Hataki kuchukua mahari yake nifanyeje??

Status
Not open for further replies.
Aje kujibu paragraph hii... Je! Yuko tayari kusuluhisha positively yaishe kwa faida yake na mwanae.
!???
Kaka sijajua una shida gani lakini mimi binafsi nimeshasuluhisha sana na kumwambia kwa ajili ya mtoto wetu ila amekataa anasema amemalizana na mimi. Niliposema hadi wazazi wanasema najibembeleza kwa mtu hanipendi ni kwa sababu kila siku nilikuwa namtafuta kusuluhisha ila ananiambia watu wameoana wakaacha sembuse sisi mahari tuu wazazi wakaona ni dharau ananifanyia. Imefika kipindi nikasema basi sasa imetosha. Ni mwezi sasa umepita toka nimeamua kukubali matokeo na kutulia kulea mtoto wangu bila yeye. Kama umesoma kuna sehemu nilisema ilinipa wakati mgumu ndio huo kusuluhisha na hataki wazazi au ndugu waingilie hili swala ansema tulitongozana wawili hayawahusu.
 
Nilikuwa nasoma comment kimya kimya ila nilipofika hapa wacha nikuulize swali moja kabla ya kukupa ushauri.

Sasa alipokataa (usirudi) kwenu baada ya kujifunga wewe ulifanyaje? Ulienda kibambe au?

Halafu hili neno usirudi Kama sijalielewa vizuri.
Mwanzoni alinikubalia nirudi lakini akaja kukataa baadae wakati nimeshakata na tiketi za ndege kabisa kutoka Mwanza -Mbeya...sababu kubwa ni ghafla mama mkwe akataka anipeleke Moshi baada ya kujua naenda nyumbani na kwa kipindi hicho haikuwezekana kwenda so nikarudi nyumbani. Anaposema urudi moja kwa moja maana yake tumeachana nibaki nyumbani misirudi kwake
 
Kaka sijajua una shida gani lakini mimi binafsi nimeshasuluhisha sana na kumwambia kwa ajili ya mtoto wetu ila amekataa anasema amemalizana na mimi. Niliposema hadi wazazi wanasema najibembeleza kwa mtu hanipendi ni kwa sababu kila siku nilikuwa namtafuta kusuluhisha ila ananiambia watu wameoana wakaacha sembuse sisi mahari tuu wazazi wakaona ni dharau ananifanyia. Imefika kipindi nikasema basi sasa imetosha. Ni mwezi sasa umepita toka nimeamua kukubali matokeo na kutulia kulea mtoto wangu bila yeye. Kama umesoma kuna sehemu nilisema ilinipa wakati mgumu ndio huo kusuluhisha na hataki wazazi au ndugu waingilie hili swala ansema tulitongozana wawili hayawahusu.
Pole best nimeumia kwa jibu hilo dah kama yupo humu niseme ana kauli chafu zaidi ya kinyesi.
 
Kama huamini basi kaka na siwezi kukulazimisha zaidi.
Kwa Sasa mpenzi tulia lea mwanao hakuna kitu kibaya kama mwanamke anaye lea mtoto awe na mawazo ndugu yangu utakonda hadi Dunia ikushangae usijaze vitu vingi kichwani unapo kuwa na mawazo mtoto afya yake ina kuwa dhaifu.
 
Sababu ni ile ile ya kurudi nyumbani. Asante sana nimeshapoa na tumekubaliana tutalea tuu mtoto pamoja. Najua hatutaweza kuwa pamoja tena sababu yeye anasema siku niliyoondoka ndio nae alivunja mahusiano moja kwa moja .
Wewe hutaweza dumu kwenye maisha ya ndoa km kweli sababu Ni hii tu ila km Kuna sababu nyingine ila hiyo ndo umeamua kuitaja sawa unawez kudumu na ndoa...

Vitu viwili visikudanganye kimoja Ni bado unalipa kwamba utapata mwanaume wakukupenda na mtoto wako na ndoa isiwe na changamoto sababu ya huyo mtoto,Cha pili eti ndoa ijayo haitakuwa na misukosuko.
 
Mkuu sio kutoa lawama kwa huyo dada niseme na huyo mwanaume nae alikuwa anatafuta sababu kama chanzo ni hicho cha kutengana ni cha kipumbavu kabisa ukizingatia Wana mtoto hawezi maisha ya ndoa hata huyo Mwanaume pia ndio maana ana kataa suruhu kwa pande mbili.
 
Mtoto wa miezi saba halafu unawaza Kuwa na mahusiano tena? Hujakauka bado Wewe. Unatafuta mahusiano ili iweje? Kuanza kuwaza mahusiano mapya ni dalili tosha Kuwa Wewe Ulikuwa unachepuka kitambo tu. Na Huenda huyo mtoto atakuwa wa mwingine. Unawaza kitoto mno. Huyo mwanao Huoni Kama anahitaji care sana toka Kwako badala ya Wewe kuanza kutaka kumpa care jitu zima?
 
Hivi mkuu umeelewa swali hapo wapi nimesema nafikiria dushe la mwanaume mwingine?? Swali langu ni mahari yake anayokataa kuchukua haitakuwa na effect baadae kama nitakuwa na mahusiano au mtu atataka kutoa mahari....Halafu kulea mtoto na dushe hakuna uhusiano maana unaruhusiwa baada ya siku arobaini tuu akishazaliwa
Unaona sawa tu baada ya siku 40? Achana na theory hizo. Unakimbilia nini? Acha kukauke huko Wewe. Mtoto anapaswa kupata malezi bila bughudha
 
Basi nikutakiemaisha maisha mema ya usingle mother.

maana naona hakuna suluhu.

KILA LA KHERI...
Natamani sana ningekupa hata proof moja tuu PM..mkuu inaonekana ulishwahi tendwa na wabena pole sana kwa hilo maana coment zote unaponda sana wabena
 
Mtoto wa miezi saba halafu unawaza Kuwa na mahusiano tena? Hujakauka bado Wewe. Unatafuta mahusiano ili iweje? Kuanza kuwaza mahusiano mapya ni dalili tosha Kuwa Wewe Ulikuwa unachepuka kitambo tu. Na Huenda huyo mtoto atakuwa wa mwingine. Unawaza kitoto mno. Huyo mwanao Huoni Kama anahitaji care sana toka Kwako badala ya Wewe kuanza kutaka kumpa care jitu zima?
Msaada ilikiwa mahari kubaki nayo haitakuwa na madhara kwa baadae sio kwamba nmeanzisha uhusiano tatizo watu huwa hawataki kuelewa mtu anahitaju kushauriwa nn
 
Habari wanajf na heri ya pasaka.

Niende kwenye lengo la uzi...mimi ni mama wa mtoto mmoja wa miezi 7 nina miaka 26. Miezi 3 iliyopita nilitengena na mzazi mwenzangu ambaye alishanitolea mahari na kunivalisha pete ya uchumba kwa sasa nipo nyumbani na mtoto wangu.

Mwanzoni nilipata wakati mgumu sana kukubali kwamba tumetengana lakini namshukuru Mungu sasa hivi nimekubaliana na hali na nipo vizuri kabisa.

Baba mtoto wangu alikataa kabisa kuchukua mahari yao na pia kuwashirikisha wazazi juu ya kutengana kwetu kwa madai tulikutana wawili tuu wakati pete tulivalishana mbele ya wazazi na ndugu wa pande zote.

Swali langu ni je naweza kuingia kwenye mahusiano mapya wakati yeye hajachukua mahari yake? Na je kwa mfano mtu akataka kuja kutoa mahari inakuwaje kuhusu mahari yao ya mwanzo haitakuwa na shida yoyote maana hataki kuchukua kabisa na watu wanasema kubaki na mahari yake itanifunga sababu kimila bado nitakuwa mke wake.

Ninachohofu mbeleni asije leta shida akasema ni mchumba wake halali sababu temetengana kienyeji sana. Naombeni msaada wa mawazo juu ya hili.

Asanteni kwa mchango wenu.
Toa sababu, kwann mpi tengana?

Na ni kweli mlikutana wawili tu hata jf hatukuwepo YAMALIZENI WENYEWE!

inaonekana kunasehemu unaliwa tigo, ndiko unataka uhamie.....!

biblia ilisema tuishi nanyie kwa AKILI.
nampongeza JAMAA kutumia AKILI yake vema, HIYO MAHARI NUNILIA NEPI MTOTO WENU.

.......wee endelea na huko.......
 
Mwanzoni alinikubalia nirudi lakini akaja kukataa baadae wakati nimeshakata na tiketi za ndege kabisa kutoka Mwanza -Mbeya...sababu kubwa ni ghafla mama mkwe akataka anipeleke Moshi baada ya kujua naenda nyumbani na kwa kipindi hicho haikuwezekana kwenda so nikarudi nyumbani. Anaposema urudi moja kwa moja maana yake tumeachana nibaki nyumbani misirudi kwake
Hapa nadhani Kuna mvutano wa Mambo ya kimira kuhusu huyo mtoto. Mama mkwe anataka mjukuu wake akafanyiwe matambiko kwa upande wao na kwenu mnataka kufanya hivyo pia. Huu ndo ukweli ambao hamuuweki wazi ndo maana mnatoleana ubabe.

Ulichotakiwa kufanya ni kumtii mumeo na mama yake. ulipokataa wakaona ni dharau kubwa Sana na wanaume wengi hatupendi dharau iwe kwetu wenyewe au kwa ndugu zetu wa karibu hasa hasa mama zetu.

Soma kwenye biblia kitabu Cha esta yule malikia vashit alitimuliwa kwa kosa dogo Sana la kuitwa na mumewe mfalume akakataa.

Mtu amekulipia mahali ina maaha uko chini yake mpaka kifo huyo ndo baba yako kwa Sasa kwa hiyo kumdharau ni kosa kubwa Sana.

Hata Mimi ningefanya Kama alivyokuwa huyo jamaa yako, wanawake wenye viburi, dharau na kutotii ndo wanaoongoza kuvunja ndoa.

Alikwambia usiende weewe ukabisha na kwenda Sasa angefanyaje?

Kuhusu kutochukua mahali yupo jamaa anafikiria njia nzuri zaidi ya kutumia, hataki aonekane au akosane na ndugu zako kwa Mambo ya kukurupuka na kuwapa usumbufu usio wa lazima.
 
Mimi nina maswali machache.
Swali #1.Huyo baba mtoto wako mlikuwa mnakaa kwao au kwake?
Swali #2. Wazazi wako ni watu wa dini sana au kawaida?
Swali #3. Kwa nini usiendelee na mambo mengine badala ya kuwaza kuhusu mahari?
Swali #4. Unafanya kazi ?
 
Maswali yote uliyo Uliza kajibu pitia comments mkuu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom