Hatimaye Dr. Slaa amjibu Nape, aingizwa 'King'?

Hatimaye Dr. Slaa amjibu Nape, aingizwa 'King'?

Kama ndivyo, kadi ni ile gamba yenye maandishi kwa nyuma. Unataka kusema nini kuhusu Karume kuwa na kadi ya ASP NA CCM? Je, kwanini na yeye hafuati ya sheria husika.
Je, yeye kutangaza kadi ya mbele ya mkutano mkuu wa ccm ni hakuna aliyelalamikia kadi hiyo ina maana kwamba wewe Rutashbolwa ni mwana ccm kuliko wale wote waliokuwepo Dodoma? Au wao wote walipitiwa kuhusu sheria husika? Naomba jibu.
Itafahamika tu baba ASP haipo ila CCM ipo.kaza mwendo
 
Mkuu hivi milioni 12 kwa mwezi ni pesa kidogo? Ujaweka nyumba na gari.

Ritz......na huyu ndiye kifaa cha kutarajiwa ndani ya cdm amabcho kinaienzi kadi ya ccm kwa kujilimbikizia mali..........................................sijui hajasoma na kuielewa imani ya 6 ya ccm................."Cheo ni dhamana na sitakitumikia cheo changu kwa manufaa yangu?"
 
Last edited by a moderator:
[U.... Hebu nielimishe Dr. Slaa kuishinikiza cdm imlipe kama mbunge huyo siyo askari wa kukodiwa... siyo mamluki?

Ruta, unaporomoka kwa kasi sana kifikra, zamani hukuwa hivi, najiuliza kulikoni?
Kwa fikra zako Katibu Mkuu wa chama kama CDM, CCM na CUF ni nafasi ndogo sana? Kwa vyama makini hiyo ni nafasi nyeti sana na ndio maana CCM kt
k miaka 12 wamekuwa na Makatibu 3!
CCM na CUF hawawalipi GS wao? CCM wanamlipa kiasi gani GS wao hadi uone Slaa analipwa nyingi?
 
Mtu wa Shamba unakhoja nzito lakini huwezi kutuambia Dr. Slaa anaienzi vipi kadi ya ccm kama siyo kulipa michango kimyakimya kama Nape alivyowatuhumu cdm............darini

Uwe mwangalifu unapokejeliwa kwenye majibu ya watu wenye akili.

Hoja iko clear. Kwa mujibu wa katiba ya CCM Dr. Slaa si mwanachama kwa kuwa ni mwanachama wa Chadema.

Mie naona kushupalia kitu ambacho kiko wazi namna hii kwa mujibu wa katiba ni upotoshaji wa makusudi.

Naona tunaondoa attention kwenye masuala ambayo yangeweza kuboresha maisha yetu. Au tukiri kuwa tumefilisika mawazo ya kujenga.
 
Mikael P Aweda Pole sana.......................kwa kutetea unga wako.....lakini mwanadamua haishi kwa mkate tu bali kwa kila neno litokalo kwenye kinywa cha Muumba...................na neno tajwa ni pamoja na kuwa mkweli..................................kumuomba Dr. Slaa ndiyo demokrasia ya wapi......................................wapi ile kitu kidogo mnayoiita.........................."people's power?".........................au ni wimbo tu wa majukwaani?

sababu yako ya pili hata siijibu maana husemi ukweli................nipe takwimu za mishahara tajwa na tuone ya ccm na wa huyu Dr. Slaa tofauti zake ziko wapi................................takwimu please...............

la tatu hizo ni hadithi za kufikirika............kwa Dr. Slaa ambaye jana kwa kinwa chake kadai anaienzi kadi ya ccm si pia na imani ya sita ya ccm?.................................: "cheo ni dhamana na sitakitumia cheo changu kwa manufaa yangu?"

suala hapa siyo marupurupu ambayo mimi sijayataja.......................suala kwa nini utofautiane na wenzio kimshahara kama lengo kweli ni kuwahudumia wananchi?

Sasa unaanza kurudi kwenye line, unajenga hoja.
Mosi, mimi sijaajiriwa na Chadema. Mimi ni graduate niliyeajiriwa na mjasiria mali mdogo on part time basis.

Pili, Sisi chadema hatushindani kwa pesa kama ccm. Sisi tunafanya utafiti kwanza. Utafiti ulionesha Dr Slaa atashinda. Tukamwambia aachie ubunge hata kama ana uhakika wa kushinda ili agombee urais kwa mujibu wa utafiti. Alifanya hivyo. Ni ndiyo maana ya kumwomba.

