Kiboko ya Jiwe
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 12,705
- 36,154
Habari,
Huu ndio ukweli. Ni wakati sasa Watanzania na viongozi tuache kutwakutwa kujivunia rasilimali za asili badala yake tuwaze maendeleo. Yaani rasilimali zifikiriwe au kutajwa pale tu tunapotaka kufanya jambo.
Tusianze kufikiri na kuzitaja rasilimali kabla ya kufikiri maendeleo (matumizi ya rasilimali). Kutwakutwa kila mtu mara eeh tuna vivutio vingi, mara ukiondoa Brazil sisi tunafuata, Mara oohh tuna rasilimali nyingi kushinda nchi nyingi. So, what?
Hata zikigundulika dhahabu kila kona ya kitanda cha Mtanzania bado ufukara utaendelea kuwaamiza Watanzania. Watanzania wengi wanatafuta asubuhi ili wale mchana, wanatafuta mchana ili wale usiku mmoja tu. Yaani mtu anatafuta akipata anakwenda kumwona mama nitilie.
Anatafuta akipata tu mbio gengeni kuhemea nyanya chungu.
Ndio maana Jiwe alikataa Lock down alijua tu maisha ya Watanzania ni kama ndege, hawana akiba ya miezi 2,3 au 4 mbele. Kama rasilimali hizi zote zilizogundulika na kuanza kutumika hazijamkomboa Mtanzania, basi vivyohivyo hata ardhi yote umbali wa mita moja chini ikijaa Almasi ni bure.
Hapa leo sijagusia malazi, elimu, mavazi na usafiri. Nimegusia msosi tu. Saa sita inakaribia wahangahikaji wanakwenda kugombania msosi wa buku kwa mama nitilie, yaani msosi wa 0.4$, imagine.
Wengine mchana wanatumia jero tu kwa lugha nyingine ni kwamba wanatumia 0.2$ kupata chakula. Wengine wananunua dagaa wa jero, unga nusu 900 nyanya ya mia mbili, maji ya mtoni, kuni. Hapo total 1600 Tshs ambapo ni msosi wa watu 4. Kila mmoja Tsh. 400 ni kama dola 0.1 na ushehe kidogo.