Hataki kuchukua mahari yake nifanyeje??

Hataki kuchukua mahari yake nifanyeje??

Status
Not open for further replies.
Habari wanajf na heri ya pasaka.

Niende kwenye lengo la uzi...mimi ni mama wa mtoto mmoja wa miezi 7 nina miaka 26. Miezi 3 iliyopita nilitengena na mzazi mwenzangu ambaye alishanitolea mahari na kunivalisha pete ya uchumba kwa sasa nipo nyumbani na mtoto wangu.

Mwanzoni nilipata wakati mgumu sana kukubali kwamba tumetengana lakini namshukuru Mungu sasa hivi nimekubaliana na hali na nipo vizuri kabisa.

Baba mtoto wangu alikataa kabisa kuchukua mahari yao na pia kuwashirikisha wazazi juu ya kutengana kwetu kwa madai tulikutana wawili tuu wakati pete tulivalishana mbele ya wazazi na ndugu wa pande zote.

Swali langu ni je naweza kuingia kwenye mahusiano mapya wakati yeye hajachukua mahari yake? Na je kwa mfano mtu akataka kuja kutoa mahari inakuwaje kuhusu mahari yao ya mwanzo haitakuwa na shida yoyote maana hataki kuchukua kabisa na watu wanasema kubaki na mahari yake itanifunga sababu kimila bado nitakuwa mke wake.

Ninachohofu mbeleni asije leta shida akasema ni mchumba wake halali sababu temetengana kienyeji sana. Naombeni msaada wa mawazo juu ya hili.

Asanteni kwa mchango wenu.
Duh...yaani jamaa kaona msambwanda wote huo anaupotezea....hatari sana
 
Hukuyasema ndiyo umeyasema sasa. Unaonekana umechoka pole, bila shaka hawa wanaJF wamekuchosha usiku kucha.

Ok kwa hiyo vikubwa vilivyokupeleka nyumbani ni.

1. Huduma mbovu na kutojaliwa ukweni.
2. Unataka utaratibu mpya wa ndoa.

Lakini, ulishayazungumza na mwenza wako kuhusu haya mambo kwa undani? Naposema kuzungumza sio kule kulalamika.

Hapana ni kutafuta sehemu tulivu ukamtajia moja baada ya jingine kisha mkaja kwenye suluhu. Hili ulipaswa ulifanye kabla ya kurudi kwenu lakini unaweza kulifanya pia.

Usiniambie ulishajibu hili kule juu, nijibu.

Yeye anasemaje kuhusu situation nzima? Msimamo wake.
Ubarikiwe nasubiri majibu 👏
 
Ohoo...
Nishasema jeuri huyu... Na mchaga jeuri za kifamba ka hizi hawezi vumilia.

Hawa watu wa Njombe huwa wanaona wao kwa wao tu... Wana mambo yao flani hivi kama si kabila lao huezi waelewa.
U
Mchaga na Mbena its the hellest combination I have ever seen. Basi tu kwa vile wana mtoto ila ingekuwa bora waachane tu.
Mkuu uliyo andika ni ukweli mtupu wachaga wanawezana wenyewe hawa viumbe ili uishi nae inahitaji akili ya ziada ni wabishi kuchukua ushauri hata kama ni mzuri.
 
Tulia kwanza kabla ya kufanya maamuzi kwa hasira. Una mtoto wa miezi 3 tafsiri yake ni kwamba mmepishana na huyo mzazi mwenzio wakati wa ujauzito jambo ambalo hata huko unakotaka kukimbilia ukidhani utapata faraja huenda yakakupata kama hayo.

Waweza kuolewa na mwanaume mwingine ila mbeleni huko si ajabu mkaja kuelewana na mzazi mwenzio mkaendeleza mahusiano wakati huo ulishaolewa kwingine, yanatokea na tunayaona
 
Hukuyasema ndiyo umeyasema sasa. Unaonekana umechoka pole, bila shaka hawa wanaJF wamekuchosha usiku kucha.

Ok kwa hiyo vikubwa vilivyokupeleka nyumbani ni.

1. Huduma mbovu na kutojaliwa ukweni.
2. Unataka utaratibu mpya wa ndoa.

Lakini, ulishayazungumza na mwenza wako kuhusu haya mambo kwa undani? Naposema kuzungumza sio kule kulalamika.

Hapana ni kutafuta sehemu tulivu ukamtajia moja baada ya jingine kisha mkaja kwenye suluhu. Hili ulipaswa ulifanye kabla ya kurudi kwenu lakini unaweza kulifanya pia.

Usiniambie ulishajibu hili kule juu, nijibu.

Yeye anasemaje kuhusu situation nzima? Msimamo wake.
Nilishazungumza na mwenzangu kuhusu hili lakini hakuna cha maana anachojibu au kuchukua hatua.
Msimamo wake ni kwamba nimeenda nyumbani basi ni moja kwa moja nimejaribu sana kusuluhisha kwa miezi 2 lakini alikataa mpaka baadae nikakubaliana na matokeo kwamba its over. Nilishamuuliza kama kuna sababu nyingine au ni hii ya kurudi nyumbani tuu anasema hakuna.
 