Tatu, People' power ni kusikiliza na kutenda matakwa ya wananchi ambao kwa mujibu wa utafiti walimtaka Dr Slaa agombee japokuwa wakati huo yeye mwenyewe hakuwa na nia hiyo.
Nne, sababu yangu ya pili ni kweli, taarifa nilizo nazo ni kwamba Hata Nape pamoja na uropokaji wake kwa mujibu wa maelezo yaka anamshinda slaa ukijumlisha malipo na maposho yake yote. Kama wewe una ushihidi wa kinyume na huo ulete.
Tano, kuhusu Slaa kuienzi kadi ya ccm mimi sikusikia kauli yake. Lakini je, nauliza sisitunaenzi majumba na njia za biashara ya utumwa maana yake tunaipenda sana hiyo biashara?
 
unajua maaana ya kadi? na anapata wapi mamlaka ya kukusanya za watu.

kix........ingependeza mwenye picha ya Dr. Slaa akibeba kadi za ccm alizopewa akiwa ndani ya cdm ingelikuwa na mvuto wa kipekee.......tunachozungumzia hapa ni unafiki wa wanasiasa wote...............
 
Last edited by a moderator:
Hivi ukienzi kaburi, maana yake, aliyezikwa humo ndani badi yu hai? Au ukienzi picha ya marehemu inaama huyo mtu bado yu hai?

Masharti ya uachama wa CCM yamo kwenye katiba, and I dont even understand CCM watatibiwa na dawa gani ili wawe wanasoma? Na kama wanashindwa kusoma mistari michache inayohusu uanachama, kwanini tuwaamini kwenye ku-sign mikataba?
unamuenzi kwasababu unampenda na alikua muhimu.
 
Sasa unaanza kurudi kwenye line, unajenga hoja.
Mosi, mimi sijaajiriwa na Chadema. Mimi ni graduate niliyeajiriwa na mjasiria mali mdogo on part time basis.

Pili, Sisi chadema hatushindani kwa pesa kama ccm. Sisi tunafanya utafiti kwanza. Utafiti ulionesha Dr Slaa atashinda. Tukamwambia aachie ubunge hata kama ana uhakika wa kushinda ili agombee urais kwa mujibu wa utafiti. Alifanya hivyo. Ni ndiyo maana ya kumwomba.

Tatu, People' power ni kusikiliza na kutenda matakwa ya wananchi ambao kwa mujibu wa utafiti walimtaka Dr Slaa agombee japokuwa wakati huo yeye mwenyewe hakuwa na nia hiyo.
Nne, sababu yangu ya pili ni kweli, taarifa nilizo nazo ni kwamba Hata Nape pamoja na uropokaji wake kwa mujibu wa maelezo yaka anamshinda slaa ukijumlisha malipo na maposho yake yote. Kama wewe una ushihidi wa kinyume na huo ulete.
Tano, kuhusu Slaa kuienzi kadi ya ccm mimi sikusikia kauli yake. Lakini je, nauliza sisitunaenzi majumba na njia za biashara ya utumwa maana yake tunaipenda sana hiyo biashara?

[MENTION]Mikael P Awenda[/MENTION].........historia yetu hata siku moja hatujaenzi biashara ya utumwa kwa kuiandika........hizo ni kumbukumbu tujue tunatoka wapi, tuko wapi na twaelekea wapi...........Khoja ya malinganisho ya mafao inafaa ijengwe kwa takwimu siyo nukuu za wahusika ambao wana masilahi ya kuongea watakacho......hoja yako ya pili na ya tatu...........zinathibitisha ya kuwa hakuna "people's power" ndani ya cdm............................

hakuna utafiti katika kuheshimu ushiriki wa wanachama katika kupiga kura za maoni......................pili, sauti ya mwanachama yatakiwa iwe ndiyo mwanzo na mwisho wa people's power...............................bado mna safari ndefu......................mkitaka kufanikiwa acheni kuwa ccm carbon paper................
 
Ndo maana niliichukia siasa tangu nikiwa mtoto, halafu wananchi tusivyo na uelewa tunakatana mapanga wakati wao wanagonganisha glass za wine, whiskey na gin duh.........................!

Kimbweka BIg poinT....................THEY ARE ALL THE SAME...
 
Last edited by a moderator:
Narudia tena: Katiba ya CCM inamvua uanachama Dr. Slaa kwa kujiunga kwake na CHADEMA.

Nanukuu katiba ya CCM.
7. (1) Mtu akikubali kuwa Mwanachama itabidi atekeleze haya yafuatayo:-
(a) Atatoa kiingilio cha Uanachama
(b) Atalipa ada ya Uanachama kila mwezi isipokuwa kama akipenda anaweza kulipa ada ya mwaka mzima mara moja.
(c) Atatoa michango yoyote itakayoamuliwa

(2) Viwango vya kiingilio, ada na michango vitawekwa na Halmashauri Kuu ya Taifa.
(3) Uanachama wa mwanachama utakwisha kwa:-
(a)Kufariki.
(b)Kujiuzulu mwenyewe.
(c)Kuachishwa kwa mujibu wa Katiba.
(d)Kufukuzwa kwa mujibu wa Katiba.
(e)Kutotimiza masharti ya uanachama.
(f)Kujiunga na Chama kingine chochote cha siasa.

(4) Mwanachama ambaye uanachama wake unakwisha kwa sababu yoyote ile hatarudishiwa kiingilio alichokitoa, ada aliyotoa wala michango yoyote aliyoitoa.
 
Sasa hujengi hoja unabisha. Neno mfu maana yake kufa, mfu inatokana na kufa. Kwa hiyo mwanachama mfu maana yake mwanachama aliyekufa kiitikadi na kiuanchama hai kwa mujibu wa sheria pia. Kwa hiyo, mwanachama mfu ni sawa sawa kabisa kwa 100% kuwa siyo mwanachama. Jenga hoja usipige kelele.

punguza povu.nini maana ya kusema mtu flani sio mwanachama kabisa na hii ya kusema mwanachama mfu.wewe unatetea vitu usiovijua ni heri ungekaa kimya kuficha aibu
 
Ndo maana niliichukia siasa tangu nikiwa mtoto, halafu wananchi tusivyo na uelewa tunakatana mapanga wakati wao wanagonganisha glass za wine, whiskey na gin duh.........................!
Kimbweka BIg poinT....................THEY ARE ALL THE SAME...

But you are supporting Nape aren't you. Sasa huo nao sio unafiki? Unaonakana unamuunga mkono anachukia siasa. Lakini kwa uzi huu unadhihirisha kuwa wewe ni mshabiki wa siasa!

Contradiction.
 
Mikael P Aweda nani kakwambia sisi tunayaenzi mambo hayo yanayodhalilisha utu wa mtu mweusi? kumbukumbu hizo ni kutukumbusha.....tu, period....tunaenzi mambo ambayo tunayojivunia nayo kama Dr. Slaa anavyojivunia u-ccm wake wa kimyakimya...............

Kuhusu biashar ya utumwa kama tunaenzi au ni kumbu kumbu sawa vyo vyote iwavyo.
Hoja yangu ni kwamba kama vile tunaendelea kutunza maeneo ndivyo hivyo Dr Slaa anaitunza kadi yake. Full stop.
Nimeomba ushahidi wa kuilipia.
 
Mikael P Aweda kuwa graduate hakukuondoi wewe kulipwa na chama wala kuajiriwa na mjasiriamali hakukuondolei wewe haki ya kulipwa na cdm. Pili una maana kwamba slaa na nape wote ni waropokaji ila wanazidiana kiwango?
 
Last edited by a moderator:
Rutashubanyuma,

Soma Katiba ya CCM toleo la mwaka 2010. Ibara ya 13. kufungu (1). Inahusu WANACHAMA NA VIONGOZI.

Uanachama utakwisha kwa:

(a) Kufariki.
(b) Kujiuzulu mwenyewe.
(c) Kuachishwa kwa mujibu wa Katiba.
(d) Kufukuzwa kwa mujibu wa Katiba.
(e) Kutotimiza masharti ya uanachama.
(f) Kujiunga na Chama kingine chochote cha siasa.
(2) Mwanachama ambaye uanachama wake unakwisha kwa sababu yoyote ile hatarudishiwa kiingilio alichokitoa, ada aliyotoa wala michango yoyote aliyoitoa.

Dr Slaa alijiunga na chama kingine cha siasa zaidi ya miaka 15 iliyopita (Nape alikuwa hajamaliza hata darasa la saba), amekuwa mbunge - wa kuchaguliwa- kupitia chama kingine cha siasa (CHADEMA) wa miongo kadhaa. Leo hii Nape & co wanauliza kadi yake ya CCM?


1. Nape na wenzake wanaijua vema katiba ya CCM? wanaelewa masharti ya uanachama?

2. Ni kifungu gani cha katiba ya CCM kinachosema kuwa ili uanachama wa CCM ukome sharti mhusika arudishe kadi?

3. Kwa zaidi ya 15 ambaye Dr Slaa amekuwa mwanachama wa chama kingine cha siasa, CCM walikuwa wapi? Why now?

You don't need to think very hard kujua kuwa CCM wanamhofia Dr Slaa. Wanajua anakubalika kwa wananchi na sasa wanachofanya ni kujaribua kumshambulia yeye (Dr Slaa) binafsi.

CCM wanafanya kosa sana kujikita kwenye hizi siasa za maji taka. Wanatakiwa wawaambie wananchi kwa nini elimu imeshuka, kwanini watu hawana maji, kwanini umeme bado ni kitendawili, kwanini hakuna dawa hospitalini, kwanini deni la taifa linaongezeka huku umaskini unamaliza watanzania? Wanatakiwa waeleze utekelezaji wa Ilani yao ya uchaguzi. Ilani yao inasema nini, na wamefanya nini?

Kuendelea kuimba Dr Slaa kila siku ni kielelezo tosha cha kufilisika hoja. Watu wamekosa majibu kwa maswali ya msingi na sasa wanakwepa kwa kuleta siasa za maji taka. Ni madharau kwa wapiga kura.

[/QUOTE FJM, kama nitakuwa nimemuelewa vema Rutashubanyuma, nadhani hoja si kuwa Dr Slaa ni mwanachama wa CCM au la. Hoja ni Dr Slaa kukubali kuingizwa kwenye mjadala wa kipuuzi na Nape. Kama kuna mtu atakuwa anaamini kuwa Dr Slaa bado ni mwanachama wa CCM, basi huyo atakuwa na aina nyingine ya matatizo
 
Last edited by a moderator:
Kuhusu biashar ya utumwa kama tunaenzi au ni kumbu kumbu sawa vyo vyote iwavyo.
Hoja yangu ni kwamba kama vile tunaendelea kutunza maeneo ndivyo hivyo Dr Slaa anaitunza kadi yake. Full stop.
Nimeomba ushahidi wa kuilipia.

mbona mkuu wewe unalazimisha watu waamini unayoamini wewe bila hoja badala yake inakuwa shuruti? Unaweza kutupa ushahidi hapa wa slaa kutokulipia kadi yake? Au wewe ndio unamtunzia?hoja hapa ni kwamba slaa ana kadi ya ccm hayo mengine hayana umuhimu kwa sasa
 
Mikael P Awenda.........historia yetu hata siku moja hatujaenzi biashara ya utumwa kwa kuiandika........hizo ni kumbukumbu tujue tunatoka wapi, tuko wapi na twaelekea wapi...........Khoja ya malinganisho ya mafao inafaa ijengwe kwa takwimu siyo nukuu za wahusika ambao wana masilahi ya kuongea watakacho......hoja yako ya pili na ya tatu...........zinathibitisha ya kuwa hakuna "people's power" ndani ya cdm............................

hakuna utafiti katika kuheshimu ushiriki wa wanachama katika kupiga kura za maoni......................pili, sauti ya mwanachama yatakiwa iwe ndiyo mwanzo na mwisho wa people's power...............................bado mna safari ndefu......................mkitaka kufanikiwa acheni kuwa ccm carbon paper................

Hapo kwenye red tuko pamoja kuhusu kadi ya Slaa.
Kadi hiyo, maana yake miaka michache ijayo Dr Slaa atakaa na watoto wake na wajukuu zake ili awaambie alikuwa ccm na ushahidi anao, akajiunga Chadema na ushahidi anao.
Tatizo, wewe unabisha Slaa kuwa na hiyo kadi ya kumbu kumbu. Huku unakubali serikali kutumia fedha kwenye maeneo yalikofanyika biashara mbaya ya utumwa.
Watz wanachukia biashara ya utumwa huku tunagharimia maeneo yalikofanyika.
Mandela anachukia kisiwa kile alichoka miaka 27 lakini waafirika kusini wanatumia fedha nyingi kuitunza - sasa imekuwa utalii.
Dr Slaa anaichukia sana ccm lakini ana kadi yake kwa ajili ya kumbu kumbu yakewajukuu wake. alikotoka na alikoishia. full stop.
 
Sioni mada ya kuchangia hapa. Hakuna taarifa kamili wala nukuu za Dr Slaa.

Afadhali umeliona hilo, nimshauri mleta mada afanyie uhariri kichwa cha habari ameuchuna, amebaki kubishana na wachangiaji wengine.
Kichwa chake cha habari ni kama Magazeti ya Udaku tu, hakina uhusiano na hoja yake.
 
Ndiyo slaa ni active member na analipia ada zote za wamachama huko anazuga tuuu kwa ushahidi njooni mjengoni mpewe data zote.na c slaa tu lipumba,hamad,zito,mbowe wote ni wanaccm

Hivi na wewe unajiita great thinker?
Ninavyowajua mlivyo wanafiki si mngeweka hizo risiti za malipo ya kadi za uanachama hapa JF ili tuone kwamba ni kweli hao ni wanachama hai! Wekeni ushahidi kama alivyoweka Rostam kwa Mtikila, baada ya kuchukua milioni tatu na kuzikana.
 
Bado siamin kama kweli Dk Slaa amekiri hvyo, mana CCM wana mtambo wa kutengeneza sms, labda Slaa ajitokeze mwenyewe akil hadharan, Nape sio mtu wa kumuamin.!!
 
Back
Top Bottom