Hataki niishi nyumba isiyo na umeme

Hataki niishi nyumba isiyo na umeme

Una maisha ya ajabu sijawahi ona duniani, kwahyo kazi unayofanya ela yake unafanyia nini?! Ina maana nyumba yako wewe inavyoonekana ina kitanda tu. Sababu unaishi kama kindege, sasa m'mke gani anapenda maisha hayo ya tunduni! Unapokuwa na mtu kubali mabadiliko usiwe kama mzee kuwa itikadi zako hazibadiliki kama mganga wa kienyeji bhna! Wew hama anza kuishi kama kijana kama Tv huna ndio ununue sasa mtoto akija anakusubiri huku akitazama series. Sasa wew una chaji ya simu tu ndani kwahyo akifika awe bize kuchart, utayaweza hayo?!!! Shauri yakooooo
 
Kwa mlio na kumbukumbu, j'5 kama sikosei nilileta ka- thread ambako niliwaomba ushauri kuhusu bi dada flani hivi anaekuja(ga) kuweka pesa kazini kwangu..

Sasa basi leo nikiwa natoka church, mara ikaingia text "B uko wapi?" nikamjibu ndo nafka hom nikitoea ibaadani.. sasa basi kulingana na mimi kuwa busy juma zima siku ambayo nakuwa nje na kazi ni siku ya leo ambayo nakuwa nimepumzika kwa ajiri ya sabato..

Basi buana, kama nilivyokuwa nimemuomba no. zake akanipa, na kumtaka kuwa naye kimahusiano(bado hajanijibu chochote), jana nilimuomba leo aje tupige story za kawaida tu maana nitakuwa na mda.. mtoto kaja mpaka maghetto.


tumepiga story kama dk 15 hv akaanzisha mada amabayo imenichanganya mpaka hivi sasa.. yeye anadai nihamie nyumba ya umeme wakati mimi kwa upande wangu hua nipo busy wakati wote yaani hua natoka asubuhi saa1 na kurudi usiku saa6, so nikifka ghetto ni kuoga na kulala hadi asubuhi yake tena, kwa iyo nikihamia chumba cha umeme nitakuwa nalipa bill ya umeme 4nothing.

Sasa basi wadau naombeni mnishauri, bi dada wa watu bado hajatoa jibu la moja kwa moja kama amenikubalai ombi lang la kuwa nae, ila anadai hawezi kuwa na mtu ambaye naishi nyumba isiyo na umeme eti kwa kigezo cha kama akiwa anakuja kunisabahi atakuwa akiboeka kukaa sehemu ilio kimya maana hata ka- music ana ka TV hakatakuwa kakim'burudisha.

Swali langu ni je, nihamie nyumba ya umeme ili nimfurahishe mchumba, ama nisihamie kitu ambacho kitamuudhi shemela/wifi yenu nifanye nini!!? Ushauri tafadhari..

Sent using Jamii Forums mobile app
Jini ilo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbali na kumfurahisha yoyote.
Umeme ni muhimu kama unaweza ku afford.
Usiishi kwako kama ndege anayeishi kwenye kiota ni kulala na kukimbia.
Hushindwi kuwa hauna hata jiko wewe, kisa hauna muda wa kupika.

The Hate U Give, Little Infants F's Everyone.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una maisha ya ajabu sijawahi ona duniani, kwahyo kazi unayofanya ela yake unafanyia nini?! Ina maana nyumba yako wewe inavyoonekana ina kitanda tu. Sababu unaishi kama kindege, sasa m'mke gani anapenda maisha hayo ya tunduni! Unapokuwa na mtu kubali mabadiliko usiwe kama mzee kuwa itikadi zako hazibadiliki kama mganga wa kienyeji bhna! Wew hama anza kuishi kama kijana kama Tv huna ndio ununue sasa mtoto akija anakusubiri huku akitazama series. Sasa wew una chaji ya simu tu ndani kwahyo akifika awe bize kuchart, utayaweza hayo?!!! Shauri yakooooo
umeniamulia!![emoji85][emoji85][emoji85][emoji85]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ukweli haupingiki, hapo ndipo wabongo tunafail.. yaan watu mnapenda maisha ya ku- act sana!!

Sent using Jamii Forums mobile app

Unafeli wewe unayeshindwa kujiongeza, kuna standard za maisha ambazo inabidi ujitahidi upige hatua utoke, sasa wewe unaona kukaa kwenye nyumba isiyo ya umeme ni sawa na umeridhika, mtu wa aina gani wewe
 
Kati ya vitu ambavyo kwangu ni priority ni nyumba. Napenda kukaa kwenye nyumba nzuri na ambayo nakuwa huru kufanya mambo yangu. Umeme ni necessity na sio luxury mkuu.



Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom