Hatimaye Dr. Slaa amjibu Nape, aingizwa 'King'?

Hatimaye Dr. Slaa amjibu Nape, aingizwa 'King'?

Kuna haja ya kupitia upya hadhi ya wanachama wapya wanaojiunga cdm ili kujua uaminifu na uzalendo wao
 
Naomba usipige kelele na usipotoshe.
Dr Slaa hakuomba kugombea urais, aliombwa. Kwa hiyo, kusema kwamba alishinikiza ni uwongo na upotoshaji. Dr Slaa alishachukua fomu ya kugombea ubunge mwaka 2010 kama unakumbuka. Sisi viongozi wa chama ndo tulimwomba huku akiwa na uhakika wa kuwa mbunge wa Karatu.
Pili, Dr Slaa analipwa pesa kidogo sana kulinganisha pesa wanazolipwa Makamba,Mkama na Kinana. Kama ubisha leta ushahidi.
Tatu, mapato ya Dr Slaa ni kidogo sana ukilinganisha na Mbunge mwenye vikao vingi vyenye marupu rupu mengi.
Kiujumla mkuu hapa unapotosha.

Mikael P Aweda Pole sana.......................kwa kutetea unga wako.....lakini mwanadamua haishi kwa mkate tu bali kwa kila neno litokalo kwenye kinywa cha Muumba...................na neno tajwa ni pamoja na kuwa mkweli..................................kumuomba Dr. Slaa ndiyo demokrasia ya wapi......................................wapi ile kitu kidogo mnayoiita.........................."people's power?".........................au ni wimbo tu wa majukwaani?

sababu yako ya pili hata siijibu maana husemi ukweli................nipe takwimu za mishahara tajwa na tuone ya ccm na wa huyu Dr. Slaa tofauti zake ziko wapi................................takwimu please...............

la tatu hizo ni hadithi za kufikirika............kwa Dr. Slaa ambaye jana kwa kinwa chake kadai anaienzi kadi ya ccm si pia na imani ya sita ya ccm?.................................: "cheo ni dhamana na sitakitumia cheo changu kwa manufaa yangu?"

suala hapa siyo marupurupu ambayo mimi sijayataja.......................suala kwa nini utofautiane na wenzio kimshahara kama lengo kweli ni kuwahudumia wananchi?
 
Last edited by a moderator:
Kwa kuongeza,
Kama ukiwa mwanachadema huku una kadi mfu ya ccm kama Dr Slaa unakuwa na ujasiri wa kuwataja mafisadi hadharani akiwepo Rais. Basi mimi jimboni kwangu nawahitaji wanaccm watakaojiunga na Chadema ambao nitawaachia kadi za ccm halafu wafanye kazi kama Dr Slaa.
[MENTION]
Mikael P Aweda[/MENTION] khoja hii ninaiafiki kama Dr. Slaa angeliwatonya wale waliokuwa wakimkabidhi kadi za ccm kuwa yeye yake iko kibindoni na anaienzi vilivyo kwa kufuata yote yaliyomo zikiwemo imani na madhumuni ya kuanzishwa ccm.......................................hivi Dr. Slaa siyo anakunywa mvinyo na kuwalazimisha wengineo wanywe........togwa au hata maji machafu?
 
Naomba usipige kelele na usipotoshe.
Dr Slaa hakuomba kugombea urais, aliombwa. Kwa hiyo, kusema kwamba alishinikiza ni uwongo na upotoshaji. Dr Slaa alishachukua fomu ya kugombea ubunge mwaka 2010 kama unakumbuka. Sisi viongozi wa chama ndo tulimwomba huku akiwa na uhakika wa kuwa mbunge wa Karatu.
Pili, Dr Slaa analipwa pesa kidogo sana kulinganisha pesa wanazolipwa Makamba,Mkama na Kinana. Kama ubisha leta ushahidi.
Tatu, mapato ya Dr Slaa ni kidogo sana ukilinganisha na Mbunge mwenye vikao vingi vyenye marupu rupu mengi.
Kiujumla mkuu hapa unapotosha.

na wewe leta ushahidi wa mapato kidogo anayolipwa slaa kwa kulinganisha na yale ya mukama na ya wabunge.vinginevyo hili povu halitakusaidia kwani watanzania wana akili kuliko wewe unavyofikiri
 
Hivi ukienzi kaburi, maana yake, aliyezikwa humo ndani badi yu hai? Au ukienzi picha ya marehemu inaama huyo mtu bado yu hai?

Masharti ya uachama wa CCM yamo kwenye katiba, and I dont even understand CCM watatibiwa na dawa gani ili wawe wanasoma? Na kama wanashindwa kusoma mistari michache inayohusu uanachama, kwanini tuwaamini kwenye ku-sign mikataba?

FJM labda muulize kibosile wenu anamaanisha nini kuienzi kadi ya ccm kama siyo kuilipia michango kimyakimya...................na hivyo kuamini yote ambayo ccm inayaamini...........
 
Last edited by a moderator:
Elizabeth Dominic Kadi ndilo jambo muhimu kulikoni yote.........................ndiyo mlango wa uzalendo na kuaminika..................kama Dr. Slaa bado ni ccm sasa khali ya cdm imekaaje? Pili kwanini hafuati sheria ya kuwa chama kimoja tu?

Unapotosha mkuu, red hapo.
Kadi ndiyo muhimu kuliko yote kwa mujibu wa nini? Biblia, Korani, au katiba ya nchi?
Kadi ndo mlango wa kuaminika - Nani kasema? Wewe umesoma wapi? Kadi ni kitambulisho tu. Uhai wa kadi ni michango ya uanachama. Lete ushahidi wa uanachama hai wa Dr Slaa huko kwenu ccm. Mbona hii hujibu?
 
FJM labda muulize kibosile wenu anamaanisha nini kuienzi kadi ya ccm kama siyo kuilipia michango kimyakimya...................na hivyo kuamini yote ambayo ccm inayaamini...........

Kama kweli Dr Slaa analipia kadi yake ya CCM, na hao CCM wanapokea hela huku wakijua fika kuwa Dr Slaa ni mwanachama wa chama kingine cha siasa - then CCM watakuwa na matatizo. Ina maana hawaijui hata katiba yao inasema nini?
 
Nami nina kadi ya CCM ambayo niliinunua kwa kulazimishwa enzi zile za chama kimoja. Hiyo kadi ni mali yangu kwa vile niliuziwa, japokuwa siyo mwanachama wa CCM. Nimeiweka kama "MEMORABILIA" kuonesha watoto na wajukuu KADI ya CHAMA KANDAMIZI na CHAMA cha MAFISADI Tanzania.
mamliki hauna sababu ya msingi wa kubaki na hiyo kadi,maji ya kijani yanawasumbua.
 
Ndo maana niliichukia siasa tangu nikiwa mtoto, halafu wananchi tusivyo na uelewa tunakatana mapanga wakati wao wanagonganisha glass za wine, whiskey na gin duh.........................!
 
FJM labda muulize kibosile wenu anamaanisha nini kuienzi kadi ya ccm kama siyo kuilipia michango kimyakimya...................na hivyo kuamini yote ambayo ccm inayaamini...........

Kwani sisi watanzania tunamaanisha nini tunapoenzi yale majengo yaliyotumika wakati wa biashara ya utumwa enzi za ukoloni pamoja na njia zake? Kwa mujibu wa maelezo yako unataka kusema tunapenda kurudisha biashara ya utumwa?
Je, wajua tofauti ya kubisha, kujenga hoja makini na kupiga kelele?
 
Dr Slaa sasa kadi ya CCM unakaa nayo ya nini wakati wewe upo Chadema. Mbona wale wanarudisha kadi kwenye mikutano yako uambii wakae nazo kama kumbukumbu.

CCM wanakumbukumbu ndogo sana kwenye historia ya siasa, wamesahau kuwa wakati Dr. Slaa anaiacha CCM wana karatu walikusanya kadi zote za CCM na kuzichoma moto ikiwemo ya Dr. Slaa ulitaka Dr. Slaa aitoe wapi kadi nyingine ya kurudisha? Ritz. Nape Nnauye anaongoza kwa kuongea ovyoo ilimradi ameongea! Atoe hizo risiti za malipo ya vogogo wa CHAEEMA za mwaka huu 2012! Aache siasa za majitaka.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu @Rutashubanyuma, mimi nashangaa sana jinsi jambo hili lilivyochukuliwa kama ajenda ya kisiasa. Unajua kadi ni kitambulisho cha uanachama. Kwa hiyo hoja hii inakuwa na mashiko tu pale inapoweza kuwa hoja ya kutosha kuthibitisha kuwa Dr. Slaa bado ni mwanachama wa CCM. Lakini katiba ya Chama cha Mapinduzi, Kifungu kinachohusu wanachama kinataja waziwazi kuwa yeyote atakayejiunga na chama kingine cha siasa amejitoa uanachama wa CCM kwa mujibu wa katiba. Nanukuu katiba hapa kwa mara nyingine:
7. (1) Mtu akikubali kuwa Mwanachama itabidi atekeleze haya yafuatayo:-
(a) Atatoa kiingilio cha Uanachama
(b) Atalipa ada ya Uanachama kila mwezi isipokuwa kama akipenda anaweza kulipa ada ya mwaka mzima mara moja.
(c) Atatoa michango yoyote itakayoamuliwa

(2) Viwango vya kiingilio, ada na michango vitawekwa na Halmashauri Kuu ya Taifa.
(3) Uanachama wa mwanachama utakwisha kwa:-
(a)Kufariki.
(b)Kujiuzulu mwenyewe.
(c)Kuachishwa kwa mujibu wa Katiba.
(d)Kufukuzwa kwa mujibu wa Katiba.
(e)Kutotimiza masharti ya uanachama.
(f)Kujiunga na Chama kingine chochote cha siasa.

(4) Mwanachama ambaye uanachama wake unakwisha kwa sababu yoyote ile hatarudishiwa kiingilio alichokitoa, ada aliyotoa wala michango yoyote aliyoitoa.

Kwa mantiki hii haijalishi kadi iko wapi, kaiweka au kaienzi (muwe waangalifu kuchambua kejeli kwenye majibu): Katiba ya CCM inathibitisha kuwa yeye si mwanachama wa CCM,
 
Bigirita unajua maaana ya kadi? na anapata wapi mamlaka ya kukusanya za watu.
 
Last edited by a moderator:
Naomba usipige kelele na usipotoshe.
Dr Slaa hakuomba kugombea urais, aliombwa. Kwa hiyo, kusema kwamba alishinikiza ni uwongo na upotoshaji. Dr Slaa alishachukua fomu ya kugombea ubunge mwaka 2010 kama unakumbuka. Sisi viongozi wa chama ndo tulimwomba huku akiwa na uhakika wa kuwa mbunge wa Karatu.
Pili, Dr Slaa analipwa pesa kidogo sana kulinganisha pesa wanazolipwa Makamba,Mkama na Kinana. Kama ubisha leta ushahidi.
Tatu, mapato ya Dr Slaa ni kidogo sana ukilinganisha na Mbunge mwenye vikao vingi vyenye marupu rupu mengi.
Kiujumla mkuu hapa unapotosha.

Mkuu hivi milioni 12 kwa mwezi ni pesa kidogo? Ujaweka nyumba na gari.
 
Majibu ya Dr. Slaa ni yepi mbona kama anajiuliza na kujijibu mwenyewe huyu mtoa hoja!? Au sijaelewa alichokiandika!?
 
Sioni mada ya kuchangia hapa. Hakuna taarifa kamili wala nukuu za Dr Slaa.
 
Kwani sisi watanzania tunamaanisha nini tunapoenzi yale majengo yaliyotumika wakati wa biashara ya utumwa enzi za ukoloni pamoja na njia zake? Kwa mujibu wa maelezo yako unataka kusema tunapenda kurudisha biashara ya utumwa?
Je, wajua tofauti ya kubisha, kujenga hoja makini na kupiga kelele?
[MENTION]
Mikael P Aweda[/MENTION] nani kakwambia sisi tunayaenzi mambo hayo yanayodhalilisha utu wa mtu mweusi? kumbukumbu hizo ni kutukumbusha.....tu, period....tunaenzi mambo ambayo tunayojivunia nayo kama Dr. Slaa anavyojivunia u-ccm wake wa kimyakimya...............
 
Mtu wa Shamba unakhoja nzito lakini huwezi kutuambia Dr. Slaa anaienzi vipi kadi ya ccm kama siyo kulipa michango kimyakimya kama Nape alivyowatuhumu cdm............darini
 
Majibu ya Dr. Slaa ni yepi mbona kama anajiuliza na kujijibu mwenyewe huyu mtoa hoja!? Au sijaelewa alichokiandika!?

[MENTION]Curriculum Specialist[/MENTION]......wewe ni "specialist"................wa kujichanganya nini........................kama hujelewa si unarudia kujisomea hadi uelewe?
 
Back
Top Bottom