Hataki kuchukua mahari yake nifanyeje??

Status
Not open for further replies.
Hapa nadhani Kuna mvutano wa Mambo ya kimira kuhusu huyo mtoto. Mama mkwe anataka mjukuu wake akafanyiwe matambiko kwa upande wao na kwenu mnataka kufanya hivyo pia. Huu ndo ukweli ambao hamuuweki wazi ndo maana mnatoleana ubabe.

Ulichotakiwa kufanya ni kumtii mumeo na mama yake. ulipokataa wakaona ni dharau kubwa Sana na wanaume wengi hatupendi dharau iwe kwetu wenyewe au kwa ndugu zetu wa karibu hasa hasa mama zetu.

Soma kwenye biblia kitabu Cha esta yule malikia vashit alitimuliwa kwa kosa dogo Sana la kuitwa na mumewe mfalume akakataa.

Mtu amekulipia mahali ina maaha uko chini yake mpaka kifo huyo ndo baba yako kwa Sasa kwa hiyo kumdharau ni kosa kubwa Sana.

Hata Mimi ningefanya Kama alivyokuwa huyo jamaa yako, wanawake wenye viburi, dharau na kutotii ndo wanaoongoza kuvunja ndoa.

Alikwambia usiende weewe ukabisha na kwenda Sasa angefanyaje?

Kuhusu kutochukua mahali yupo jamaa anafikiria njia nzuri zaidi ya kutumia, hataki aonekane au akosane na ndugu zako kwa Mambo ya kukurupuka na kuwapa usumbufu usio wa lazima.
Sisi kwetu hatuna mambo ya mila kabisa na hajafanyiwa chochote labda kama wao ndio walitaka kumfanyia huko kwao.
 
Sisi kwetu hatuna mambo ya mila kabisa na hajafanyiwa chochote labda kama wao ndio walitaka kumfanyia huko kwao.
Sawa. Mimi Kama Mimi nimeona utii tu ndo umepungua hapo.vinginevyo mlikuwa hampendani au Kuna sababu nyingine nyuma ya pazia kwako au kwake.

Haya fanya kutulia kwanza Kama miezi mitatu au minne, ukiona roho yako ina amani Waite ndugu zako mrudishe mahali yake.kinyume na hapo we kausha ila akikuomba urudi Rudi fasta na usimbishie tena.
 
Hivi mkuu umeelewa swali hapo wapi nimesema nafikiria dushe la mwanaume mwingine?? Swali langu ni mahari yake anayokataa kuchukua haitakuwa na effect baadae kama nitakuwa na mahusiano au mtu atataka kutoa mahari....Halafu kulea mtoto na dushe hakuna uhusiano maana unaruhusiwa baada ya siku arobaini tuu akishazaliwa
Kufikiria dushe la mwanaume mwingine ni pale uliposema je unaweza kuingia kwny mahusiano mengine. Sa huko si ndio kufikiria dushe!
Kikubwa tulizana kwanza Lea mwanao kwanza bado mdogo utamharibu mtoto bure tu.
tatizo mnaingia kwnye mahusiano ilihali bado mnapenda kuendelea kuish kwenu.
 
They usually say women alsway know their next boyfriend.

Dalili zote za wewe kuchumbiwa na mtu mwingine naziona.
Let's me tell you unachokitafuta na umekaribia kukipata but madhala yake si madogo kwa uhusiano unaokaribia kuuingia .

Rudi kwa mume wako acha kujiingiza kwenye maisha yaa ajabu .mwanamke lazima unyenyekee kwa mume wako hiyo ndio sifa kuu.
 
Natamani sana ningekupa hata proof moja tuu PM..mkuu inaonekana ulishwahi tendwa na wabena pole sana kwa hilo maana coment zote unaponda sana wabena
OhOo PM tena... Hutotoka salama.
Ntakuongezea idadi buree..

😂😂😂😂😂
 
Huyu dada Hana hatia ya moja kwa moja hata haya majibu Ni kwasababu tunampanikisha tu haya mahusiano wazazi ndo wanayaharibu...

Nimesoma vizuri majibu yake nimejifunza amepitia mengi japokuwa hasemi yote ila hapa tatizo Ni wazazi na mumewe kakosa msimamo
 
OhOo PM tena... Hutotoka salama.
Ntakuongezea idadi buree..

wala mimi sina hiyo tabia. Sema watu hawanielewi kuuliza kuhusu mahusiano mapya au mtu kutoa mahari sio kwamba nina mtu au nategemea hapana...Nia yangu ilikuwa kujua madhara ya kubaki na mahari sababu wanasema forever nitabaki kuwa mkewe hata kama hatutakuwa pamoja.
 
nmwenza wangu anamsikiliza sana mama yake hata kitu mkikubaliana wawili anamshirikisha mama akikataa basi na yeye anakubali tuu hadi mambo personal.
Mfano mzuri tulitaka kubadilisha dada wa kwazi sababu alikuwa ana mambo ya wanaume sana asingeweza kulea mtoto tukakubaliana na mwenzangu nikamwomba mama yangu atutafutie akampata kabisa ikabaki kumwagiza aje tunapokaa.Mwenzangu alipomshirikisha mama yake akakataa tusibadilishe nae akakubali kumbuka alishafatutwa mpya.
Je hakufukiria mtoto wake ataishije na dada anayeshinda kwa wanaume pale sisi tutakapoenda kazini? Hajui madhara yake?

Duh bhasi dada yote kwa yote kaeni tu umwambia ukweli huyo mmeo kuwa hupendi hiyo tabia kuwa mvumilivu
Una miaka 25 unaweza kuolewa tena but sikubaliani kuachana na huyo mmeo
Kaeni myamalize usiwe na haraka.
 
Mkuu sio kutoa lawama kwa huyo dada niseme na huyo mwanaume nae alikuwa anatafuta sababu kama chanzo ni hicho cha kutengana ni cha kipumbavu kabisa ukizingatia Wana mtoto hawezi maisha ya ndoa hata huyo Mwanaume pia ndio maana ana kataa suruhu kwa pande mbili.
Kiukweli mi nimekuja kumuelewa huyu dada nilivyosoma comments zake kosa sio lake moja kwa moja nimempata vzr tu
 
Kiukweli mi nimekuja kumuelewa huyu dada nilivyosoma comments zake kosa sio lake moja kwa moja nimempata vzr tu
Hata kama kosa lake mkuu hiyo ni sababu ya kumuacha ukizingatia bado ana mtoto hajui kama mama akiwa hana furaha na mawazo tele mtoto ana kuwa dhaifu.
 
Hata kama kosa lake mkuu hiyo ni sababu ya kumuacha ukizingatia bado ana mtoto hajui kama mama akiwa hana furaha na mawazo tele mtoto ana kuwa dhaifu.
Mama akiwa hana furaha analea watoto bila kujali hisia zao na hapo ndo mtoto anakosea kdg mama anampa adhabu iliyopitiliza..
 
Alitoa,mahari kiasi gani?Akikomaa mpatie mtoto wake..na wew uendelee kumtamfuta wa kukufariji kwa sababu usipoitumia itapotea.
 
Kawaida hiyo mahari ni ya kutunzia mtoto.
Usijeanza kudai matunzo ya mtoto wakati mna pesa zake na ndugu zako
 
Kawaida hiyo mahari ni ya kutunzia mtoto.
Usijeanza kudai matunzo ya mtoto wakati mna pesa zake na ndugu zako
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom