Elimu ya kitaa: Je, unajua kwanini wapangaji wengi hawapendi kuishi nyumba moja na mmiliki?

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
2,042
2,000
Maisha ni safari, nimetoka mbali, leo nmekumbuka maisha nliyopitia ya kuishi vyumba vya kupanga.

Kiukweli ni ndoto ya kila kijana kuanza kuishi maisha ya getoni iwe single room ama self-contained kabla hajajenga au kununua nyumba yake.

Nikiwa kama mtu nliewahi kupitia maisha hayo, nlikumbana pia na changamoto zake katika ishu za kuwekea kipaumbele kuishi sehemu isiyo na mmiliki

Basi nitatumia teknolojia hii ya intaneti kuwamegea japo ka elimu kidogo kupitia humu JamiiForums.

Kwanza niweke wazi Wapangaji wengine ni wastaarabu ila Kuna wengine ni vichomi ndo wanaopelekea mtu akitaka chumba lazima aulizie kama mwenye nyumba anakaa hapohapo ili hio nyumba aikwepe.

Sababu ni hizi:

Kukosa amani ukichelewesha kodi. Yani mtu anaekudai kodi anakukosesha raha maana mpo nyumba moja, Anaweza kukudai Kodi ukasema hauna , kimbembe kipo ukipika nyama atakuja mlangoni kukukaripia hela ya kumlipa huna ila unakula nyama, sasa anataka ulale njaa? Pia kwa wale wa viti virefu mkikutana huko bar anaweza kukukata hilo jicho ukaishiwa amani acha tu, sasa anatake usistarehe?

Wivu - Wengine watoto wao unakuta wamenaliza vyuo ila hawana kazi na wewe una kazi basi huwa kuna wivu, ukitwanga kitunguu swaum tu ndani anakufuata na maneno hodi hodi kwanini unatoboa ukuta wangu unajua bei ya siment wewe.

Wengi huwa na funguo spea, hali hii huwa inawapa wasiwasi na woga wapangaji huenda mwenye nyumba huwa anapiga chabo wakiwa hawapo.

Usumbufu wa bili za maji na umeme, Michango itayokusanywa kwa wapangaji mara nyingi ni kwa ajili ya matumizi yake, bili zikitoka hawaonyeshi mnaambiwa tu ni kiasi kazaa, ukiuliza utackia kama umechokaa hama.

Kubanwa Uhuru, Vijana wanaondoka nyumbani na kwenda kupanga ili kuwa huru lakini anapoenda kumkuta tena mwenye nyumba inakuwa kama bado anaishi nyumbani, masharti kibao Mara usichelewe kurudi, Usiingize mwanamke, Kupeleleza kila unachoingiza room, n.k. jamani hivi vitu ni serious msidhani ni story.
 
Roadmap

JF-Expert Member
Aug 19, 2013
2,461
2,000
Unoko unavusha pisi tatu ndani ya siku moja, Maza house anaanza kuchonga unafanya house party anaanza kununa.
 
SN.BARRY

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
3,925
2,000
Wapangaji jengeni ili mpunguze kujishtukia.

Pia kuepuka matatizo na mwenye nyumba hakikisha unapohamia mnasaini mkataba serious hadi kwa Mwenyekiti wa mtaa tena apige mhuri kabisa.
 
SN.BARRY

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
3,925
2,000
Hakuna mwenye nyumba atakubali hayo yote wakati nyumba ya kwake, Unataka kumtawala.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Kwa hiyo ndugu yangu unaweza kulipa kodi ya miezi 6 au mwaka mmoja bila mkataba wa kueleweka?

Yaani kodi laki na nusu kwa mwezi utoe laki tisa ya miezi 6 bila mkataba na mhuri juu? Kwa mwenyekiti wa mtaamhuri ni elfu 5 tu.
 
bievinii

JF-Expert Member
May 12, 2021
490
500
Mwenye nyumba Ni lazima awe mtata ili kukupa motisha ya kujenga yako
Akiwa anakudekesha anajua wazi kuwa utajisahau kujenga yako

Hata Mimi nikipata nyumba ya kupangisha nitakuwa mtata hivyo
 
sengobad

JF-Expert Member
Aug 13, 2017
4,572
2,000
Mwenye nyumba Ni lazima awe mtata ili kukupa motisha ya kujenga yako
Akiwa anakudekesha anajua wazi kuwa utajisahau kujenga yako

Hata Mimi nikipata nyumba ya kupangisha nitakuwa mtata hivyo
Ni njaa tu wala hakuna cha motisha, unadhani hivyo vituko vinatokea kwa wenye nyumba walio na vipato vyao vizuri. Mara nyingi ni wazee, mama wa nyumbani hasa wale wapika vitumbua.
 
TASK FORCE

JF-Expert Member
Apr 7, 2017
2,479
2,000
Maisha ni safari, nimetoka mbali, leo nmekumbuka maisha nliyopitia ya kuishi vyumba vya kupanga.

Kiukweli ni ndoto ya kila kijana kuanza kuishi maisha ya getoni iwe single room ama self-contained kabla hajajenga au kununua nyumba yake.

Nikiwa kama mtu nliewahi kupitia maisha hayo, nlikumbana pia na changamoto zake katika ishu za kuwekea kipaumbele kuishi sehemu isiyo na mmiliki

Basi nitatumia teknolojia hii ya intaneti kuwamegea japo ka elimu kidogo kupitia humu JamiiForums.

Kwanza niweke wazi Wapangaji wengine ni wastaarabu ila Kuna wengine ni vichomi ndo wanaopelekea mtu akitaka chumba lazima aulizie kama mwenye nyumba anakaa hapohapo ili hio nyumba aikwepe.

Sababu ni hizi:

Kukosa amani ukichelewesha kodi. Yani mtu anaekudai kodi anakukosesha raha maana mpo nyumba moja, Anaweza kukudai Kodi ukasema hauna , kimbembe kipo ukipika nyama atakuja mlangoni kukukaripia hela ya kumlipa huna ila unakula nyama, sasa anataka ulale njaa? Pia kwa wale wa viti virefu mkikutana huko bar anaweza kukukata hilo jicho ukaishiwa amani acha tu, sasa anatake usistarehe?

Wivu - Wengine watoto wao unakuta wamenaliza vyuo ila hawana kazi na wewe una kazi basi huwa kuna wivu, ukitwanga kitunguu swaum tu ndani anakufuata na maneno hodi hodi kwanini unatoboa ukuta wangu unajua bei ya siment wewe.

Wengi huwa na funguo spea, hali hii huwa inawapa wasiwasi na woga wapangaji huenda mwenye nyumba huwa anapiga chabo wakiwa hawapo.

Usumbufu wa bili za maji na umeme, Michango itayokusanywa kwa wapangaji mara nyingi ni kwa ajili ya matumizi yake, bili zikitoka hawaonyeshi mnaambiwa tu ni kiasi kazaa, ukiuliza utackia kama umechokaa hama.

Kubanwa Uhuru, Vijana wanaondoka nyumbani na kwenda kupanga ili kuwa huru lakini anapoenda kumkuta tena mwenye nyumba inakuwa kama bado anaishi nyumbani, masharti kibao Mara usichelewe kurudi, Usiingize mwanamke, Kupeleleza kila unachoingiza room, n.k. jamani hivi vitu ni serious msidhani ni story.
Yote ayo ili waone uchungu siku wajenge nyumba zao,
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom