwa) maana mtu anakuwa guilty of the offence baada ya mahakama kudeclare hayo kuwa ana hatia na hapo ndipo walipaswa wao wamfukuze kazi.
Ila iwapo amefukuzwa kazi kabla mahakama haijamdeclare kuwa guilty of the offence kisheria ni kosa
Na Jerry kwa sasa hana hatia ni mtu huru na hajapatikana na kosa alilostakiwa nalo na ana uhuru wa kuajiriwa na kupata ajira popote pale
Sema kama kuna sababu nyingine kama kudanganya elimu au makosa mengine ya Jerry as Jerry ila ana haki zote kama raia ikiwepo ya kuajiriwa
 
Hawakuwa na kesi; toka mwanzo wengine tulibeza kesi nzima na kile kilichoitwa 'ushahidi' wa 'pingu'! waste of people's resources kwa kweli. grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr keep fighting!
Naukumbuka sana ule mjadala wa pingu, ukachagizwa na zile Picha za 'pingu za Sikonge'......

He is a fighter...
 
Sheria za nchi zinasema ukishashtakiwa mahakamani hutakiwi kuajiriwa tena na kampuni yoyote ile. Huyu Jerry Murro imekula kwake moja kwa moja.
Mbona kuna baadhi ya wabunge walishtakiwa na wakaendelea kula hela ya walipa kodi?hiyo sheria ipo kwa baadhi ya watu tu?
 
Back
Top Bottom