Yes endelea na maisha... weka mawazo yako kwa mtoto saiv... Fanya mpango ukutane na ndugu wa pande zote mbili i mean kwa mfano wajomba zake na wako au babu zenu.. mahari hua hairudishwi ila ni mambo yanaongelewa tuu then kila mtu anafuta swala lake....
 
Mkuu uliyo andika ni ukweli mtupu wachaga wanawezana wenyewe hawa viumbe ili uishi nae inahitaji akili ya ziada ni wabishi kuchukua ushauri hata kama ni mzuri.
Sasa ndo kakutana na mbena... Mbena ni hatari zaidi. Sioni ndoa hapa.
 
Hapo kuna mambo kadhaa yanaleta mkanganyiko. lakini naweza ng'amua yafuatayo

1. Kama jamaa hakupendi na hakutaki angeichukua hiyo mahari.
wewe ni Mkristo au muislam??.
Kama ni Mkristo mahari si walipewa wazazi wako. Wewe huna jukumu lolote la kuirudisha mahari bali wazazi ndio wahusika. Au umeshaongea nao??.

2. Mtoto anamiezi saba unawaza habari za kuchumbiwa upya kwa kutolewa mahari. Ndio maana unahofia huko mbeleni mshikaji asije kukuharibia mpango mzima. Kama wewe si mwenye tatizo mbona unaulizia habari za kurudisha mahari mapema yote hii kama mtu anayejihami.

3. Inaonekana alikupa mimba kwa starehe tuu. Aidha hukumpenda au hakukupenda. Yaani ilikuwa ni bahati mbaya. Na ndipo akalazimika kutoa pesa ya kukuchafua na mahari juu ili kuua Soo. Kama ni hivyo hapa unapaswa uwe makini zaidi kwani ukicheza unaweza shangaa ukapewa mimba ya pili mpaka ya tatu na wanaume tofauti tofuati kama Mbwa.

4. Kama wote ni Wakristo na mnafanana kitabaka na kihadhi yaani elimu na hali ya uchumi. Sidhani kama hili ni jambo kubwa la kutengana. Lakini kama hamfanani na mlikutana kukidhi haja ya mwili basi kuna ugumu kidogo.

Ushauri; Kuolewa ukiwa single Mama kuna athari kubwa sana. Usijidanganye wala asikudanganye mtu. Kama hutanyanyasika wewe basi mtoto atanyanyasika. Mimi nimeishi maisha hayo. Naelewa ninachokisema. Kama hakuna ulazima wa kuachana Fight huyo mshikaji awe mumeo.

Sababu ya kuachana hakuna. Kumbuka sababu kubwa ya kutengana ni Kufumaniwa, Au mwanaume/mwanamke kupatwa na matatizo makubwa ya kiakili.

Pia huna ushahidi kuwa jamaa kakuacha. Hivyo hapa unatafuta ruhusa ya kuharibu future yako au ya mtoto.
Ushauri mzuri sana...sasa ni bora akasoma hii post tena na tena.
 
Nilishazungumza na mwenzangu kuhusu hili lakini hakuna cha maana anachojibu au kuchukua hatua.
Msimamo wake ni kwamba nimeenda nyumbani basi ni moja kwa moja nimejaribu sana kusuluhisha kwa miezi 2 lakini alikataa mpaka baadae nikakubaliana na matokeo kwamba its over. Nilishamuuliza kama kuna sababu nyingine au ni hii ya kurudi nyumbani tuu anasema hakuna.
Naye ni mtoto....ila kama mwanaume anasababu zake za kukasirika. Wanaume tunapenda kuonekana kwenye jamii kila jambo lipo undercontrol yetu na tunapenda ieleweke hivyo. Inapotokea tofauti na hapo tunaona tumedhalilika.

Ndiyo maana amekuambia hataki ushirikishe wazazi. Alitaka pande mbili zielewe hajakushindwa na hakushindwa kukuhudumia.

Kikubwa shirikisha wazazi wa pande zote mbili wakati mnayajadili onyesha unataka mambo yaishe mjenge future ya mtoto wenu. Kauli/kiimbo kwenye kumaliza tofauti ni suala la msingi saana.

Pia usiendelee kuvutana naye kwenye suala la mahari jikalie kimya. Fikiria maisha uliyo nayo mbele ni marefu kuliko uliyohangaika. Mpo kwenye kipindi cha mpito hata mgogoro wenu sio mkubwa...ukitajiwa migogoro ambayo watu wamekutana nayo na ikaisha utajishangaa na kushukuru haraka.
 
Nilishazungumza na mwenzangu kuhusu hili lakini hakuna cha maana anachojibu au kuchukua hatua.
Msimamo wake ni kwamba nimeenda nyumbani basi ni moja kwa moja nimejaribu sana kusuluhisha kwa miezi 2 lakini alikataa mpaka baadae nikakubaliana na matokeo kwamba its over. Nilishamuuliza kama kuna sababu nyingine au ni hii ya kurudi nyumbani tuu anasema hakuna.
Hatuwezi kuendeleza mjadala huu wa upande mmoja ...

muite jamaa hapa nae aseme.. Hata mahakamani kuna mshtaki na mshtakiwa.
 
Nina kauzoefu kadogo kutokana na yalomkuta rafiki yangu. Situation kama yako.
Ila, kimila, mwanamke akishatolewa mahari yule tayari ni mke. Na kwa hakika yaweza zuia mwanamke asiolewe.

Waweza pata mwanaume mwingine na yule wa mwanzo akaja kukuharibia kwa kusema kuwa wewe ni wake na alishakutolea mahari.

Nini kifanyike?

Talaka itolewe.
Ndo kithibitisho pekee kuwa nyie hamko pamoja
 
Sasa ndo kakutana na mbena... Mbena ni hatari zaidi. Sioni ndoa hapa.
Mwanamke ukiwa na mwanaume mchanga ukubali tu kujishusha hawa viumbe wa kabila hili akishikilia jambo hata umuelimishe ubishi ni asili kwako(joke wachaga watani zangu sitaki povu) 😀😀😀
 
Naye ni mtoto....ila kama mwanaume anasababu zake za kukasirika. Wanaume tunapenda kuonekana kwenye jamii kila jambo lipo undercontrol yetu na tunapenda ieleweke hivyo. Inapotokea tofauti na hapo tunaona tumedhalilika.

Ndiyo maana amekuambia hataki ushirikishe wazazi. Alitaka pande mbili zielewe hajakushindwa na hakushindwa kukuhudumia.

Kikubwa shirikisha wazazi wa pande zote mbili wakati mnayajadili onyesha unataka mambo yaishe mjenge future ya mtoto wenu. Kauli/kiimbo kwenye kumaliza tofauti ni suala la msingi saana.

Pia usiendelee kuvutana naye kwenye suala la mahari jikalie kimya. Fikiria maisha uliyo nayo mbele ni marefu kuliko uliyohangaika.
Asante sana kwa ushauri lakini swala la kushirikisha wazazi hataki anasema tumeachana wawili sababu tulikutana wawili wazazi hawakuwepo.
 
Kikubwa shirikisha wazazi wa pande zote mbili wakati mnayajadili onyesha unataka mambo yaishe mjenge future ya mtoto wenu. Kauli/kiimbo kwenye kumaliza tofauti ni suala la msingi saana.
Aje kujibu paragraph hii... Je! Yuko tayari kusuluhisha positively yaishe kwa faida yake na mwanae.
!???
 
Nina kauzoefu kadogo kutokana na yalomkuta rafiki yangu. Situation kama yako.
Ila, kimila, mwanamke akishatolewa mahari yule tayari ni mke. Na kwa hakika yaweza zuia mwanamke asiolewe.

Waweza pata mwanaume mwingine na yule wa mwanzo akaja kukuharibia kwa kusema kuwa wewe ni wake na alishakutolea mahari.

Nini kifanyike?

Talaka itolewe.
Ndo kithibitisho pekee kuwa nyie hamko pamoja
Ndio nilikuwa nahitaji ushauri kama huu je kubaki na mahari yake kuna impact gani lakini watu wamechukulia personal sana. Asante sana kwa ushauri
 
Matatizo ya watanzania hawasomi wakaelewa kabisa. Wapi nimesema nimeingia au ninaingia kwenye mahusiano mapya?? swali lilikuwa je kubaki na mahari yake haina shida kama kutakuwa na mtu atataka kutoa mahari kwa baadae? Sikuchepuka wala sina hiyo tabia aliniacha kwa sababu hakutaka nirudi kwetu baada ya kujifungua.
Nilikuwa nasoma comment kimya kimya ila nilipofika hapa wacha nikuulize swali moja kabla ya kukupa ushauri.

Sasa alipokataa (usirudi) kwenu baada ya kujifunga wewe ulifanyaje? Ulienda kibambe au?

Halafu hili neno usirudi Kama sijalielewa vizuri.
 
Asante sana kwa ushauri lakini swala la kushirikisha wazazi hataki anasema tumeachana wawili sababu tulikutana wawili wazazi hawakuwepo.
Hapana. Jiulize kwanini ulipotoka kwake ulienda kwa wazazi wako? Au kwanini ulipokuwa kwake ulihudumiwa na mzazi wake?

Wao wamewakuza, wakawahudumia mkafika hapo mlipo. Wanawajua zaidi mjijuavyo...wataliweka sawa.

Anafichia madhaifu yake hapo. Wazazi waambiwe na walijue.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom