Hatimaye Dr. Slaa amjibu Nape, aingizwa 'King'?

Hatimaye Dr. Slaa amjibu Nape, aingizwa 'King'?

Kuna watu ndani wako kwenye Payroll ya Kinana ili kushinda humu kupotosha umma juu ya siasa za nchi hii hasa kuanzia na mtandao huu ambao ni mwiba kwa CCM. Wana JF tusipokuwa makini kubaini na kuchambua malengo ya watu hao, tunaweza kupotoshwa kwa hoja za watu hao kama akina Muchambuzi na hoja za udhaifu wa CDM.
 
dr slaa hata kwenye mdahalo wa uraisi ambao kikwete alikimbia mbio alishawahi sema anayo kadi ya ccm kaiweka kama kumbu kumbu ina mana nape alisahau siku zote hizo hadi mwaka huu ndio katizama hiyo clip?... ccm inaweza kuwa chama kizuri ila kina watu wabaya kama jk. nape, Ritz , zomba na wengine wengi wote...

Kikwete hawezi kufanya mdahalo na Dr Slaa, sio saizi yake Dr Slaa, anatakiwa afanye mdahalo na kina Mrema, Dovutwa.
 
Last edited by a moderator:
Kuna watu ndani wako kwenye Payroll ya Kinana ili kushinda humu kupotosha umma juu ya siasa za nchi hii hasa kuanzia na mtandao huu ambao ni mwiba kwa CCM. Wana JF tusipokuwa makini kubaini na kuchambua malengo ya watu hao, tunaweza kupotoshwa kwa hoja za watu hao kama akina Muchambuzi na hoja za udhaifu wa CDM.

PMNBuko Jibu khoja.....acha hisia
 
Last edited by a moderator:
Kichwa cha habari hakiendani na habari iliyoandikwa! Mtoa uzi ni mwehu tu - kaathirika na CCM, kafisadi kadogo hako achana nako.

Tutor B huu ni ushahidi hizi khoja hazina ubishi..................vinginevyo ungelizibu...............hiki sasa ni kibanio chako na Dr. Slaa wako......
 
Last edited by a moderator:
Kwani kadi ni mali ya nani?mbona mnaichukulia kadi ya Slaa kama ni inshu kuuuuuuubwa!

Magwangala.........issue is why Dr. Slaa is not walking the talk.....................Is he not drinking wine telling everybody else to drink muddy water?
 
Last edited by a moderator:
Dr Slaa sasa kadi ya CCM unakaa nayo ya nini wakati wewe upo Chadema. Mbona wale wanarudisha kadi kwenye mikutano yako uambii wakae nazo kama kumbukumbu.

Nami nina kadi ya CCM ambayo niliinunua kwa kulazimishwa enzi zile za chama kimoja. Hiyo kadi ni mali yangu kwa vile niliuziwa, japokuwa siyo mwanachama wa CCM. Nimeiweka kama "MEMORABILIA" kuonesha watoto na wajukuu KADI ya CHAMA KANDAMIZI na CHAMA cha MAFISADI Tanzania.
 
aiseeeeee babaangu dr slaa si jupo humu jf ngoja aje ajibu hoja mwenyewe haina haja ya kumjibia
 
Suala la msingi


Dr Slaa sasa kadi ya CCM unakaa nayo ya nini wakati wewe upo Chadema. Mbona wale wanarudisha kadi kwenye mikutano yako uambii wakae nazo kama kumbukumbu.
 
Ruta, mbona kichwa cha habari hakioani na habari yenyewe? Itakuwa vema ukihariri hiyo heading.
Pili, nashangazwa na baadhi yetu kupokea madai ya Nape na kuhitimisha kuwa ni sahihi, are we really serious? Yaani mnakubaliana na hoja dhaifu kama hiyo kumshinikiza Dk Slaa kuijibu? Afadhali hoja hiyo ingetolewa na Col Kinana, lau yeye huwa ana hoja na ni muungwana kukubali mahali penye udhaifu.
 
Acha uzushi wewe, alikufuata kwenu ndio akakwambia hayo?

Mijitu mingine sijui inatabia gani, kama wewe ni mwanamme basi ulizaliwa kwa makosa na kama ni mwanamke basi wewe ni hung soy yeng

Mimi nilikuwa najiuliza hapa kwamba dr slaa kasema lini kwamba anayo kadi ya ccm na anaienzi kwa maslahi binafsi na ccm

Nimesoma kila sentensi sijaona kauli ya Dr Slaa inayosema kwamba kadi hiyo inampa maslahi.

Watu wengine ni wapuuzi sana.
Kwamba kadi ni issue ya msingi sana inayoongelewa na kiongozi wa kitaifa wa ccm.
Kwamba ajenda ya ccm kwa miezi kadhaa sasa ni kadi ya ccm aliyowahi kuwa nayo Dr Slaa?
Kwamba sheria ya vyama vya siasai asemajekuhusu kadi?

Pathetic creatures!!

ImageUploadedByJamiiForums1354599280.037255.jpg
 
ii) Je kwa kuienzi kadi ya ccm ambayo ni mali ya ccm huku kila nafasi ikijitokeza Dr. Slaa hupokea kadi za ccm kutoka kwa wanachama wapya wa cdm ambao wanatoka ccm haoni yeye ni mnafiki? Dr. Slaa kadi yake kumbe kaibana lakini za ccm anapokea badala ya kuwaasa nao wazienzi au hata basi kubaini masilahi ya muda mrefu aliyonayo juu ya kadi husika........... badala ya kuzipokea kadi za ccm huku yeye binafsi ana masilahi mazito ya kuienzi kadi tajwa tena kimya kimya.


Mkuu kwenye red hapo juu.
Kwanza mimi sijui kama Dr Slaa ana hiyo kadi au hana.
Hata kama anayo, vyombo vya habari vya kiccm vinasema Dr Slaa and kadi ya ccm kwa kwa ajili ya kumbukumbu. Wewe unasema kuna maslahi nyuma ya kadi ya Dr Slaa. Je, huoni kama ni vizuri ukaweka ushahidi jamvini kwa faida ya wengi?
Hii itaondoa hisia kuwa umechukua hoja yako na kuichanganya na ushabiki wa kiccm.
 
what baffles me honestly is our media not giving us the quality news that we so deserve and instead gets into this charade of who said this and who said that which really doesnt prove a point to anything when it comes to their intention of being in their party

Kenyans so rightly not to be wooed by the media started a petition to focus on issues and not partisan politics, we in JF especially now more so than ever, should call our politicians and Media this being one form of it, to focus now on issues otherwise we shall be basking in news of who endorses Lowassa, who cast the vote that helped Kikwete, who has CCM Card and is in CHADEMA, yes these are stuff we can discuss but honestly we shouldnt be consumed by this, its making us lose the goal post and our focus as a nation,

As a nation we should come strong with issues which both opposition and ruling party have failed to adress , these are afterall what really matters, if you read the news today, UHURU is shouting about Slaa's CCM Card, Majira is counterattacing the very thing,
Lets agree to put these guys to task, have you not noticed that we get so carried away in petty issues and emerge very late and realised we havent questioned what really matters ?

We praise Nape to give hell to opposition but we should praise NAPE to do his job itikadi na uenezi, which to me means he has to really concur as many of us into CCM, ensure party strategy is known, endorsed, followed, yes he can check on Dr Slaa et al, but that shouldnt consume him

As for Dr Slaa, its about time he ups his game as well, yes we heard all about Mafisadi, all about how you are not getting anywhere with the police and all those other stuff that are done to you which are unjustly, but yes we need to see your strategy into ensuring those things will be put into a stop when we decide to give you the driver's seat, we need you to show where CCM have failed and WHAT YOU COULD HAVE DONE IN THEIR SHOES, yes show problems , uncover issues but also show your strategy into dealing with those issues, afterall thats what Roomney's strategy was, which wasnt bad, he didnt win the war but he did surely not lose the battle, Obama recognised his importance even as he is now running the country, Roomney's shadow is so strong, he had to call a truce meeting because he knows he has to appreciate some strategy that Roomney was about to start if he was elected, the re-elected president, didnt diss his enemies, because that will mean you are dissing the people who casted their votes for him, you cant say that JAKAYA is only serving CCM members or those who voted for him, he is serving all of us, so people should raise against those hate speeches and start to question real issues


Borrowing from Mugo who started a Kenyan petition; Lets raise agianst this buffonery only we can take charge of our destiny as a nation

CC Nnauye Jr, Zitto, Dr.W.Slaa, Kitila Mkumbo et al ( i cant tag people to thread ) someone help me to tag these party stalwarts
 
Last edited by a moderator:
Ruta, mbona kichwa cha habari hakioani na habari yenyewe? Itakuwa vema ukihariri hiyo heading.
Pili, nashangazwa na baadhi yetu kupokea madai ya Nape na kuhitimisha kuwa ni sahihi, are we really serious? Yaani mnakubaliana na hoja dhaifu kama hiyo kumshinikiza Dk Slaa kuijibu? Afadhali hoja hiyo ingetolewa na Col Kinana, lau yeye huwa ana hoja na ni muungwana kukubali mahali penye udhaifu.
 
Kwani kadi ni mali ya nani?mbona mnaichukulia kadi ya Slaa kama ni inshu kuuuuuuubwa!
A very good question. Nilikuwepo siku mzee Paulo Ndobo anajiunga tena na CCM kutoka NCCR. Alipewa kadi ya CCM na mwenyekiti Mkapa, akaeleza wazi kuwa ataendelea kuitunza kadi yake ya NCCR kama kumbukumbu ya kuwahi kuwa mwanachama huko na ni mali yake, akaendelea kusema kuwa hata kadi ya TANU bado anayo hadi leo. Hakuna asiyejua kuwa Dr Slaa amewahi kuwa mwanachama wa CCM. kuwa kwake na kadi sijui kwa nini iwe issue ya kujadiliwa humu. Nape analo jukumu la kututoa kwenye mambo muhimu. Tutakuwa wajinga tukinasa kwenye mtego wake.
 
Kikwete hawezi kufanya mdahalo na Dr Slaa, sio saizi yake Dr Slaa, anatakiwa afanye mdahalo na kina Mrema, Dovutwa.

Hata membe anafahamu na alikili kwa kusema hatutaki tena raisi ambaye hawezi kujieleza akimlenga kikwete jk ni domo zege hadi aandikiwe na makamba sasa ndio maana alikimbia mdahalo na dr slaa
 
Nami nina kadi ya CCM ambayo niliinunua kwa kulazimishwa enzi zile za chama kimoja. Hiyo kadi ni mali yangu kwa vile niliuziwa, japokuwa siyo mwanachama wa CCM. Nimeiweka kama "MEMORABILIA" kuonesha watoto na wajukuu KADI ya CHAMA KANDAMIZI na CHAMA cha MAFISADI Tanzania.

Hapo umenena.
Kama kuwa na kadi ni uanachama basi makamu mkiti wa ccm karume naye si mwanaccm bali mwana ASP. Nape angeanza na Karume kwanza ambaye anajiita mwanaccm huku ana kadi ya ASP kabla ya Dr Slaa mwanachadema ambaye anadaiwa kuwa na kadi mfu ya ccm.
 
Magwangala.........issue is why Dr. Slaa is not walking the talk.....................Is he not drinking wine telling everybody else to drink muddy water?


Rutashubanyuma, naomba majibu yangu yale uwaquote Dr Slaa, ZItto , Nape na some other verified users ambao ni watu wa maamuzi, sorry sijui unafanyaje kutag mtu
 
mi navyoona tu some extent dr.slaa anaweza akawa na huruma na CCM kama sio spy na hii ndiyo sababu uu naomba kila siku uchaguzi ujao dr.slaa asigombee kiti cha urais sababu gani unakumbuka uchaguzi uliopita cdm ilishinda kiti cha urais
lakini cha ajabu ni kwamba ccm wakatuibia kula lakini jambo la kushangaza ni kwamba badala ya slaa kuwaamuru watu waingie mitaani wasikubali yeye kataka kujifanya mcha mungu sana eti msimwage damu!

sasa atakayemwaga damu nani?wananchi au polisi na ule uchaguzi dunia nzima unauangalia ukiua watu 20 tu kesi hiyo The Hague,vikwazo vya kiuchumi,vikwazo vya kusafiri na kutaifishiwa mali uswisi sasa hakuja kuwa na sababu ya kuwazuia watu waliokuwa tayari kuingia mitaani wasiingie!!

labda unaweza ukawa na mashaka na ninachoongea!!unakumbuka mwaka 95' mrema?naye alishinda uchaguzi ule lakini akawaruhusu kwa makusudi ccm kuiba kura zake halafu yeye akatulia tuli akiwaambia watu wasifanye fujo wakati wanaona wanaibiwa waziwazi!!kuja kugundulika baadae ni spy wa ccm aliyepandikizwa kuja kuua upinzani na kweli kazi aliiweza, kwani alikuwa anaogopa akiwaambia watu waandamane atakiua chama kile kile alichotumwa kuja kukijenga-ccm,

sasa haya mambo ya slaa inawezekana akawa kama mrema mana ni sababu ipi iliyomfanya akawaambia watu wasiandamane wakati anajua kabisa alishinda uchaguzi na wasimamizi wote wa nje walishasem yeye alishinda na walishautangaza duniani uchaguzi kuwa haukuwa wa haki na usawa angewaacha watu wapiganie haki yao na kama ccm ingewapiga risasi basi ICC ingekuwa inawaita wao hadi wakuu wote wa polisi na jeshi na hii nchi wasingeweza kuitawala mana misaada yote ingezuiwa,

na hii nchi inategemea misaada,hivyo wangeshindwa tu na ICC ingetaifisha mali zao za nje ya nchi ikiwemo uswis,ndio maana nasisitiza tena ni afadhali hata mtu mwingine akagombea urais cdm ila mtu huyo asiwe Zitto mana naye ni kibaraka tu wa magamba.nawasilisha.
 
Rutashubanyuma,

Soma Katiba ya CCM toleo la mwaka 2010. Ibara ya 13. kufungu (1). Inahusu WANACHAMA NA VIONGOZI.

Uanachama utakwisha kwa:

(a) Kufariki.
(b) Kujiuzulu mwenyewe.
(c) Kuachishwa kwa mujibu wa Katiba.
(d) Kufukuzwa kwa mujibu wa Katiba.
(e) Kutotimiza masharti ya uanachama.
(f) Kujiunga na Chama kingine chochote cha siasa.
(2) Mwanachama ambaye uanachama wake unakwisha kwa sababu yoyote ile hatarudishiwa kiingilio alichokitoa, ada aliyotoa wala michango yoyote aliyoitoa.

Dr Slaa alijiunga na chama kingine cha siasa zaidi ya miaka 15 iliyopita (Nape alikuwa hajamaliza hata darasa la saba), amekuwa mbunge - wa kuchaguliwa- kupitia chama kingine cha siasa (CHADEMA) wa miongo kadhaa. Leo hii Nape & co wanauliza kadi yake ya CCM?


1. Nape na wenzake wanaijua vema katiba ya CCM? wanaelewa masharti ya uanachama?

2. Ni kifungu gani cha katiba ya CCM kinachosema kuwa ili uanachama wa CCM ukome sharti mhusika arudishe kadi?

3. Kwa zaidi ya 15 ambaye Dr Slaa amekuwa mwanachama wa chama kingine cha siasa, CCM walikuwa wapi? Why now?

You don't need to think very hard kujua kuwa CCM wanamhofia Dr Slaa. Wanajua anakubalika kwa wananchi na sasa wanachofanya ni kujaribua kumshambulia yeye (Dr Slaa) binafsi.

CCM wanafanya kosa sana kujikita kwenye hizi siasa za maji taka. Wanatakiwa wawaambie wananchi kwa nini elimu imeshuka, kwanini watu hawana maji, kwanini umeme bado ni kitendawili, kwanini hakuna dawa hospitalini, kwanini deni la taifa linaongezeka huku umaskini unamaliza watanzania? Wanatakiwa waeleze utekelezaji wa Ilani yao ya uchaguzi. Ilani yao inasema nini, na wamefanya nini?

Kuendelea kuimba Dr Slaa kila siku ni kielelezo tosha cha kufilisika hoja. Watu wamekosa majibu kwa maswali ya msingi na sasa wanakwepa kwa kuleta siasa za maji taka. Ni madharau kwa wapiga kura.

 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom